Christian Bwaya retweeted
Big Ben anaeleza kuwa mojawapo ya sifa kubwa za Mwalimu Julius Nyerere ilikuwa uwezo wake wa kusikiliza. Kwa mujibu wa Benjamin Mkapa, Nyerere alikuwa tayari kusikiliza hata kile ambacho wengine wangeweza kukiona kama “upuuzi” — na muhimu zaidi, alikusikiliza hadi mwisho bila kukukatiza.
Katika kitabu cha wasifu wa Nyerere (Biography of Nyerere, Vol. 1), mwandishi Saida Yahya anaeleza kuwa mama yake Nyerere, Mama Mgaya, alikuwa na mchango mkubwa katika kumjenga Mwalimu kuwa msikilizaji mzuri badala ya kuwa mtu wa kuzungumza zaidi.
Yahya anasimulia tukio moja ambapo Nyerere alikuwa nyumbani kwake pamoja na viongozi wenzake waliomtembelea. Mama Mgaya aliwakaribisha na kuwaacha waendelee na mazungumzo yao. Hata hivyo, baada ya muda mrefu, sauti iliyotawala mazungumzo ilikuwa ya Nyerere pekee.
Mama yake alipoona hivyo, alimwendea na kumwambia: “Unaongea sana na huwapi watu wengine nafasi ya kuzungumza.” Alimweleza kwa lugha yao ya nyumbani, Kizanaki. Nyerere akawaeleza wageni wake alichosema mama yake, ndipo mmoja wao, Said Maswanya, akamuunga mkono kwa kusema: “Lakini mama yuko sahihi!”
Huenda tukio hili lilikuwa miongoni mwa masomo yaliyomsaidia Nyerere kutambua kuwa mawasiliano bora si kuzungumza tu, bali pia kuwapa wengine nafasi ya kutosha ya kueleza mawazo yao bila kukatizwa.
Lakini mchango wa Mama Mgaya haukuishia hapo. Yahya anaeleza pia jinsi alivyokuwa na ushawishi katika namna Nyerere alivyovaa.
Baada ya uhuru, Nyerere alikuwa akienda kuhutubia mikutano ya hadhara akiwa amevaa suti na tai maridadi. Siku moja, alipokuwa akijiandaa kwenda kwenye mkutano, mama yake alimwangalia na kumuuliza:
“Wewe mtoto, umevaa umependeza hivyo unaenda kuoa wapi?”
Ingawa Nyerere hakurudi kubadilisha nguo siku hiyo, inasemekana kuanzia hapo alianza kuvaa zile suti zake maarufu za Kaunda, zisizokuwa na kola — mavazi ambayo baadaye yalihusishwa sana na utambulisho wake.
Funzo kubwa hapa ni kwamba ushawishi wa mzazi katika kumjenga mtoto unaweza kuwa mkubwa kuliko tunavyodhani. Mama Mgaya hakumlea tu Nyerere; alichangia pia kujenga baadhi ya sifa zilizomfanya akumbukwe kama kiongozi.
Wakati mwingine, mtoto hahitaji hotuba ndefu kutoka kwa mzazi wake. Anahitaji mtu mwenye ujasiri wa kumwambia ukweli, hata pale anapokuwa mtu mkubwa na mwenye mamlaka.
Wazazi wana nguvu ya kuathiri namna watoto wao wanavyofikiri, wanavyowasiliana na hata wanavyoongoza. Na pengine, moja ya zawadi kubwa zaidi ambayo mzazi anaweza kumpa mtoto wake ni kumfundisha kusikiliza kabla ya kuzungumza.
@bwaya @MkukiNaNyota @Udadisi @MabalaMakengeza
Si kila mtu wa jinsia tofauti anayekusogelea huwa ana njaa ya kupendwa kimwili apate utoshelevu wa kimwili. Kuna watu ukitaka kuharibu na kuwachosha endekeza mazungumzo mepesi-mepesi yenye mwelekeo wa kuwatamani kimwili. Hawa, aghalabu, ni watu wenye mahaba makubwa na kujifunza mambo mapya.
