Paul Bonaventure (@Phbhimself) header
Paul Bonaventure (@Phbhimself) profile picture

|| PEACE MAKER ✌🏿 || Author | A human. Being. | Meditation & Energy-Based Teacher 🧘‍♀️| HipHop🎶 |

Somewhere in Africa
Joined January 2015
Watu wengi wamekuwa wakijifunza meditation tangu karne na karne, miaka na miaka. Sio kitendo kilichoanza hivi sasa bali ni kitendo kilichoanza tangu zamani na kimekuwa na faida mbalimbali kwa watu waliojifunza na kufanya taamuli. Wengine ni kutokana na kupunguza stress, kujifunza kuongoza akili zao, kuachana na mazoea wanayoshindwa kuyaacha na kutokana na kuongeza hekima ya kiimani. Ningependa kuelezea faida chache nzuri ambazo zinapatikana pale mtu anapofanya taamuli vyema na kwa mara kwa mara. • Taamuli (Meditation) inasaidia kutengeneza furaha ya ndani. Tunaposema furaha ya ndani tunamaanisha nini? Ni furaha unayotembea nayo wakati wote. Ni furaha isiyotegemea maisha yako yapoje, ni furaha isiyotegemea una vitu gani bali ni furaha inayopatikana ndani mwako. Wengi hupata furaha kutokana na hali na vitu, na kipindi cha wakati mgumu wao hukosa furaha kwani furaha yao inategemea vitu vya nje ambavyo havidumu milele. Lakini katika meditation unajifunza kuachana na kujishikilia na mawazo, fikra, hisia, na milango ya ufahamu. Unajifunza kuingia ndani na kutafuta kisicho na mwanzo wala mwisho. Ambacho wakati wowote upo nacho, nacho kinakuunganisha source/chanzo na ufahamu mkuu wa Ulimwengu ambao wakati wote mpo pamoja.
9
18
156
52,553
KUTOKA UHAINI HADI UCHOCHEZI Kesi ya Tundu Lissu imehitimishwa kwa matokeo yenye sura mbili tofauti. Mahakama Kuu haikuridhika kuwa upande wa mashtaka umethibitisha kosa la uhaini chini ya kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu. Lakini ikamtia hatiani kwa kosa la uchochezi chini ya kifungu cha 390 cha sheria hiyo hiyo, kwa kutumia mamlaka ya kifungu cha 319 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai. Ili kuelewa uzito wa uamuzi huu, ni lazima kutenganisha makosa hayo mawili kisheria. Makosa hayo hayana viambato vinavyofanana kikamilifu, hayalindi maslahi ya kisheria kwa kiwango kilekile, na hayahitaji kuthibitishwa kwa namna moja. Kifungu cha 39(2)(d) cha Penal Code kinahusu mtu aliye chini ya utii wa Jamhuri ya Muungano ambaye anatengeneza nia ya kutekeleza au kuchochea, kushawishi, Kushauri au kuelekeza mtu au kundi la watu kutekeleza kitendo chenye lengo la kuitisha Executive, Legislature au Judiciary ya Jamhuri ya Muungano. Sheria inahitaji pia nia hiyo ionyeshwe kwa maandishi yaliyochapishwa au kwa kitendo cha wazi yaani overt act or deed na adhabu iliyowekwa ni kifo. Hapa kuna mambo muhimu ya kuthibitishwa, kwamba mashtaka yalipaswa kuonyesha kuwa Lissu alikuwa chini ya utii wa Jamhuri ya Muungano, alitengeneza nia mahsusi inayotakiwa na kifungu hicho. Nia hiyo ilihusiana na kitendo cha kuitisha chombo kinachotajwa na sheria, na aliidhihirisha kwa namna inayotakiwa kisheria. Katika hukumu ya leo, mahakama haikubishia suala la uraia na utii wa Lissu kwa Jamhuri. Msingi wa kuanguka kwa shtaka la uhaini ulikuwa katika kipengele cha nia. Mahakama iliona kuwa tafsiri za mashahidi kuhusu hotuba yake hazikutosha kuthibitisha nia mahsusi ya kuitisha Serikali. Ilitofautisha pia shinikizo la kisiasa la kutaka mageuzi na kitendo cha kuitisha mihimili ya dola. Hii ni tofauti muhimu sana kwamba kiongozi wa kisiasa anaweza kutumia lugha kali, kutaka wananchi washiriki maandamano, kususia uchaguzi au kushinikiza Serikali kubadili sera. Hayo hayawi moja kwa moja uhaini, ili yafikie kiwango cha kifungu cha 39(2)(d), lazima kuthibitishwe nia maalumu ya kuitisha chombo kinachotajwa na sheria, pamoja na namna nia hiyo ilivyoonyeshwa. Naweza kusema mahakama iliposema kipengele cha nia hakijathibitishwa, ilikataa kiini cha tuhuma ya uhaini. Hili halimaanishi kwamba mahakama ilisema kila neno lililotamkwa lilikuwa halina athari yoyote ya kisheria, lakini ilimaanisha kuwa ushahidi haukufikia kiwango cha kuthibitisha kosa hilo mahsusi. Tukiangalia kifungu cha 390 cha Penal Code kinaeleza kuwa mtu anayemshawishi au kumchochea mwingine kutenda kosa yaani, solicits or incites another to commit an offence anatenda kosa la uchochezi, hata kama ushawishi au uchochezi huo haukuzaa matokeo. Tofauti yake na uhaini ni kubwa sana, Kifungu cha 390 hakihitaji kuthibitisha kwamba mtuhumiwa alikusudia kuitisha Serikali, Bunge au Mahakama. Kinahitaji kuthibitisha kuwa alichochea mtu mwingine kutenda kosa. Lakini kuna jambo ambalo halipaswi kupuuzwa, sheria haisemi kwamba kila hotuba kali, kauli ya kisiasa au wito wa kutokushirikiana na Serikali ni uchochezi. Lazima kuwe na kitendo cha kumshawishi au kumchochea mtu mwingine kutenda kosa linalotambulika kisheria. Hili ni muhimu kwa sababu kifungu cha 390 kinatumia maneno commit an offence, na mahakama inapohukumu mtu kwa uchochezi, Inapaswa kubainisha ni kosa gani alilokuwa akimchochea mwingine kulitenda na ushahidi unaothibitisha uhusiano huo. Ni kweli kwamba kifungu cha 390 kinasema uchochezi unaweza kuwa kosa hata kama haukuzaa matokeo. Kwa hiyo mashtaka hayalazimiki kuthibitisha kwamba mtu aliyechochewa alifanikiwa kutenda kosa hilo. Lakini kutokuhitajika kwa matokeo hakufuti wajibu wa kuthibitisha kitendo cha uchochezi na nia inayohitajika kisheria.
2
12
53
3,765
Tukiangalie kifungu cha 319 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya Jinai. Hapa ndipo uamuzi wa mahakama unakuwa na mjadala mkubwa zaidi wa kisheria. Kifungu cha 319(1) kinaruhusu mahakama kumtia mtu hatiani kwa kosa dogo yaani minor offence pale ambapo shtaka lina viambato kadhaa, Baadhi yake vikithibitishwa vinaunda kosa jingine kamili, lakini viambato vingine havijathibitishwa. Kifungu cha 319(2) pia kinaruhusu hukumu ya kosa dogo pale ambapo ukweli uliothibitishwa unapunguza kosa aliloshtakiwa nalo na kulifanya kuwa kosa dogo. Kifungu hiki kinazuia hali ambayo mtu anaweza kuachiliwa kabisa wakati ushahidi umeonyesha kosa jingine dogo lililomo ndani ya kosa kubwa aliloshtakiwa nalo. Lakini mamlaka hayo hayapaswi kutafsiriwa kuwa ruhusa ya mahakama kubuni shtaka jipya lisilokuwa na uhusiano wa kisheria na lile la awali. Jambo la kujiuliza hapa ni kama uchochezi chini ya kifungu cha 390 ulikuwa kosa dogo lililomo ndani ya uhaini uliokuwa ukijadiliwa, Au ulikuwa kosa tofauti lenye viambato vyake ambavyo havikuwasilishwa kama shtaka mahsusi. Mahakama ilichukua msimamo kuwa uchochezi ulikuwa kosa linalohusiana kwa karibu yaani cognate offence na tuhuma ya uhaini, Kwa sababu kesi nzima ilihusu madai kwamba Lissu alichochea umma kuzuia uchaguzi. Iliona kuwa ushahidi uliowasilishwa na pande zote ulihusu pia suala la uchochezi, hivyo Lissu alikuwa na taarifa na nafasi ya kujibu hoja hizo. Lakini katika rufaa, hoja itakayohitaji kuchunguzwa kwa kina ni kama uhusiano wa kihistoria au wa kimatukio kati ya makosa hayo unatosha kuyafanya uchochezi kuwa kosa dogo ndani ya uhaini kwa maana ya kifungu cha 319. Kuwa makosa mawili yametokana na hotuba ileile hakumaanishi moja kwa moja kwamba kosa moja ni sehemu ya jingine. Lazima kuwe na uhusiano wa kisheria katika viambato vya makosa hayo, na siokufanana kwa mazingira pekee. Lissu amesisitiza kuwa hakushtakiwa kwa uchochezi na hakupewa nafasi ya kujitetea dhidi ya kosa hilo. Mahakama imejibu kuwa madai ya uchochezi yalikuwa sehemu ya ushahidi na hoja zilizojadiliwa wakati wa kesi. Hapa kuna tofauti kati ya notice of facts na notice of the legal charge, kwamba mshtakiwa anaweza kujua maneno yanayodaiwa kuyatamka, kujua mashahidi waliowasilisha ushahidi na hata kujibu tafsiri ya maneno hayo. Lakini bado kuna swali kama alipewa taarifa ya kutosha kwamba anatakiwa kujibu viambato vyote vya kosa la uchochezi chini ya kifungu cha 390. Kwa mfano, utetezi dhidi ya uhaini unaweza kujikita katika kukataa nia ya kuitisha Serikali. Utetezi dhidi ya uchochezi unaweza kuhitaji kupinga kosa mahsusi ambalo mtuhumiwa anadaiwa kuwahamasisha wengine kulifanya, aina ya ushawishi uliotolewa, na nia ya kusababisha mtu mwingine alitende. Hivyo haki ya kujitetea haipimwi kwa kuangalia kama mshtakiwa alizungumza mahakamani au aliulizwa maswali kuhusu hotuba yake pekee. Inapaswa kuangaliwa kama alipewa nafasi ya kujibu hoja zote muhimu za kisheria na kiushahidi zinazounda kosa ambalo hatimaye limetumika kumtia hatiani. Hii ndio sababu kifungu cha 319 lazima kisomwe pamoja na haki ya kusikilizwa kwa haki. Mamlaka ya kutoa hukumu ya kosa dogo haiwezi kuondoa wajibu wa kuheshimu haki ya mshtakiwa kujua na kujibu tuhuma zinazoweza kuamua hatima yake. Mahakama ilirejea mashahidi walioeleza kuwa maneno ya Lissu yaliwaathiri na kwamba baadhi yao walijiunga na watu waliokuwa na nia ya kuvuruga uchaguzi. Ushahidi huo unaweza kuwa muhimu katika kuthibitisha kwamba maneno yalifikishwa kwa watu na yalikuwa na athari kwa baadhi ya wasikilizaji. Lakini kuna tofauti kati ya nia ya mzungumzaji na tafsiri au hatua zilizochukuliwa na msikilizaji. Mtu anaweza kusikiliza hotuba na kuamua kufanya jambo ambalo mzungumzaji hakulikusudia. Pia, mtu anaweza kuelewa ujumbe kwa namna tofauti na mazingira yaliyo kusudiwa na mtoa hotuba. Naweza kusema, ushahidi kwamba baadhi ya watu waliathiriwa na maneno hauondoi wajibu wa mahakama kuchunguza kama Lissu mwenyewe alikusudia kuwachochea kutenda kosa.
