Pinned Tweet
Mithali 9:11
Maana, kwa msaada wangu siku zako zitazidishwa; Na miaka ya maisha yako itaongezwa. Amina 🙏
Happy Birthday 🎂 To Me 🙏
Necto Kitiga retweeted
TANGAZO: IBADA YA KUMBUKUMBU
Habari Wanajumuiya!
TCA inaandaa Ibada ya Kumbukumbu Jumamosi, 31 Oktoba 2026, kuwakumbuka na kuwaenzi ndugu waliopoteza maisha 29–30 Oktoba 2025 nchini Tanzania.
📍 TUMAINI SWAHILI CHAPEL
6740 W. North Avenue, Chicago, IL 60707
📅 31 Oktoba 2026 | Muda: 3:00 PM – 7:00 PM
Mnakaribishwa kushiriki. Tushirikiane kuwakumbuka wapendwa wetu.
Ahsanteni. Mungu awabariki.
Necto Kitiga retweeted
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kimewasilisha barua rasmi kwa Rais wa Kenya, William Ruto ya kumuomba kuingilia kati suala la madai ya kutekwa kwa Mwanaharakati Twaha Mwaipaya.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, leo Oktoba 27, 2026 Jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika
amesema barua hiyo imewasilishwa leo katika Ofisi za Ubalozi wa Kenya Nchini Tanzania, ikiwa na kichwa cha habari kinachosomeka “Urgently Appeal for Your Personal Intervention in the Abduction of Twaha Mwaipaya and Protection of Democratic Activists in East Africa.”
Kupitia barua hiyo, CHADEMA imemuomba Rais Ruto kutumia nafasi yake kuingilia kati suala hilo, huku kikisisitiza umuhimu wa kulinda usalama wa Wanaharakati wa Demokrasia katika Ukanda wa Afrika Mashariki.
#MillardAyoUPDATES
Necto Kitiga retweeted
Asasi za kiraia nchini Kenya zimeungana kupaza sauti kuhusu tukio la kutekwa Twaha Mwaipaya wakati huo Asasi za kiraia nchini Tanzania zimejikausha kimya as if hakuna kilichotokea.
Wanaogopa kumkwaza Nduli Idd Amin Mama, eniwei acha tuendelee kumpazia sauti ndugu yetu #TwahaMwaipaya
Necto Kitiga retweeted
Pumbavu nyie chawa wa ccm. Mmeniweka kwenye list ya wanaotakiwa kutekwa mnadhani nitaogopa niache kutetea haki?
Kwa sasa nipo nabeba box hapa Carmel, Indiana kwenye county ya Hamilton. Njooni mniteke mbwa nyie
📌SITISHIKI NA SITANYAMAZA KAMWE MPAKA UONEVU UISHE TANZANIA 🇹🇿 📌
Necto Kitiga retweeted
#BREAKING: LISSU ASITISHA MGOMO WA KULA BAADA YA KUKUTANA NA NDUGU YAKE NDANI YA GEREZA
Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesitisha mgomo wa kula aliouanza Jumanne baada ya kuruhusiwa kukutana faraghani na mdogo wake, wakili wake mkuu Rugemeleza Nshala amethibitisha.
Awali, taarifa zilizotolewa Jumamosi zilieleza kuwa Lissu alikusudia kuanza mgomo huo Jumatatu akipinga vizuizi vya mashauriano ya siri na mawakili wake.
Hata hivyo, aliahirisha hatua hiyo baada ya kuahidiwa kupata fursa ya kukutana nao. Baada ya ahadi hiyo kutotekelezwa, Lissu alianza kugoma kula Jumanne asubuhi.
Akizungumza na shirika la habari la The Associated Press, Nshala alisema tayari Lissu alikuwa amekataa , kifungua kinywa na chakula cha mchana kabla ya kuhitimisha mgomo huo baada ya mkutano wa kifamilia.
Lissu, ambaye alinusurika jaribio la mauaji mwaka 2017 kwa kupigwa risasi mara 16 na baadaye kuishi uhamishoni kutokana na vitisho vya usalama, anakabiliwa na kesi ya uhaini inayoweza kumpelekea hukumu ya kifo.
Amekuwa mahabusu kwa zaidi ya miezi 18, huku hukumu ya mwisho ikitarajiwa kutolewa Novemba 6.
Necto Kitiga retweeted
WHERE IS TWAHA MWAIPAYA?
