VIDEO:
Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya na mwanaharakati wa kupinga mapenzi ya jinsia moja Dudu Maba, Mamba24 amewajibu waliofanya tamasha la mapenzi ya jinsia moja na kudai kuwa watamshitaki.
Aliyekuwa Makamu wa Rais Dkt. Emmanuel Nchimbi, ameonekana nchini Dubai hivi karibuni akiwa kwenye mapumziko, taarifa ambazo zinafuta uvumi uliokuwa ukienea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kutoonekana kwake wiki kadhaa tangu ajiuzulu
VIDEO:
Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, DCP David Misime, kwa niaba ya jeshi hilo, ametoa onyo kali kwa yeyote anayejihusisha na mipango ya kihalifu, kwani jeshi halitasita kuchukua hatua kali kwa mujibu wa sheria kwa watakaobainika.
VIDEO:
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Paul Makonda amekosoa wanasheria wa kampuni ya Sandaland kutangaza kumshitaki badala ya kuchukua hatua ya kwenda mahakamani moja kwa moja.
VIDEO:
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu ametuma salamu za Pole kwa Rais Samia Suluhu Hassan na familia yake kufuatia kifo cha Mwalimu Hafidh Ameir.
VIDEO:
Mtangazaji Edwin Odemba [ @chiefodemba ] ambana Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Laban Kihongosi kuhusu alipo aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Emmanueli Nchimbi, na sababu za kufukuzwa uwanachama.
VIDEO:
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo Septemba 03, 2026, baada ya kesi yake kuahirishwa ametumia maneno kutoka katika wimbo wa Bob Marley.
Lissu amerudishwa rumande hadi hapo kesho Septemba 04, 2026 ambapo shahidi wake wa tatu ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Amani Golugwa ataanza kuulizwa maswali ya dodoso na Mawakili wa Serikali.
VIDEO:
Ujumbe wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu kwa wanaosema Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho John Heche anakwamisha yeye (Lissu) kutoka gerezani.
Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amesema kupata uzoefu na kuondoa dhana ya watendaji kujenga ‘falme’ katika maeneo wanayohudumu ni miongoni mwa sababu zilizomfanya kufanya mabadiliko na kuwahamisha baadhi ya wakuu wa mikoa.
Dkt Samia ameeleza hayo Jumatano Septemba 2,2026 wakati wa akiwaapisha wakuu wa mikoa na katibu tawala aliowateua hivi karibuni. Uapisho huo umefanyika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Kusini Unguja.
“Moja ni kupata uzoefu kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine. La pili, kutotengeneza ufalme pale ulipo, kwamba ndio kwangu na himaya ulizozijenga ndio za kwako. Hapana, wewe ni mtumishi wa umma, unaweza kutumika popote pale,” ameeleza.
Rais Samia amekumbusha kuwa katika mkutano wake wa mwisho na wakuu wa mikoa aliwaambia kuwa yeye anawachukulia kama jeshi lake, hivyo hatarajii kuona jeshi hilo likichafuka.
“Huko mliko nimekuwa nikipata taarifa hizi, zile; huyu ana hivi, huyu ana lile. Sasa kuwabadilisha ni kuwaondosha katika matatizo yale ambayo nayapokea. Sasa kama ulikuwa unajijua una tabia mbaya au yoyote, nenda kajirekebishe, tumikia wananchi kama inavyotakiwa,” amesema Dkt Samia.
1
6
1,889
VIDEO:
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mohamed Kawaida ametaja moja ya sababu zilizopelekea aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Emmanueli Nchimbi kufukuzwa uwanachama wa CCM.
Amesema Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya chama hicho kwa kushirikiana na NEC, ilitoa maelekezo ya Nchimbi kuitwa katika kamati ya maadili, lakini kwasababu ya kiburi na kudharau maelekezo ya chama, Nchimbi alikaidi wito huo.
Amesema hayo leo Agosti 29, 2026, jijini Dodoma, muda mfupi baada ya kushuhudia kuapishwa kwa Makamu mpya wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi.
VIDEO:
Mbunge wa Jimbo la Geita vijijini Joseph Kasheku Musukuma, amemuomba Makamu wa Rais Mteule, kutofanya mambo kama yaliyopelekea taifa kurudi katika mchakato wa kumpata Makamu wa Rais mwingine.