1
2
8
449
Kifungu cha 390 hakihitaji uchochezi uwe na matokeo, lakini kinahitaji kuthibitishwa kuwa uchochezi ulitokea. Hivyo mahakama ilipaswa kutofautisha kati ya kusikilizwa kwa hotuba, kushawishika kwa wasikilizaji, na kuthibitishwa kwa nia ya kumshawishi mtu kutenda kosa. Pia, katika hukumu ya uhaini mahakama iliona kuwa ushahidi haukuthibitisha nia ya kuitisha Serikali. Katika hukumu ya uchochezi, iliona kuwa ushahidi huohuo, ukitazamwa chini ya kosa tofauti, ulitosha kuthibitisha uchochezi. Hilo linawezekana kisheria ikiwa viambato vya kosa la pili vimejitegemea na vimethibitishwa. Lakini mahakama lazima ionyeshe kwa uwazi ni ushahidi gani unathibitisha kila kiambato cha kosa hilo. Kwa kuwa kifungu cha 390 hakijaweka adhabu mahsusi, mahakama ilitumia kifungu cha 35 cha Penal Code. Kifungu hicho kinaruhusu kifungo kisichozidi miaka mitano, faini au vyote viwili. Lissu aliomba mahakama izingatie faini, kutokuwa na hukumu za awali, hali yake ya afya na muda aliokaa gerezani. Mahakama ilikiri kuwa pale sheria inapoweka faini na kifungo, faini inaweza kuwa chaguo la kwanza kuzingatiwa. Lakini, iliamua kutoa kifungo cha miaka minne, ikirejea pia wajibu wa kulinda haki za watu wengine chini ya Ibara ya 30(1) ya Katiba. Hoja ya kisheria hapa ni kama sababu zilizotolewa zinaeleza vya kutosha kwa nini faini haikutosha na kwa nini kifungo cha miaka minne kilikuwa adhabu inayolingana na kosa, mazingira yake na hali binafsi ya mshtakiwa. Kifungu cha 35 chenyewe kinaweka njia tatu za adhabu, lakini hakitaji ndani ya maneno yake kwamba faini lazima itolewe katika kila kesi kabla ya kifungo. Lakini, pale mahakama inaposema faini ni chaguo la kwanza kuzingatiwa, inapaswa kueleza kwa nini iliona kuwa haitoshi katika mazingira ya kesi husika. Kisheria, Lissu hajaachiwa bila hatia katika kesi nzima. Ameondolewa kwenye hatia ya uhaini, lakini amehukumiwa kwa uchochezi. Matokeo haya hayawezi kuitwa ushindi kamili wa upande mmoja wala ushindi kamili wa upande mwingine bila kuchambua misingi ya kila uamuzi. Kilicho wazi ni kwamba mahakama haikuthibitisha kosa kubwa lililokuwa msingi wa shtaka la awali, lakini ilitumia kifungu cha 319 kuamua kuwa ushahidi unatosha kwa kosa jingine. Mabadiliko hayo yanaibua maswali mazito kuhusu maana ya kosa dogo, uhusiano wa viambato vya makosa mawili, taarifa ya kisheria aliyopewa mshtakiwa na haki yake ya kujitetea. Katika rufaa, Mahakama ya Rufani inaweza kuhitajika kuchunguza kama kifungu cha 319 kilitumika ndani ya mipaka yake. Kama uchochezi chini ya kifungu cha 390 ulikuwa kweli kosa dogo lililomo ndani ya uhaini ulioshtakiwa. Kama kosa mahsusi ambalo Lissu alidaiwa kuchochea lilitambuliwa na kuthibitishwa, na kama utaratibu uliotumika uliheshimu haki ya kusikilizwa kwa haki. Kwa kifupi, suala kubwa la kisheria katika kesi hii sio kwamba mahakama imebadilisha jina la kosa kutoka uhaini kwenda uchochezi. Ila ni kama ilikuwa na mamlaka ya kufanya mabadiliko hayo kwa mazingira na ushahidi uliokuwepo, na kama ilifanya hivyo bila kuathiri haki za msingi za mshtakiwa. Hapo ndipo msingi wa mjadala wa rufaa ulipo BYE
3
11
312
Hili ni swali muhimu, lakini kuna tofauti kati ya kuwa na kesi mbili zinazohusu tuhuma zinazofanana na kutoa hukumu katika kesi moja wakati nyingine bado inaendelea. Kwa kanuni za jumla za mwenendo wa jinai, Jamhuri inaweza kuendesha kesi mbili tofauti dhidi ya mshtakiwa mmoja ikiwa kila kesi ina shtaka na msingi wake wa kisheria. Kuwepo kwa kesi nyingine inayoendelea hakuzuii moja kwa moja mahakama kutoa hukumu katika kesi iliyofikia hatua ya mwisho. Lakini hairuhusiwi kutumia kesi mbili kumwadhibu mtu mara mbili kwa kosa lilelile kinyume cha sheria, au kukiuka haki yake ya kusikilizwa na kujitetea. Lakini katika kesi ya Lissu kuna jambo la msingi la kulisahihisha, kesi nyingine iliyofunguliwa pamoja na kesi ya uhaini haikuwa kesi ya uchochezi. Taarifa zilizoripotiwa wakati wa kufunguliwa kwa mashauri zinaonyesha kuwa alikabiliwa na kesi ya uhaini na mashitaka matatu ya kuchapisha taarifa za uongo chini ya kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao. Hayo yalikuwa mashauri tofauti. Kilichotokea leo ni tofauti, Mahakama Kuu haikutoa hukumu katika kesi nyingine ya uchochezi iliyokuwa ikiendelea, ila ilimwachia Lissu huru kwenye shtaka la uhaini. Lakini ikatumia kifungu cha 319 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kumtia hatiani kwa kosa dogo linalohusiana na shtaka hilo, yaani uchochezi chini ya kifungu cha 390 cha Kanuni ya Adhabu. Kwa hiyo naweza kusema sio suala la Jamhuri kutoa hukumu kwenye kesi ya uhaini wakati kesi ya uchochezi inaendelea. Ila ni suala la Mahakama kubadilisha kosa ndani ya shauri la uhaini na kutoa hukumu ya kosa jingine ambalo haikuwa sehemu ya shtaka la awali. Hapo ndipo hoja nzito ya kisheria ilipo, kwamba, kosa la uchochezi lilikuwa kosa dogo linalohusiana vya kutosha na shtaka la uhaini kiasi cha kuruhusu matumizi ya kifungu cha 319? Na je, Lissu alipata nafasi ya kutosha kujitetea dhidi ya kosa hilo? Hizi ni hoja zinazoweza kupingwa kwenye rufaa.
Replying to @Phbhimself
Ndugu Paul naomba unifafanulie hili ,Lissu ana kesi ya uchochezi na ilifunguliwa pamoja na hii,je ni sawa jamihuri kutoa hukumu kwenye kesi ya uhaini wakati ya uchochezi inaendelea ???
6
11
33
5,342
Paul Bonaventure retweeted
To my learned brothers, how fast can he file his appeal, kesi ianze kusikilizwa ili apewe dhamana? @TitoMagoti @omari_manyama @Phbhimself – at Dar es Salaam, Tanzania
1
3
1
39
3,409
Katika uamuzi wa adhabu, Jaji Ndunguru amesema mahakama imezingatia hoja za pande zote, ikiwemo ombi la dhamana ili kukata rufaa, hali ya afya ya mshtakiwa na ukweli kwamba hana hukumu ya awali. Mahakama imeeleza kuwa kifungu cha 390 hakijaweka adhabu yake mahsusi, hivyo kifungu cha 35 cha Kanuni ya Adhabu kinatumika. Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa mahakamani, adhabu inayohusika ni kifungo kisichozidi miaka mitano, faini au vyote kwa pamoja. Mahakama imetambua kuwa pale ambapo sheria inaruhusu faini au kifungo, faini inaweza kuwa chaguo la kwanza. Lakini, baada ya kuzingatia maamuzi mbalimbali na hoja zilizowasilishwa, imeamua kumhukumu Lissu kifungo cha miaka minne jela. Jambo muhimu la kisheria linalobaki ni sababu mahsusi zilizofanya mahakama ichague kifungo cha miaka minne badala ya faini au adhabu nyepesi zaidi, hasa baada ya kutambua kutokuwepo kwa hukumu za awali na hoja za afya. Hapa ndipo suala la uwiano wa adhabu yaani proportionality of sentence, linapopata uzito. Pia niwa dokeze kidogo, haki ya kukata rufaa aliyoitambua mahakama ni muhimu. Katika rufaa, hoja ya msingi haitakuwa kama ushahidi ulitosha kuthibitisha uchochezi pekee, Bali pia kama mahakama ilikuwa na msingi halali wa kubadilisha shtaka na kumhukumu kwa kosa ambalo halikuwa katika hati ya mashtaka, na kama Lissu alipata nafasi ya maana ya kujitetea dhidi ya kosa hilo. ALUTA CONTINUA ✌🏾
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 502 Mhe. Lissu anaendelea Anasema uamuzi huu wa kunikuta na hatia na kosa ambalo sikushtakiwa nalo, sikujitetea ni kosa la kutengeneza, effect yake ni kwamba unatoa kinga ya kisiasa kwa wale ambao walihusika mauaji amkubwa ya kisiasa, watatoka na kusema wauaji walishapataikana. Serikali ya Samia imeua watu wengi zaidi ukiachilia historia ya vita vya majimaji, hawa mass murderers watashangilia sana na uamuzi huu kwasababu mmewapa sababu ya kusema aliyesababisha mauaji ya Oktoba 2025 amepatikana na hatia lakini hii haitafunika ukweli. Serikali ya Mwalimu Nyerere iliuwa watu 37 mwaka 1977 na iliwajibika, Peter Kisumo alikuwa Mkuu wa Mkoa w Shinyanga alijiuzulu, na wengine akiwemo Mwinyi. Leo watu 518 walioripotiwa kwa uchache hakuna aliyewajibishwa, uamuzi wenu hautaficha hiyo kashfa. Kwenye sentences guidelines za Mahakama hii, inasema lazima adhabu ya faini itolewe isipokuwa kama ni grave offence, kosa nililoshtakiwa nalo sio grave. Waheshimiwa Majaji hukumu mnayo, ambayo mmeagizwa muitoe, itoeni nawashukuruni sana. Jaji Ndunguru anawasha mic anasema tumesikiliza hoja za pande zote na katika kutoa adhabu tumezingatia sababu kadha wa kadha. Kwanza mshtakiwa umeomba dhamana ili ukate rufaa, tumeangalia hoja ya ugonjwa na kuwa wewe ni mkosaji wa kwanza, hoja ya adhabu ya faini au kifungo. Kifungu cha 390 hakijatoa adhabu na ukisoma kanuni ya adhabu kifungu cha 35 kinahusika pale ambapo hakuna adhabu. Adhabu ni kifungo kisichozidi miaka 5 au fani au vyote viwili na hakijaelekeza faini ni kiasi gani. Tunajua kuwa pale ambapo fani na kifungo vinakuwa vinatolewa first option ni faini. Tumesoma na maamuzi mbalimbali na mengine ambayo tumeshayasema mfano kuzuia uchaguzi ni kukiuka katiba, ukisoma Ibara ya 30(1) imeeleza kuwa hutakiwa kuingilia haki za mtu mwingine. Mahakama inatoa adhabu kwa mshitakiwa kutumikia kifungo cha muda wa miaka 4 na una haki ya kukata rufaa. Majaji wanatoka. Naomba Repost yako.
