
Inform | Engage | Empower | You can also follow our Updates through @JamiiForums , @JamiiCheck
Joined April 2025
- Tweets1K
- Following6
- Followers119
- Likes406
JamiiForums Uganda retweeted
Media Investment Trends - promoting digital resilience, AI readiness & bridging the online and offline divide: Lessons from the region, Case of JamiiAfrica - session led by a delegation from @JamiiAfrica
@MAZ_Zim @IMSforfreemedia @InfoMinZW @NigelNyamutumbu @ZinefZimbabwe1
JamiiForums Uganda retweeted
Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” imeendelea kuwa na matokeo mabaya katika Hatua ya Makundi kuwania Kufuzu Michuano ya AFCON 2027 kwa kupata kichapo cha magoli 3-1 kutoka kwa Nigeria kwenye Uwanja wa Godswill Akpabio, leo Novemba 13, 2026.
Baada ya matokeo hayo Guinea-Bissau inaongoza msimamo wa Kundi L kwa kuwa na pointi 7, Nigeria ya pili ina 6, Madagascar ina 2 na Tanzania ina alama 1.
Michezo ijayo ya Kundi hilo itapigwa Novemba 15, 2026, Guinea-Bissau Vs Madagascar, Tanzania Vs Nigeria (Uwanja wa Amaan – Zanzibar).
Zaidi jamii.app/NigeriaVsTanzania
#JamiiForums #JFSports #JFAFCON2027
JamiiForums Uganda retweeted
Dkt. David Mgaya, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mfumo wa Mkojo na Mbobezi wa Afya ya Uzazi kwa Wanaume anasema “Kuna sababu tofauti za tatizo la nguvu za kiume, kwa vijana inaweza kuhusishwa na changamoto za Kisaikolojia, Watu Wazima magonjwa, pia vipandikizi vinavyowekwa kipo cha miaka 15 na kingine kinachoweza kudumu maisha yote.”
Fuatilia zaidi jamii.app/UpasuajiMuhimbili
#JamiiForums #JFAfya
JamiiForums Uganda retweeted
ENGLAND: Tangu alipoteuliwa kuwa kocha wa Manchester United Januari 2026 hadi Novemba 2026, Michael Carrick ameiongoza timu hiyo katika Mechi 32, Ushindi 15, Sare 8 na Kupoteza 9.
Viongozi wa Manchester United wanatarajiwa kumtangaza Mauricio Pochettino, kocha wa timu ya taifa ya Marekani (#USMNT), kumrithi Carrick. Pochettino alisaini mkataba mpya Agosti 3, 2026, utakaomuweka kazini hadi 2030, ukiwa na kipengele cha kuvunja kwa Pauni Milioni 7.5 sawa na Tsh. Bilioni 26.4.
Soma jamii.app/CarricOutUnited
#JamiiForums #JFSports
JamiiForums Uganda retweeted
Tarehe 31 Oktoba na 1 Novemba 2026, #JamiiAfrica kwa kushirikiana na #ZAFAYCO walifanya mafunzo maalumu kwa Wananchi kuhusu Uwajibikaji na Ushiriki wa Wananchi Kupitia Majukwaa ya Kidijitali.
Inaendelea👇
JamiiForums Uganda retweeted
ENGLAND: Timu ya #ManchesterUnited imeendelea kupata matokeo ya kusuasua katika Ligi Kuu ya England "Premier League” baada ya kupata sare ya magoli 4-4 kutoka kwa #AstonVilla kwenye Uwanja wa Old Trafford.
Matokeo hayo yanaendelea kuiweka Man United katika nafasi mbaya kwenye msimamo wa ligi, ikiwa nafasi ya 18 kwa alama 8 ikiwa ni ya tatu kutoka chini.
United ilikuwa nyuma kwa magoli 2-0 ikasawazisha 2-2 kisha ikawa nyuma tena kwa 4-2 ikasawazisha.
