SALA YA ASUBUHI
+Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
Tuusifu Utatu Mtakatifu wa Mungu mmoja, sasa na siku zote na milele amina. Ee utatu Mtakatifu wa Mwenyezi Mungu; +Baba, +Mwana na +Roho Mtakatifu. Ninasadiki kuwa upo hapa na mahali pote.
Ee Mungu wangu, umeniumba, umenikomboa, umenifanya mkristu, umenizidishia neema zako, umenitayarishia makao yangu mbinguni.
Ee Mungu wangu, nakuabudu, nakushukuru, nakuomba toba, nakupenda. Ee Mungu wangu, ninakutolea roho yangu, na mawazo, na maneno, na kazi na furaha, na mateso yangu, uyapokee unipe neema yako nisitende leo dhambi, Amina.
BABA YETU.
Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
Utupe leo mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni. Amina.
SALAMU MARIA.
Salamu, Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe, umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu, mzao wa tumbo lako, amebarikiwa.
Maria mtakatifu, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
KANUNI YA IMANI.
Nasadiki kwa Mungu, Baba Mwenyezi, Muumba wa mbingu na dunia; na kwa Yesu Kristo Mwanae pekee, Bwana wetu, aliyetungwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria, akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato, akasulubiwa, akafa, akazikwa, akashukia kuzimu; siku ya tatu akafufuka kutoka wafu, akapaa mbinguni; ameketi kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi; kutoka huko atakuja kuwahukumu walio hai na wafu.
Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa takatifu Katoliki, ushirika wa Watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili, na uzima wa milele. Amina.
AMRI ZA MUNGU.
1. Ndimi Bwana Mungu wako, usiabudu miungu wengine.
2. Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako.
3. Shika kitakatifu siku ya Mungu.
4. Waheshimu baba na mama; upate miaka mingi na heri duniani.
5. Usiue.
6. Usizini.
7. Usiibe.
8. Usiseme uongo.
9. Usitamani mwanamke asiye mke wako.
10. Usitamani mali ya mtu mwingine.
AMRI ZA KANISA.
1. Hudhuria Misa takatifu Dominika na Sikukuu zilizoamriwa.
2. Funga siku ya Jumatano ya Majivu; usile nyama siku ya Ijumaa Kuu.
3. Ungama dhambi zako walau mara moja kila mwaka.
4. Pokea Ekaristi Takatifu hasa wakati wa Pasaka.
5. Saidia Kanisa katoliki kwa zaka.
6. Shika sheria katoliki za ndoa.
Ee Maria Bikira Mtakatifu, Mama wa Mungu na Mama yangu, nawe Mtakatifu Yosefu, Nawe Malaika Mlinzi wangi, Nanyi watakatifu somo wangu, nanyi Watakatifu wote, Niombeeni nipate kuacha dhambi, nilindeni siku ya leo na siku zote, na saa ya kufa kwangu, Amina.
MALAIKA WA BWANA
•Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria, Naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
~Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria mtakatifu Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
•Ndimi mtumishi wa Bwana, Nitendewe ulivyonena.

•Neno wa Mungu akatwaa mwili, akakaa kwetu.

Utuombee Mzazi mtakatifu wa Mungu, tujaliwe ahadi za Kristo.
Tuombe:
Tunakuomba, ee Bwana, utie neema yako mioyoni mwetu, ili sisi tuliojua kwa maelezo ya Malaika kwamba Mwanao amejifanya mtu, kwa mateso na msalaba wake utufikishe kwenye utukufu wa ufufuko. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu Amina.
SALA KWA MALAIKA MLINZI
Malaika mlinzi wangu, unilinde katika hatari zote za roho na za mwili. Amina.
Moyo Mtakatifu wa Yesu, Utuombee
Roho za waamini marehemu wapate rehema kwa Mungu wapumzike kwa amani.
+Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
Hamkupeperushiwa bendera nusu mlingoti kuwaenzi. Siku moja Bendera hii adhimu inayotambulisha utaifa na ardhi iliyofungua kinywa kupokea damu zenu, itapepea nusu mlingoti kuwaenzi.
Mioyo yetu itaendelea kupepea nusu mlingoti tunaendelea kuwakumbuka na kuwaombea!💔🇹🇿
Waliangamizwa wengi, wengine miili ikapatikana, wengine hata miili yao tu haikuonekana hafi leo. Ndugu wamebaki na majeraha ya kudumu kudhulumiwa si tu uhai wa ndugu zao bali hata maiti zao pia. Huu ni unyama na ukatili wa hali ya juu sana.
