
Clinician/ Entrepreneur / Mshauri afya uzazi, na ushauri nasaha. Positive thinker. #Confidenceforselfdevelopment
Tanzania
Joined August 2013
- Tweets12.8K
- Following2.5K
- Followers3.2K
- Likes17.6K
Winnie Prosper retweeted
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 496
Upande wa mashtaka walieleza kuwa kauli ya mshtakiwa inatakuwa itazamwe katika muktadha mzima kuwa aliitishia serikali na kuwa mshtakiwa alikuwa na lengo la kuitisha serikali regardless kama serikali ilitishika au la!
Ushahidi wa upande wa utetezi mshtakiwa alisema maneno hayo lazima yapimwe katika muktadha wa kisiasa na lengo kwa kauli hiyo ilikuwa ni kueleza msimamo wa kisiasa wa Chadema na lengo lake halikuwa kuitishia Serikali, mtazamo huu ulingwa mkono na shahidi wa 2,3,4 na 5 kuwa kauli ya No reforms, No election ililenga kueleza ushawishi wa kisiasa.
Upande wa utetezi ulisema neno uasi lazima nilitazamwe katika muktadha wa kisiasa na kauli hiyo haikuwa na lengo la kuitishia Serikali au kuchochea vurugu.
Mshtakiwa alieleza kuwa upande wa mashtaka walipaswa kuthibitisha nia hiyo kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia serikali na sio hisia tu. Mshtakiwa alieleza kuwa upande wa mashtaka walishindwa kuthibitisha
Kwa ushahidi uliotolewa kuna mambo ambayo hayabishaniwi, kwanza Chadema imekuwa inatetea mabadiliko ya kikatiba, na mfumo wa uchaguzi na msimamo wa No reforms, No election, kupitia mkutano huo wa 3/4/2025 mshtakiwa alitoa hayo maneno mbele ya viongozi wenzake, wanachama, watia nia na waandishi wa habari na mkutano huo ulirushwa live.
Upande wa utetezi wamemaintain kuwa kauli hiyo ni ya kisiasa ililenga umma to boycott uchaguzi na sio kuitishia serikali.
Tumeangalia kauli zilizotolewa na mshtakiwa na tumeona kuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja hatujaona kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia Serikali, tumeangalia tafsiri ya shahidi wa 1,2 na 16 tumeona ni assumption haziwezi kuthibitisha kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia Serikali.
Tumeona kwamba ushahidi uliotolewa na mashtaka una fall short kuthibitisha shitaka la uhaini hivyo katika kiini hiki cha pili tunaona ushahidi haujakidhi kuonyesha nia ya uhaini.
Kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) kuna vitu vitatu ikiwemo factuai issues, mahakama lazima iangalie ushahidi kujiridhisha na tatu ni ushahidi uoi umetolewa.
Mahakama inaona kwamba tafsiri ya maneno ya Lissu bila tangible evidence tumeongozwa na kanuni kwamba nia (mens rea) ni internal state of mind lazima liambatane na ushahidi wa kimazingira na vitendo vya kufanya uhaini.
Nia ovu siku zote inakuwa inferred kutoka kwa maneno na matendo ya mshtakiwa.
Part 497 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
Winnie Prosper retweeted
Hadi watoto, malaika wa Mungu na wajawazito na vichanga tumboni walipigwa risasi na Samia Suluhu October 29 2025……..
Winnie Prosper retweeted
Salamu za faraja kwa wote mliopoteza wapendwa wenu. Nguvu, Upendo na Matumaini viwe nanyi.
Zaidi jamii.app/RmbrncOctDths
#JamiiForums
Winnie Prosper retweeted
Binafsi nafurahi sana wanafunzi wanavyotupostia hizi video.
Nafurahi kwa sababu zinaonesha uhalisia ambao kila mara unapuuzwa kwa nyimbo na mapambio ya watawala.
Kwangu mimi hizi video ni aina ya protest.
Ni kilio cha mamilioni ya wanafunzi waliotelekezwa kwenye mabanda yanayoitwa shule pasipokuwa na uwezo wowote wa kutoa elimu.