Zaidi jamii.app/ManUnVsAstonVilla
#JamiiForums #JFSports #JFEPL2026
JamiiForums Uganda retweeted
Katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, Mahakama haijamkuta na hatia ya kosa la uhaini.
Hata hivyo, Mahakama imemtia hatiani Lissu kwa kosa dogo la uchochezi.
Fuatilia zaidi jamii.app/HkmLissuUchochezi
#JamiiForums #JFMatukio
JamiiForums Uganda retweeted
Mahakama imemhukumu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu kifungo cha miaka minne gerezani kwa kosa la uchochezi kwa kuvuruga uchaguzi, kitendo ambacho Jaji Ndunguru amekitafsiri kuwa ukiukwaji wa Katiba. Akitoa uamuzi huo kwa kutumia Kifungu cha 35 kutokana na Kifungu cha 390 cha Kanuni ya Adhabu kutobainisha kiwango cha adhabu, Jaji amesisitiza katika kudai haki, mtu hapaswi kuingilia haki za wengine.
Pamoja na mahakama kuzingatia hoja za afya na ugonjwa wa mshtakiwa, imeelekeza kuwa maombi yoyote ya dhamana yatafanyika tu baada ya yeye kuanza kutumikia adhabu hiyo gerezani, huku akiwa na haki ya kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo. Awali Lissu alikabiliwa na shtaka la uhaini lakini Mahakama ilimuachia huru kwa shtaka hilo baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha nia ya kutenda kosa hilo.
Zaidi jamii.app/Lissu4YrsJela
#JamiiForums #JFMatukio
JamiiForums Uganda retweeted
ENGLAND: Timu ya Manchester United bado inaendelea kuwa katika hali tete baada ya kupoteza mchezo wa Premier League dhidi ya Chelsea kwa magoli 2-0.
Hali ilizidi kuwa ngumu kwa United baada ya mchezaji wao, Lisandro Martínez, kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 63.
Baada ya matokeo hayo, Manchester United inabaki na pointi 7 katika kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England ikiwa imeshinda mechi moja tu.
jamii.app/ManchesterUnitedVs…
#JamiiForums #JFSports
JamiiForums Uganda retweeted
Salamu za faraja kwa wote mliopoteza wapendwa wenu. Nguvu, Upendo na Matumaini viwe nanyi.
Zaidi jamii.app/RmbrncOctDths
#JamiiForums
JamiiForums Uganda retweeted
Uwanja wa Raila Odinga International Stadium, uliopo Talanta Sports City jijini Nairobi, utafunguliwa rasmi Januari 5, 2027, kwa mechi maalumu kati ya Bayern Munich na AFC Ajax
Uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000 una miundombinu ya kisasa, ikiwemo skyboxes 52 za kifahari na maeneo maalumu ya wageni waalikwa
More jamii.app/UfunguziUwanjaOdin…
#JamiiForumsKE #KenyaNews
JamiiForums Uganda retweeted
Jengo la ghorofa lililokuwa likijengwa limeanguka eneo la Eastleigh, Nairobi, Ijumaa, Oktoba 23, na ambapo operesheni ya uokoaji inaendelea huku kukiwa na hofu kuwa watu wamekwama chini ya vifusi
Jengo hilo lilikuwa kando ya Barabara ya Yusuf Haji, karibu na duka la Day to Day Supermarket, Mtaa wa 9. Picha kutoka eneo hilo zilionesha jengo hilo likiwa limebomoka na kuacha marundo ya vipande vya zege, huku waokoaji wakikusanyika katika eneo la tukio
More jamii.app/JengoNairobi
#JamiiForumsKE #KenyaNews
JamiiForums Uganda retweeted
Mamlaka zimeanzisha msako wa kumtafuta mwenye jengo lililoporomoka Eastleigh, Nairobi, Oktoba 23, 2026
Gavana Johnson Sakaja alisema jengo hilo lilikuwa limeidhinishwa kujengwa, lakini halikuwa na cheti cha kuruhusu matumizi, hali iliyoibua maswali kuhusu kuanza kutumika kwake kabla ya kukamilika kwa ujenzi
More jamii.app/JengoMmiliki
#JamiiForumsKE #KenyaNews
JamiiForums Uganda retweeted
Oktoba 7, 2026, Mkurugenzi Mtendaji wa #JamiiAfrica, Maxence Melo atashiriki kikao kazi cha "The Face of Digital Democracy 2026" Mjini Copenhagen kilichoandaliwa na Good Commons ambao ni umoja ulioanzishwa na JamiiAfrica kutoka Tanzania, IMS kutoka Denmark na Splice Media kutoka Singapore.
