Tesha retweeted
Kuna Muda unaona kama Mungu anachelewa kujibu sana,
Ndugu zetu waliuliwa kinyama sana, Mungu uliona ila upo kimya,
Leo mtu aliye tuhumiwa kwa kosa fulani, kakutwa hana hatia hapo hapo kabambikiziwa kosa na kifungo juu,
Na hili utakaa kimya MUNGU?
Tunaomba utujibu, SSH AFE.
Tesha retweeted
Hela ya faini ya TAL mnayo nyinyi @sportybettz mme freez account yangu kwa sababu ya kupuna 33m??? Fungueni account yangu ukuma sipendelei kwenye mambo ya fedha 😡
Tesha retweeted
Aliyevujisha taarifa za kufungwa miaka mitano ni nani basi mahakama yetu haipo huru mamae free Tundu Lissu
Tesha retweeted
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 496
Upande wa mashtaka walieleza kuwa kauli ya mshtakiwa inatakuwa itazamwe katika muktadha mzima kuwa aliitishia serikali na kuwa mshtakiwa alikuwa na lengo la kuitisha serikali regardless kama serikali ilitishika au la!
Ushahidi wa upande wa utetezi mshtakiwa alisema maneno hayo lazima yapimwe katika muktadha wa kisiasa na lengo kwa kauli hiyo ilikuwa ni kueleza msimamo wa kisiasa wa Chadema na lengo lake halikuwa kuitishia Serikali, mtazamo huu ulingwa mkono na shahidi wa 2,3,4 na 5 kuwa kauli ya No reforms, No election ililenga kueleza ushawishi wa kisiasa.
Upande wa utetezi ulisema neno uasi lazima nilitazamwe katika muktadha wa kisiasa na kauli hiyo haikuwa na lengo la kuitishia Serikali au kuchochea vurugu.
Mshtakiwa alieleza kuwa upande wa mashtaka walipaswa kuthibitisha nia hiyo kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia serikali na sio hisia tu. Mshtakiwa alieleza kuwa upande wa mashtaka walishindwa kuthibitisha
Kwa ushahidi uliotolewa kuna mambo ambayo hayabishaniwi, kwanza Chadema imekuwa inatetea mabadiliko ya kikatiba, na mfumo wa uchaguzi na msimamo wa No reforms, No election, kupitia mkutano huo wa 3/4/2025 mshtakiwa alitoa hayo maneno mbele ya viongozi wenzake, wanachama, watia nia na waandishi wa habari na mkutano huo ulirushwa live.
Upande wa utetezi wamemaintain kuwa kauli hiyo ni ya kisiasa ililenga umma to boycott uchaguzi na sio kuitishia serikali.
Tumeangalia kauli zilizotolewa na mshtakiwa na tumeona kuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja hatujaona kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia Serikali, tumeangalia tafsiri ya shahidi wa 1,2 na 16 tumeona ni assumption haziwezi kuthibitisha kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia Serikali.
Tumeona kwamba ushahidi uliotolewa na mashtaka una fall short kuthibitisha shitaka la uhaini hivyo katika kiini hiki cha pili tunaona ushahidi haujakidhi kuonyesha nia ya uhaini.
Kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) kuna vitu vitatu ikiwemo factuai issues, mahakama lazima iangalie ushahidi kujiridhisha na tatu ni ushahidi uoi umetolewa.
Mahakama inaona kwamba tafsiri ya maneno ya Lissu bila tangible evidence tumeongozwa na kanuni kwamba nia (mens rea) ni internal state of mind lazima liambatane na ushahidi wa kimazingira na vitendo vya kufanya uhaini.
Nia ovu siku zote inakuwa inferred kutoka kwa maneno na matendo ya mshtakiwa.
Part 497 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
Tesha retweeted
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 495
Suala la uhalali wa hati ya mashtaka liliwahi kulalamikiwa mwanzoni mwa shauri hili na Mshtakiwa na katika uamuzi wake wa Sept 2025 ilieleza kuwa hati ya mashtaka ilikuwa sahihi.