Kinachoimarisha ukaribu wenu si msisimko wa kimwili kama ulivyozoea bali msisimko wa kiakili unaotokana na uwezo wa kubadilishana maarifa na uzoefu. Ukiweza kuidodosa misimamo yake na kuchokoza fikra zake kwa staha kwa kuuliza maswali sahihi na kumshirikisha uzoefu bila kumfanya ajione mjinga, mnakuwa marafiki mlioshibana sana. Mahaba yenu yanajengwa kwenye ukuaji wa kiakili.
Hili kwa hakika si kwa urafiki wa kawaida peke yake bali hata uhusiano wa kimapenzi. Kama tulivyoona awali, hata mapenzi hayajengwi na mvuto na utoshelevu wa tamaa za mwili. Ukiwa aina ya mtu unayeweza kusisimua akili ya mpenzi wako na kuichokoza kufikiri tofauti bila kumvunjia heshima unaimarisha ukaribu wenu kwa kiasi kikubwa—kuliko hata mtu anayetumia muda mwingi kujifunza ufundi wa ngono.
Christian Bwaya retweeted
Kinachokufanya uwe karibu zaidi na mtu (intimacy) sio ngono. Unaweza kulala na mtu kila siku na bado ujisikie ukaribu wowote. Ngono isiyoanza na kufahamiana inaweza kabisa kuzidisha upweke na hata kuharibu uhusiano wenu.
Ukaribu, kwa kawaida, unabebwa na kina cha kufahamiana na mtu unayeamini anakuelewa na hata anaposhindwa kukuelewa bado ana utayari wa kuheshimu mtazamo wako. Kufahamiana na mtu kunaanza na imani kuwa uliyenaye ni mtu salama, mtu unayeamini unaweza kumwambia mapungufu yako, mapito yako, siri zako, na hata majeraha uliyowahi kupitia na bado akaendelea kukuheshimu na kukustahi.
Unapokuwa na mtu mwenye tabia zinazokufanya uamini unamjua vizuri, anachokisema ndicho anachomaanisha, unachokiona usoni ndicho kinachozungumza moyoni mwake, anachokuambia ndio ukweli wenyewe, huo sasa ndio unaitwa upendo.
Christian Bwaya retweeted
Ukiweza kutofautisha hisia za ngono na mapenzi uwezekano wa mahusiano unayoyaanzisha kudumu unakuwa mkubwa. Hisia za ngono, tamaa, ni msukumo wa kimwili unaowachochea wanyama kuzaliana. Nzi, pamoja na udogo wake anazo hisia hizi—sexual instincts—ingawa hana mapenzi.
Hisia za ngono (tamaa) zikiwa kipaumbele chako, vigumu kuwekeza kwenye mahusiano yanayokutanisha fikra na kuruhusu mikinzano ya mawazo kujenga utambulisho wa pamoja—intimacy. Ukaribu wako na mtu, aghalabu, utalenga kukutanisha miili kuliko fikra, imani na mambo yanayowatambulisha (identities). Utavutiwa na mwonekano, utamtamani, ukifanikiwa kukidhi tamaa za mwili hisia hizo zitapoa. Usipozimudu hisia hizi, kama ilivyo kwa nzi, unaweza kucheza na wengi kwa mpigo—maana huwapendi.
Mapenzi, tofauti na hisia za ngono, ndizo zinatutofautisha na wanyama wengine. Ukimpenda mtu unahamia kwenye fikra, imani na misimamo yenu. Upendo unakuchochea kuweka mazingira ya kumwamini, kumfanya kuwa sehemu ya faragha yako, na hivyo unampandisha ngazi ya kumruhusu kukufahamu, kuyafahamu matumaini yako, kuzijua aibu zako. Upendo unakuchochea kujitoa ili kumheshimu, kumstahi na kumfanya kuwa sehemu ya maisha yako.
Ukaribu wa kiwango hiki ndio unaochochea muunganiko wa utambulisho wenu (identity) ili kuufanya kuwa mmoja. Huo ndio upendo unaodumu, kwa mujibu wa mshunuzi Sternberg. Ingawa uwezo huu anao mwanadamu, ukishakosa upendo wa mzazi utotoni, inaweza kukuwia vigumu mno kumpenda mtu mwingine au hata kumruhusu mtu mwingine akupende kwa kiwango hiki. Katika mazingira kama haya, watu wengi huishia kwenye hisia za ngono, na uwezekano wa ajali nyingi za mahusiano unakuwa mkubwa zaidi.