Ni ujumbe wa wanafunzi kwa mamlaka na umma kwa ujumla.
Ni barua inayosema “mnavuna mlichokipanda. Ukipanda upuuzi utavuna upuuzi na unapovuna upuuzi usiogope kujivunia mavuno yako.”
Kazi ya shule, among other things, ni kutengeneza character ya mwanafunzi.
Character inajengwa kwa kum-keep busy mtoto na mambo ya msingi, ikiwemo ufundishaji, vitabu, michezo, vilabu vya fani mambalimbali, kazi za mikono, na mengine mengi ya aina hiyo.
Mtoto aliyepo busy kufanya experiments maabara, kujenga kipaji chake kwa kushiriki michezo mbalimbali, kusoma vitabu maktaba, kujihusisha na mashindano mbali mbali ndani na nje ya shule, etc., kamwe hawezi kuwa na muda wa kufanya jambo lolote linaloonekana kuwa la kipuuzi.
Hawezi kwa sababu amefanywa kuwa busy na mambo ya msingi.
Kinyume chake ni sahihi pia. Mtoto anayenyimwa mambo yote haya, ni lazima atafute namna ya kuziba ombwe ikiwemo kwa kufanya mambo ya kipuuzi.
Theory nyepesi ni hii: Mwanafunzi lazima awe busy. Usipomkeep busy na mambo ya msingi na tija, atakuwa kept busy na mambo ya kipumbavu kwa sababu hiyo ni nature yake.
U-busy ndio shule halisi ya mtoto; kinachomkeep busy ndicho kinachomfundisha.
Ni bahati mbaya sana kwamba tuna utamaduni wa kufunika kombe mwanaharamu apite.
Baada ya hizi video kuonekana, ghafla maaskari wa maadili wameingia kazini.
Mara Waziri Gwajima ametoa tamko; Mara Mkuu wa Wilaya amewaita wanafunzi na wazazi na kuwashurutisha kuomba msamaha.
Maelfu ya wanafunzi wa TEMEKE walipopata zero na Div 4 mwaka jana, fasta tukamuona Mkuu wa Mkoa ameita wazazi na walimu na kuanza kulaumu “malezi mabovu.”
Jibu lake? “Tutajenga shule za kijeshi zenye walimu wanajeshi….”
Yani kwa sababu tu una nyundo, basi kila kinachoonekana kwako kinageuka msumari.
Matokeo yake tunafunika kidonda huku tukiamini tumekiponya. Tunaacha tatizo, tunadeal na product ya tatizo.
Uhalisia ni huu: KAMA HATUTOKUBALI KUBADILISHA HAYA MABANDA YA NG’OMBE ILI YAWE SHULE, HAKIKA TUJIANDAE KISAIKOLOJIA.
Niwakumbushe tu kuwa zaidi ya wanafunzi million 3 wanaanza kidato cha kwanza kwa mkupuo January 2028.
Wacha tuendelee kujitekenya na kucheka!!
Winnie Prosper retweeted
Tusambaze huu ujumbe kwa REPOST ZA KUTOSHA labda wakenya watatuelewa.
#FreeTwahaMwaipaya
Winnie Prosper retweeted
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 433
Jaji Ndunguru anawasha kipaza sauti anasema tumesikia hoja za mshtakiwa na Mahakama inatamka kwamba shauri kwa upande wa utetezi limefikia mwisho.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji kwa vile sasa kesi ya pande zote mbili imefungwa tunaomba Mahakama itupangie siku ya kuja kuwasilisha hoja za mwisho.
Sijawasiliana na upande wa mashtaka naomba nipendekeze tarehe yangu ya kuwasilisha hoja za mwisho.
Waheshimiwa Majaji natambua kwamba shauri limepangwa kuisha tarehe 25 September 2026 na mwenendo wa kesi una kurasa zaidi ya 1000, itakuwa kazi kubwa sana lakini naomba mimi kuanzia Jumatano ya tarehe 23 Septemba 2026 nitakuwa tayari kwa ajili ya kufanya final submission.
Jaji Ndunguru: Upande wa mashtaka mnasemaje?