1
17
1
63
5,826
TAL amehoji kama taarifa ya Tume ya Jaji Chande iliwasilishwa kama ushahidi katika shauri hili na kama kuna ushahidi unaothibitisha kuwa kauli zake ndizo zilizosababisha vurugu hizo. Hapa kuna hoja muhimu ya causal nexus, kwamba Jamhuri ikitaka kutumia madhara hayo kuongeza adhabu, lazima ionyeshe uhusiano wa ushahidi kati ya kauli za Lissu na matukio yanayotajwa. Madai ya jumla kuhusu hali ya nchi hayawezi kuchukua nafasi ya uthibitisho wa wajibu binafsi. Lissu pia amefafanua kuwa hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai, licha ya kukabiliwa na mashauri kwa zaidi ya miaka 24. Hili ni jambo muhimu katika hatua ya adhabu. Yaani ni lazima Mahakama itofautishe kati ya mtu aliyewahi kushtakiwa na mtu aliyewahi kupatikana na hatia. Kwa maana mashitaka ya zamani yasiyoishia kwenye hukumu ya hatia hayawezi kuhesabiwa kama previous convictions. Hoja nyingine imehusu msiba wa Mzee Alutte, mtu ambaye Lissu amesema alimlea na kumwezesha kuwa mwanasheria, ameeleza kuwa alitarajia kupata nafasi ya kwenda kumzika. Hali hii ni sehemu ya mazingira ya kifamilia ambayo Mahakama inaweza kuyazingatia katika mitigation, yaani kupunguza uzito wa adhabu. Lissu amekumbusha pia muda wa siku 577 aliokaa gerezani na madai ya kunyimwa haki mbalimbali, ikiwemo kuwasiliana na mawakili wake, viongozi wa CHADEMA na kupata nafasi ya kuomba Mungu. Ameirejea hukumu ya jopo la Majaji Mruma, Dkt. Longopa na Rumisha kuhusu mazingira aliyopitia akiwa gerezani. Hoja hizi zinastahili kutathminiwa kwa kuzingatia maamuzi hayo na athari zake halisi za kisheria. Kuhusu historia yake, Lissu ameeleza kuwa amewahi kuwa Mbunge, kuhudumu Jeshini na kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria. Ameziwasilisha sifa hizi kama sehemu ya historia yake ya kulitumikia taifa. Tukumbuke katika kutoa adhabu, Mahakama inaweza kuzingatia tabia na historia ya mshtakiwa, lakini lazima ifanye hivyo kwa misingi ya sheria na sio umaarufu au nafasi yake ya kisiasa. Hoja nzito zaidi ni hali yake ya afya, TAL amesema amefanyiwa operesheni 25, ana risasi moja iliyobaki mwilini, ana kisukari kwa takribani miaka sita na anahitaji ufuatiliaji wa matibabu katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven nchini Ubelgiji. Pia amesema amekosa miadi minne ya matibabu kutokana na kesi hii. Hali ya afya ni jambo muhimu katika kuamua adhabu inayofaa. Mahakama inapaswa kuzingatia mahitaji ya matibabu na ushahidi wa kitabibu, ili kuhakikisha adhabu yoyote inayotolewa haipuuzi utu na afya ya mshtakiwa. Jambo la mwisho, Lissu ameomba dhamana ili aweze kukata rufaa akiwa nje na kupata nafasi ya kwenda kumzika Mzee Alutte.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 501 Wakili wa Serikali kimsingi anasema kwamba matukio ya vurugu za Oktoba 2025 yalitokana na kauli zangu kama nimemuelewa sawa sawa. Kwenye kesi hii sina hakika kama mmeletewa ushahidi wa hotuba ya Jaji Chande wala yeye hajaja kutoa ushahidi hapa kuthibitisha hizo vurugu zilisababishwa na vurugu za wanasiasa gani. Mnaambiwa mnitolee adhabu kali kwa kosa ambalo kama lipo limefanyika kwazaidi ya miezi 6 limefanyika baadae mimi nikiwa gerezani, mkikubaliana na hoja hiyo huu utakuwa ni uthibitisho mwingine kwamba huu ni uamuzi wa maelekezo. Watu kicheko😂😂😂😂😂 Wakili wa Serikali Mkuu anataka muamini projo za mitandaoni, mkikubali utakuwa ni uthibitisho kuwa ni maagizo. Wakili wa Serikali Mkuu amewaambia vile vile kwasasa hawana taarifa zozote kama hili ni kosa langu la kwanza, maana yake anaashiria kwamba kuna previous conviction, sasa kwavile hana uhakika mimi nitawaambia ukweli, sijawahi kutiwa hatiani na kosa lolote la jinai, wamenishtaki kwa zaidi ya miaka 24 tangu 2002 hawajawahi kunipata, I have never ever been convicted for a criminal offence, kwahiyo mnapofikiria adhabu lazima mjue kwamba mnatoa adhabu kwa mtu ambaye hajawahi kupatikana na hatia. Mhe. Lissu anaendelea Waheshimiwa majaji nafaham mnajua kwamba nina msiba mkubwa sana wa mtu aliyenilea, amenifanya mimi kuwa mwanasheria, kwasabu sikupata nafasi ya kumuuguza, nilikuwa natumaini kuwa Mahakama itaniacha niende nikamzike Mzee Alutte, I was hoping that, inaelekea kuwa hiyo haipo kwenye mahesabu yenu, mnapokuwa mnafikiria adhabu mfikirie na hilo, family obligationdls is a factor kuamua adhabu, huyu mtu amefiwa, Dunia nzima inajua, magazeti everywhere, I was hoping that nitapata nafasi ya kwenda kumzika huyu aliyenilea. Waheshimiwa majaji leo ni mwaka na miezi 7 niko gerezani, mnapofikiria adhabu kali muitoe msije mkasahau kwamba huyu mtu ameshakaa gerezani kwa kosa ambalo mmelisema wenyewe kuwa sio kosa, halijathibitishwa na wala msije mkasau walichokisema jopo la Majaji watatu wenzenu: Jaji Mruma, Dkt. Longopa na Jaji Rumisha kuhusiana na niliyotendewa gerezani. Wamesema nimenyimwa fursa ya kuwasiliana na mawakili wangu, Viongozi wenzangu wa chama halali cha Chadema, nimenyimwa fursa hata ya kuomba Mungu. Majaji wenzenu wamesema hayo yaliyotendeka nilinyimwa fursa na haki ya kujitetea, msije mkasau hayo mnapofikiria adhabu kali. Waheshimiwa Majaji mimi ni raia mwema wa nchi hii, mzalendo wa nchi hii, nimetumikia nchi hii kama Mbunge wa kuchaguliwa na Wananchi mara 2 nimekwenda Jeshini, nimekuwa Rais wa Chama cha Wanasheria wa nchi hii, mimi sio mpiga kelele, I am a patriotic, ndio maana nimeona na mabalozi wako Mahakamani, wanajua mimi ni patriotic hivyo mnapofikiria adhabu msije mkasahau hoja hii. Waheshimiwa Majaji gerezani sio mahali pazuri sana, nasema hivyo kwasababu nimeishi kwa siku 577, nakaa kwenye chumba cha sita kwa sita, sio sheraton hotel, unaweza ukasema tu funga kama hujui Gereza ni nini? Nasema haya kwasababu mimi sio mzima sana, kwenye huu mwili wangu nina operesheni 25, visu vya madaktari, ninatembea na risasi mwilini. Katika risasi 16 zilizoingia mwilini moja walishindwa kuitoa, ninatakiwa niwe naenda Hospital Ubeligiji, Hospital ya chuo kikuu cha Luven nilikotibiwa baada ya yaliyonikuta miaka 9 iliyopita, nimeshamiss appointment 4 kwasababu ya kesi hii, juu ya yote hayo Majaji nina kisukari huu mwaka wa 6 sasa, kwahiyo mtakapokuwa mnatafakari hiyo adhabu kali, mkumbuke hilo kwamba hali yangu ya kiafya sio nzuri sana. Waheshimiwa majaji kosa la uchochezi mara ya mwisho nilipoangalia ni kosa lenye dhamana, kama itawapendeza Kwa vile hili kosa lina dhamana, mnipe dhamana ili nikatie uamuzi wenu huu rufaa nikiwa nje kwa dhamana lakini muhimu zaidi pia ili nikamzike huyu aliyelala (Mzee Alute), nilisema sina mpango wa kuomba ila dhamana naomba. Part 502 itaendelea kwenye post inayofuata, Naomba Repost yako.