Mkusanyiko huo utajumuisha Waandishi wa Habari na Waendeshaji wa Majukwaa mbalimbali kutoka Kabul, Dar es Salaam, Amman na Copenhagen, wakijadili masuala mbalimbali kuhusu Demokrasia Kidigitali.
Mjadala huu ni sehemu ya maadhimisho ya kila mwaka ya Demokrasia Mitandaoni kutoka Digital Democracy Initiative.
Zaidi jamii.app/DigitalDemocracy20…
#JamiiForums #DigitalDemocracy2026 #DigitalRights
JamiiForums Uganda retweeted
DAR: JamiiAfrica kwa kushirikiana na kampuni ya kiteknolojia kutoka Canada, Viamo, wamezindua teknolojia ya Akili Unde (Al) ya sauti "Ask Viamo Anything" (AVA), inayowawezesha wananchi kupata taarifa na majibu ya maswali mbalimbali bila kuhitaji intaneti, katika hafla iliyofanyika Septemba 29, 2026.
Huduma ya AVA kwa sasa inapatikana kwa watumiaji wa Vodacom kwa kupiga Namba 0901760321 na kisha unachagua AVA.
Fuatilia zaidi, shiriki jamii.app/UzinduziAVA
#JamiiForums #OngeaNaAVA #MuulizeAVA #MshirikisheAVA
JamiiForums Uganda retweeted
Leo, Septemba 30, 2026, #JamiiAfrica imepata ugeni wa Balozi Mteule wa Sweden nchini Tanzania, Ingrid Teresia Johansson.
Balozi Mteule aliambatana na maafisa wa Ubalozi, wakiongozwa na Bi. Sandra Diesel ambaye ni Mkuu wa Ushirikiano wa Kimaendeleo (Head of Development Cooperation) wa Ubalozi huo.
JamiiForums Uganda retweeted
Uzinduzi huo umefanyika Septemba 29, 2026, jijini Dar es Salaam, katika hafla iliyohudhuriwa na Balozi wa Canada nchini Tanzania, Emily Burns, pamoja na wadau wa habari, asasi za kiraia na teknolojia nchini Tanzania.
Zaidi jamii.app/UzinduziAVA
#OngeaNaAVA #LaunchAVA #AskViamoAnything
JamiiForums Uganda retweeted
JamiiAfrica kwa kushirikiana na kampuni ya kiteknolojia kutoka Canada, Viamo, wamezindua teknolojia ya Akili Unde (Al) ya sauti inayowawezesha wananchi kupata taarifa na majibu ya maswali mbalimbali bila kuhitaji intaneti kwa kupiga namba 0901760321 kwa Watumiaji wa Vodacom kwa sasa.
JamiiForums Uganda retweeted
DAR ES SALAAM: JamiiAfrica leo tarehe 23 Septemba 2026 imeingia makubaliano ya ushirikiano wa miaka miwili na Ubalozi wa Norway.
#JamiiAfrica #StrategicPartnerships
JamiiForums Uganda retweeted
KIGOMA: Mdau wa JamiiForums.com anatoa Wito kwa mamlaka husika kufanya Uchunguzi kwenye mradi wa kujenga Kiwanda cha Sukari Kasulu.
Mdau, una maoni gani?
Zaidi jamii.app/MradiSukariKigoma
#JamiiForums #Uwajibikaji #JFMdau2026






