Ukweli hauwi uongo kwa sababu tu unahatarisha maslahi ya wenye madaraka. Ukweli ni ukweli tu.
Mkristo anaitwa kutafuta ukweli, si kuubuni. Anaitwa kuutetea, si kuufisha.
Mungu anajua ukweli wote, hata pale wanadamu wanapouficha au kushindwa kuusema.🇹🇿
Kuna wakati kunyamaza si hekima, bali ni kuiacha dhuluma iendelee.
Tunapowakumbuka waliouawa, tunapaswa kujiuliza pia: wale waliokuwa na uwezo wa kutetea haki walifanya nini? Wale waliokuwa na nafasi ya kutafuta ukweli walichukua hatua gani? Na sisi wenyewe tulifanya nini tuliposikia kilio cha wengine?
Nabii Isaya anatoa wito: “Jifunzeni kutenda mema; takeni haki; wasaidieni walioonewa” (Isaya 1:17).
Ni wito wa kutambua kwamba hakuna mwanadamu aliye juu ya wajibu wa kimaadili.
Kiongozi anapaswa kuambiwa ukweli hata pale ukweli huo unapomuumiza. Taasisi zinapaswa kuulizwa maswali hata pale maswali hayo yanapowafanya watu wasijisikie vizuri. Na madai mazito kuhusu vifo yanapaswa kuchunguzwa kwa ushahidi, si kufunikwa kwa vitisho au kejeli.
Dhamiri inatukataza kufanya uongo kuwa silaha, lakini pia inatukataza kuufanya ukimya kuwa kisingizio cha kutokutafuta haki.
Tunawakumbuka waliouawa kwa heshima. Tunaitaka jamii itafakari kwa kina. Tunawaomba viongozi wasikilize kilio cha watu. Na tunajikumbusha kwamba siku moja, kila mmoja wetu atawajibika kwa namna alivyotumia nafasi yake kutetea au kupuuza utu wa wengine.
Tusikubali hofu itufundishe kusahau kile ambacho dhamiri inatuamuru kukikumbuka!!
KANISA LINAPOHUBIRI UTAKATIFU WA UHAI, LAZIMA LIUTETEE UHAI HATA PALE INAPOKUWA NGUMU.
Injili haiishii madhabahuni. Inapaswa kuonekana pia katika namna tunavyowatendea waliodhulumiwa, tunavyowafariji waliofiwa na tunavyosimama mbele ya maswali magumu ya haki.
Yesu alisema: “Nilikuwa na njaa, mkanipa chakula; nilikuwa na kiu, mkaninywesha” (Mt 25:35). Katika Injili hiyo hiyo, anatufundisha kumwona Kristo katika watu walio katika mazingira ya uhitaji na mateso.
Hii inatualika kutafakari kwa kina kuhusu wajibu wa Kikristo tunapokabiliwa na vifo vya watu, hasa pale mazingira ya vifo hivyo yanapohitaji uchunguzi na uwajibikaji.
Kanisa halipaswi kuwa mahali pa kulipiza kisasi. Lakini pia halipaswi kuruhusu lugha ya upatanisho itumike kufunika maumivu au kuzuia maswali ya haki kuulizwa.
Kuwafariji waliofiwa ni huduma. Kudai uchunguzi wa haki ni wajibu wa kimaadili. Kukataa chuki na kulinda ukweli ni sehemu ya ushuhuda wa Kikristo.
Kanisa linapouzungumzia utakatifu wa uhai, sauti yake inapaswa kusikika pia kwa niaba ya wale ambao sauti zao hazisikiki tena.
Tuwakumbuke waliouawa katika sala zetu, tuwaombee familia zao, na tuendelee kutetea utamaduni unaoheshimu maisha, ukweli na haki.
Kwa sababu imani inayompenda Mungu haiwezi kutenganishwa na wajibu wa kumheshimu mwanadamu aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu.
Tunawakumbuka waliouawa. Tunazikumbuka familia zilizobaki na maumivu. Tunakataa kusahau thamani ya uhai wa mwanadamu.
Na tunasisitiza kwamba kiongozi, kama kila mwanadamu mwingine yeyote yule, atasimama mbele ya Mungu kutoa hesabu ya namna alivyotumia mamlaka aliyopewa!
