millardayo (@millardayo) header
millardayo (@millardayo) profile picture

Award winning TV/Radio Personality | Hosting Amplifaya on CloudsFM |Journalist from Tanzania covering East Africa and beyond | Bookings [email protected]

Joined April 2010
Photo by millardayo (@millardayo)Photo by millardayo (@millardayo)Photo by millardayo (@millardayo)Photo by millardayo (@millardayo)Photo by millardayo (@millardayo)Photo by millardayo (@millardayo)Photo by millardayo (@millardayo)Photo by millardayo (@millardayo)Photo by millardayo (@millardayo)Photo by millardayo (@millardayo)
millardayo retweeted
Leo ndio siku ambayo inamalizika countdown ya viatu 10 bora vya kike vya SKECHERS vilivyoongoza kwa kuuza zaidi katika Maduka ya SKECHERS Jijini Dar es salaam ambapo countdown hii inahitimishwa kwa kukitazama kiatu hiki namba moja. Rekodi za mauzo za Maduka ya SKECHERS yaliyopo Morocco Square pembeni ya Mataa ya Morocco Kinondoni, Mlimani City Mall na Aura Mall zimedhihirisha wazi kuwa kiatu hiki ndio kimeongoza kwa kupendwa zaidi na Wasichana/Wanawake na ndicho kilichouzika kuliko viatu vyote vya kike katika Maduka hayo. Kiatu hiki kimeundwa kwa ubunifu wa hali ya juu unaochanganya mitindo ya kisasa na uhalisia wa mahitaji ya Mwanamke wa kileo, ubora wake unatokana na material ya ngozi na hivyo kukifanya kiwe na uwezo wa kudumu kwa muda mrefu huku kikibakia na muonekano wa kuvutia kikiwa ni ni kiatu kilichoundwa kwa kutumia akili ya fashion hivyo kinaweza kuvaliwa kwenye mazingira mbalimbali, iwe kazini, mitoko au matembezi ya kawaida na kuendana na mavazi ya aina nyingi. Kwa wale Warembo wanaotafuta mchanganyiko wa ubora na mtindo unaovutia, basi hiki ndicho kimekuwa chaguo bora zaidi na kinapatikana kwa bei ya shilingi laki mbili tu ( 200,000 ) kwenye maduka yote ya Skechers jijini Dar es Salaam ambayo yako wazi kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa nne usiku siku za weekend kuanzia Ijumaa, Jumamosi na Jumapili. #MillardAyoSHOPPING
2
3
60
48,995
#VIDEO Katika siku kumi kuanzia leo July 10 2025, tegemea kukutana na countdown ya viatu 10 bora vya SKECHERS vya Wanawake ambavyo vimeongoza kwa kununuliwa zaidi katika Maduka ya SKECHERS yaliyopo Morocco Square Mall pembeni ya mataa ya Morocco, Mlimani City Mall pamoja na Aura Mall. Post hii inakihusu kiatu kilichoshika namba 10 katika orodha hiyo ambacho ni SKECHERS GO RUN ambacho ukiachia mbali rangi yake kuvutia Wanawake wengi, sifa zake pia zimekipa Mashabiki wengi huku kikiuzwa shilingi laki mbili. Mikidadi ambaye ni Meneja wa Maduka ya SKECHERS Tanzania, kwenye mahojiano na Millard Ayo ndani ya Duka la SKECHERS Morocco Square, ameeleza yafuatayo "kutokana na Watoto wa kike ( Wanawake ) kuingia sana kwenye kufanya mazoezi wengi wamekinunua kwa ajili ya mazoezi kwakuwa kimetengenezwa na mesh ambayo inapitisha hewa kwenye miguu wakiwa wanafanya mazoezi, wakati wa kukimbia, kuruka kamba n.k"
6
2
70
76,495
TotalEnergies Marketing Tanzania Limited inakaribisha washirika wenye uwezo wa kusambaza bidhaa zetu za gesi ya kupikia nchi nzima. Vigezo: * Mtaji wa TZS milioni 50 hadi TZS milioni 70 kwa kuanzia. * ⁠Uwepo wa rasilimali watu wenye ari na ufanisi katika uendeshaji wa biashara. * Umakini wa hali ya juu katika kutoa huduma bora kwa wateja. * Uzoefu uliothibitishwa wa biashara yenye ushindani na mzunguko mkubwa. * Uwezo wa kumiliki rasilimali muhimu kama maghala na vifaa vya usambazaji bidhaa kama malori na pikipiki. * Utayari wa kufanya kazi kwa misingi madhubuti na utaratibu wa mkataba. * Mbinu thabiti za kupenya na kukuza masoko. * Kuzingatia sera za TotalEnergies na viwango vya juu vya Afya na Usalama. * Uadilifu wa hali ya juu katika biashara. @totalenergies_tz Faida za kushirikiana Nasi * Upanuzi wa Soko: Fursa ya kupanua na kuimarisha uwepo wa chapa. * ⁠Msaada wa kibiashara: Upatikanaji wa mipango kamili ya biashara na mwongozo wa kimkakati. * ⁠Upekee wa usambazaji: Haki za kipekee za usambazaji katika maeneo maalum. Kwa mawasiliano zaidi, wasiliana nasi kupitia [email protected] au piga simu bure 0800750242.