Katuga: Tunaungana na mshtakiwa ila hajasema tufanye kwa maandishi au kwa mdomo.
Kwa tarehe aliyoipendekeza sisi tutajitoa Jumatano hiyo hiyo na sisi tutakuwa tayari kufanya final submission. Waheshimiwa majaji ingawa upande wa utetezi umefunga kesi ila tulikuwa na hamu sana ya kufanya cross kwa mashahidi wa Lissu waliokuwa wamebakia
Watu wanacheka sana, wanamuona Katuga kama kituko😂😂😂😂
Jaji Ndunguru: Hiyo amri mbona mahakama bado haijaitoa?
Tunakubaliana kuwa siku ya Jumatano shauri litakuja kwa ajili ya mawasilisho ya mwisho saa tatu kamili asbuhi
Imepigwa High Coooouuuuurrrrtttttt
Majaji wanatoka,
Mhe. Lissu anaangana na Mawakili wake pamoja na Viongozi wa Chama pamoja na watu mbalimbali waliojitokeza Mahakamani.
Naomba Repost yako.
Winnie Prosper retweeted
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo September 18, 2026
Last time tuliishia part 431 so leo tunaendelea na -;
Part 432.
Mhe. Tundu Lissu ameingia Mahakamani watu wana vibe sana wanaimba Mwamba Mwamba huku wakipiga makofi mengi sana.
Majaji wote watatu wameingia na kuketi kwenye viti vyao.
Wakili wa Serikali Ajuaye amesimama na kutambulisha jopo lake na kuwa wako tayari kuendelea.
Mhe. Lissu na yeye anasema niko tayari kuendelea.
Mhe. Lissu amesimama na kusema kwamba nimekutana na Kamishna wa Polisi Ramadhani Kingai ambaye nilikuwa nimependekeza awe shahidi wangu wa leo, nimekutana nae Mahakamani kwenye chumba hiki hiki waheshimiwa majaji, naweza kuthibitisha kwamba ameheshimu wito wa Mahakama amekuja na nimezungumza nae kuhusu yeye kuwa shahidi wa upande wa utetezi na nimezungumza nae kiasi cha kutosha, baada ya kumueleza maeneo ambayo ningependa ayatolee ushahidi ameniambia kwamba yeye hawezi na hayuko tayari kutoa ushahidi kwa upande wangu kwa maneno yake mwenyewe amesema
“Yeye yuko upande wa wale wanaoomba na watakaoshangilia nikipatikana na hatia”
Kwahiyo amesema hayupo tayari kuja kutoa ushahidi kwa niaba yangu.
Nimemuelewa Waheshimiwa Majaji kama hayuko tayari siwezi kumlazimisha kutoa ushahidi ambao hataki kuutoa.
Waheshimiwa Majaji Kingai ameniambia kitu kingine kuhusiana na mashahidi wengine wawili IGP Camillius Wambura na CDF Jacob Mkunda, amesema vilevile hata wao watakaporejea nchini na kupata wito wa Mahakama msimamo wao utakuwa ni huo huo kwamba na wao hawatakuwa tayari kutoa ushahidi kwa upande wa utetezi kwasababu ile ile kuwa wako upande wa wale wanaoombea na watakaoshangilia nikipatikana na hatia.
Katika Mazingira haya waheshimiwa majaji maana yake ni kwamba sina mashahidi zaidi kwahiyo naomba kufunga ushahidi kwa upande wa utetezi.
Ni hayo tu waheshimiwa majaji.
Naomba Repost yako.
The EPP Group has nominated lawyer, human rights activist and politician Mr Tundu Lissu as a candidate for the Sakharov Prize.
After surviving a 2017 assassination attempt, Mr Lissu returned to Tanzania to continue advocating democratic reform, only to face arrest, treason charges and exclusion from the 2025 presidential election, while his party was barred from participating.
His case reflects the wider erosion of democratic pluralism and political competition in Tanzania.