Dhuluma inapotokea, swali si la mtendaji peke yake bali pia la jamii iliyoishuhudia dhuluma hiyo.
Katika Mithali 31:8-9, tunasoma wito wa kusema kwa ajili ya wale wasioweza kujitetea na kuhukumu kwa haki.
Huu ni ukumbusho kwamba imani ya Kikristo haitualiki kuishi kwa kujali wokovu wetu binafsi pekee huku tukipuuza mateso ya wengine.
Tunapowakumbuka waliouawa, dhamiri zetu zinapaswa kutuchochea kuuliza maswali magumu: Je, tulitafuta ukweli? Je, tulisikiliza familia zilizofiwa? Je, tuliheshimu utu wa walioathirika?
Kunyamaza si dhambi katika kila mazingira; wakati mwingine mtu hunyamaza kwa sababu ya hofu, ukosefu wa taarifa au hatari halisi.
Lakini pale ambapo tuna uwezo wa kusaidia kutafuta ukweli kwa njia salama na za haki, hatupaswi kugeuza kutokujali kuwa hekima.
Dhamiri ya Kikristo inahitaji zaidi ya kutosema uongo; inatuita pia kutafuta mema, kutetea walio hatarini na kukataa kushiriki katika udhalilishaji wa wengine.
Ubinadamu wetu haupimwi tu kwa jinsi tunavyowatendea walio hai, bali pia kwa heshima tunayowapa waliopoteza maisha na familia walizoziacha.
UPATANISHO BILA UKWELI NI JENGO LINALOKOSA MSINGI.
Katika maisha ya Kikristo, upatanisho ni zawadi na wajibu. Tunaitwa kujenga upya mahusiano yaliyovunjika na kuondoa chuki zinazotutenganisha.
Lakini upatanisho wa kweli haupaswi kuchanganywa na kufuta kumbukumbu, kuficha ushahidi au kuwashinikiza waliojeruhiwa wanyamaze.
Yesu anasema katika Mathayo 5:23-24 kwamba mtu anapokumbuka kuwa ndugu yake ana jambo dhidi yake, anapaswa kwanza kushughulikia uhusiano huo kabla ya kuendelea na ibada yake.
Fundisho hili linaonyesha kwamba mahusiano na wajibu wetu kwa wengine ni muhimu katika maisha ya kiroho.
Tunapozungumzia vifo vya watu, upatanisho wa kweli unahitaji huruma kwa familia zilizofiwa, utayari wa kusikiliza, uchunguzi wa haki na uwajibikaji pale makosa yanapothibitishwa.
Hakuna anayepaswa kunyimwa haki ya kutafuta ukweli kwa sababu tu wengine wanataka kuendelea na maisha kana kwamba hakuna kilichotokea.
Kusamehe si kusema kwamba uovu ulikuwa wema. Kupatanisha si kufuta WAJIBU. Na kutafuta haki si lazima kumaanishe kutafuta kisasi.
Tukumbuke waliouawa. Tuheshimu familia zao. Tukatae chuki na taarifa zisizothibitishwa. Lakini pia tusikubali ukimya wa uongo inayotegemea kusahaulisha maumivu badala ya kuyashughulikia.
Upatanisho wa kweli hauogopi ukweli. Unautafuta, unakabiliana nao na kuujenga kuwa msingi wa maisha mapya.
Maisha ya waliouawa mwaka jana yalikuwa na thamani, familia zao zina haki ya heshima, na jamii ina sababu ya kutafuta ukweli.
Uongo hauponyi taifa. Ukweli, haki na uwajibikaji ndivyo vinavyoweza kuanza kuliponya.
Kiongozi si lazima ajue kila kitu kuhusu tukio fulani. Anaweza kukiri kwamba tukio lilitokea. Anaweza kuomba msamaha. Anaweza hata kurekebisha kauli yake baada ya kupata ushahidi mpya.
Hayo si udhaifu. Ni uaminifu.
Tatizo huanza pale ambapo kulinda taswira kunakuwa muhimu kuliko kujua kilichotokea, na pale ambapo maswali ya msingi yanaonekana kuwa maadui badala ya nafasi ya kutafuta haki.
Sifa za mwanadamu ni za muda. Lakini uaminifu ni wajibu wa dhamiri.
Kuna maumivu ya kufiwa na mpendwa. Lakini kuna maumivu mengine yanayoweza kuongezeka pale waliofiwa wanapoona kwamba maswali yao yanapuuzwa au kwamba ukweli unaonekana kuwa tishio kwa wenye mamlaka.