4
16
95
14,599
Hoja kuu ya TAL ni kwamba Mahakama imemwondolea hatia ya uhaini lakini imemkuta na hatia ya uchochezi chini ya kifungu cha 390, Kosa ambalo anasema hakuwahi kushtakiwa nalo kama shtaka linalojitegemea. Kwa mtazamo wake hali hiyo inaonyesha kwamba alikaa gerezani kwa siku 577 akikabiliwa na shtaka ambalo Mahakama yenyewe imeshindwa kulithibitisha, na kwamba kosa la uchochezi limeingizwa mwishoni mwa shauri. Hii ni hoja nzito inayogusa legality, adequate particulars na haki ya mshtakiwa kujua kosa analotakiwa kujibu. Katika mfumo wa haki ya jinai, Mahakama inaweza kuwa na mamlaka ya kumtia mshtakiwa hatiani kwa kosa dogo katika mazingira yanayotambuliwa na sheria. Lakini mamlaka hayo yana masharti, ni lazima kuwe na msingi wa kisheria, ushahidi unaothibitisha viini vya kosa mbadala na utaratibu unaolinda haki ya kusikilizwa. Naweza kusema hoja ya Lissu kwamba hakushtakiwa kwa uchochezi inapaswa kupimwa pamoja na maelezo ya Mahakama kwamba alikuwa na taarifa ya kutosha na nafasi ya kujitetea. Swala la msingi hapa sio jina la kosa pekee, bali kama taarifa aliyopewa na mwenendo wa shauri vilimpa nafasi ya kweli ya kujibu viini vya kifungu cha 390. Hapo ndipo uhalali wa matumizi ya kifungu cha 319 cha CPA unapokuwa muhimu. Lissu ameenda mbali zaidi na kusema kuwa kwake hukumu hii ni uthibitisho wa kile alichokiita political persecution. Anasema kesi iligeuzwa kuwa uwanja wa mapambano ya kisiasa na kwamba Mahakama imetafuta kosa jingine ili asiondoke bila hatia yoyote. Pia amelinganisha hukumu hiyo na kesi ya Jomo Kenyatta ya mwaka 1954 nchini Kenya. Tukumbuke haya ni madai na tafsiri za Lissu kuhusu mazingira na madhumuni ya shauri, na sio hitimisho ambalo tunaweza kulichukulia kama limethibitishwa na Mahakama. Lakini kisheria, hoja yake inaibua swali moja zito sana kwamba, Matumizi ya kosa dogo yalifuata masharti ya sheria na haki ya kusikilizwa, Au yalizua tatizo la mshtakiwa kuhukumiwa kwa kosa ambalo halikuwa msingi wa shtaka lake la awali. Lissu pia amesisitiza kwamba hataki maelezo yake yatafsiriwe kama kuomba msamaha. Amesema hana hatia na kwamba mtu asiye na hatia haombi msamaha kwa kosa asilolitenda. Kauli hii ni sehemu ya msimamo wake kuhusu kutokubali hukumu, lakini pia inaweka wazi kuwa maelezo yake katika hatua ya adhabu hayapaswi kuchukuliwa kuwa ni kukiri kosa. Pia akaeleza hoja ya kisheria ambayo ina umuhimu wa moja kwa moja katika uamuzi wa adhabu, Yaani ameikumbusha Mahakama kwamba Wakili Mkuu wa Serikali alirejea kifungu cha 35 na kueleza kuwa adhabu ya juu ni kifungo cha miaka mitano, faini au vyote kwa pamoja. Lissu amerejea uamuzi wa Salum Shaban v R (1985) TLR 71, akisema kuwa pale ambapo sheria imetoa chaguo la faini au kifungo, Mahakama inapaswa kuzingatia faini kwanza. Ameongeza rejea za Alice Nyawira Ndungu v R, Criminal Appeal No. 40 of 2022 na Elias Ndikumana v R, Criminal Appeal No. 39 of 2022 kama sehemu ya hoja yake. Hapa kuna jambo muhimu la kisheria la kuelewa kwamba, pale sheria inapotoa adhabu mbadala, tafsiri ya kifungu na maamuzi ya Mahakama za juu ndio huamua namna mamlaka ya kutoa adhabu yanavyotumika. Hoja ya Lissu ni kwamba Mahakama haipaswi kuanza kwa kuchagua kifungo bila kuzingatia kanuni iliyowekwa na Mahakama ya Rufani kuhusu matumizi ya faini pale inapopatikana kama adhabu mbadala. Naweza kusema, Mahakama inapaswa kuchambua maamuzi aliyoyataja na kubaini kama yanahusu mazingira na kifungu cha adhabu kinachotumika katika shauri hili.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 500 Mhe. Lissu amemaliza kuteta jambo na Mawakili wake, Mawakili wanarudi kwenye nafasi zao. Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa majaji nashukuru kwa nafasi, naomba mnisikilize kwa umakini na muandike kwa umakini. Leo ni siku ya 577 nikiwa gerezani kwa kuitwa Mhaini, kosa ambalo kwa katiba ya nchi yetu ndio kosa kubwa kuliko yote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ndio kosa pekee lililotamkwa katika katiba, kosa ambalo kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu, adhabu yake inaweza kuwa kifo baada ya siku 577 za hilo wingu jeusi la adhabu ya kifo kuning’ing’inia juu ya kichwa changu, mmeniita mchochezi kosa ambalo halijapangiwa adhabu. Mmeniita mchochezi na Wakili wa Serikali Mkuu anahangaika kutafuta adhabu yake ni nini???? Maana yake ni nini waheshimiwa majaji? Kosa nililoshtakiwa nalo halikuwa kosa na nyie wenyewe mmesema halikuwa kosa, kwahiyo nilikaa siku 577 Gereza la Ukonga bila kosa lolote. Waheshimiwa majaji kauli yenu kwamba halikuwa kosa mmekubaliana na msimamo wangu na ushahidi wangu. Kuna kitu kimoja hamjakisema na nitakisema for the record na ushahidi wangu umethibitisha kwamba hii ilikuwa ni kesi ya kisiasa tuu, kugeuza Mahakama ya jinai kuwa uwanja wa mapambano ya kisiasa. Kwa hukumu yenu ya leo mmethibitisha hilo, ni Political persecution, hivyo inabidi visababu vitengenezwa vya kumfunga huyu mpinzani wao wa kisiasa na visababu vyenyewe ni kosa la uchochezi ambalo nyie Majaji mmelitengeneza, sikushtakiwa kwa uchochezi, nilishtakiwa nje ya uhaini. Nilishtakiwa kwa kusambaza taarifa za uongo, mmetafuta kosa ambalo halikuwepo, with all due respect mmefanya hivi kwasababu ya maelekezo ya kisiasa, hana kosa ila asiachiwe hivi hivi ataonekana ameshinda, Serikali itaaibika, anayetupa Ujaji ataaibika, ndivyo mlivyofanya leo. Ninajua mnahukumu, ninajua, I feel it in my heart kwa bahati mbaya sana mmefanya kile ambacho Mahakama kuu ya Kenya ilikifanya mwaka 1954 kwenye kesi ya Jomo Kenyatta. Mahakama Kuu ya Kenya ilimpata na hatia Mzee Kenyatta ingawa historia ilikuwa inajua kuwa hamna kosa lolote, ndicho ambacho mmefanya leo Waheshimiwa majaji. Historia haijawa na wema sana kwa Majaji ambao wamegeuza Mahakama zao kuwa mahali pakuadhibia wasiokuwa na hatia ili kuwaridhisha walioko madarakani kwasababu mnaadhibu mtu ambaye mnajua hana hatia na Dunia inajua hana hatia. Waheshimiwa Majaji Wasiokuwa na hatia kama mimi huwa hawaombi msamaha, unaomba msamaha kama una hatia au kama umekosa. Huombi msamaha unapokuwa huna hatia, nataka niwe very clear kuwa haya nitakayoyasema yasichukuliwe kuwa naomba msamaha, I am completely innocent lakin kwa vile Wakili mkuu wa Serikali amezungumza naomba nimjibu, Kwanza kabisa, amesema kwenye kifungu cha 35 ambacho amekiombea adhabu kali amesema adhabu ya juu ni kifungo cha miaka 5 au faini au vyote viwili. Sheria inapotoa adhabu ya aina hiyo faini au kifungo, Mahakama inatakiwa ifanye nini? katika kesi ya Salum Shaban vs R (1985) TLR 71 ambapo Mahakama hii ilisema pale ambapo Bunge limetoa option ya faini au kifungo, Mahakama lazima itoe kwanza adhabu ya faini kwanza. Kwahiyo mnapotafakari adhabu kali iliyoombwa na Wakili Mkuu wa Serikali msije mkasahau msimamo huu wa kisheria ikiwemo kesi ya Alice Nyawira Ndungu vs R Criminal Appeal No 40 of 2022, Elias Ndikumana vs R Criminal Appeal No 39 of 2022 na mashauri mengine mengi ambayo nina uhakika mnayafaham. Kuna maneno yamezungumzwa hapa na Wakili Mkuu wa Serikali, amejigeuza kuwa shahidi, amesema kwamba haya makosa ya uchochezi yamekuwa ni makosa mengi sana kwa mujibu wa taarifa za polisi, na kwa mujibu wa hotuba ya Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman. Part 501 itaendelea kwenye post inayofuata. Naomba Repost yako.
2
9
73
11,113
Ikiwa kanuni hiyo inatumika, itakuwa na umuhimu mkubwa katika kuamua kama faini inapaswa kupewa kipaumbele kabla ya kifungo. Tukumbuke hili sio suala la huruma, ila ni suala la kufuata tafsiri ya sheria iliyowekwa na Mahakama yenye mamlaka ya juu. Hoja nyingine ya Lissu inahusu maelezo ya Wakili Mkuu wa Serikali kwamba makosa ya uchochezi yameongezeka nchini, akirejea taarifa za polisi na hotuba ya Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman. Lissu amesema kwa kufanya hivyo Wakili Mkuu wa Serikali amejigeuza kuwa shahidi. Kisheria, hoja hii inagusa tofauti kati ya submissions na evidence, yaani wakili anaruhusiwa kutoa hoja na kueleza namna ushahidi uliopo unavyopaswa kutafsiriwa. Lakini hoja za wakili haziwezi kuwa ushahidi mpya wa kuthibitisha ukweli wa jambo ambalo halikuletwa na kuthibitishwa kwa utaratibu wa ushahidi. Ikiwa Jamhuri inataka Mahakama izingatie ongezeko la makosa ya uchochezi, athari zake au hali ya usalama nchini, Inapaswa kuweka msingi unaokubalika wa taarifa hizo na kuonyesha uhusiano wake na kosa ambalo Lissu amepatikana nalo na hatia. Taarifa za jumla kuhusu mwenendo wa makosa nchini haziwezi moja kwa moja kuwa ushahidi wa kwamba mshtakiwa huyu alisababisha madhara yote yanayotajwa. Kingine taarifa ya Tume ya Chande inaweza kuwa na maudhui yanayostahili kuchunguzwa, Lakini Mahakama inapaswa kutofautisha kati ya maelezo ya jumla kuhusu sababu za vurugu na ushahidi unaomwunganisha Lissu binafsi na madhara yanayotajwa. Sentencing inapaswa kujengwa juu ya kosa lililothibitishwa na mambo yanayohusiana nalo, na sio madai mapana yasiyo na causal nexus ya kutosha.