MEDIA INVITE: FILING OF HABEAS CORPUS WRIT APPLICATION FOR THE PRODUCTION OF TWAHA MWAIPAYA.
Twaha Mwaipaya is a human rights defender,youth organizer and political activist who has spent years mobilizing for democracy, justice, human rights, civic freedoms and accountability in Tanzania.
He has been a prominent youth leader within Tanzania's main opposition party, CHADEMA, serving as national mobilization coordinator of it's youth wing.
Twaha was abducted in Kenya on Sunday afternoon and his whereabouts are yet to be known.
We are calling upon Human Rights Defenders,Active Citizens and Civic Voices to join us for a press briefing tomorrow Wednesday at the Milimani Law Courts, Nairobi.
#FreeTwahaMwaipaya #EndAbductionsEA #PASNet
Necto Kitiga retweeted
Muda wa Maridhiano ulishapita, Huu ni Muda wa uwajibikaji.
#FreeTwahaMwaipaya
Necto Kitiga retweeted
#BREAKING: CHADEMA WAVUMBISHA KENYA! RUTO KIKAANGONI KUFUATIA UTEKAJI WA MWANAHARAKATI MWAIPAYA
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, amesema barua hiyo imewasilishwa leo katika Ubalozi wa Kenya nchini Tanzania ili imfikie Rais Ruto haraka, ikiwa ni hatua nyingine ya chama hicho kufuatilia suala la kutoweka kwa Mwaipaya.
ZAIDI: youtu.be/t_w6DqjSbuc
Necto Kitiga retweeted
Chama cha Wanasheria Uganda (ULS) kimesema ni aibu kwa eneo la Afrika Mashariki kuona watu wanaotetea maslahi ya umma wakilazimika kuchagua kati ya kutoa maoni yao na kubaki salama katika nchi zao, kikionya kuhusu kuongezeka kwa vitendo vya ukandamizaji vinavyovuka mipaka ya nchi.
Katika taarifa iliyotolewa Kampala, Uganda, Oktoba 26, 2026, na kusainiwa na Makamu wa Rais wa ULS, Asiimwe Anthony, chama hicho kimelaani taarifa za kutekwa kwa Twaha Mwaipaya, mwanaharakati wa upinzani kutoka Tanzania, ambaye aliripotiwa kuchukuliwa na watu wasiojulikana Oktoba 25, mwaka huu, katika eneo la Kamulu, Kaunti ya Machakos nchini Kenya.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mwaipaya alitekwa majira ya saa nane mchana akiwa safarini kwa teksi kwenda kuwatembelea marafiki zake, huku mahali alipo pakibaki hapajulikani hadi wakati taarifa hiyo inatolewa.
ULS imesema matukio ya watu kutoweshwa kwa nguvu, kutekwa, kukamatwa kiholela na kutishwa kwa watu wenye misimamo tofauti yamewalazimu wanaharakati wa kisiasa, waandishi wa habari, wanasheria, majaji na watetezi wa haki za binadamu kukimbilia uhamishoni ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), lakini hata baadhi ya nchi wanazokimbilia zimeendelea kuwa na changamoto za usalama.
Chama hicho kimetolea mfano wa Robert Kabera, aliyekuwa mwanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Rwanda na aliyekimbilia Uganda mwaka 2020, ambaye kwa mujibu wa taarifa hiyo, alikutwa amekatwa kichwa katika Wilaya ya Mpigi nchini Uganda, Oktoba 17, 2026. ULS imesema Serikali ya Uganda bado haijatoa maelezo kuhusu kifo hicho.
Kuhusu Mwaipaya, ULS imesema iwapo Serikali ya Tanzania ina tuhuma za jinai dhidi yake, inapaswa kufuata utaratibu rasmi wa kisheria wa kumrejesha nchini kupitia mchakato wa extradition, huku ikihakikisha anapata haki ya kusikilizwa kwa mujibu wa sheria za Kenya.
Chama hicho kimesisitiza kuwa hakuna tuhuma za jinai zinazoweza kuhalalisha kukwepa sheria na kumnyima mtu ulinzi wa mahakama, kikitaja pia suala la Dkt. Kizza Besigye na msaidizi wake, Obeid Lutale, kuwa jeraha ambalo bado halijapona katika eneo hilo.