Mchoro: Akili Ige (AI)
Christian Bwaya retweeted
Hatuponi kwa kuukana ukweli.
Hatuponi kwa kuikimbia historia.
Hatuponi kwa kujiaminisha haikutokea.
Hatuponi kwa kujisahaulisha maumivu.
Hatuponi kwa kujifanya tumepona.
Hatuponi kwa kuigiza furaha isiyokuwepo.
Hatuponi kwa kuwalaumu wengine.
Hatuponi kwa kuuzoea upweke.
Hatuponi kwa kujitenga.
Hatuponi kwa kuigiza hatumhitaji mtu.
Hatuponi kwa kulipiza kisasi.
Hatuponi kwa kuwaumiza waliotuumiza.
Hatuponi kwa kuwachukia waliotuumiza.
Hatuponi kwa kushuhudia mateso ya wabaya wetu.
Tunapona tukiacha kujidanganya.
Tunapona tukiukubali ukweli.
Tunapona tukiaminiwa tena.
Tunapona tukisikika tena.
Tunapona tukionekana tena.
Tunapona tukithaminika tena.
Tunapona tukijisikia kueleweka.
Tunapona tukijisikia ni salama kuwa sisi.
Tunapona tukiachilia ubaya.
Tunapona tujisamehe kwa kukosea.
Tunapona tukiwasamehe waliotukosea.
Tunapona tukiweza kumwamini mtu tena.
Tunapona tukijisikia kupendwa.
Tunapona tukiamini kuna mtu anasikiliza.
Tunapona tukiamini kuna mtu anaelewa.
Tunapona tukiamini tunauishi ukweli na hatujidanganyi tena.
Christian Bwaya retweeted
Uhusiano na mtu unaweza kuanza na mvuto mkubwa wa mapenzi lakini unadumishwa na vitu vingine. Ukitegemea uhusiano wako ushikiliwe na mvuto wa mapenzi na ufundi wa ngono, Steinberg aligundua ni vigumu mno kufika mbali na mtu na kujenga uhusiano wenye utoshelevu. Unaweza kuwa na mtu anayekuvutia sana kimwili lakini msipowekeza kwenye nguzo muhimu za uhusiano inaweza kuwasumbua kushughulikia migogoro bila kuacha majeraha makubwa.
Steinberg anataja nguzo kuu zinazoshikilia uhusiano wa kimapenzi wenye sifa za kufika mbali kuwa ni 1) kufahamiana kwa kina na mtu anayekuvutia na 2) kutumia kipindi cha mwanzo wa uhusiano kuwekeza. Tafsiri yake ni kwamba usiishie kuvutiwa na mtu. Mvuto hauna nguvu ya kuwapeleka mahali na kuwaandaa kukabiliana na dhoruba. Uhusiano unadumishwa kwa juhudi za makusudi zinazolenga kumfahamu mtu kupitia mazungumzo ya kina yanayokusaidia kujua mambo ya msingi kumhusu mwenzako—anafikiri nini, anaamini nini, anayatazamaje maisha, anaelekea wapi, analea uwezo upi, anauguza nini na kadhalika.
Kisha nenda hatua ya pili. Mazungumzo hayana maana ikiwa yanabaki kuwa maneno na ahadi tupu. Uwekezaji unaodumisha uhusiano ni ule utayari wako wa kuchukua hatua na kufanya kile unachojua mwenzako anakihitaji na kuacha kufanya kile unachojua kinamsumbua mwenzako. Hili ndio gumu zaidi maana linakulazimisha kuushinda ubinafsi wako na kwa hakika linachokoza utaratibu wako wa kawaida wa maisha. Ukiweza kukimeza kiburi chako ukalipa gharama ya kubadilika, Steinberg anasema ‘unawekeza’ kwa sababu hufanyi kukidhi tamaa zako za muda mfupi bali kudumisha uhusiano na mtu unayemfahamu vizuri.