2
9
391
Jaji Ndunguru ametangaza rasmi kuwa Mahakama imemkuta Tundu Lissu na hatia ya kosa la uchochezi chini ya kifungu cha 390 cha Kanuni ya Adhabu. Haya ni mabadiliko makubwa katika mwelekeo wa shauri, kwa sababu shtaka lililomfikisha Lissu Mahakamani lilikuwa la uhaini chini ya kifungu cha 39(2)(d), Lakini Mahakama imeamua kwamba ushahidi unaweza kuunga mkono kosa dogo la uchochezi. Mahakama imesema inaamini kwamba Lissu alikuwa na taarifa ya kutosha kuhusu kosa hilo dogo na alipata nafasi ya kujitetea. Kwa mtazamo wa Mahakama ushahidi uliotolewa katika shauri ulijikita katika madai ya uchochezi, na Lissu alikuwa na nafasi ya kujibu madai kwamba maneno yake yalilenga kuchochea umma kuzuia uchaguzi wa mwaka 2025. Lakini hoja hii ina uzito wa kikatiba na kiutaratibu, kwamba kuwepo kwa ushahidi unaogusia uchochezi sio sawa moja kwa moja na kuthibitisha kwamba mshtakiwa alikuwa na taarifa ya kutosha kuhusu kila kiini cha kosa hilo. Notice of the charge inapaswa kumpa mshtakiwa uelewa wa tuhuma zinazomkabili, na right to be heard inapaswa kumpa nafasi halisi ya kuzijibu. Niseme msingi wa Mahakama kwamba Lissu alikuwa na taarifa na nafasi ya kujitetea ni sehemu muhimu ya hukumu inayostahili kuchunguzwa kwa kuangalia hoja na ushahidi uliotolewa wakati wa shauri. Mahakama imeridhika kwamba maneno aliyoyatamka Lissu hadharani yalikuwa na lengo la kuchochea umma kuzuia uchaguzi wa 2025. Na hapa Mahakama imefanya hitimisho kuhusu maana na nia ya maneno hayo na kuyahusisha na kifungu cha 390. Lakini katika uchambuzi wa kisheria, ni muhimu kutenganisha utamkaji wa maneno, namna yalivyopokelewa na wasikilizaji, na nia ya jinai ya mzungumzaji. Kukubali kwamba maneno yalitamkwa hakumalizi mjadala wa kama yalitimiza viini vyote vya kosa la uchochezi. Baada ya kutangaza hatia, Mahakama imeingia katika hatua ya kusikiliza hoja za adhabu yaani sentencing hearing. Upande wa Jamhuri, kupitia Wakili Katuga, umeomba Mahakama ipokee taarifa na ushahidi wa ziada kwa madhumuni ya kuamua adhabu inayofaa, akirejea kifungu cha 339 cha CPA. Hoja ya upande wa mashtaka imejengwa kwenye madhumuni ya adhabu, kwamba kumwonya aliyepatikana na hatia asirudie kosa, na kutoa ujumbe wa kuzuia wengine wenye nia ya kutenda makosa yanayofanana. Hii ni dhana ya deterrence, ambayo ni moja ya madhumuni yanayoweza kuzingatiwa wakati wa kutoa adhabu. Jambo la kuzingatia ni kwamba upande wa Jamhuri umekiri kuwa hauna rekodi za awali za makosa ya jinai dhidi ya Lissu, hili ni jambo muhimu katika tathmini ya adhabu. Kutokuwepo kwa rekodi za awali kunaweza kuwa sababu ya kupunguza uzito wa adhabu, ingawa sio lazima kuondoe uwezekano wa adhabu nyingine kulingana na mazingira ya kosa na mambo mengine yanayokubalika kisheria. Badala yake, upande wa mashtaka umejaribu kuwasilisha picha pana ya athari za uchochezi nchini. Umedai kuwa kumekuwa na ongezeko la watu wanaochochea umma kwa maslahi ya kisiasa au kiuchumi, Na kwamba vitendo hivyo vinaweza kuathiri amani, uchumi, mali za umma na binafsi, pamoja na kuleta hofu kwa wananchi wanaotaka kuendelea na shughuli zao za kiuchumi. Hapa kuna suala muhimu la ushahidi, yaani athari za jumla zinazodaiwa kutokea nchini haziwezi kuhusishwa moja kwa moja na mshtakiwa bila kuonyesha uhusiano wa ushahidi kati ya kauli zake na madhara hayo. Katika hatua ya adhabu, Mahakama inaweza kuzingatia madhara yanayohusiana na kosa, Lakini inapaswa kutofautisha kati ya madhara yaliyothibitishwa, madai ya jumla na matukio ambayo hayajaunganishwa na kitendo cha mshtakiwa. Upande wa mashtaka pia umeirejea taarifa ya Tume ya Uchunguzi iliyoongozwa na Jaji Chande, ukidai kwamba taarifa hiyo ilieleza kuwa kauli za baadhi ya wanasiasa zilichangia vurugu wakati na baada ya uchaguzi wa 2025.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 499 Jaji Ndunguru anasema kwamba Mahakama inaamini kwamba mshtakiwa alikuwa na notice ya kosa dogo hivyo alikuwa na nafasi ya kujitetea na ushahidi wote uliotolewa umejikita kwenye uchochezi na alichochea umma kuzuia uchaguzi wa 2025 Kwa mujibu wa kifungu cha 390 cha Kanuni ya Adhabu Mahakama imeridhika kwamba Lissu alitenda kosa la uchochezi kwa mujibu wa kifungu cha 390 cha Kanuni ya Adhabu. Hivyo Mahakama hii inamtia hatiani kwa kosa hili la Uchochezi. Jaji Ndunguru: Upande wa mashtaka Anasimama Katuga anasema Kamba kwa mujibu wa kifungu cha 339 cha CPA mahakama hii inaweza kupokea mpaka ushahidi kwenye kutoa proper sentence. Upande wa Jamhuri tunajua adhabu ina malengo mojawapo ni kutoa onyo kwa mtu aliyetenda kosa ili asirudie kosa hilo au makosa mengine na linakuwa onyo kwa watu wengine wenye nia ya kutenda kosa hilo ambalo mshtakiwa ametiwa hatiani. Upande wa Jamhuri mbali na kutokuwa na previous records za mshtakiwa za makosa ya nyuma, kwa mujibu wa taarifa zilizopo polisi kumekuwa na ongezeko kubwa sana la watu wenye kutenda kosa la kuchochea umma wa watanzania kwa maslahi yao binafsi either ya kisiasa au ya kiuchumi. Vitendo ambavyo mara zote vinaharibu amani ya nchi, vinaathiri uchumi wa nchi kwa maana ama vinapelekea uharibifu wa mali za umma zikiwemo na mali binafsi. Hivi vitendo vya kichochezi vinaathiri uchumi wa nchi na vimepelekea umma wa watanzania kuwa na hofu kuwa kutakuwa na matukio ya uvunjifu wa amani hivyo wanashindwa kufanya shughuli za kiuchumi. Waheshimiwa vitendo vya kiuchochezi vinaathiri uchumi wa wananchi na hili ni kosa kisheria, wakati mnatoa adhabu tunawaalika katika hotuba halali ya Jaji Chande na Tume yake baada ya kufanya uchunguzi bila kuchagua upande wowote walisema sababu za vurugu wakati na baada ya uchaguzi wa 2025 zilisababishwa na kauli za baadhi ya wanasiasa. Kifungu cha 35 kinatoa general punishment ambayo adhabu yake ni miaka 5 hivyo tunaomba mahakama hii iangalie athari ambazo zimetokea kutokana na kauli ambazo mshtakiwa ametiwa hatiani pamoja na hotuba ya jaji chande. Taarifa ya Chande inaonyesha hasara inayotokana na uchochezi uliotokana na kauli hizo. Tunaomba adhabu kali Waheshimiwa majaji ili iweze kukidhi nia ya adhabu kisheria. Waheshimiwa kifungu hiki kinasema adhabu kubwa ni miaka 5 au pamoja na faini. Ni faini kiasi gani ni Mahakama kuangalia athari kutokana na athari zilizotokea. Ni hayo tu. Jaji Ndunguru anamuuliza Mshtakiwa kama analolote la kusema? Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa majaji nina maneno ya kuzungumza ila naomba dakika 5 nifanye consultations na mawakili wangu ili niweze kuzungumza hayo ninayotaka kuzungumza. Jaji Ndunguru:Sawa Part 500 itaendea kwenye post inayofuata. Naomba Repost.
6
19
1
78
15,997
Jamhuri imeomba Mahakama izingatie taarifa hiyo katika kupima uzito wa adhabu, pamoja na athari za vurugu zilizotajwa ndani yake. Lakini hapa pia kuna tofauti ya kisheria inayopaswa kuzingatiwa sana, kwamba kuwepo kwa taarifa ya tume kuhusu sababu za vurugu nchini hakumaanishi moja kwa moja kwamba kila mwanasiasa aliyetajwa kwa ujumla anawajibika kwa kila madhara yaliyotokea. Mahakama inapaswa kuchunguza kama taarifa hiyo inaunganisha kwa ushahidi maalumu kauli za Lissu na madhara ambayo Jamhuri inataka yatumike kuongeza adhabu yake. Naweza kusema causal nexus ni muhimu hata katika hatua ya hukumu. Jamhuri imeomba adhabu kali, ikirejea kifungu cha 35 cha Kanuni ya Adhabu na kueleza kuwa adhabu ya jumla inayotumika ni kifungo cha hadi miaka mitano au faini, au vyote kwa pamoja, kwa mujibu wa kifungu hicho. Mahakama ndio yenye jukumu la kuamua adhabu inayofaa baada ya kupima sheria, uzito wa kosa, mazingira yake, rekodi ya mshtakiwa na hoja za pande zote. Ni muhimu kutambua kwamba adhabu sio chombo cha kutoa ujumbe wa kisiasa au kuadhibu mshtakiwa kwa hali ya jumla ya nchi. Adhabu inapaswa kuwa ya mtu binafsi yaani individualised sentencing na ilenge kosa ambalo Mahakama imethibitisha, na sio makosa mengine au madhara ambayo hayajaunganishwa naye kwa ushahidi. Baada ya kusikiliza maombi ya Jamhuri, Jaji Ndunguru amempa Lissu nafasi ya kusema jambo lolote kabla ya uamuzi wa adhabu. Lissu ameomba dakika tano ili kufanya mashauriano na mawakili wake kabla ya kutoa maelezo yake, Mahakama imekubali ombi hilo. Ombi hilo lina umuhimu kwa sababu maelezo ya mshtakiwa kabla ya hukumu ya adhabu yanaweza kuwa na mchango katika kuwasilisha mazingira yake binafsi, rekodi yake, Hali zinazoweza kupunguza adhabu yaani mitigating factors na msimamo wake kuhusu kosa alilopatikana nalo na hatia. Ni sehemu ya haki ya kusikilizwa katika hatua ya adhabu. MOYO WANGU UNAVUJA DAMU