Mshtakiwa alisema kuwa Kifungu cha 39(2)(d) kinahitaji kushawishi kikundi cha watu na sio umma kama ilivyoandikwa hivyo alisema hati hiyo inakinzana na Ibara ya 13 ya Katiba ya Tanzania inayohusu uhalali wa kisheria (principal of legality)
Katika pingamizi la pili alisema upande wa mashtaka haukueleza taasisi ya serikali ambayo anadaiwa kuitishia na katika hoja ya tatu mshtakiwa alisema haijasema nia au lengo la kufanya huo uhaini kwasababu pia maneno ambayo hayajatumika katika sheria hivyo alisema mahakama ione hati ina mapungufu
Upande wa mashtaka walikiri kuwa ni kweli hati ya mashtaka imetumia neno public lakini tafsiri ya neno public kinajumuisha mtu yeyote au kikundi cha watu hivyo walikidhi matakwa ya sheria, katika hoja ya pili walisema hati ya mashtaka imetumia neno executive.
Upande wa mashtaka walieleza kuwa majukumu ya Executive ni kutekeleza sheria hivyo mshtakiwa alikuwa anaelewa maana ya neno Serikali na hivyo aliweza kuelewa na kutoa utetezi wake.
Mahakama inaona kwamba mapingamizi ya mshtakiwa kuhusu hati ya mashtaka hayana mashiko kwasababu ilishatolea uamuzi huko nyuma na inamaelezo ya kutosha.
Neno public katika tafsiri ya kifungu cha 5 cha Kanuni ya Adhabu kinazumzia mtu yeyote au kikundi cha watu, tumeangalia pia kwa umakini ushahidi na utetezi hivyo mshtakiwa alielewa hati ya mashtaka.
Maelezo katika hati ya mashtaka yanajitisheleza kabisa na kwa mujibu wa shauri la Nasibu Mahakama inatakiwa kutumia neno kama lilivyo hivyo neno executive linaeleweka kama lilivyotajwa kwenye hati ya mashtaka.
Katika hoja ya tatu tunakubaliana kuwa upande wa mashtaka lazima waeleze nia mahususi kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d), hivyo tunaona kwamba mapingamizi yote hayana mashiko kwasababu tulishayatolea uamuzi.
Kinachofuata sasa ni kuangalia viini vitatu, viini hivyo ni-;
1. Endapo mshtakiwa yuko chini ya utii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d).
Ni jukumu la upande wa mashitaka kuthibitisha hili, pande zote mbili wanakubaliana kwamba 3/4/2025 mshtakiwa alikuwa chini ya utii wa JMT.
Hata katika usikilizwaji wa hoja za awali mshtakiwa alikubali kuwa alikuwa na utii wa JMT ni mzaliwa wa Tanzania, ana pasipoti ya Tanzania na 3/4/2025 alitoa maneno hayo akiwa ndani ya JMT, Mahakama inaona kwamba mshtakiwa alikuwa na utii wa JMT.
2. Kiini cha pili ni endapo mshtakiwa alitenegeneza nia ya kuhamasisha umma kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025 kwa lengo la kuitishia serikali kinyume na kifungu cha 39(2)(d).
Upande wa mashataka wana wajibu wa kuthibitisha nia hiyo tofauti na political criticism, nia ni internal state of mind na lazima kifafanuliwe na ushahidi, matendo ya mshtakiwa.
Upande wa mashtaka waliegemea kwenye hoja kwamba 3/4/2025 mshtakiwa alisema tutazuia uchaguzi, tutahamasisha uasi, tutauvuruga uchaguzi, upande wa mashtaka waliegemea kuwa mshtakiwa alikuwa na nia ya kuitishia Serikali na waliegemea kwa upande wa ushahidi wa mashahidi wao kuwa mshtakiwa ni mtu mwenye ushawishi ndani na nje ya Tanzania.
Upande wa Jamhuri waliegemea upande wa ushahidi wa shahidi wa kwanza ambaye aliona maneno hayo yanaviashiriia vya uhaini.