6
4
2
57
17,177
Muda huu maandalizi ya kuelekea Sikukuu ya Mei Mosi yanaendelea katika Uwanja wa Bombadia uliopo Mkoani Singida, ambapo shughuli mbalimbali za maandalizi na mapambo yanaendelea kufanyika. Baada ya shamrashamra zilizoshuhudiwa Mkoani humo katika siku za hivi karibuni, ikiwemo maonesho na burudani kesho Mei 1 ndiyo kilele cha Maadhimisho hayo kitaifa ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho hayo. #MillardAyoUPDATES
16
14
709
49,482
Wanajeshi wa Rwanda wamewasindikiza Wanajeshi wa ujumbe wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Kusini mwa Afrika (SADC) kutoka Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuelekea nchini Tanzania. Jeshi la Rwanda limewasindikiza Wanajeshi wa vikosi vya SADC vinavyotoka Kongo kupitia ardhi ya nchi ya Rwanda kwenda Tanzania huku wakiondoka eneo la mashariki mwa Kongo, Msemaji wa jeshi la Rwanda amethibitisha. Jumuiya ya SADC yenye nchi 16 Wanachama katikati ya mwezi March ilisema kwamba ilikuwa imefuta mamlaka ya ujumbe wake nchini Kongo, SAMIDRC, na ingeanza kuondoa vikosi vyake kwa awamu kutoka Kongo. Ujumbe wa SADC ulitumwa Kongo kuisaidia Serikali ya DRC kupambana na makundi ya Waasi upande wa mashariki mnamo December 2023 ambapo baadaye Wanajeshi kadhaa waliuawa wakiwemo wa Tanzania na Afrika Kusini. #MillardAyoUPDATES (✍️ DW Kiswahili)
48
15
816
86,909
Daniel Balili Buberwa, Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Diploma ya Uhandisi wa Kompyuta katika Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT), amepotea tangu Aprili 23, 2025 na taarifa zinasema mara ya mwisho alionekana akiwa Chuoni na baadaye kuonekana maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam ikiwemo Lumumba, Tazara na Temeke. Mama mzazi wa Daniel, Sophia Gura ambaye anaishi Kinyerezi Kibaga karibu na Mahakama au Kituo cha Polisi kwenye Mtaa wa Engineer Mmari anaomba kwa yeyote mwenye taarifa kuhusu Mtoto wake kuwasiliana kupitia namba 0713 502 353 au 0717 521 700 anaomba msaada wa haraka ili Mtoto wake apatikane salama. #MillardAyoUPDATES
59
84
2
866
84,742
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa wito kwa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu kuchukua hatua kufuatia matukio ya Polisi kuwakamata Viongozi na Wananchi waliojitokeza kusikiliza kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es salaam April 24,2025 huku wengine wakipigwa, kuteswa na kuumizwa. Akiongea na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam leo April 30,2025, Mnyika amesema “Tunatoa wito kwa Rais Samia Suluhu Hassan akiwa ni Amiri Jeshi Mkuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuchukua hatua kwa upande wake , tunafahamu huko nyuma yamewahi kujitokeza matukio ya Polisi kusema uongo baada ya kuvunja sheria na Marais waliokuwepo wakati huo walichukua hatua” “Mtakumbuka kuna Wafanyabiashara wa madini waliuawa Polisi wakasema walikuwa Majambazi iliundwa Tume ukweli ukajulikana na hatua zikachukuliwa kwa baadhi ya Wahusika, katika tukio la kuuawa kwa Mwanahabari mwenzenu Daudi Mwangosi Polisi walitoa taarifa za uongo, ikaundwa Tume na hatua zikachukuliwa” “Tunatoa wito kwa Rais Samia, Watu 25 kupigwa wengine wakivunjwa miguu sio tukio dogo kwa Amiri Jeshi Mkuu kukaa kimya huku Polisi wakisema uongo” “Tunatoa wito kwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ipitie matukio na simulizi zote za April 24,2025 na ushahidi wa video na Tume ichukue hatua zake” #MillardAyoUPDATES
