ππ« ο£Ώ retweeted
Dodoma inazidi kung'ara kwa kazi kubwa zinazotekelezwa chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Maono yanageuka vitendo, maendeleo yanaonekana!
ππ« ο£Ώ retweeted
Asante Prof. Samia Suluhu Hassan.
Karibu Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma
#KaribuMtumba #SiNdotoTena
ππ« ο£Ώ retweeted
Mji wa Serikali Mtumba wajengewa kilomita 59.1 za barabara za lami
Rais Samia Suluhu Hassan amezindua barabara za lami zenye urefu wa kilomita 59.1 zilizojengwa katika Mji wa Serikali wa Mtumba mkoani Dodoma....
ππ« ο£Ώ retweeted
Dodoma inazidi kunoga Mama Samia anetekeleza kwa vitendo, watanzania tunatembea kifua mbele.
ππ« ο£Ώ retweeted
Tanzania na Angola Kukubaliana Kuunganisha Reli Zao, Kufungua Njia ya Usafirishaji Kati ya Bahari ya Atlantiki na Hindi
Tanzania na Angola zimekubaliana kuunganisha mitandao yao mikubwa ya reli ili kutengeneza njia ya usafirishaji inayovuka bara la Afrika na kuunganisha Bahari..
ππ« ο£Ώ retweeted
Tanzania na Angola Kukubaliana Kuunganisha Reli Zao, Kufungua Njia ya Usafirishaji Kati ya Bahari ya Atlantiki na Hindi
Tanzania na Angola zimekubaliana kuunganisha mitandao yao mikubwa ya reli ili kutengeneza njia ya usafirishaji inayovuka bara la Afrika na kuunganisha...
ππ« ο£Ώ retweeted
Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiagana na Mhe. JoΓ£o Manuel ConΓ§alves LourenΓ§o, Rais wa Jamhuri ya Angola katika uwanja wa gwaride, Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma, tarehe 30 Oktoba, 2026.
ππ« ο£Ώ retweeted
Tanzania na Angola Kukubaliana Kuunganisha Reli Zao, Kufungua Njia ya Usafirishaji Kati ya Bahari ya Atlantiki na Hindi
Tanzania na Angola zimekubaliana kuunganisha mitandao yao mikubwa ya reli ili kutengeneza njia ya usafirishaji inayovuka bara la Afrika na kuunganisha Bahari ya Atlantiki na Bahari ya Hindi.
Makubaliano hayo yametangazwa na Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Rais wa Angola, JoΓ£o LourenΓ§o, wakati wa mazungumzo yao jijini Dar es Salaam.
Mradi huu mkubwa unalenga kurahisisha biashara kati ya nchi za Afrika, kuimarisha usafirishaji wa bidhaa na madini, pamoja na kufungua fursa mpya za kiuchumi kwa nchi zinazopitiwa na reli hiyo.
Mambo Muhimu Kuhusu Makubaliano Hayo:
1. Kuunganisha Reli Mbili Kubwa
Mpango huu unahusisha kuunganisha Reli ya Benguela ya Angola, ambayo ni sehemu muhimu ya Ukanda wa Lobito unaoelekea katika Bahari ya Atlantiki, na Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), ambayo inaishia katika Bandari ya Dar es Salaam kwenye Bahari ya Hindi.
2. Njia Mpya ya Usafirishaji Afrika
Mradi huo utakapokamilika, utawezesha kuwepo kwa njia moja ya reli inayounganisha Bahari ya Atlantiki na Bahari ya Hindi kupitia Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Zambia na Tanzania.
Hii itarahisisha usafirishaji wa bidhaa, madini na malighafi kutoka nchi za ndani ya Afrika kwenda kwenye bandari za kimataifa. Pia itachochea biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo.
3. Umuhimu wa Kimkakati na Kisiasa
Makubaliano haya yanaunganisha miradi miwili mikubwa ya reli ambayo imekuwa ikipata uwekezaji kutoka kwa mataifa yenye nguvu kiuchumi duniani.
Reli ya TAZARA inaungwa mkono na China kupitia makubaliano ya uwekezaji wa takribani dola za Marekani bilioni 1.4 kwa ajili ya kuifanyia maboresho na kuifanya iwe ya kisasa zaidi.
Kwa upande mwingine, Ukanda wa Lobito umepokea mabilioni ya dola katika uwekezaji na ufadhili kutoka Marekani na Umoja wa Ulaya.
Rais Samia pia ametangaza kuwa Tanzania itafungua tena ubalozi wake nchini Angola, ambao ulifungwa mwaka 1993 kutokana na changamoto za kifedha.
ππ« ο£Ώ retweeted
Tarehe 24 Septemba 1973 Mkutano Mkuu wa 16 wa TANU uliamua Makao Makuu ya Tanzania yahamishiwe Dodoma. Tangu wakati huo, kila awamu ya uongozi imeendeleza azimio hilo, nami leo nimeungana na Rais wa Jamhuri ya Angola, Mheshimiwa JoΓ£o LourenΓ§o, kuzindua majengo ya ofisi za Wizara na Taasisi za Serikali pamoja na barabara za lami katika Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma.