For the EPP Group, Mr Lissu represents a powerful combination of personal courage, democratic conviction and geopolitical relevance. His nomination affirms that Europe stands with those defending constitutional democracy and political freedom in Africa and in other partner countries of the EU. Mr Lissu embodies the defence of democracy, political pluralism, the rule of law and fundamental freedoms at extraordinary personal cost.
The Sakharov Prize for Freedom of Thought is the highest tribute paid by the European Union to human rights work.
Winnie Prosper retweeted
Leo baada ya kesi kuhairishwa, nimemuomba Mwenyekiti @TunduALissu atupe ujumbe wa siku. Kwa kuzingatia leo ni siku ya demokrasia, Tundu Lissu ametoa wito kwa Watanzania – “Demokrasia haidondoki kutoka mbinguni; inapiganiwa na ina gharama zake. Ukitaka demokrasia, lazima uwe tayari kulipa bei inayotakiwa na historia.” #FreeTunduLissu
Winnie Prosper retweeted
HABARI:
Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kyela Victoris Swebe ameyasema hayo wakati akizungumza katika Msiba wa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Kyela Mkoani Mbeya.
Winnie Prosper retweeted
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 413
Upande wa Jamhuri wanamfanyia Cross- Examination Makam Mwenyekiti Mhe. John Heche.
Katuga: Mahakama iliposema ana kesi ya kujibu Lissu uliridhika au hukuridhika?
Heche: Sikuridhika.
Katuga: Je uliwahi kuzungumza ushahidi wa Prosecution kuhusu hii kesi kwamba PW fulani ni muongo?
Heche: Sikuwahi kuzungumzia hilo.
Katuga: Mh. Lissu ana chombo chochote cha habari?
Heche: Hana wala hamiliki.
Katuga: Lissu akitaka kudeliver message anafanyaje?
Heche: Anahutubia Mikutano.
Katuga: Lissu amewahi kuitisha watanzania wote wakusanyike sehemu moja?
Heche: Hajawahi
Katuga: Ni sahihi kwamba akitaka ku deliver hotuba yake kwa umma wa Watanzania anaongea na waandishi wa habari?
Heche: Sio kweli
Katuga: Ushahidi wa mwenyewe Lissu amesema anaita waandishi wa habari je hizi shahidi zinafanana au hazifanani?
Heche: Inategemea na context
Katuga: Hujui au unajua?
Heche: Sijui.
Katuga: Kama kwenye ushahidi wako nilikusikia unasema Mapolisi walikuwa wanaingiza kura feki kwenye vibegi?
Heche: Nimewahi kumuona Askari akiingia na kibegi kwenye kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Nyanungu.
Katuga: Umeeleza Askari kwenye vibegi kuwa aliingiza huko Nyanungu vibegi na wakati wa ushahidi hukusema?
Heche: Nchi nzima, siku ya kupiga kura Askari huwa wanafanya hivi.
Katuga: Unajua Tanzania hii kuna tuhuma mbalimbali za mauaji kwa sababu zao mbalimbali ikiwemo mapenzi na wivu?
Heche: Najua
Katuga: Mauaji ni kosa la jinai sio kosa la uchaguzi?
Heche: Inawezekana
Katuga: Ulisema kwamba Msafiri Mbwambo alichinjwa kwa ajili ya yeye kulalamikia Sheria ya Uchaguzi?
Heche: Tulikuwa kwenye kampeni.
Katuga: Ulisema sababu za Msafiri mbwambo kuuwawa.
Heche: Nilisema sababu za kisiasa. Sikueleza sababu in details moja baada ya nyingine.
Katuga: Kama katika ushahidi umeeleza sababu Mahsusi ya Bwana Msafiri Mbwambo kuchinjwa?
Heche: Nimesema sababu za Uchaguzi.
Katuga: Kipindi cha 2012 huko Arumeru alipofariki Sumari kuna kesi inayohusu viongozi wa Chadema kumteka mtu anaitwa Paul Mafie na Bariki na walipelekwa Mlimani kuteswa?
Heche: Sijui
Katuga: Mtu yeyote anaweza kushitakiwa kwa kosa la utekaji akifanya?
Heche: Mtu yeyote anaweza.