105
122
3
1,302
68,316
Zikiwa zimebaki saa kadhaa kuelekea kilele cha siku ya Wafanyakazi Duniani ( Mei Mosi ) Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasili katika Viwanja vya Bombadia Mkoani Singida leo Aprili 30, 2025, kushiriki kikao maalum na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi ) yanayotarajiwa kuadhimishwa kitaifa hapo kesho Mkoani humo. Shangwe na hamasa vimetawala mapokezi yake huku Viongozi mbalimbali wa Serikali na Vyama vya Wafanyakazi wakimkaribisha kwa heshima kubwa leo ikiwa ni siku moja kabla ya maadhimisho hayo kitaifa yatakayofanyika Mkoani humo. #MillardAyoUPDATES
19
14
1
526
42,669
Msanii Staa wa Rap kutoka Tanzania, Claudia Lubao maarufu Chemical (@chemical_tz ) , leo April 30,2025 ameamka na habari njema iliyoandika historia mpya kwenye maisha yake huku ‘Dr’ ikiongezeka mwanzo wa jina lake baada ya kufaulu mtihani wake wa mwisho wa shahada ya uzamivu (PhD) kwenye masuala ya sanaa na sasa anaitwa rasmi Dkt. Lubao. Chemical amehitimu shahada hiyo katika Chuo Kikuu cha St Andrews, nchini Uingereza ambako alikwenda kusoma baada ya kupata ufadhili wa kimasomo kufuatia kufanya vizuri na kuwa Mshindi wa kwanza wa tafiti bora Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) 2020/2021 alikosoma shahada ya kwanza (Bachelor Degree) ya sanaa za maonesho, baadaye shahada ya uzamili (Masters) ya sanaa katika usimamizi wa urithi wa kitamaduni. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Chemical ameelezea furaha yake kwa kuikamilisha ndoto aliyokuwa nayo na leo kuamka akiwa anaitwa Dr. Lubao ambapo amewashukuru Wasimamizi , Familia, Marafiki na Watu wote wakiwemo Mashabiki waliompa moyo katika safari yake hiyo inayomfanya kuwa Msanii wa kwanza wa Rap kusoma na kuhitimu PhD Chuoni hapo. #MillardAyoUPDATES
140
114
5
3,198
168,685
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemvua rasmi uanachama aliyekuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema kutokana na kuleta dharau dhidi ya Mamlaka ya Chama na kuleta ukaidi dhidi ya kuheshimu miiko, tamaduni na misingi ya Chama. Katibu wa Tawi la Bonyokwa CHADEMA, Solomini Kagoruki leo amemuandikia barua ya kumvua uanachama Mrema ambaye amekuwa akilisema pia kundi la G 55 ambapo kwenye barua hiyo Kagoruki amenukuliwa akimwambia Mrema “Rejea barua yenye KUMB/CDM/MTG/KND/01.2025 ya April 16,2025 Iliyokuwa pamoja la mambo mengine ikikutaarifu kuhusu wito wa kufika mbele ya kamati tendaji ya tawi lako la Bonyokwa kujieleza juu ya mambo kadhaa ambayo yalitajwa kwenye barua husika, lakini pia barua ilikutaka uwasilishe utetezi wako kwa maandishi ndani ya muda tajwa kwenye barua” “Napenda kukujulisha kuwa kamati tendaji ya tawi la bonyokwa iliyoketi jana April 29,2025 Bonyokwa /Segerea kwa pamoja ilipitia na kujadili tuhuma dhidi yako na kubaini baada ya kupokea barua tajwa hapo juu ulidharau mamlaka yako ya nidhamu kwa kuibeza barua husika na kuisambaza kwenye mitandao ya kijamii badala ya kutumia