Ukiangalia mchoro huu uliobuniwa na mshunuzi Steinberg unaona hatari kubwa ya wapenzi kuwekeza kwenye mvuto wa mapenzi usioenda sambamba na juhudi ya kufahamiana (intimacy). Kufahamiana kunaimarisha kuaminiana na kisha huongeza uwekezaji. Mvuto wa mapenzi, Steinberg anasema, haudumu. Utajiweka kwenye mwonekano mzuri na kujifunza staili zote za ngono lakini bila kuwekeza kwenye kuunganisha fikra na mtazamo wenu, ni suala la muda tu ‘grafu’ itawarudusha panapostahili na mtaanza kutafuta sababu za kuachana.
Mchoro: Akili Ige (AI)
Christian Bwaya retweeted
Upendo ni ‘chakula bora’ cha nafsi. Ukikikosa chakula hicho unakaukiwa. Uso unakosa nuru katikati ya wingi wa vipodozi, unajisikia mpweke katikati ya watu, mnyonge katikati ya mafanikio, mkali kwa vitu visivyohitaji hasira, mshindani kwa wasioshindana, na kuwa mbabe kwa wasio na madhara na katili hata kwa walio wema.
Huupati upendo kwa wingi wa watu unaokutana na kufahamiana nao. Upendo unaupata kwa mtu mmoja anayekupokea vile ulivyo, anakupa uhakika kuwa unaaminika, unasikika, unaeleweka, na kukuhakikishia kuwa unaweza kuwa wewe na bado ukawa salama bila shinikizo la kubadilika kukidhi orodha ya matarajio yanayozidi uhalisia wako.
Je, nafsi yako ina uhakika wa ‘chakula bora’? Je, unadhani una uwezo wa kumpatia rafiki yako ‘chakula kilicho bora’ au unamtumia kupunguza hali ya nafsi kukaukiwa?

Sababu wanawake kuongezeka vyuoni
mwananchi.co.tz/mw/habari/ma…
Uhusiano na mtu unaweza kuanza na mvuto mkubwa wa mapenzi lakini unadumishwa na vitu vingine. Ukitegemea uhusiano wako ushikiliwe na mvuto wa mapenzi na ufundi wa ngono, Steinberg aligundua ni vigumu mno kufika mbali na mtu na kujenga uhusiano wenye utoshelevu. Unaweza kuwa na mtu anayekuvutia sana kimwili lakini msipowekeza kwenye nguzo muhimu za uhusiano inaweza kuwasumbua kushughulikia migogoro bila kuacha majeraha makubwa.
Steinberg anataja nguzo kuu zinazoshikilia uhusiano wa kimapenzi wenye sifa za kufika mbali kuwa ni 1) kufahamiana kwa kina na mtu anayekuvutia na 2) kutumia kipindi cha mwanzo wa uhusiano kuwekeza. Tafsiri yake ni kwamba usiishie kuvutiwa na mtu. Mvuto hauna nguvu ya kuwapeleka mahali na kuwaandaa kukabiliana na dhoruba. Uhusiano unadumishwa kwa juhudi za makusudi zinazolenga kumfahamu mtu kupitia mazungumzo ya kina yanayokusaidia kujua mambo ya msingi kumhusu mwenzako—anafikiri nini, anaamini nini, anayatazamaje maisha, anaelekea wapi, analea uwezo upi, anauguza nini na kadhalika.
Kisha nenda hatua ya pili. Mazungumzo hayana maana ikiwa yanabaki kuwa maneno na ahadi tupu. Uwekezaji unaodumisha uhusiano ni ule utayari wako wa kuchukua hatua na kufanya kile unachojua mwenzako anakihitaji na kuacha kufanya kile unachojua kinamsumbua mwenzako. Hili ndio gumu zaidi maana linakulazimisha kuushinda ubinafsi wako na kwa hakika linachokoza utaratibu wako wa kawaida wa maisha. Ukiweza kukimeza kiburi chako ukalipa gharama ya kubadilika, Steinberg anasema ‘unawekeza’ kwa sababu hufanyi kukidhi tamaa zako za muda mfupi bali kudumisha uhusiano na mtu unayemfahamu vizuri.