2
16
963
Jaji Ndunguru ameanza kwa kurejea uamuzi wa Mahakama ya Rufani katika kesi ya DPP v Zombe, akieleza kuwa matumizi ya kifungu cha 319(1) na (2) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) sio jambo la moja kwa moja. Mahakama haiwezi kubadilisha kosa na kumtia mshtakiwa hatiani kwa kosa ambalo hakushtakiwa nalo bila kuzingatia haki yake ya kusikilizwa na kupewa taarifa ya kosa analotakiwa kujibu. Hili ni jambo muhimu sana kuelewa, Katika mfumo wa haki ya jinai, haki ya kusikilizwa sio utaratibu wa pembeni. Mshtakiwa anapaswa kujua kwa uwazi tuhuma zinazomkabili ili aweze kuandaa utetezi unaolenga viini vya kosa hilo. Kosa la jinai linaweza kuwa na maneno yanayofanana na kosa jingine, lakini kufanana kwa maneno hakumaanishi kwamba viini vyake vinafanana au kwamba mshtakiwa tayari amepata nafasi ya kujibu shtaka hilo. Lakini baada ya kuweka msingi huo, Mahakama imeeleza kuwa kifungu cha 390 kinaweza kuwa kosa dogo yaani minor offence, linalohusiana na kifungu cha 39(2)(d). Imejenga hoja kwamba uchochezi yaani incitement ni sehemu ya mantiki ya kosa la uhaini linalodaiwa katika shauri hili, na kwamba sio lazima uchochezi huo uwe umeshtakiwa kama kosa linalojitegemea ili Mahakama iweze kuutazama katika muktadha wa kosa dogo. Hapa ndipo nimejiuliza swalia ambalo bado naliwaza kwamba, Mahakama imeeleza kuwa haitumii kifungu cha 319 bila kumpa mshtakiwa taarifa na nafasi ya kusikilizwa, lakini sasa inasema kifungu cha 390 ni kosa dogo linaloweza kutumika. Nawaza hivi Mahakama imeridhika kwamba Lissu alikuwa na taarifa ya kutosha kuhusu viini vya kosa hilo na alipata nafasi halisi ya kujitetea dhidi yake. Jibu la swali hilo ni muhimu kwa sababu fair hearing haihusu jina la kifungu cha sheria pekee, bali pia maudhui ya tuhuma na nafasi ya mshtakiwa kuzijibu. Mahakama pia imeitazama kifungu cha 390 kama kifungu chenye lengo la kuzuia uhalifu katika hatua za awali, kabla madhara kwa umma hayajatokea. Ndio maana imezungumzia dhana ya prevention of crime na present danger. Kwa tafsiri ya Mahakama, kifungu hiki kinaweza kuingilia kati pale ambapo maneno au uchochezi unaelekezwa kwenye kumshawishi mtu mwingine kutenda kosa, hata kabla madhara yanayokusudiwa hayajatokea. Lakini hapa kuna tofauti ambayo haipaswi kupotea bila kuielewa, kwamba kuthibitisha kwamba maneno yaliwasilishwa kwa umma sio sawa na kuthibitisha kwamba mzungumzaji alikusudia mtu au watu fulani wachukue hatua ya kutenda kosa. Hayo ni mambo mawili tofauti na Jamhuri inapaswa kuonyesha sio kwamba maneno yalisikika pekee, bali pia kwamba yalikuwa na maudhui na mwelekeo wa kisheria unaotakiwa na kifungu husika. Na hoja ya mens rea bado ipo hapa, kama kifungu cha 390 kinahitaji nia ya kumshawishi au kumchochea mtu mwingine kutenda kosa, Mahakama inapaswa kubainisha kosa gani lililokusudiwa, ni watu gani waliolengwa, na ni ushahidi gani unaothibitisha kwamba Lissu alikuwa na nia hiyo. Kauli ya jumla kwamba alitaka uchaguzi uvurugwe haitoshi yenyewe kujibu maswali hayo bila kuchambua maana ya maneno, mazingira yake na viini vya kosa linalotumika. Mahakama imesema kwamba kutokana na ushahidi uliopo, Lissu alitamka maneno hadharani na kwamba hakukana kuyatamka. Pia imetaja kuwa mashahidi wa utetezi hawakupinga ukweli wa utamkaji wa maneno hayo. Lakini, kukubali kwamba maneno yalitamkwa sio sawa na kukubali kwamba yalikuwa ya jinai. Hii ndio tofauti ambayo imekuwa kiini cha utetezi tangu mwanzo wa shauri hili, yaani admission of words is not admission of criminal intent. Mtu anaweza kukubali kuwa alitamka maneno fulani, lakini akapinga tafsiri inayotolewa na upande wa mashtaka kuhusu nia na maana yake ya kisheria. Mahakama inapaswa kupima maneno hayo kwa ujumla wake na katika mazingira yake, sio kuyachukua kama ushahidi wa moja kwa moja wa nia ya kutenda kosa.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 498 Jaji Ndunguru anasema katika kutafisiri hicho kifungu cha 319(1-2) cha CPA Mahakama ya Rufani ilielezea kwa marefu na mapana kwenye kesi ya DPP vs Zombe kuhusu kifungu hicho kuwa sio automatic. Kwakuwa mshtakiwa hakushtakiwa na kosa dogo, Mahakama pia haiwezi kutumia kifungu hicho bila kumpa mshtakiwa haki ya kusikilizwa au kumpa notice. Kwa mujibu wa ushahidi uliopo kuwa maneno hayo yalirushwa live ili kuuhabarisha umma na video hizo video hazikutolewa mahakamani na kwa vile hajakanusha kutamka maneno hayo na upande wa jamhuri umesema kuwa alilenga kuchochea umma na mashahidi wa upande wa utetezi nao hawajakataa kuhusu mshtakiwa kutamka maneno hayo. Tumeridhika kwamba mshtakiwa kutamka maneno hayo hadharani mbele ya umma alilenga kuchochea umma ili kuvuruga uchaguzi wa 2025 kwa njia isiyo ya amani kutokana na maneno yake hivyo basi tukiongozwa na maamuzi mbalimbali na kwa muktadha wa kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu kosa lililotengenezwa na kifungu cha 390 ni kosa dogo la uhaini, kifungu cha 390 kinalengo la kuzuia crime katika hatua ya mwanzo before public harm. Kwa tafsiri yetu tunasema kifungu hiki kina prevent nia na present danger. Upande wa mashtaka wanapaswa kuthibitisha kuwa maneno ambayo mshtakiwa aliyatamka kufanya instigation yalikuwa communicated, pia mshtakiwa alilenga kuwa mtu au watu watende kosa. Tunaelewa kwamba kifungu cha 390 kinatumika kwenye kosa lolote hakijataja kosa lolote pale, tunaamini kwamba kufanya kosa la uchochezi kunaweza kupelekea present danger, tunaamini ni minor offence na ni cognate offence kwa mujibu wa 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu. Ni kwa mtazamo wetu sasa kwamba ni common sense kwamba incitement ni component ya offence ya treason hivyo sio lazima mtu awe charged independently. Kulingana na ushahidi uliotolewa mshtakiwa alichochea umma kuvuruga uchaguzi, kuzuia uchaguzi, kuhamasisha uasi na kukinukisha vibaya sana. Upande wa utetezi haujaonyesha ni kwa namna gani walipanga kuzuia uchaguzi, kuhamasisha uasi, na mashahidi wa upande wa Jamhuri walieleza namna ambavyo walishawishika na maneno ya mshtakiwa mfano shahidi wa 4, 5,8 ,11, 13, 14 walishawishika na kujiunga na wale ambao walishawishika ili waweze kuvuruga uchaguzi. Part 499 itaendelea kwenye post inayofuata, Naomba Repost yako.
1
6
51
7,624
Hoja nyingine inayostahili kuangaliwa ni pale Mahakama inaposema kuwa utetezi haujaonyesha namna walivyopanga kuzuia uchaguzi, kuhamasisha uasi au kutekeleza maneno yaliyotamkwa. Kwa heshima ya kanuni za ushahidi wa jinai, kutokuwepo kwa maelezo ya kina kutoka kwa utetezi hakuwezi kuchukua nafasi ya wajibu wa Jamhuri kuthibitisha kosa. Mzigo wa kuthibitisha kila kiini cha kosa unabaki kwa upande wa mashtaka, mshtakiwa hana wajibu wa kuthibitisha kwamba hakupanga uhalifu, ila Jamhuri ndio inayopaswa kuthibitisha kwamba alikusudia na kutenda kile kinachodaiwa. Mahakama pia imetaja mashahidi wa upande wa Jamhuri namba 4, 5, 8, 11, 13 na 14 ambao ilisema walishawishika na maneno ya Lissu na kujiunga na watu wengine waliokuwa na nia ya kuvuruga uchaguzi. Ushahidi huu unaweza kuwa na umuhimu katika kuthibitisha namna ujumbe ulivyopokelewa na baadhi ya wasikilizaji. Lakini bado kuna maswali ya kisheria hapa kwamba, Mashahidi hao walishawishika kufanya kosa gani hasa na Walieleza kwamba Lissu aliwaelekeza kutenda kosa hilo. Pia nia yao ya kufanya vurugu ilitokana na maneno yake au kulikuwa na sababu nyingine. Hapa ndipo causal nexus na attribution zinapokuwa muhimu sana, kwamba ukweli kwamba mtu alisikia hotuba na baadaye akawa na nia ya kufanya vurugu hauonyeshi moja kwa moja kwamba mzungumzaji alikusudia kumshawishi kufanya vurugu. Lazima kuwe na ushahidi unaounganisha maudhui ya ujumbe, nia ya mzungumzaji na kosa ambalo inadaiwa alitaka lifanywe. Pia, ushahidi kwamba mashahidi fulani walishawishika hauwezi kutumika kama uthibitisho wa moja kwa moja kwamba kila msikilizaji alielewa ujumbe kwa namna hiyo hiyo. Mahakama inapaswa kutathmini uaminifu wa mashahidi, ujuzi wao binafsi, mazingira ya kauli zao na uzito wa ushahidi wao. Idadi ya mashahidi wanaotoa tafsiri inayofanana sio mbadala wa uchambuzi wa viini vya kosa.