muda huo kutekeleza takwa la barua hiyo la kujitetea mbela ya Tawi” “Pia katika hali ya kushangaza pamoja na kuwa ulikuwa umetakiwa kujieleza uliendelea na kutenda kosa kwa kuendelea kupinga na kudhihaki misimamo na programu za Chama na ulifanya hivyo waziwazi kwenye mkutano wako na Waandishi April 22,2025 ambao uliendelea kushikilia msimamo wako wa kukituhumu Chama hadharani huku ukijua kuwa huo siyo utamaduni wa CHADEMA na wala siyo misingi yake” “Baada ya mjadala wa kina dhidi ya tuhuma zako, Kamati ilifikia uamuzi wa pamoja kuwa umepoteza sifa za kuwa Mwanachama wa CHADEMA kwa mienendo yako hiyo na kwa hivyo kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA ya mwaka 2006 toleo la 2019 ibara ya 5.4.3 Umevuliwa rasmi uanachama wako wa CHADEMA wa Tawi la Bonyokwa kuanzia tarehe ya barua hii lakini pia tunapenda kukutaarifu kuwa kwa mujibu wa kifungu tajwa hapo juu unayo fursa ya kukata rufaa kwa ngazi ya juu kama hujaridhika na adhabu hii” #MillardAyoUPDATES
204
151
13
2,125
205,295
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Abdul Mombokaleo leo Jumatano April 30. Kikao hicho kilijadili namna ya kuzalisha umeme kwa nishati ya jua (solar power) katika viwanja vya ndege nchini ambapo Kusaga ameambatana na Yang Xitong ambaye ni Makamu Mkurugenzi wa China Energy Engineering Group (CEEG) ambao imeonesha nia ya kushirikiana na Mampaka hiyo katika kutengeneza miundombinu ya nishati ya umeme wa jua katika viwanja vya ndege nchini. Akiongea katika kikao hicho Kusaga amesema Tanzania ina fursa ya ya kuzalisha nishati safi na kuokoa fedha pia kutengeneza ajira kwa Vijana wengi nchini, ili kuendana na falsafa ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuona Tanzania inatumia nishati safi na kutunza mazingira. #MillardAyoUPDATES
22
15
7
363
55,768
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na maandalizi kuelekea sherehe za siku ya Wafanyakazi duniani zitakazofanyika kesho Mei mosi, 2025 kitaifa Mkoani Singida katika Uwanja wa Bombadia. Ameyasema hayo leo Jumatano Aprili 30, 2025 alipopokea taarifa na kukagua maandalizi ya Maadhimisho ya sherehe hizo ambapo Mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan. PM Majaliwa ameipongeza kamati inayoratibu sherehe hizo na kuwataka kuhakikisha wanakamilisha maeneo machache yaliyobaki ambayo yanahitaji maboresho. Awali, akitoa taarifa ya maandalizi hayo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Ridhiwani Kikwete amesema maandalizi yamekamilika kwa kiasi kikubwa na wapo tayari kumpokea Rais Dkt. Samia kwa ajili ya sherehe hizo. #MillardAyoUPDATES
8
10
1
685
46,971
millardayo retweeted
MillardAyoMagazetiTanzania May 1, 2025, instagram.com/p/DJGHSh9iPS0/…
2
3
21
11,041
millardayo retweeted
MillardAyoMagazetiniKENYA May 1, 2025, instagram.com/p/DJGJbqdiv1L/…
2
2
20
10,845
millardayo retweeted
Mwalimu wa Shule ya Sekondari Nyakabungo, Edward Bihemo (43) ameripotiwa kutapeliwa shilingi milioni 12 na Mganga wa tiba asilia Edward Emmanuel (38) kwa ahadi ya kuzalishiwa fedha nyingi zaidi kupitia njia ya miujiza. Tukio hilo lilitokea April 18, 2025 huko Mwanza ambapo Mganga huyo alimweleza Mwalimu Bihemo kuwa fedha hizo zingeongezeka endapo angeziweka kwenye begi maalum na kutoa sadaka mara kwa mara, jambo alilolifanya kwa matumaini ya kupata zaidi. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbroad Mutafungwa amesema baada ya kutopata matokeo yoyote, Mwalimu huyo alirudi kwa Mganga huyo kudai fedha zake na ndipo alipoelewa kuwa ametapeliwa hali iliyosababisha Mtuhumiwa kukamatwa. #MillardAyoUPDATES
