Hussein Momieh Hamis retweeted
WAZUNGU WANASEMAGA "A WARNING SHOT HAS BEEN FIRED"
RAIS SAMIA leo tarehe 27 Novemba 2026 akiwaapisha viongozi wapya amezungumza mambo kadhaa wa kadhaa yanayohusu serikali yake na nchi kwa ujumla wake.
KUBWA ZAIDI ni kauli ya Rais Samia kwa Makamu wa Rais na Waziri Mkuu juu ya utendaji wao kazi na kwa kauli ile ya Rais ni wazi kuwa kuna mambo yanamtia kichefuchefu sana anapoyaona yanafanywa na wasaidizi wake.
TULISEMA hapa siku chache zilizopita juu ya mkanganyiko wa Makamu wa Rais kuingilia majuklumu yasiyo ya kwake na kutoa amri zisizo na kichwa wala miguu akidhania kufanya hivyo ndiyo kutimiza majukumu ya umakamu wa Rais au kumuwakilisha Rais.
Makamu wa Rais amekuwa akizunguka huko akisema katumwa na Rais! Sijui nimeagizwa na Rais Dokta Samia hivi mara vile.. Haya sasa aliyekutuma anawezaje kuhoji alichokutuma?
TUMEKUWA tunasema hapa Makamu wa Rais hajajua bado majukumu yake. Anafanya kazi za Waziri Mkuu na ndiyo kisa cha huu mkanganyiko lakini wengi hawakutaka kusikia haya mambo. Makamu wa Rais anatakuwa kutuliza kichwa na kuiga vile Dokta Mpango alikuwa anafanya,vile Dokta Bilal alikuwa anafanya ,vile Dokta Shein alikuwa anafanya.. LAKINI kwa kuwa ana haraka na anaona anachelewa matokeo yake ndiyo haya sasa inafika mahali Mhe Rais mwenyewe anasimama na kusema haya kwa taifa na watanzania.
RAIS kaongea kuwa Makamu wa Rais anarudi na kutoa ripoti mambo ni yale yale aliyofanya Waziri Mkuu..Maana yake ni nini?Maana yake ni kuwa Makamu wa Rais anafanya kazi ambazo ni za Waziri Mkuu na siyo majukumu yake ambayo inawezekana bado hajajua ni yapi.
HAYA yote yanatokea mapema hivi kwa kuwa watu wameacha jukumu la kumsaidia Rais kuongoza nchi na wamejikita kufanya "personal branding" yaani Makamu Wa Rais anataka kuji brand kuwa maarufu sana kuliko Rais. Makamu wa Rais anataka kujiona anajua mambo sana kuliko Waziri Mkuu ambaye ndiye mtendaji wa serikali.. Makamu wa Rais anataka kujiona ana uchungu sana na watanzania kuliko Rais ambaye alizunguka nchi nzima kuomba dhamana ya kuchaguliwa na kuwa Rais.. Matokeo ya haya yote kwa ujumla ndiyo sasa yanakuja kuleta na kuwapa ajali watu za mtindo huu na Rais anaamua kuwachana hadharani hivi.
WAZIRI MKUU kama mtendaji mkuu wa serikali ana mipaka yake na anacheza ndani ya mipaka yake lakini Rais kawapa angalizo wakuu wa mikoa,wakuu wa wilaya na mawaziri juu ya kumsaidia majukumu yake na apumzike kwa ajili ya kuratibu serikali na shughuli zake kuliko kwenda kusikiliza kero za wananchi ambazo zingeweza kusikilizwa na watu walioko huko chini..
WATENDAJI wa serikali huko chini hawafanyi kazi zao ndiyo maana watu wanasubiri viongozi kama Waziri Mkuu waende huko kwenye ziara ndiyo waeleze kero zao! Hili ni jambo la hovyo na linapaswa kukomeshwa mara moja kwa kuwa linachukua muda wa Waziri Mkuu kushughulika na mambo "petty" wakati kuna mambo makubwa ya kuyafanyia kazi kwenye serikali..
MIMI siyo mtabiri na wala sitaki kufanya kazi ya kutabiri lakini mimi najua kusoma nyakati na kwa kauli hii ya Rais ina maana hafurahishwi na mwenendo na maigizo ya msaidizi wake ambaye anakanyagakanyaga watu tu kwenye ziara zake na kuharibu taswira ya taasisi ya urais. Pili Rais hafurahishwi na jinsi ambavyo wakuu wa mikoa na wilaya wanapoacha kero za watanzania zinasubiri waziri mkuu aje azitatue wakati wao wapo kwa ajili ya kazi hiyo na mwisho hajapendezwa na ripoti zile zile za mambo anayofanya waziri mkuu anakuja makamu wa Rais kuzileta anapotoka ziarani.
MAANA yake kuna mtu anafanya majukumu ambayo siyo ya kwake na kuna mtu hajui majukumu yake ni yepi na kuna mtu ataona 2030 mbali sana!
NIMEKAA PALEEEEE 👉🏼
#KigogoMediaUpdates
Hussein Momieh Hamis retweeted
Distancing yourself from people doesn't mean you're enigmatic or dramatic, it's just about protecting yourself,try to protect your inner mind pls
Hussein Momieh Hamis retweeted
The prison has no walls. 👁️
It runs on habit and unwatched thought.
Attention is the real currency.
Take yours back, one quiet moment.
What still has your consent?



















