
PCVE Expert|Views are mine😉|Justice Lover ⚖️|Quran is my 📖|+259 (Zanzibar)|Ibwera my roots|Co-Founder @kijana_hai| Zanzibar National Coordinator - THRDC
Dar es Salaam & Zanzibar
Joined June 2013
- Tweets22.1K
- Following2.2K
- Followers4.6K
- Likes11.8K
Chief Suleimān M. M. Baitani retweeted
UCHAGUZI 29 OKTOBA. Ee Mungu Tunawaombea marehemu wetu raha ya milele. Tuwazike kwa heshima, kuwafariji wafiwa, kuuguza majeruhi, kusaidia waathirika. Tuombe toba kuondosha sifa za taifa letu kwa kutotambua HAKI ndiyo msingi wa yote na haina mbadala. Twakuomba utusikie
Chief Suleimān M. M. Baitani retweeted
Today, 7th November 2025, we, the undersigned Civil Society Organizations (CSOs), strongly condemn widespread human rights violations that occurred before, during, and after Tanzania’s 2025 General Elections.
These include killings of civilians, unlawful arrests, abductions, enforced disappearances, suppression of media freedoms, an internet shutdown, and denial of due process rights.
There are verified reports of excessive use of force against unarmed demonstrators, including reprisal killings of civilians, some in their own homes. Families have been left traumatized, and children have witnessed violence against their parents.
Journalists were not spared: Master Tindwa (Clouds Media) was killed at his home in Temeke, Kelvin Lameck Mwakangondya (Baraka FM, Mbeya) was killed while on duty, A journalist from Azam Media was seriously injured, and two others, Godfrey Thomas (Ayo TV) and Alphonce Kusaga (Sunrise Radio), were arrested in Arusha. A religious leader, Sheikh Msopa, was shot dead at his home in Dar es Salaam.
We also note reports of mass arrests and detentions of hundreds of civilians, particularly youth, across several regions, many still held without bail or court appearance. For six consecutive days since 29th October, the nationwide internet shutdown restricted access to information, monitoring of elections, and exposure of rights violations, in direct breach of Article 18 of the Constitution and international obligations.
We stand in solidarity with all victims and urge the Government to:
1️⃣ Release all detainees or bring them before the court.
2️⃣ Allow families to bury their loved ones.
3️⃣ Permit independent investigations into the killings.
4️⃣ Prosecute those responsible.
5️⃣ Uphold freedom of expression and the media.
6️⃣ Work toward reconciliation and national healing.
7️⃣ Compensate affected families.
Signed by: LHRC, Twaweza, Foundation for Civil Society, JamiiAfrica, Msichana Initiative, Centre for Strategic Litigation, and Internet Governance Tanzania Working Group.
📄 Full statement attached.
This is powerful. 🫡🫡
Mlisali, mkafunga na mkamwomba Mungu kwa dua na machozi. Maombi yenu yamefika mbinguni. Mnafikiri haya mauaji na mateso ya watoto wenu ndiyo majibu kutoka kwa Mungu? Hapana. Msihofu. Mungu yupo, na bado anafanya kazi yake kwa njia zake.
Kila tone la damu lililomwagika lina thamani mbele zake. Kila kilio, kila pumzi ya mwisho, ni ushahidi wa mateso yasiyo na hatia. Mungu hawezi kupuuza machozi ya waja wake. Atalipa, na kwa wakati wake, haki itatimia.
Msiache kuamini. Jipeni moyo, maana imani ndiyo tumaini letu pekee. Wengi wamekufa, wengi wamepotea, lakini hakuna kinachopotea bure machoni pa Mungu. Siku moja, mtaona kuwa maumivu haya yote hayakuwa ya bure. Siku moja, machozi yatafutwa, na moyo uliojeruhiwa utapata amani. Na hapo mtasema kwa machozi ya furaha “Asante Mungu, kwa sababu ulikuwa nasi hata katika giza.”
Kuna muda nahisi, this is not Tanzania. Madogo wanatazama game la arsenal wote wanapoteza uhai. What happened to humanity?
This quoted post is unavailable.
Deeply disturbed by the abduction of Mr. Humphrey Polepole. We stand united for his safety & justice. Tanzania must protect all voices, not silence them. #JusticeForPolepole #HumanRightsDefenders #THRDC
#SCATZ 👏👏👏
*Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umefanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania*
Leo Mei 05, 2025 Mratibu wa Kitaifa THRDC, Wakili Onesmo Olengurumwa na Wakili Paul Kisabo Mkuu wa Idara ya Utetezi THRDC wamefanya ziara ya kimkakati na kukutana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson. Ziara hiyo imefanyika katika Ofisi ndogo ya Bunge iliyopo jijini Dar es Salaam.
Lengo kuu la ziara hiyo lilikuwa ni kueleza shughuli ambazo THRDC na Washirika wake ambao ni Jumuiya ya Wanasheria wa Afrika Mashariki (EALS), Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) na Jumuiya ya Wanasheria wa Afrika (PALU) wamepanga kuzifanya kwa kushirikiana na wadau wa masuala ya haki za binadamu, taasisi zinazohusika na utawala wa Sheria nchini ili kuimarisha mchango wa Bunge katika masuala ya utawala wa sheria na haki za binadamu nchini.