167
29
28
661
73,991
millardayo retweeted
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kupitia kwa Kamanda wake Muliro Jumanne, limesema limemkamata Mtu mmoja kwa tuhuma za kumshambulia Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania Padri Charles Kitima jana. Taarifa ya Polisi imeeleza kuwa jana tarehe 30 April 2025 saa nne usiku maeneo ya Baraza la Maaskofu Kurasini Dar e salaam, ilipokelewa taarifa ya kujeruhiwa kwa Padri Kitima ambapo tangu saa tatu asubuhi Viongozi wa dini mbalimbali walikuwa katika kikao. Imeelezwa kuwa baada ya kikao kuisha saa moja jioni, Padri huyo alikwenda Kantini alikokaa hadi saa nne na robo usiku ambapo aliponyanyuka kwenda maliwatoni pembeni ya Kantini hiyo kushambuliwa kichwani na Watu wawili ambao walitumia kitu butu kumshambulia. Taarifa ya Polisi imeeleza kuwa Padri huyo aliwaishwa Hospitali na anaendelea vizuri kwa sasa ambapo tayari Mtu mmoja kati ya wawili hao amekamatwa na kutajwa kuwa Rauli Mahabi Haraja Mkazi wa Kurasini ambaye anashikiliwa na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo "uchunguzi wa kina unaendelea ili hatua kali na za haraka zichukuliwe kwa Wahusika" #MillardAyoUPDATES
126
30
4
824
100,937
millardayo retweeted
Baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia Katibu wa Tawi la Bonyokwa Solomini Kagoruki kuandika barua ya kumvua uanachama Mkurugenzi wa zamani wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya nje wa Chama hicho John Edward Mrema, amejitokeza na kusema bado yeye ni Mwanachama halali wa Chama hicho. Katika taarifa yake kwa Vyombo vya Habari, Mrema amefafanua kama ifuatavyo...... 1. Mimi John Mrema ambaye ni Mwanachama wa CHADEMA mwenye kadi ya uanachama namba 0111 na kuwa wanachama wa CHADEMA tunatambulika kwa namba za kadi kwa mujibu wa Kanuni ya 5.1 na 5.2, barua inayosambaa hainihusu mimi kwani haikutaja namba ya uanachama wangu labda kuna Mtu tunafanana majina. 2. Ikumbukwe kuwa Chama hiki ni cha kimtandao/Kidigitali, hata kadi yangu ya uanachama ambao inadaiwa nimefutwa haikutajwa hivyo inawezekana kabisa barua hii hainihusu hata kidogo. 3. Tawi langu sio Binywokwa kwani nimesajiliwa tawi la Makongo, mimi sijasajiliwa kwenye tawi tajwa la Bonyokwa na taarifa hizi zinapatikana kwenye mfumo wa kidigitali wa Chama 4. Mimi sio Mwanachama wa tawi la Bonyokwa kwa mujibu wa kanuni za chama Kanuni ya 5.3. ( imeweka utaratibu wa Mwanachama kutakiwa kuwasilisha taarifa zake kwa katibu wa tawi pindi anapohama kutoka eneo moja kwenda eneo lingine hivyo kuishi eneo husika haihalalishi kuwa tayari ni Mwanachama wa tawi husika wakati utaratibu wa kanuni husika haujafuatwa na ndio maana sijawahi kushiriki kikao chochote cha tawi la Bonyokwa kwani hilo sio tawi langu. 5. Tawi tajwa la Bonyokwa hawana mamlaka ya kunivua uanachama wangu kwani mimi sio Mwanachama wa tawi hilo na kadi yangu inajieleza imesajiliwa tawi lipi na inapatikana kwenye mfumo rasmi wa Chama wa Chadema Digital. Mimi John Edward Mrema, ni Mwanachama halali wa Chadema mpaka hapo nitakapochukuliwa hatua kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Chama. #MillardAyoUPDATES