3
1
10
736
Jaji Ndunguru amerejea kifungu cha 10 cha Kanuni ya Adhabu na kueleza kwamba nia ya jinai haiwezi kutazamwa kwa kujitenga na matendo ya mshtakiwa. Hapa tunazungumzia uhusiano kati ya mens rea na actus reus. Yaani nia ni hali ya ndani ya akili ya mtu, lakini katika kuthibitisha kosa, Mahakama inapaswa kutafuta msingi wa ushahidi unaoonyesha namna nia hiyo ilivyojitokeza katika matendo yake. Ni kweli kwamba mens rea inaweza kuthibitishwa kwa ushahidi wa mazingira yaani circumstantial evidence), ila sio lazima mshtakiwa akiri nia yake. Lakini tunapaswa kuelewa kwamba, hitimisho la nia lazima litokane na mazingira yenye msingi wa ushahidi, yanayounganisha mshtakiwa na kosa linalodaiwa. Mahakama haiwezi kuchukua tafsiri ya shahidi na kuifanya kuwa ukweli wa kisheria bila kuipima dhidi ya ushahidi mwingine. Ndio maana Mahakama imeona kuwa Jamhuri iliegemea zaidi katika tafsiri za mashahidi namba 1, 2 na 16 kuhusu maana ya maneno ya Lissu. Tatizo sio kwamba mashahidi hawakuwa na haki ya kutoa maoni yao, bali kwamba maoni hayo hayakuambatana na ushahidi wa kutosha kuthibitisha nia mahsusi ya kuitishia Serikali. Opinion of a witness haiwezi kuchukua nafasi ya ushahidi unaothibitisha criminal intent. Mahakama pia imeweka mpaka kati ya political advocacy na criminal liability, yaani Kauli kali, ukosoaji wa Serikali, wito wa mageuzi au ujumbe unaohamasisha mabadiliko ya kisiasa hauwi moja kwa moja kosa la jinai. Katika shauri hili, utetezi ulieleza kuwa kauli za Aprili 3, 2025 zilikuwa sehemu ya msimamo wa CHADEMA wa No Reforms, No Election. Mahakama ilipaswa kuchunguza kama Jamhuri imethibitisha kwamba nyuma ya kauli hizo kulikuwa na nia mahsusi ya uhaini, badala ya nia ya kushinikiza mageuzi ya kisiasa. Hii haimaanishi kwamba hotuba ya kisiasa haiwezi kamwe kuwa sehemu ya kosa la jinai. Inamaanisha kwamba mazingira ya kisiasa ni muhimu katika kutafsiri maana na nia ya maneno, lakini hatimaye kipimo kinabaki kuwa viini vya kosa vilivyowekwa na sheria. Hoja nyingine yenye uzito ni suala la publication na attribution, Jamhuri ilidai kwamba kwa kuwa Lissu alizungumza mbele ya waandishi wa habari na mkutano ukarushwa mubashara, basi alihusika katika kuchapisha au kusambaza maneno hayo. Lakini Mahakama imekubaliana na utetezi kwamba hakuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa Lissu ndiye aliyepakia video kwenye YouTube ya Jambo TV. Hapa kuna tofauti muhimu ya kisheria, kuonekana mbele ya kamera sio sawa na kuwa mtu aliyeendesha matangazo, kurekodi, kupakia au kusambaza video. Attribution inahitaji ushahidi unaomtambulisha mtendaji wa kitendo kinachodaiwa. Uwepo wa mtu katika tukio hauwezi peke yake kuthibitisha kwamba ndiye aliyetekeleza kila kitendo kilichofanyika katika tukio hilo. Mahakama imekubali kwamba shahidi wa 17 alikuwepo kwenye mkutano na alieleza kuwa matangazo yalirushwa mubashara kwa lengo la kuhabarisha umma kuhusu msimamo wa No Reforms, No Election. Ushahidi huo unaweza kuthibitisha kwamba matangazo yalifanyika na maneno yalisikika. Lakini haujibu moja kwa moja swali la nani aliyepakia video kwenye jukwaa la YouTube. Hii ndio maana ya proof of occurrence is not necessarily proof of attribution na kuthibitisha kwamba jambo lilitokea sio sawa na kuthibitisha kwamba mshtakiwa ndiye aliyefanya kitendo kinachohusishwa nalo. Kuhusu kutokuwepo kwa video clip, Mahakama imeeleza kuwa hali hiyo haifuti moja kwa moja ushahidi wa mdomo uliotolewa na shahidi wa 17. Kisheria, ushahidi wa mdomo unaweza kuthibitisha jambo ikiwa unatoka kwa shahidi mwenye ujuzi binafsi na unakubalika kwa mujibu wa sheria. Lakini ushahidi wa shahidi kwamba alisikia maneno ukithibitisha utamkaji wake, hauwezi moja kwa moja kuthibitisha kwamba Lissu ndiye aliyepakia video kwenye YouTube. Haya ni masuala mawili tofauti yenye mahitaji tofauti ya uthibitisho. Kwa msingi huo, Mahakama imehitimisha kwamba Jamhuri haijathibitisha kuwa Lissu alilenga kutenda kosa la uhaini.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 497 Jaji Nduguru anasema, pia tunasukumwa hivyo na kifungu cha 10 cha Kanuni ya adhabu kuwa nia ya mtu lazima iambatane na matendo ya dhahiri ya mshtakiwa na sio maneno tu. Kwa mtazamo wetu dai kwamba upande wa utetezi walifanya kwa lengo la kushinikiza Serikali kufanya mabadiliko haimaanishi ni kuwa ni kuitishia Serikali ni msimamo wetu kuwa kesi ya upande wa mashtaka imeegemea zaidi katika maoni kuwa maneno ya mshtakiwa yalilenga kuitishia serikali. Mahakama inaamua kuwa sio lazima provocative speeches zinaweza to constitute kosa kwa maana zinalenga kuhamasiha mabadiliko hivyo sio lazima ziwe kosa la jinai. Hatujapata ushahidi wa moja kwa moja ukiachia ushahidi wa namba 1,2 na 16 ambao ni tafsiri zao, sisi tunaona kutokuwa na ushahidi tunasema kwamba maneno hayo sio kwamba yanapelekea uhaini. Tunajua kuwa Serikali ina wajibu wa kusimamia uchaguzi, sheria na hivyo maneno yanayo desrupt election yanaconstitute kosa la uhaini. Hoja ya tatu na ya mwisho ambayo ni ambayo mshtakiwa alidhihirisha nia hiyo ya kuchochea umma kuvuruga uchaguzo kwa lengo la kuitishia serikali. Tukiangalia ushahdi wa Jamhuri hasa namba 1,2 na 16 ambao waliegemea kuwa maneno hayo yalirushwa mubashara na walisema kusambazwa kwa maneno hayo kulifanywa kupitia mawasiliano ya moja kwa moja kati ya mshtakiwa na watu waliokuwepo kwenye mkutano huo, shahidi namba 17 alieleza kwamba matukio hayo yalirushwa live ili kuuhabarisha umma kuhusiana na msimamo wa No reforms, No election. Upande wa mashtaka wanaeleza kuwa kwa kuwa maneno hayo yalirushwa mubashara na mshtakiwa kukiri kuwa aliongea maneno hayo basi mahakama ione kuwa upande wa mashtaka umethibitisha publication hata kama hakuna picha mjongeo. Upande wa utetezi ulieleza kuwa sio Lissu aliyesambaza maneno hayo, na kukosekana kwa video hakuna uthibitisho kuwa Lissu alichapisha. Tunakubaliana na Lissu kuwa hakuna ushahidi kuwa yeye ndio alichapisha na kusambaza hayo maneno kwenye YouTube ya Jambo TV. Kitendo cha kuonekana tu kwenye Jambo TV sio lazima kuwa Tundu Lissu ndiye aliyepandisha kwenye Jambo TV. Tumeona kwamba upande wa mashtaka wamethibitisha kwamba kauli hiyo ilitolewa na mshtakiwa, na kuwa ilisambazwa na mshtakiwa alitoa hotuba hiyo katika umma sio kwa kificho hivyo kauli za mshtakiwa hazikuwa kauli za siri. Mahakama hii inaona kwamba kauli hizo kupandishwa kwenye mtandao wa Jambo TV haimaanishi kuwa Lissu ndiyo aliyepandisha. Hivyo basi kutothibitisha uhusika wa Lissu kuchapisha maneno hayo kwenye Jambo TV upande wa mashtaka walipaswa kuthibitisha element za kosa. Kwa kitendo cha kutokutolewa video clip does not defeat ushahidi wa mdomo ambao ulitolewa na shahidi wa 17 ambaye alikuwepo na mshtakuwa hapingi maneno hayo. Kutokana na ushahidi uliopo, upande wa mashtaka hawajatupa ushahid kuwa Lissu alilenga kutenda kosa la uhaini. Failure kuleta ushahidi hoja ya tatu inakuwa pia haina mashiko, treason per see kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) haijathibitishwa na kifungu hiki hakina minor offence lakini ni jukumu la ku evaluate ushahidi na kuona kama kuna kosa dogo. Kwa mujibu wa kifungu cha 319(1-2) cha CPA kinaelekeza mahakama kwamba inaweza to substitute kosa pale ushahidi unapoonyesha kwamba kunaweza kuwa na kosa dogo. Part 498 itaendelea kwenye post inayofuata, Naomba Repost yako.
3
9
57
9,605
Pia haijaona ushahidi wa kutosha unaomhusisha na kitendo cha kupakia video kwenye YouTube ya Jambo TV. Hivyo viini vinavyohusu nia na kitendo cha kuidhihirisha nia hiyo havijathibitishwa kwa kiwango kinachotakiwa. Mahakama imeendelea kugusia uwezekano wa kosa dogo chini ya kifungu cha 319(1) na (2) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai. Hili ni suala tofauti na uthibitisho wa uhaini. Substitution of a minor offence haiwezi kuwa njia ya kubuni kosa jingine ili kuokoa shtaka lililoshindwa kuthibitishwa. Mahakama inapaswa kujiridhisha kwamba kosa mbadala linatambulika kisheria, viini vyake vinaungwa mkono na ushahidi na mshtakiwa amepata nafasi ya kutosha kujibu msingi wa kosa hilo.
1
6
397
LEO NI SIKU YA HUKUMU Leo, Ijumaa tarehe 6 Novemba 2026, siku ya kusubiri hukumu ya Tundu Antipas Lissu imewadia. Kwa miezi mingi, tumekuwa tukifuatilia ushahidi, tukisikiliza mashahidi, tukichambua vifungu vya sheria na kupima hoja za mashtaka na utetezi. Sasa safari inafika mahali ambapo Mahakama inapaswa kusema, kwa kutumia sheria na ushahidi, imefikia hitimisho gani. Nikiitazama rekodi ya ushahidi kama ilivyojadiliwa katika shauri hili, hoja za utetezi zimeibua maswali mazito kuhusu uthibitisho wa mens rea, actus reus, attribution, publication na maana ya deed chini ya kifungu kinachotumika. Haya sio maswali ya pembeni, ila yanagusa kiini cha shtaka lenyewe. Kwa mfano, kuthibitisha kwamba Lissu alitamka maneno fulani sio sawa na kuthibitisha kwamba maneno hayo yalikuwa na nia ya uhaini. Kuthibitisha kwamba mkutano ulifanyika sio sawa na kuthibitisha kwamba uliitishwa kwa madhumuni ya kutenda kosa. Na kuthibitisha kwamba matangazo yalirushwa moja kwa moja hakujibu moja kwa moja swali la nani aliyekuwa na jukumu la kuyachapisha au kusambaza. Yaani kila kiungo kinahitaji ushahidi wake.
2
19
85
3,769
Ndio maana, kwa mtazamo wangu wa kisheria, ushahidi uliojadiliwa unaibua shaka yenye msingi kuhusu kama Jamhuri imeweza kuthibitisha kila kipengele cha kosa beyond reasonable doubt. Hili ni muhimu sana, kwa sababu katika haki ya jinai, mshtakiwa hana wajibu wa kuthibitisha kutokuwa na hatia. Ni upande wa mashtaka unaopaswa kuthibitisha hatia yake. Kwa msingi huo, tathmini yangu ya ushahidi uliowasilishwa inaelekea kwenye hitimisho kwamba Lissu hana hatia ya kosa la uhaini linalomkabili, kwa sababu maswali muhimu kuhusu viungo vya shtaka hayajaondolewa kwa kiwango kinachotakiwa na sheria. Lakini tukumbuke hitimisho rasmi ni la Mahakama, na ni muhimu kusoma sababu zitakazotolewa katika hukumu. Ningependa tukumbuke jambo moja kamba, Mahakama inapomwachia mtu huru kwa sababu mashtaka hayajathibitisha hatia, haimpi zawadi wala haionyeshi upendeleo. Lakini inatekeleza wajibu wake wa kulinda presumption of innocence, na ikithibitisha hatia kwa ushahidi unaokidhi kiwango cha sheria, nayo inapaswa kueleza msingi wa hitimisho hilo.