Vilevile, THRDC imewasilisha ombi kwa Mhe. Spika la kuanzishwa kwa Kamati Maalumu ya Bunge ya Masuala ya Haki za Binadamu ambayo wabunge watashirikiana na Watetezi wa haki za binadamu na Mashirika ya haki za binadamu katika kufanya kazi kwa pamoja.
Mhe. Dkt. Tulia amepongeza jitihada zinazofanywa na THRDC na washirika wake katika kuimarisha ushirikiano na taasisi zinazohusika na masuala ya haki za binadamu na utawala wa sheria nchini. Ameahidi kuwa ofisi yake itatoa ushirikiano katika shughuli ambazo THRDC na washirika wake wanazifanya.
Ziara hii ni sehemu ya utekelezaji wa mradi ambao Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Jumuiya ya Wanasheria wa Afrika Mashariki (EALS), Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) na Jumuiya ya Wanasheria wa Afrika (PALU) wanafadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) unaolenga “Kuboresha Utawala wa Sheria, Utawala Bora, Nafasi ya Kiraia, na Uwajibikaji nchini Tanzania kupitia Ushirikiano Ulioimarishwa.”
*Imetolewa na:*
*Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC)*
*05 Mei 2025*
Chief Suleimān M. M. Baitani retweeted
Leo Mei 06, 2025 Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) na Jumuiya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) wamefanya ziara ya kimkakati na kukutana na Uongozi wa Mahakama Kuu Zanzibar. Kikao hicho kimefanyika Mahakama Kuu, Tunguu, Unguja, Zanzibar. Lengo kuu la kikao hicho lilikuwa ni kujadiliana namna bora ya kushirikiana katika kufanya Mkutano wa pamoja kati ya Majaji, Mahakimu, Mawakili na wadau wengine wa haki (Bar – Bench Forum).
THRDC iliongozwa na Mratibu wa Kitaifa Wakili Onesmo Olengurumwa @OlengurumwaO , Suleiman Mujuni Baitani – Mratibu THRDC Zanzibar, Wakili Paul Kisabo @Advocate_Kisabo – Mkuu wa Idara ya Utetezi THRDC na Wakili Shadida Omari – Afisa Programu THRDC Zanzibar, na Wakili Salma Omary – Afisa Programu ZAFELA. Mahakama Kuu Zanzibar iliongozwa na Mrajis Mhe. Jaji Valentina Katema, Naibu Mrajis Mhe. Jaji Faraji Shomari, Mkurugenzi wa Mipango Mhe. Mohamed Salim na maofisa wengine wa Mahakama Kuu Zanzibar.
Katika kikao hicho wamejadili namna ya kushirikiana kwa pamoja katika maandalizi ya kufanya Mkutano wa pamoja kati ya Majaji, Mahakimu, Mawakili na wadau wengine wa haki (Bar – Bench Forum). Kikao kimeafiki kuunda Kamati Maalumu ya kufanya maandalizi ya mkutano huo. Kamati hiyo itajumulisha Mahakama, Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Chama cha Wanasheria Zanzibar, Wizara ya Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar na Sekretarieti kutoka THRDC, EALS, ZAFELA na PALU.
Kikao cha leo ni sehemu ya utekelezaji wa maazimio ya kikao cha taasisi zinazohusika na masuala ya haki za binadamu, utawala bora pamoja na wadau wengine wa haki ambacho kilifanyika Aprili 8, 2025 jijini Dodoma na kuazimia kuunda Kamati ya Kitaifa kwaajili ya kuandaa Mkutano wa pamoja kati ya Majaji, Mahakimu, Mawakili na wadau wengine wa haki (Bar – Bench Forum).
Vilevile hii ni sehemu ya utekelezaji wa mradi ambao Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA), Jumuiya ya Wanasheria wa Afrika Mashariki (EALS) na Jumuiya ya Wanasheria wa Afrika (PALU) unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) unaolenga “Kuboresha Utawala wa Sheria, Utawala Bora, Nafasi ya Kiraia, na Uwajibikaji nchini Tanzania kupitia Ushirikiano Ulioimarishwa.”
*Imetolewa na:*
*Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC - Zanzibar)*
*Mei 06, 2025*
Chief Suleimān M. M. Baitani retweeted
Building Strategic Engagement and Partnerships among rule of law actors. With me are Chief Justice of Zanzibar, Hon. Khalid Ramadhani, Chief Kadhi, Hon Shekh Othman Omary, Deputy Kadhi , Registrar’s HC Zanzibar , President Zanzibar Law Society and representatives from PÀLU , EALS, ZAFELA and THRDC -Zanzibar.
THRDC Zanzibar plays a fundamental role in ensuring judicial reforms process are effective, inclusive and based on human rights approaches. We are very proud to see the current progress made by the Judiciary of Zanzibar for past few years. For the last few years the Judiciary of Zanzibar has made a significant change in upholding the rule of law, judicial reforms, access to justice, particularly in ensuring fair administration of justice and strengthening public trust in legal institutions.