Aidha, ULS imezitaka Mahakama ya Afrika Mashariki na mahakama za nchi wanachama wa EAC kuzungumzia ukiukwaji huo, huku ikiwataka wakuu wa mahakama kutoa kauli za wazi na kuhakikisha serikali zinawajibika kwa kukomesha ukandamizaji unaovuka mipaka. Pia, imezitaka viongozi wa Umoja wa Afrika (AU), Umoja wa Mataifa (UN) na wakuu wa balozi za nchi mbalimbali kuacha ukimya kuhusu suala hilo, ikihitimisha kwa wito wa kupinga uvunjaji wa sheria na kumwachia huru Twaha Mwaipaya.
Necto Kitiga retweeted
DAR: Akizungumza na Waandishi wa Habari, leo Oktoba 27, 2026, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika amesema Kamati kuu ya Chama hicho inaendelea kusisitiza Uchunguzi huru wa Mauaji yaliyotokea Oktoba 29, 2025 na siku zilizofuata.
Zaidi jamii.app/MnyikaOktoba29
#JamiiForums #Demokrasia #Uwajibikaji
Necto Kitiga retweeted
Tundu Lissu on hunger strike:
Tanzania opposition leader Tundu Lissu on hunger strike
Lissu demands access to his legal team
Chadema party leader is facing treason charges
#CitizenBriefs
VIDEO:
Kufuatia taarifa za kutekwa kwa Mwanaharakati na Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 Twaha Mwaipaya, chama hicho kimesema kimeandila barua rasmi kwenda kwa Rais wa Kenya William Ruto kumtaka kuingilia kati sakata hilo.
Hayo ameyaeleza Katibu wa chama hicho John Mnyika akizungumza na waandishi wa hanari leo Oktoba 27, 2026 akieleza kuwa tayari barua hiyo imeshafikishwa Ubalozi wa Kenya uliopo hapa nchini.
Necto Kitiga retweeted
Kama hukushauri mazungumzo kabla ya mauaji ya oktoba 29,2025 na siku zilizofuata, kaa kimya kama ulivyokalia kimya mauaji, utekaji, wizi wa kura nk.
it's better watch your back. Hali ni mbaaaayaaaaaaa!!
#FreeCollethaNtidyicha #FreeTwahaMwaipaya
Kama hukushauri mazungumzo kabla ya mauaji ya oktoba 29,2025 na siku zilizofuata, kaa kimya kama ulivyokalia kimya mauaji, utekaji, wizi wa kura nk.
it's better watch your back. Hali ni mbaaaayaaaaaaa!!
#FreeCollethaNtidyicha #FreeTwahaMwaipaya
Necto Kitiga retweeted
#KENYA: UPINZANI KENYA WALAANI UTEKWAJI WA MWANAHARAKATI MWAIPAYA
Vuguvugu la Linda Mwananchi limetoa taarifa kali kulaani utekwaji wa mwanaharakati wa upinzani kutoka Tanzania, Twaha Mwaipaya, katika eneo la Kamulu, Kaunti ya Machakos, likionya kuwa Kenya inageuzwa kuwa uwanja wa kukandamiza sauti za upinzani katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa ripoti za Amnesty International, Mwaipaya alitekwa akiwa ndani ya teksi na watu waliokuwa wakitumia magari matatu. Hadi sasa hajulikani alipo.
Linda Mwananchi imetaka mamlaka za Kenya zitoe mara moja taarifa kuhusu alipo, kuhakikisha usalama wake na kuzuia kuondolewa kwa nguvu kutoka nchini.
Taarifa hiyo imeunganisha tukio hili na mfululizo wa utekaji wa mipakani, ikikumbusha kisa cha kiongozi wa upinzani wa Uganda Dkt. Kizza Besigye aliyechukuliwa Nairobi Novemba 2024 na kupelekwa Uganda, pamoja na utekwaji wa mwanaharakati wa Tanzania Maria Sarungi Tsehai Januari 2025.
Linda Mwananchi imeshutumu serikali ya Rais William Ruto kwa kushindwa kulinda taswira ya Kenya kama kimbilio la wakimbizi wa kisiasa, ikionya kuwa taifa linaweza kuonekana kushirikiana na utawala kandamizi wa kikanda.
Vuguvugu hilo limeitaka kufanyike uchunguzi huru na kuwawajibisha wote waliohusika, likiahidi kuendelea kusimama kidete kulinda demokrasia, haki za binadamu na utawala wa sheria katika ukanda huu.
