Shahidi alieleza kuwa mshtakiwa kutoa maneno hayo mbele ya waandishi wa habari na kusambazwa maneno hayo, mshtakiwa alikusudia kuitishia serikali.
Shahidi wa 16 upande wa mashtaka alieleza kuwa alipoona hayo maneno walipanga kuwapiga mawe wapiga kura, shahidi wa 17 alisema alikuwepo kwenye mkutano na kuwa ulirushwa live kwenye mitandao ya kijamii, alisena maneno aliyotamka Lissu hakuona kama yanashida yoyote ile.
Part 496 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
Tesha retweeted
MUNGU ULIETENDA KWA PAUL NA SILA GEREZANI TENDA NA KWA✌️TUNDU A.LISSU ........na wote tuseme Amina 🙏 #FREEDOM_FIGHTER
Tesha retweeted
Moyo wangu umejiandaa KUUMIZWA na hii hukumu, ikitokea itanifurahisha basi NITAFURAHI kweli kweli.
ON GOD🙏
Tesha retweeted
Tomorrow, Tanzania’s opposition leader and IDU Executive Vice Chair Tundu Lissu could be convicted of treason, a capital charge, for demanding free elections. Calling for reform is not treason. A conviction would criminalise dissent and silence Tanzania’s opposition Read more here: idu.org/idu-statement-ahead-… #FreeTunduLissuNow 🇹🇿
Tesha retweeted
WEEKEND WINNING TEAMS ❣️✅️
🎉 Arsenal FC To Win
🎉 Real Madrid To Win
🎉 Bayern Munich To Win
🎉 Manchester City To Win
🎉 PSG to Win
🎉 PSV To win
🎉 Sporting CP To win
🎉 Benfica To Win
🎉 Porto To Win
🎉 Rapid Wien To Win
🎉 Olympiacos To Win
🎉 Club Brugge To Win
🎉 Mersaille To Win
🎉 FC Noah To Win
🎉 Slavia Praha To win
🎉 Union SG To win
🎉 Atletico Madrid To win
🎉 Bodo Glimt To win
🎉 Viking To win
🎉 Molde To win
🎉 Paok To win
🎉 Apollon L To win
🎉 Zenit To Win
Tesha retweeted
Kuna kila dalili MAAMUZI ya mahakama kesho juu ya MHE Lissu lengo lake kubwa ni kutukatisha TAMAA wanachadema na wapenzi wa HAKI.
Kinachotakiwa ni nini ndugu zangu?
Tayari MHE Lissu katuambia hana shida na mateso ambayo WAKOLONI WEUSI wataendelea kumpa, sisi wafuasi wake tunatakiwa kubaki imara kutokumuangusha kwenye msimamo wake wa kudai haki.
Ni ukweli usiofichika kuwa LISSU hana kosa, ila wanafanya haya yote kwasababu ya misimamo yake ya kisiasa na kupigania haki kwenye hili taifa.
Hatuhitaji kuumia na maamuzi ya kesho zaidi ya kuendelea kukaza maana tupo mwisho.
Tesha retweeted
Mwenyekiti Tundu Lissu.
Wewe ni mtu mwema sana, Mzalendo unaeipenda Nchi yetu na watu wake kuliko hata unavyojipenda mwenyewe.
Umetoa maisha yako na umepitia matatizo na maumivu makubwa sana kwaajili ya watu wa Nchi hii.
Umedai maisha bora, ajira, maji, umeme maendeleo na matibabu bora kwa Watanzania wote.
Umedai rasilimali nyingi za Nchi hii zitumike kwaajili ya manufaa ya Watanzania wote ambao wanateswa na umasikini mkubwa wa makusudi, unaosababishwa na ccm.
Kwasababu hiyo serikali hiii ya CCM chini ya utawala huu huu walijaribu kukuua wakakupiga risasi 36 Mungu mkuu akakuokoa.