Ndiyo maana uwajibikaji baada ya vifo vya watu ni suala la haki na pia la utu.
Usiwaambie watu wawe na amani kabla hujasikiliza kwa nini wanalia.
Amani ni jambo jema. Umoja wa jamii ni muhimu. Lakini amani ya kweli haiwezi kujengwa kwa kudharau maumivu ya waliofiwa au kuyachukulia maswali yao kama usumbufu.
Katika Injili ya Yohane 11:33-35, Yesu anakutana na Maria, Martha na wengine waliokuwa wakiomboleza kifo cha Lazaro. Yesu anaguswa na huzuni yao, na Injili inasema: “Yesu akalia machozi.”
Hili ni fundisho lenye uzito wa kiroho: mbele ya kifo, huruma si udhaifu. Ni sehemu ya upendo.
Ikiwa Yesu hakudharau machozi ya waliokuwa wamefiwa, sisi ni nani hata tuwadharau watu wanaotafuta majibu kuhusu wapendwa wao?
Viongozi wanapaswa kuelewa kwamba jamii haiwezi kuponya majeraha ambayo hairuhusiwi hata kuyazungumzia.
Kuwasikiliza walioathirika hakumaanishi kuhitimisha mapema kwamba kila madai ni ya kweli. Kunamaanisha kuyachukulia kwa uzito na kuhakikisha kwamba ukweli unatafutwa bila upendeleo.
Amani inayodumu haiogopi maswali. Umoja wa kweli hauhitaji watu wajifanye kwamba hawajaumia. Na upatanisho hauwezi kuwa wa kina ikiwa maumivu ya wahanga yanadharauliwa.
Tuwape waliofiwa nafasi ya kuomboleza. Tuheshimu maswali ya jamii.
ROZARI TAKATIFU, ALHAMISI (MATENDO YA MWANGA)
1. Yesu anabatizwa mto Yordani. - Tumwombe Mungu atujalie uaminifu kwa ahadi zetu za ubatizo
2. Yesu anageuza maji kuwa Divai huko Kana.
- Tumwombe Mungu atujalie kuukoleza ulimwengu kwa chachu ya Injili.
3. Yesu anatangaza Ufalme wa Mungu.
- Tumwombe Mungu atujalie tupokee ufalme wake kwa toba ya kweli.
4. Yesu anageuka sura.
- Tumwombe Mungu atujalie neema ya kuung'arisha ulimwengu kwa uso wa Yesu.
5. Yesu anaweka Sakramenti ya Ekaristi.
- Tumwoombe Mungu atujalie neema ya kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine
Bikira Maria Malkia wa Rozari Takatifu, Utuombee!
Tunakataa kusahaulishwa yaliyotokea. Tunakataa kulazimishwa kuona ilikuwa jambo la kawaida. Tunakataa unyama uliofanywa ndani ya nchi yetu na wenye mamlaka. Tunakataa wenye nguvu kupuuza maisha ya wanyonge. Tunakataa kusahau damu isiyo na hatia iliyomwagika.
HATUTASAHAU KAMWE!🇹🇿
Tunapowakumbuka waliouawa, hatuitafuti jamii inayotawaliwa na kisasi. Tunaitafuta jamii inayothamini maisha, inayosikiliza waliofiwa na inayokataa kufunika makosa yaliyo wazi.
Amani ya kweli haijengwi kwa kusahau waliopoteza uhai wao. Inajengwa kwa kuhakikisha kwamba maisha yao hayakupotea bila jamii kujifunza, kutafuta haki na kuchukua hatua zinazostahili.
💔🕊️🇹🇿🕯️ Tarehe kama ya leo 29 Oct 2025, risasi na mabomu yalikatisha maisha ya ndugu, jamaa na marafiki zetu wengi, zikaacha watoto yatima, wazazi wakiwa na vilio na familia zikiwa na maumivu yasiyoelezeka. Wengine walitoka nyumbani bila kujua kuwa hawatarudi tena.
Ee Mwenyezi Mungu, uwapokee ndugu zetu na uwafariji wote waliobaki na majeraha ya kudumu mioyoni mwao. Uhai wa mwanadamu una thamani.
Raha ya milele uwape Ee Bwana, na mwanga wa milele uwaangazie. Wapunzike kwa amani, Amina🙏