Ninawashukuru Marais wote walionitangulia kwa kuendeleza maono ya Baba wa Taifa. Pia, nawapongeza viongozi, watendaji wa serikali na sekta binafsi, makandarasi na wananchi wote walioshiriki katika kutekeleza mradi huu. Kazi yenu ni ya thamani na itaenziwa katika historia ya nchi yetu.
Mji huu uliojengwa kwa fedha za ndani umebuniwa kuwa kitovu cha shughuli za Serikali, huduma kwa wananchi, diplomasia na shughuli za kiuchumi na kijamii. Ni wajibu wetu kuhakikisha uwekezaji huu unaleta tija kwa kuwahudumia wananchi kwa heshima, weledi na ufanisi. Hata hivyo, huduma ziwafuate wananchi walipo kupitia mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), badala ya kuwalazimu kufika Dodoma kuzifuata.
Ili kuendeleza ustawi wa Mji huu na Makao Makuu kwa ujumla, nimetoa maelekezo yafuatayo:
1. Majengo, miundombinu na mazingira yatunzwe na kuwa safi wakati wote.
2. Mamlaka husika zisimamie kikamilifu utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Uendelezaji wa Jiji la Dodoma wa mwaka 2019β2039.
3. Wizara zinazohusika na huduma za kijamii zihakikishe huduma hizo zinapatikana kikamilifu.
4. Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji iendelee kuhamasisha na kuvutia uwekezaji ili kuunga mkono maendeleo ya Jiji la Dodoma.
ππ« ο£Ώ retweeted
WATUMISHI WA UMMA MUWE WATUMISHI WA WANANCHI NA MUWATUMIKIE KWA HESHIMA - RAIS SAMIA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewataka watumishi wa umma kutumia mazingira bora ya kazi yaliyowekwa katika Mji wa Serikali Mtumba kuwahudumia wananchi kwa heshima, uadilifu, uwajibikaji na ufanisi.
Rais Samia ametoa rai hiyo leo, Oktoba 30, 2026, wakati akizindua majengo ya ofisi za Wizara na Taasisi za Serikali pamoja na barabara za lami na miundombinu mingine muhimu katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Amesema Serikali imewekeza katika ujenzi wa majengo imara na ya kisasa pamoja na miundombinu inayowezesha watumishi kutekeleza majukumu yao katika mazingira bora, hivyo ni wajibu wao kuhakikisha uwekezaji huo unaleta matokeo chanya kwa wananchi.
Amesisitiza kuwa pamoja na huduma mbalimbali kupatikana katika Mji wa Serikali Mtumba, wananchi hawapaswi kulazimika kusafiri hadi Makao Makuu ya nchi kufuatilia kila huduma ambayo inaweza kutolewa katika mikoa na wilaya wanazoishi.
Ameeleza kuwa Serikali inataka mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) itumike kikamilifu kuhakikisha huduma zinapatikana kwa urahisi katika maeneo ya wananchi, huku mifumo ya taasisi mbalimbali za Serikali ikiwasiliana na kubadilishana taarifa.
Ametoa mfano wa wananchi kutoka mikoa ya Rukwa, Kagera, Mtwara na Kigoma ambao hawapaswi kutumia muda na fedha nyingi kusafiri hadi Dodoma kufuatilia masuala yanayoweza kutatuliwa katika maeneo yao.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuunganisha mifumo ya TEHAMA ya Wizara na Taasisi za Serikali ili kuondoa urasimu na kuepusha wananchi kuhitajika kuwasilisha taarifa zilezile katika taasisi tofauti.
Rais Samia amesema teknolojia iliyowekwa katika Mji wa Serikali inapaswa kusaidia kurahisisha kazi, kuongeza tija na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Amehitimisha kwa kuwataka watumishi wa umma kutambua kuwa dhamana waliyopewa ni kuwatumikia wananchi, hivyo wanapaswa kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia misingi ya utumishi bora.
ππ« ο£Ώ retweeted
πSamia: Kukamilika Mji wa Mtumba, tumetimiza ndoto Serikali kuhamia Dodoma
Rais Samia Suluhu Hassan, amesema ametimiza ndoto ya Baba wa Taifa wa Julius Nyerere, kwa kukamilisha ujenzi wa majengo ya wizara,‡οΈ
ππ« ο£Ώ retweeted
NIMETIMIZA WAJIBU WANGU KWA KUKAMILISHA UJENZI WA MJI WA SERIKALI MTUMBA, KUTIMIZA MAONO YA BABA WA TAIFA - RAIS SAMIA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema ametimiza wajibu wake kwa kuendeleza na kukamilisha ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya kutekeleza ndoto na maono ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ya kuhamishia Makao Makuu ya nchi Dodoma.