Musukuma amemtaka Ndejembi akamsaidie Rais kwa uaminifu mkubwa, kwani Taifa linamtegemea na lisingependa kumuona Rais Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye 'stress' (msongo wa mawazo)
VIDEO:
Neno la Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu, baada ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Emmanueli Nchimbi, kuvuliwa uwanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi amefukuzwa uanachama wa chama hicho.
Dk Nchimbi amefukuzwa unachama siku moja baada ya kumwandikia barua Rais Samia Suluhu Hassan kumwomba kujiuzulu nafasi ya Makamu wa Rais ambapo ombi hilo lilikubaliwa.
Uamuzi wa kufukuzwa uanachama, umetangazwa usiku wa leo Jumatano, Agosti 26, 2026 na Katibu Mkuu wa CCM, Dk Asha Rose- Migiro alipozungumza na waandishi wa habari, ofisi ndogo za chama hicho, Lumumba jijini Dar es Salaam.
Ambapo alikuwa akitoa maazimio ya vikao vya kamati kuu na Halmashauri Kuu vilivyokutana jijini Dar es Salaam kuanzia asubuhi hadi usiku wa leo Jumatano.
Dk Migiro amesema kulikuwa na ajenda ambazo zilijadiliwa na miongoni ni suala la maadili lililokuwa linamkabili mwanachama wetu Dk Nchimbi na vikao vyote vilijadili
VIDEO:
Wakili Peter Madeleka amesema kuwa uanaharakati hauna uhusiano wowote ule na vitendo vya kigaidi, na kwamba yeyote anayefanya ugaidi anatenda kosa kama makosa mengine na sio kwasababu ya kazi ya harakati anayoifanya.
VIDEO:
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mnyika, amesema kuwa pesa za michango ya tone tone ziko salama na kwamba tuhuma za matumizi mabaya ya pesa hizo zimetengenezwa kwa lengo la kuwatoa kwenye reli.
VIDEO:
Hali ilivyo katika mitaa mbalimbali ya Kimara, Ubungo, Dar es Salaam leo tarehe 07/07/2026, saa moja asubuhi.
VIDEO:
Mbunge wa zamani wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Mrisho Gambo amesisitiza kuwa maridhiano yanayohubiriwa Nchini yanapaswa kuwa na ukweli, nia thabiti na dhamira ya kweli ya kulirejesha Taifa katika misingi ya Upendo, mshikamano na amani.
Gambo amebainisha hayo Jumapili Juni 21, 2026 wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye harambee ya kuchangia ujenzi wa Makao Makuu ya Kanisa la Pentecoste Revival Church la Jijini Arusha, akisema haki ikitendeka kwenye jamii, kazi ya kuridhiana itakuwa rahisi kwasababu wahusika wataelewa lengo la kutaka kuridhiana kwao.
Katika harambee hiyo jumla ya Shilingi 116, 206,000 zilipatikana huku Mwanasiasa huyo akichangia Shilingi Milioni 10 pamoja na Shirika la hifadhi ya Taifa likichangia Shilingi Milioni kumi katika kufanikisha ujenzi wa Kanisa hilo.
"Mtu yoyote anayehubiri amani lazima aanze na haki. Mahali ambapo kuna haki, hapatakuwa na manung'uniko. Amani ni tunda la haki." Amesema Mrisho Gambo.
Gambo amesisitiza kuwa ujenzi wa Taifa ni jukumu la kila mwananchi, akionya kwamba Taifa likiharibika hakuna mtu atakayenufaika, akisema Taifa haliwezi kujengwa kwa ujanjaujanja, bali kwa misingi ya ukweli, haki na uwajibikaji ili kudumisha amani na umoja Nchini.
Aidha, katika hatua nyingine Mrisho Gambo amewaasa viongozi wa dini kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhubiri amani na mshikamano, huku wakisisitiza umuhimu wa haki katika nyanja zote za maisha, kuanzia katika taasisi za dini, jamii na hata serikalini.
VIDEO:
Mbunge wa Jimbo la Katavi, Thomas Kampala Maganga, ametoa wito kwa serikali na jamii kuongeza juhudi katika kupambana na tabia za mapenzi ya jinsia moja, kwani pasipo kufanya hivyo utekelezaji wa Dira ya Maendelo 2025-2050 utakuwa kizungumkuti kwani vijana wengi wanaangamia kwa kuangukia katika tabia hizo, huku akiutuhumu Mkoa wa Dar es Salaam kuwa chanzo kikubwa cha tatizo hilo.