Ukiangalia mchoro huu uliobuniwa na mshunuzi Steinberg unaona hatari kubwa ya wapenzi kuwekeza kwenye mvuto wa mapenzi usioenda sambamba na juhudi ya kufahamiana (intimacy). Kufahamiana kunaimarisha kuaminiana na kisha huongeza uwekezaji. Mvuto wa mapenzi, Steinberg anasema, haudumu. Utajiweka kwenye mwonekano mzuri na kujifunza staili zote za ngono lakini bila kuwekeza kwenye kuunganisha fikra na mtazamo wenu, ni suala la muda tu ‘grafu’ itawarudusha panapostahili na mtaanza kutafuta sababu za kuachana.
Mchoro: Akili Ige (AI)
Christian Bwaya retweeted
Usiku huu mimi na wapenzi wenzangu astronomia wa sayansi ya anga (astrophiles), tumetumia muda kuutazama mwezi wa sayari yetu katika anga lisilo na mawingu. Pia tumefanikiwa kuitafuta na kuipata Sayari ya Zohali (Saturn) na kuona pete yake. Uzuri wa maumbo haya, hauachi kushangaza.
Mwezi wa sayari yetu unaitwa *Luna* _(neno la Kilatini likimaanisha Mwanga au Kungaa)_. Luna uko takribani kilometa 384,000 kutoka tuliko sisi.
Umbo hili ndilo lenye mwanga angavu zaidi angani wakati wa usiku kuliko yote likifuatiwa na Sayari Zuhura (Venus).
Hata hivyo mwezi wetu, kama ilivyo kwa miezi ya sayari zingine, sio chanzo cha mwanga bali unaakisi mwanga wa jua.
Kwa upande wake, Zohali iko umbali wa kilometa bilioni 1.272 kutoka sayari yetu. Pamoja na pete imezungukwa na miezi 293, mkubwa ukiwa ni Titan _(moja ya miungu wenye nguvu katika mitholojia ya Kigiriki)_.
Titan ni mwezi wa pili kwa ukubwa katika mfumo wetu wa jua, huku Luna ukiwa ni wa tano.
Luna na Zohali ni kati ya maumbo-anga ambayo hayachoshi kuyatazama kiutafiti kutokana na uzuri na uajabu wake.
Christian Bwaya retweeted
Replying to @bwaya
Hapa wajuzi wa Ngono watakuja sisi WENYE ndoa tukae pembeni maana hatukuoa Kwa ajili ya ngono
Hatuponi kwa kuukana ukweli.
Hatuponi kwa kuikimbia historia.
Hatuponi kwa kujiaminisha haikutokea.
Hatuponi kwa kujisahaulisha maumivu.
Hatuponi kwa kujifanya tumepona.
Hatuponi kwa kuigiza furaha isiyokuwepo.
Hatuponi kwa kuwalaumu wengine.
Hatuponi kwa kuuzoea upweke.
Hatuponi kwa kujitenga.
Hatuponi kwa kuigiza hatumhitaji mtu.
Hatuponi kwa kulipiza kisasi.
Hatuponi kwa kuwaumiza waliotuumiza.
Hatuponi kwa kuwachukia waliotuumiza.
Hatuponi kwa kushuhudia mateso ya wabaya wetu.
Tunapona tukiacha kujidanganya.
Tunapona tukiukubali ukweli.
Tunapona tukiaminiwa tena.
Tunapona tukisikika tena.
Tunapona tukionekana tena.
Tunapona tukithaminika tena.
Tunapona tukijisikia kueleweka.
Tunapona tukijisikia ni salama kuwa sisi.
Tunapona tukiachilia ubaya.
Tunapona tujisamehe kwa kukosea.
Tunapona tukiwasamehe waliotukosea.
Tunapona tukiweza kumwamini mtu tena.
Tunapona tukijisikia kupendwa.
Tunapona tukiamini kuna mtu anasikiliza.
Tunapona tukiamini kuna mtu anaelewa.
Tunapona tukiamini tunauishi ukweli na hatujidanganyi tena.