Rais Samia ameyasema hayo leo, Oktoba 30, 2026, wakati akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa majengo ya ofisi za Wizara na Taasisi za Serikali, barabara za lami pamoja na miundombinu muhimu na wezeshi katika Mji wa Serikali Mtumba.
Amesema baada ya kukabidhiwa dhamana ya kuongoza nchi mwaka 2021, aliamua kuendeleza ujenzi wa mji huo kwa kushirikiana na watendaji wengine wa Serikali, kwa kujenga majengo ya kudumu ya ghorofa, barabara za lami na miundombinu mingine muhimu.
Ameeleza kuwa hatua hiyo imekamilisha sehemu muhimu ya azma ya kuwa na Mji wa Serikali wenye mazingira bora, imara na ya kisasa kwa ajili ya kurahisisha utendaji wa Serikali na utoaji wa huduma kwa wananchi.
Aidha, Rais Samia amewashukuru marais waliomtangulia, Hayati Ali Hassan Mwinyi, Hayati Benjamin Mkapa na Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuendeleza maono ya Baba wa Taifa katika hatua mbalimbali.
Kwa Kipekee, amemshukuru Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwa uamuzi na uthubutu wake wa mwaka 2016 wa kuhamishia shughuli za Serikali Dodoma, pamoja na kuzindua Mji wa Serikali Aprili 13, 2019, wakati huo ukiwa na majengo ya awali ya kujishikiza yaliyowezesha Wizara na Taasisi kuanza kutoa huduma.
Rais Samia amesema mafanikio hayo yamepatikana kutokana na usimamizi wa karibu wa viongozi na watendaji wa Serikali, akiwatambua aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Hayati John Kijazi na Katibu Mkuu Kiongozi wa sasa Balozi Moses Kusiluka pamoja na kamati za wataalamu zilizoshiriki katika kuratibu utekelezaji wa azma hiyo.
Ameongeza kuwa Serikali imetekeleza ujenzi huo kwa kutumia fedha zake yenyewe, bila msaada wa taasisi nyingine, hivyo kuwataka Watanzania kujivunia mafanikio hayo.
ππ« ο£Ώ retweeted
Rais. Dkt Samia Suluhu Hassan azindua majengo, miundombinu ya kisasa mji wa serikali Dodoma.
ππ« ο£Ώ retweeted
Dkt Samia: Serikali kuhamia Dodoma ni fursa kiuchumi, biashara
Rais Samia Suluhu Hassan, amesema kuhamia kwa Serikali Dodoma kumechochea ukuaji wa jiji hilo, kuongeza idadi ya watu, shughuli za biashara, uwekezaji na huduma mbalimbali.
ππ« ο£Ώ retweeted
Samia: Kukamilika Mji wa Mtumba, tumetimiza ndoto Serikali kuhamia Dodoma
Rais Samia Suluhu Hassan, amesema ametimiza ndoto ya Baba wa Taifa wa Julius Nyerere, kwa kukamilisha ujenzi wa majengo ya wizara, taasisi za Serikali pamoja na barabara za lami katika Mji wa Serikali wa Mtumba jijini Dodoma.
Amesema mwaka 2021 wakati akichukua uongozi wa nchi, mradi huo ulikuwa na majengo ya awali ya kujishikiza, hivyo yeye pamoja na viongozi wenzake waliongeza jitihada za ukamilishaji wake.
Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa wakati wa uzinduzi wa majengo ya wizara, taasisi za Serikali pamoja na barabara za lami katika Mji wa Serikali wa Mtumba jijini Dodoma.
βPamoja na majengo ya awali ya kujishikiza, tuliamua kuendeleza mradi wa ujenzi huu wa majengo ya Serikali kwa kujenga majengo ya kudumu ya ghorofa, barabara za lami na miundombinu mengine wezeshi,β amesema na kuongeza kuwa;
βNamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kutimiza tulioyakusudia, hakika tunapaswa kujipongeza sote Watanzania kwa mafanikio makubwa haya,β amesema Rais Samia.
Samia: Kukamilika Mji wa Mtumba, tumetimiza ndoto Serikali kuhamia Dodoma
Rais Samia Suluhu Hassan, amesema ametimiza ndoto ya Baba wa Taifa wa Julius Nyerere, kwa kukamilisha ujenzi wa majengo ya wizara, taasisi za Serikali pamoja na barabara za lami katika Mji wa Serikali wa
Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa wakati wa uzinduzi wa majengo ya wizara, taasisi za Serikali pamoja na barabara za lami katika Mji wa Serikali wa Mtumba jijini Dodoma.
βPamoja na majengo ya awali ya kujishikiza, tuliamua kuendeleza mradi wa ujenzi huu wa majengo ya