1
1
9
383
BEYOND REASONABLE DOUBT Katika criminal jurisprudence, kuna kanuni moja ambayo haiwezi kupuuzwa, kupunguzwa wala kubadilishwa kwa sababu ya uzito wa shtaka, ambayo ni the prosecution must prove its case beyond reasonable doubt. Hiki sio kipimo cha kawaida cha ushahidi ila ni kiwango cha juu cha uthibitisho kinachotenganisha tuhuma na hatia, mashaka na hitimisho la kimahakama, pamoja na mamlaka ya Serikali ya kushtaki na wajibu wake wa kuthibitisha kosa. Maana yake ni kwamba Jamhuri haitoshi kuonyesha kuwa kuna uwezekano Lissu alitenda kosa. Lakini inapaswa kuwasilisha ushahidi unaoaminika, unaokubalika kisheria na wenye probative value ya kutosha kuthibitisha kila essential ingredient ya kosa linalodaiwa. Mahakama inapaswa kuridhika kwa kiwango cha kisheria kwamba ushahidi unaunga mkono hitimisho la hatia, bila kubaki na shaka yenye msingi inayotokana na rekodi ya shauri. Hapa kuna tofauti muhimu ambayo mara nyingi hueleweka vibaya, kwamba beyond reasonable doubt haimaanishi kutokuwepo kwa kila shaka inayoweza kufikiriwa. Sheria haitaki uhakika wa kihisabati, wala haidai Jamhuri ijibu kila nadharia ya kubuniwa. Lakini inachotaka ni kuondoa reasonable doubt shaka inayotokana na ushahidi, mantiki na mazingira halisi ya shauri. Shaka ya kubahatisha haina nguvu ya kisheria, lakini shaka inayotokana na contradiction ya msingi, pengo la ushahidi, kutokuthibitishwa kwa ingredient au ushahidi usioaminika haiwezi kufutwa kwa maelezo ya jumla. Katika kesi ya Lissu, kipimo hiki kinahitaji Mahakama kuchunguza kwa umakini mens rea yaani nia mahsusi inayodaiwa, actus reus yaani kitendo kinachounda kosa, tafsiri ya deed chini ya kifungu cha 39(2)(d). Attribution ya vitendo vinavyodaiwa na publication ya maneno kupitia Jambo TV. Haya ni maeneo tofauti ya kisheria yanayohitaji uthibitisho. Kwamba maneno yalitamkwa hakuthibitishi moja kwa moja nia ya uhaini, kwamba video ilisambazwa hakuthibitishi moja kwa moja nani aliyeichapisha. Na kwamba mkutano ulifanyika hakuthibitishi moja kwa moja kwamba ulikuwa na madhumuni ya kutenda kosa la uhaini. Hapo ndipo evidentiary nexus inapokuwa muhimu, yaani Mahakama inapaswa kuona uhusiano wa kimantiki na wa kisheria kati ya ushahidi uliowasilishwa na kila kipengele cha kosa. Haiwezi kuruka kutoka kwenye mazingira yanayotia shaka hadi kwenye hitimisho la hatia bila kuonyesha namna ushahidi unavyothibitisha kiungo hicho.
3
18
82
9,294
Katika ushahidi wa mazingira, chain of inference inapaswa kuwa thabiti, yaani ikiwa kuna pengo muhimu linaloacha maelezo mengine yenye msingi, Mahakama inapaswa kulichunguza badala ya kulifunika kwa dhana. Vilevile cumulative assessment of evidence haimaanishi kukusanya mashahidi wengi na kuhitimisha kwamba shtaka limethibitishwa. Inamaanisha kupima ushahidi wote kwa pamoja, huku kila kipande kikipewa uzito unaostahili kulingana na chanzo chake, uthabiti wake, uaminifu wa shahidi na uwezo wake wa kuthibitisha jambo husika. Credibility ya shahidi na probative value ya maelezo yake ni mambo yanayohusiana, lakini sio kitu kimoja. Shahidi anaweza kuwa na uwezo wa kutoa ushahidi, lakini Mahakama bado ikahitaji kuchunguza kama ushahidi wake unaaminika na una uzito wa kuthibitisha ingredient inayobishaniwa. Na hapa ndipo material contradictions zinapopata umuhimu, kwamba sio kila tofauti ya maelezo inavunja kesi. Lakini tofauti inayogusa utambulisho wa mtendaji, namna kitendo kilivyofanyika, chanzo cha taarifa au uhusiano wa mshtakiwa na tukio haiwezi kuchukuliwa kama kasoro ndogo bila uchambuzi. Mahakama inapaswa kujiuliza, tofauti hiyo inaathiri nini? Inadhoofisha reliability ya ushahidi kwa kiwango gani? Haya ndio maswali yanayofanya tathmini ya ushahidi kuwa kazi ya kimahakama, sio zoezi la kuhesabu mashahidi. Lakini kuna kanuni nyingine ambayo ni moyo wa haki ya jinai, kwamba the burden of proof never shifts to the accused. Lissu hana wajibu wa kuthibitisha kutokuwa na hatia. Hata kama utetezi haujajibu kila hoja ya Jamhuri, au kama ushahidi wa upande wa utetezi una mapungufu, hilo haliwezi kujaza mapengo ya mashtaka. Mahakama haiwezi kutoa conviction kwa sababu maelezo ya mshtakiwa hayajaridhisha pekee, ila lazima iridhike kwamba ushahidi wa mashtaka wenyewe umetimiza kiwango cha uthibitisho kinachotakiwa. Hii ndio maana ya presumption of innocence, yaani sio kauli ya mapambo katika vitabu vya sheria, bali ni kinga ya kikatiba na ya kimahakama inayomzuia mtu kuhukumiwa kwa tuhuma, hisia, shinikizo la umma au tafsiri isiyothibitishwa. Kadiri shtaka linavyokuwa zito, ndivyo umuhimu wa Mahakama kuzingatia kwa makini viwango vya uthibitisho na uhalali wa kila ingredient unavyokuwa mkubwa. Na mwisho niseme, kuna ukweli mmoja wa kisheria unaopaswa kubaki wazi, kwamba reasonable doubt sio zawadi anayopewa mshtakiwa, wala sio upendeleo wa Mahakama. Lakini ni matokeo ya kushindwa kwa upande wa mashtaka kuthibitisha kosa kwa kiwango kinachotakiwa na sheria. Ikiwa ushahidi umethibitisha kila ingredient, sheria itoe matokeo yake. Ikiwa shaka yenye msingi imebaki kwenye ingredient muhimu, presumption of innocence lazima ipate maana yake halisi. Kwa sababu katika haki ya jinai, mtu hahukumiwi kwa kile ambacho huenda alikusudia kufanya, wala kwa kile ambacho wengine wanaamini alifanya. Ila anahukumiwa kwa kile ambacho Jamhuri imeweza kuthibitisha kisheria, na hapo ndipo mstari kati ya tuhuma na hatia unapochorwa. Sio kwa hisia, bali kwa ushahidi, sheria na reasonable doubt.
1
6
343
SIKU 1 KABLA YA HUKUMU YA LISU JAMHURI DHIDI YA TUNDU ANTlPAS LISSU, KESI YA JINAI NA. 19605/2025 Kesho ni siku ya hukumu, baada ya miezi ya kusikiliza ushahidi, kuchambua nyaraka, kuhoji mashahidi na kupima hoja za mawakili, safari hii ndefu ya kimahakama inafika kwenye kilele chake. Kwa Tundu Lissu, ni siku inayobeba uzito wa hatima yake. Kwa mfumo wa haki, ni wakati wa kuona namna sheria inavyotumika mbele ya shtaka zito kama uhaini. Lakini kabla ya Mahakama kutoa uamuzi, kuna swali ambalo linapaswa kubaki akilini mwa kila anayefuatilia shauri hili. Je, ushahidi umefikia kiwango cha kuthibitisha hatia, au uzito wa shtaka umeacha nafasi ya mashaka yenye msingi? Katika criminal jurisprudence, sio tuhuma zinazothibitisha kosa, ila ni ushahidi unaokidhi kila kipengele cha kisheria. Burden of proof iko kwa Jamhuri, na kiwango chake ni beyond reasonable doubt. Hii ndio nguzo inayolinda presumption of innocence. Narudia tena mshtakiwa hahitajiki kuthibitisha kutokuwa na hatia, wala Mahakama haiwezi kujaza mapengo ya ushahidi wa mashtaka kwa kutegemea udhaifu wa utetezi. Kwenye kesi hii, macho yako kwenye tafsiri ya kifungu cha 39(2)(d), uthibitisho wa mens rea, uwepo wa actus reus, maana ya deed, pamoja na uhusiano kati ya Lissu na kitendo cha uchapishaji kinachodaiwa. Haya ni masuala ambayo hayawezi kutatuliwa kwa hisia, msimamo wa kisiasa au tafsiri ya maneno nje ya mazingira yake. Yanahitaji strict construction of penal statutes, uchambuzi wa ushahidi na sababu za kimahakama zinazoweza kusimama mbele ya sheria. Pia kuna uzito wa credibility assessment, yaani Mahakama inapaswa kuangalia sio mashahidi walisema nini pekee, Bali walijuaje, walikuwa na nafasi gani ya kujua, maelezo yao yanaendana kwa kiwango gani, na contradictions zilizojitokeza zinaathiri vipi kiini cha shtaka.
8
47
184
8,815
Ushahidi wa mazingira nao unahitaji complete chain of inference, kwamba haiwezekani kuruka kutoka kwenye uwepo wa tukio hadi kwenye dhima ya mshtakiwa bila kuthibitisha uhusiano unaotakiwa kisheria. Lakini kesho, jambo muhimu zaidi halitakuwa kama Lissu atapatikana na hatia au la. Ila litakuwa pia namna Mahakama itakavyofafanua mpaka kati ya freedom of expression na criminal liability. Hotuba ya kisiasa inaweza kuwa kali, yenye ukosoaji mkubwa na hata yenye kuleta mvutano. Lakini, wajibu wa Mahakama ni kuamua kama ushahidi unaonyesha kosa lililofafanuliwa na sheria, na sio kuadhibu kauli kwa sababu tu zimezua mjadala. Na hapa ndipo hisia za kesi hii zinapokutana na ukali wa sheria. Nyuma ya jalada kuna binadamu, familia, wafuasi na jamii inayosubiri majibu. Lakini Mahakama haiwezi kuongozwa na huruma wala shinikizo la umma. Ila inapaswa kuongozwa na sheria na ushahidi. Haki ya kweli haichagui upande, ila inahakikisha kila mtu anapimwa kwa kiwango kilekile cha kisheria. Kesho, kila hoja itakuwa imefikishwa mwisho wake, walaa hakutakuwa tena na shahidi wa kuongeza maelezo, wala wakili wa kuwasilisha hoja mpya. Kutabaki ushahidi uliorekodiwa, sheria inayotumika na tafakari ya Mahakama. Na tunaposubiri, tukumbuke jambo moja muhimu sana, kwamba uhaini ni shtaka zito, lakini uzito wa shtaka hauwezi kuwa mbadala wa uthibitisho. Ikiwa kila ingredient imethibitishwa, sheria itumike, na ikiwa shaka yenye msingi inabaki kwenye kipengele muhimu, sheria hiyo hiyo inapaswa kulinda presumption of innocence. Kesho sio siku ya kelele, ila ni siku ya sababu za kimahakama. Sio siku ya hisia kushinda ushahidi, ila ni siku ya ushahidi kupimwa kwa sheria. Na kwa mtu anayesubiri hatima yake, tofauti kati ya tuhuma na uthibitisho sio tofauti ya maneno pekee, ila ni tofauti inayoweza kubeba maisha yake yote. KESHO, MAHAKAMA ITAZUNGUMZA. NA TUNACHOTARAJIA SI TU KUSIKIA UAMUZI, BALI KUELEWA SABABU ZA KISHERIA ZILIZOUFIKISHA HAPO.
1
7
388