Christian Bwaya retweeted
Watoto wanaproject uhalisia unaokinzana na delusion tuliyojijengea.
Inabidi siku moja tukutane kulijadili hili kwa kina.
Ukiweza kutofautisha hisia za ngono na mapenzi uwezekano wa mahusiano unayoyaanzisha kudumu unakuwa mkubwa. Hisia za ngono, tamaa, ni msukumo wa kimwili unaowachochea wanyama kuzaliana. Nzi, pamoja na udogo wake anazo hisia hizi—sexual instincts—ingawa hana mapenzi.
Hisia za ngono (tamaa) zikiwa kipaumbele chako, vigumu kuwekeza kwenye mahusiano yanayokutanisha fikra na kuruhusu mikinzano ya mawazo kujenga utambulisho wa pamoja—intimacy. Ukaribu wako na mtu, aghalabu, utalenga kukutanisha miili kuliko fikra, imani na mambo yanayowatambulisha (identities). Utavutiwa na mwonekano, utamtamani, ukifanikiwa kukidhi tamaa za mwili hisia hizo zitapoa. Usipozimudu hisia hizi, kama ilivyo kwa nzi, unaweza kucheza na wengi kwa mpigo—maana huwapendi.
Mapenzi, tofauti na hisia za ngono, ndizo zinatutofautisha na wanyama wengine. Ukimpenda mtu unahamia kwenye fikra, imani na misimamo yenu. Upendo unakuchochea kuweka mazingira ya kumwamini, kumfanya kuwa sehemu ya faragha yako, na hivyo unampandisha ngazi ya kumruhusu kukufahamu, kuyafahamu matumaini yako, kuzijua aibu zako. Upendo unakuchochea kujitoa ili kumheshimu, kumstahi na kumfanya kuwa sehemu ya maisha yako.
Ukaribu wa kiwango hiki ndio unaochochea muunganiko wa utambulisho wenu (identity) ili kuufanya kuwa mmoja. Huo ndio upendo unaodumu, kwa mujibu wa mshunuzi Sternberg. Ingawa uwezo huu anao mwanadamu, ukishakosa upendo wa mzazi utotoni, inaweza kukuwia vigumu mno kumpenda mtu mwingine au hata kumruhusu mtu mwingine akupende kwa kiwango hiki. Katika mazingira kama haya, watu wengi huishia kwenye hisia za ngono, na uwezekano wa ajali nyingi za mahusiano unakuwa mkubwa zaidi.
Mchoro: Akili Ige (AI)
Kinachokufanya uwe karibu zaidi na mtu (intimacy) sio ngono. Unaweza kulala na mtu kila siku na bado ujisikie ukaribu wowote. Ngono isiyoanza na kufahamiana inaweza kabisa kuzidisha upweke na hata kuharibu uhusiano wenu.
Ukaribu, kwa kawaida, unabebwa na kina cha kufahamiana na mtu unayeamini anakuelewa na hata anaposhindwa kukuelewa bado ana utayari wa kuheshimu mtazamo wako. Kufahamiana na mtu kunaanza na imani kuwa uliyenaye ni mtu salama, mtu unayeamini unaweza kumwambia mapungufu yako, mapito yako, siri zako, na hata majeraha uliyowahi kupitia na bado akaendelea kukuheshimu na kukustahi.
Unapokuwa na mtu mwenye tabia zinazokufanya uamini unamjua vizuri, anachokisema ndicho anachomaanisha, unachokiona usoni ndicho kinachozungumza moyoni mwake, anachokuambia ndio ukweli wenyewe, huo sasa ndio unaitwa upendo.
Christian Bwaya retweeted
Pale unapolazimika kujitenga na familia ili uwe mtu timamu
mwananchi.co.tz/mw/habari/ma…
Replying to @bwaya
Kuna siku nilikua najithamini binafsi
Nikasema Hivi maisha yangu na mienendo yangu kuna mdada anataka niwe mume wake / au sifa nilizokua nazo na maisha ninayoishi kila siku yanaweza kunifanya Mume / Baba bora
Nikatabasamu nikasema hapa inabidi nijitengeneze sana