Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza orodha ya awali ya wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa klabu ya Simba SC, baada ya kukamilika kwa mchakato wa mchujo.
Katika nafasi ya uenyekiti, majina yaliyotangazwa ni Anindumi Semu, Geofrey Nyange, Dkt. Seif Muba na Swedy Mkwabi. Hata hivyo, jina la mwenyekiti wa sasa wa klabu hiyo, Murtaza Mangungu, halipo kwenye orodha hiyo.
Rais Samia Suluhu Hassan amesema anachukizwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA) kupasua barabara nyingi ambazo huharibiwa na mvua za masika.
105
TCRA yatakiwa kuongeza uwezo wa kuchuja maudhui yasiyo na maadili clickhabari.com/tcra-yatakiw…
1
53
Rais Samia Suluhu Hassan amesema hawezi kuruhusu viongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuendelea kuvutana kuhusu ukamilishaji wa miundombinu kwa ajili ya mashindano AFCON), wakati Shirikisho la Soka Afrika (CAF) linasubiri viwanja vikamilike.
1
110
Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi na wadau mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano wa Tatu wa Kitaifa wa Kisayansi kuhusu Afya ya Uzazi, Mama, Mtoto mchanga, Mtoto, Vijana na Lishe katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
143
"Nikiwa kinara wa afya ya mama na mtoto, nalichukua suala la uzazi, afya ya mama na mtoto kwa umuhimu mkubwa kutokana na adha wanazopata wanawake na watoto." - Rais Samia Suluhu Hassan akifungua Mkutano wa Tatu wa Kisayansi wa Afya ya Uzazi, Mama, Mtoto, Vija na Lishe
88
"Kuna ujenzi wa vituo vya watoto njiti ndani ya mahospitali yetu. Kwa wale wanaozaliwa hawajatimia, tunaongeza jitihada na tuna majadiliano ya kujenga vituo 26 vingine kwa ajili ya kuweka watoto njiti." - Rais Samia Suluhu Hassan
90
Mahakama nchini Kenya imesema serikali ilikiuka baadhi ya vifungu vya Katiba wakati wa ujenzi wa kituo cha karantini ya ugonjwa wa Ebola kinachoungwa mkono na Marekani.
Mahakama hiyo pia imeamuru kusimamishwa kwa shughuli zote za ujenzi wa kituo hicho hadi serikali itakapotekeleza masharti iliyoyaweka, ikiwemo kuweka wazi maelezo ya makubaliano iliyofanya na serikali ya Marekani kuhusu ujenzi wa kituo hicho.
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Dkt. Bashiru Kakurwa kuwa Waziri wa Mifugo.
Kabla ya Uteuzi huo, Dkt. Bashiru alikuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi.
104
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Hamis Mwinjuma (Mwana FA) kuwa Waziri wa Uvuvi.
Kabla ya uteuzi huo, Mwinjuma alikuwa Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Ayub Rioba kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari - Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali.
87
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema Serikali imejiandaa kuhakikisha usalama wa wageni wote watakaokuja nchini Tanzania kushuhudia mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Makonda amesema Serikali pia imejiandaa kuhakikisha timu zote zitakazocheza nchini zinapata huduma na mahitaji yao yote kwa mujibu wa sheria na miongozo ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
129
Wateja waruhusiwa kushtaki BASATA mafundi wanaochelewesha nguo clickhabari.com/wateja-waruh…
73
Rais Samia Suluhu Hassan, amekutana na kuzungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Miao Deyu, Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo.
104
Rais Samia Suluhu Hassan, akiwaapisha mabalozi mbalimbali kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo.
166
Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) imetangaza Senegal kuwa mabingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), baada ya kukata rufaa kupinga uamuzi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) wa kuinyang’anya timu hiyo ubingwa.
Senegal iliifunga Morocco bao 1-0 lakini CAF iliivua ubingwa kwa madai ya kukiuka kanuni za mashindano baada ya wachezaji wake kuondoka uwanjani kupinga maamuzi ya mwamuzi.
5
355
Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi, leo amekagua ujenzi wa soko la Kirumba, Wilayani Ilemela, Jijini Mwanza, unaotekelezwa chini ya Mradi wa Uendelezaji wa Miji Tanzania (TACTIC).
Mradi huo wa shilingi bilioni 14.7, unaojumuisha barabara ya kilomita 2.9 inayoelekea sokoni, umefikia asilimia 76.6 na unatarajiwa kukamilika Januari 2027.
1
110
"Viongozi wetu [Tanzania na Uganda] wamekubaliana kuchukua hatua za kuondoa vikwazo vya kibiashara ambavyo vimekuwa vikiongeza gharama za biashara na kuzuia bidhaa kufika sokoni kwa urahisi." - Makame Mbarawa, Waziri wa Uchukuzi akizungumza na vyombo vya Habari kuhusu ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Uganda
90
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema hakitakubali kufanya mazungumzo ya maridhiano ikiwa mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu yuko gerezani.
Makamu mwenyekiti wa chama hicho, John Heche amesema mazungumzo hayo lazima yawe na msuluhishi wa kimataifa anayeheshimika na anayeweza kuleta pande mbili zinazokinzana pamoja.





