60
15
4
375
41,914
millardayo retweeted
Uchapakazi ni nguzo imara ya maendeleo ya taifa letu. @totalenergies_tz TotalEnergies inakutakia heri ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, shujaa wa kweli ni yule anayejitolea kwa bidii kila siku! #ShujaaWaKazi #MayDay2025 #totalenergiestz
2
2
24
10,304
millardayo retweeted
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kuwa mwaka huu Serikali imeongeza kima cha chini cha mshahara kwa Watumishi wa Umma kwa 35.1% ambapo kwa ongezeko hili sasa kima cha chini kitapanda kutoka 370000 hadi 500000. Akiongea leo May 01,2025 kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Mkoani Singida, Rais Samia amesema “Mwezi May mwaka jana wakati wa Siku ya Wafanyakazi Serikali ilieleza ugumu wa uchumi ulivyokuwa wakati ule na kuwasihi tusiongeze gharama kwa Serikali kwa kuongeza mishahara bali tuliendelea na upandishaji wa madaraja na kutoa maslahi mengine ya Wafanyakazi” “Sasa kwa mapenzi makubwa na kwa namna mlivyoiunga mkono Serikali ilipowaomba mfunge mkanda na mkaamua kujituma na kufanya kazi kwa bidii na kufanya uchumi wetu ukue kwa 5% mwaka huu, kwakuwa Mcheza kwao hutunzwa, Wafanyakazi oyeee, miamvuli oyee, naona miamvuli imepanda sasa wakati wote ilikuwa chini sasa imepanda” “Sasa kwakuwa Mcheza kwao hutunzwa, Mimi na wenzangu na baada ya kuangalia uchumi ulivyopanda na umepanda kwasababu ya nguvu zenu Wafanyakazi, ninayo furaha ya kuwatangazia kwamba mwaka huu Serikali itaongeza kima cha chini cha mshahara kwa Watumishi wa Umma kwa 35.1%, Wafanyakazi oyeee” “Nyongeza hii itakayoanza kutumika mwezi July mwaka huu itaongeza kima cha chini cha mshahara kutoka 370000 hadi Tsh. 500000, ngazi nyingine za mshahara nazo zitapanda kwa kiwango kizuri jinsi bajeti inavyoruhusu lakini nataka niwaambie nyongeza nzuri ipo” #MillardAyoUPDATES
138
82
12
1,570
146,853
millardayo retweeted
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kuwa mwaka huu Serikali imeongeza kima cha chini cha mshahara kwa Watumishi wa Umma kwa 35.1% huku akisema kwa upande wa Sekta binafsi Bodi ya kima cha chini cha mshaharaa kwa Sekta binafsi inaendelea kufanya mapitio ili kuboresha viwango vya chini vya mshahara kwa Wafanyakazi wa Sekta hiyo. Akiongea leo May 01,2025 kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Mkoani Singida, Rais Samia amesema “Kwa upande wa Sekta binafsi Bodi ya kima cha chini cha mshaharaa kwa Sekta binafsi inaendelea kufanya mapitio ili kuboresha viwango vya chini vya mshahara kwa Wafanyakazi wa Sekta hiyo” “Pamoja na kazi inayofanywa na Bodi hiyo, naendelea kuvihimiza Wizara na Vyama vya Wafanyakazi, kufanya majadiliano na Waajiri ili kutekeleza mikataba ya hali bora ya Wafanyakazi katika Sekta binafsi waendane sambamba na wenzao wa Sekta ya Umma” “Ahadi yetu kwenu Wafanyakazi ni kwamba tutaendelea kuboresha mazingira ya kazi yakiwemo maslahi ya Wafanyakazi kadri hali ya uchumi itakavyoruhusu” #MillardAyoUPDATES
49
21
3
772
65,877