Katuga: Kwa ushahidi wa kwamba Msafiri Mbwambo aliuwawa na watu wanaosadikika ni wana CCM. Je huo ushahidi ni wa kuona, hisia au kunusa?
Heche: Ushahidi wa kuona na kusikia. Niliona kwenye Gazeti kwani wewe hiyo karatasi hapo unaona au unahisi uliyonayo hapo?
Katuga: Ni wewe uliona Daniel Yona akishambuliwa Hananasif?
Heche: Sikuwepo.
Katuga: Viapo vya Mawakala nani anaeweza kuvifuatilia?
Heche: Mgombea, Viongozi wa Chama na watu wote.
Katuga: Ule uchaguzi mdogo wa Kinondoni, uliousema alikuwa anagombea nani?
Heche: Salum Mwalimu
Katuga: Kulikuwa na Mawakala wangapi?
Heche: Vituo zaidi ya 800 nafikiri
Katuga: Mlikuwa mnafunga kampeni kwenye uwanja wa Buibui siku hiyo.
Heche: Kweli
Katuga: Jioni ilitoka hamasa na kwenda kwa Mkurugenzi kinondoni?
Heche: Ndio nini unasema hapo? Weka clarity
Katuga: Mlihamasishana kufanya maandamano kwenda kwa Mkurugenzi.
Heche: Sio kweli
Katuga: Ulisema idadi ya hao watu walioenda huko kwa Mkurugenzi?
Heche: Sikusema.
Katuga: Si mlizuiwa pale Mkwajuni?
Heche: Mimi nakaa Sirari na Mwanza mambo ya Mkwajuni tena najuaje. Ni pale bondeni liko Kinondoni.
Katuga: Kwahiyo mlikuwa kundi.
Heche: Ndio
Part 414 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
Winnie Prosper retweeted
Kumbe mkakati ni kumfrustrate Makam @HecheJohn apoteze focus ili afeli kwenye cross - examination ndo maana mnaona tangu juzi watu wale wale waliokuwa wanasema Heche ameiba hela za #ToneTone, watu hao hao ambao daily huwa wanapinga misimamo yote ya Chadema, wameanza kumshambulia Mhe. Heche kuhusu hilo swala la kutokwenda Kizimkazi.
Kuanzia leo hadi Mhe. Heche atakapo maliza kutoa ushahidi wake press za kumshambulia zitakuwa nyingi sana wanataka mpaka akose utulivu na mashambulizi yao yatajikita kwenye hoja ya kwamba amegoma kwenda Kizimkazi kumpa pole Nduli Idd Amin Mama, wewe uliona wapi mtu analazimishwa kwenda kutoa pole????
Jambo lilianza Friday kuhakikisha weekend yote Mhe. Heche anakosa Utulivu, ashindwe kujiandaa na kesi halafu limerudiwa tena leo asubuhi siku ambayo anatakiwa kufanyiwa cross- examination.
Anyways tuendelee na kesi maana Mahakama tayari imeshaanza soon nitawaletea Live updates za kesi.
Winnie Prosper retweeted
Mombo ameiharibu sana TiSS, imekuwa ya kiwaki sana, inafanya mambo ambayo hata ukisikia aibu unaona wewe
Nguvu ya Mamlaka inatumika hadi kuamua kesi za mapenzi?
Winnie Prosper retweeted
ICE HOCKEY 🏒
🟢🟢Odds 2+ 🏒⤵️
BETSITE: PARIPESA
𝗖𝗢𝗗𝗘 𝗬𝗔 𝗠𝗞𝗘𝗞𝗔:👉 U7XVH
JISAJILI PARIPESA Tushinde pamoja 👊🏿
Reg link: paripesa.bet/nuh3
paripesa.bet/nuh3
Sehemu ya Promocode jaza: 𝗡𝘂𝗵𝟯
📍Jitahidi usisahau kujaza promo code tajwa👉 𝗡𝘂𝗵𝟯 muda wa usajili ili uungwe katika moja ya member watakaonufaika na #BONUS
APP: paripesa.bet/nuh3app




