This collaboration aligns with Zanzibar’s Judicial Strategic Plan and broader governance reforms aimed at promoting justice and human rights. We also seek to explore opportunities to deepen engagement between the Judiciary, bar associations, civil society, and key stakeholders to improve legal awareness and strengthen civic space protections. @LawyersofAfrica @ealawsociety @TanganyikaLaw @zafela @THRDCOALITION @ThrdcZanzibar @judiciarytz @Mwabuk2Boniface @EUinTZ @SwedeninTZ @MBaitani
"Ziko wapi enzi za ulumbi na waneni wenye Kiswahili mufti? Kitabu hiki kinarejesha hadhi ya lugha na kueleza ukombozi wa Afrika na Tanzania kama kinara wake. Ni mwenge wa matumaini kwa kizazi cha sasa na kijacho." @NkumbiJoram
Hiki kitabu ni fumbua macho! Hongera sana 👏👏
Chief Suleimān M. M. Baitani retweeted
So excited to have this special visit from ACT Party Leader @SemuDorothy akiwa katika ziara yake ya kutembelea wadau mbalimbali. We value the role of political parties katika harakati za kujenga democracy na rule of law. Tunasisitiza kwa vyama kuweka mambo y’a haki za binadamu kwenye ilani zao za uchaguzi. Vyama vya upinzani jitahidini kuwa pamoja mnapotafuta mageuzi makubwa nchini. @ACTwazalendo
Ninafurahishwa sana na jitihada zisizo na mwisho za Mratibu wa Taifa @THRDCOALITION katika kuhakikisha haki za binadamu zinaheshimiwa na kulindwa. Hongera za dhati kwa Kaka zangu @ExMayorUbungo, @IAMartin_, na @zittokabwe kwa mchango wao mkubwa katika jambo hili la msingi. 🇹🇿
Tunatoa shukran za dhati kwa Mhe Mama Samia @SuluhuSamia kwa kutumiza a hadi na kulipia gharama za awali za upasuji mkubwa wa ndugu @Sativa255 tumepokea nakala ya malipo kiasi cha 35 milion kwenda Agakhan Hosptali. Leo jioni Sativa atafanyiwa upasuaji. Hizi ni gharama za awali tuombe kila kitu kiende sawa na gharama zisiwe kubwa huko mbele. Kuna faida kubwa kwa Mhe Rais kuweka mkono wake katika hili. Hii ni salamu kwa walioko nyuma ya swala hili. Pili tunaamini pia ushauri wetu wa tume huru atafanyia kazi. Kama mzazi na mama swala hili pia limemgusa. Asante pia Mhe @zittokabwe kwa jitihada zako. Tunashukuru sana Boni na MM pamoja na wananchi wote online kwa kujitoa pia kwa hali na mali katika swala hili @ExMayorUbungo @IAMartin_ Sote tuungane kulinda uhai wa mmoja wetu unapokuwa ´mashakani. @THRDCOALITION
Chief Suleimān M. M. Baitani retweeted
A blind person. Very eloquent. Great messages. Perfect English. Very calm. A uniting force. A good leader. Compare with other African representatives. Comment if you must.
Chief Suleimān M. M. Baitani retweeted
**THRDC Yashiriki Katika Uzinduzi wa Ripoti Muhimu Kupinga Ukatili kwa Watoto Viziwi Dar es Salaam**
Dar es Salaam, 30 Juni 2024 – Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umeonyesha dhamira yake thabiti ya kulinda haki za watoto wenye ulemavu kwa kushiriki kikamilifu katika uzinduzi wa ripoti muhimu inayoangazia ukatili dhidi ya watoto viziwi. Uzinduzi huu, uliofanyika tarehe 29 Juni 2024 katika ukumbi wa Lion Hotel, uliandaliwa na Furaha ya Wanawake Wajasiriamali kwa Viziwi Tanzania (FUWAVITA).
Ripoti hii inatoa mwanga juu ya hali halisi ya ukatili unaowakabili watoto viziwi nchini Tanzania na inatoa mapendekezo muhimu kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kupunguza na hatimaye kumaliza kabisa ukatili huu. THRDC, kupitia mwakilishi wake kutoka dawati la watetezi wenye ulemavu, Bw. Emmanuel Majeshi, alitoa pongezi kwa FUWAVITA kwa kazi yao kubwa katika kuandaa ripoti hii, ambayo inaashiria hatua muhimu katika kulinda haki na ustawi wa watoto viziwi nchini.
Mbali na kushiriki katika uzinduzi, THRDC pia iliwasilisha salamu za Mratibu wa Taifa wa Mtandao, ikisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya mashirika mbalimbali katika kulinda haki za watoto wenye ulemavu. Ripoti hii inatarajiwa kuwa nyenzo muhimu kwa serikali, Asasi za Kiraia, na wadau wengine katika kuunda mikakati madhubuti ya kukabiliana na ukatili dhidi ya watoto viziwi.




