Leo watu hao hao waliojaribu kukuua wakashindwa wanataka kukufunga kwa uongo na kesi ya kubumba.
Wanaweza kufanya hivyo kwasababu mahakama ni zao na wanaweza kuzielekeza nini cha kufanya.
Kitu ambacho hawatafanikiwa ni kushinda kwa kutumia uovu na mauaji yao, kwa hakika hilo watalipia wao na familia zao.
Naomba Watanzania wote tumuombee Mwenyekiti
Tuombee Chama chetu
Tuombee Nchi yetu na demokrasia tunayoipigania.
Tutashinda.
Tesha retweeted
Mwezi wa 4 mwaka 2025. Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam.
Bwana Jumanne Muliro aliongea na vyombo vya habari, akaeleza kwamba ana taarifa ya watu kwenda mahakamani Kisutu kuhudhuria kesi ya Mwenyekiti wetu Tundu Lissu na kwamba watu hao wamejipanga kufanya fujo mahakamani na kusababisha mahakama ishindwe kufanya kazi yake.
Tarehe 24/4/2025 wakati wa kesi.
Polisi walizingira Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, wakakamata watu wengi kwa mamia.
Watu wakapigwa, wakavunjwa miguu, wengine mikono na viungo mbalimbali vya miili yao.
Wengine wakafunguliwa Mbwa wa polisi kama ambavyo makaburu wazungu walifanya dhidi ya Waafrika weusi kule Afrika kusini au Marekani.
Siku hiyo watu wengine wakauwawa.
Watu Kama Boniphace Mwangi na Agatha Atuhaire wa Uganda wakafanyiwa matendo ya kinyama kabisa na kutupwa maporini.
Viongozi wetu kadhaa akiwemo Makamu Zanzibar walitupwa kwenye misitu nje ya Dar baada ya kupigwa na kufanyiwa unyama wote.
Mimi binafsi nilishikiliwa na kujaribu kupelekwa porini,mpaka wasaidizi wangu waliposhikilia usukani wa gari ya polisi na kupata upenyo wa kukimbia kutoa taarifa kuhusu mimi kushikiliwa
Mpaka sasa hakuna polisi hata mmoja alikamatwa na kushitakiwa kwa unyama ule dhidi ya binadamu.
Leo Mwaka mmoja na miezi sita baadae Muliro anatoa kauli kama hiyo hiyo bila uthibitisho wowote wakati wa kwenda kusikiliza hukumu ya kesi ya Mwenyekiti.
Mwenyekiti Lissu ni kiongozi wa Chama ana watu wengi, hakuna mtu anaepanga kufanya fujo yoyote hata kama tunajua uovu wanaopanga kufanya kesho kutwa.
Watu wanataka kuhudhuria na kusikiliza kesi ya kiongozi wao na kiongozi mkubwa wa kisiasa Nchini.. kauli za Muliro ni tishio na mipango ya kutaka kuumiza watu..
Bwana Muliro zama hizi za internet kila unachosema kinabaki na kuna siku watu watauliza na mtatakiwa kutoa majibu.
Acheni kutishia watu walindeni waje wasikilize kesi ya kiongozi wao.
Tesha retweeted
Tumezika Picha youtu.be/_95d_3UxM6U?is=88gt… via @YouTube
Tesha retweeted
Wanachama na viongozi wa CHADEMA usiku huu wakishiriki tukio la kumbukizi ya mwaka mmoja wa mauaji ya Oktoba 29, 2025, lililoandaliwa na Chama katika Makao Makuu ya CHADEMA, Edwin Mtei House.
Tesha retweeted
Happy Birthday mwanangu🎊
Ukiwa na mwaka 1 tu, Baba yako nilikuwa ktk kipindi kigumu cha kesi, mateso na kifungo. Nilitamani kuwa karibu nawe, ila mazingira hayakuruhusu. Leo,Mungu amenivusha na kunipa nafasi ya kukuona ukikua
Mungu akulinde na akupe maisha marefu yenye kusudi.






























