Hatari ya majengo jijini
Familia ya Alex Mutua Ogare inataka haki baada ya mpendwa wao kufariki kufuatia kuporomoka kwa ukuta katika eneo la Riverside, jijini Nairobi
@ruga_eval #NTVWikendi
Aliyemuua afande apatikana
Msako wa takribani miaka minne wa kumsaka mshukiwa mkuu wa mauaji ya aliyekuwa Naibu Afisa Mkuu Msimamizi wa Kituo cha Polisi wa Rumuruti umefikia kikomo baada ya polisi kumkamata Onesmas Kipkoech Tiony, ambaye amekuwa mbioni.
@ruga_eval #NTVWikendi
Upinzani wakashifu matamshi ya rais
Viongozi wa upinzani wamemuonya Rais William Ruto dhidi ya matumizi ya lugha isiyofaa anapozungumzia wapinzani wake wa kisiasa.
@ruga_eval #NTVWikendi
Mbarika ya sakata ya World Bank
Ripoti ya Benki ya Dunia kuhusu mradi wa reli ya kisasa wa SGR imezua mvutano wa kisiasa, baada ya Rais William Ruto kupuuza ukosoaji wa upinzani na kuelekeza lawama kwa utawala ulioanzisha mradi huo.
@ruga_eval #NTVWikendi
Ruto apigiwa upatu Nakuru
Seneta Aaron Cheruiyot ameongoza viongozi wa Kenya Kwanza katika kutafuta uungwaji mkono wa kuchaguliwa tena kwa Rais William Ruto katika Kaunti ya Nakuru, wakipuuza matokeo ya kura za maoni zinazoashiria ushindani mkali kati ya rais Ruto na Edwin Sifuna kwenye kinyang'anyiro cha urais.
@ruga_eval #NTVWikendi
Utatu wa Ruto Magharibi
Ukanda wa Magharibi ni eneo ambalo Rais William Ruto anahitaji kuvuna kura nyingi kuelekea uchaguzi wa mwaka 2027. Lakini badala ya kutegemea kiongozi mmoja, Rais Ruto ameyajukumuisha makundi matatu kufanikisha hili.
@ruga_eval #NTVWikendi
Hofu ya maandalizi ya uchaguzi
Vinara wa upinzani wameibua wasiwasi kuhusu maandalizi ya uchaguzi mkuu wa 2027 wakitilia shaka usawa katika usajili wa wapiga kura na kutaka vyama vya upinzani kufikia makubaliano ya pamoja kuhusu mgombea wa urais.
@ruga_eval #NTVWikendi
Ruto akemea vurugu za Narok
Rais William Ruto amekemea machafuko yaliyoshuhudiwa Jumamosi Narok katika tamasha za Maa, wafuasi wa Gavana Patrick Ole Ntutu na Mbunge Gabriel Tongoyo walipokabiliana na kusababisha majeraha na uharibifu.
@ruga_eval #NTVWikendi
Nuksi ya 'stori za jaba' Mombasa
Kioja kimezuka huko Mombasa baada ya jamaa mmoja kumdunga rafiki yake kwa makasi hadi kufa wakiwa kwenye starehe ya kula miraa.
@ruga_eval #NTVWikendi
Makovu ya manusura wa ajali
Manusura wa ajali za barabarani sasa wanalaumu uzembe wa madereva wenzao kuwa chanzo cha ajali nyingi zinazowaletea ulemavu wa kudumu na kuvuruga maisha yao.
@ruga_eval #NTVWikendi
Katikati ya mzunguko wa barabara, kwenye eneo la Uthiru, kando ya barabara kuu ya Waiyaki, kuna makanisa kadhaa, makazi ya watu na biashara ndogondogo, vyote vikiwa vimejengwa katika eneo dogo.
Wakazi sasa wanakabiliwa na hofu ya kupoteza makazi yao kutokana na upanuzi wa barabara ya Waiyaki.
@ruga_eval #NTVWikendi
Akina mama walisafiri kutoka kaunti za Marsabit na Baringo kuwakilisha jamii zao katika COP 31.
Hii ikiwa mara ya kwanza kwa akina mama hao kushiriki katika kongamano la Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya anga.
@ruga_eval #NTVWikendi
KPA yaibuka kidedea
Mabingwa watetezi wa mpira wa vikapu, Kenya Ports Authority (KPA), wamefanikiwa kuhifadhi taji lao la Ligi Kuu ya Wanawake ya Shirikisho la Mpira wa vikapu Kenya baada ya kuwanyuka Equity Hawks kwa alama 95-46 katika mchezo wa fainali.
@ruga_eval #NTVWikendi
Hali ya wasiwasi yatanda katika kijiji cha Kambi Asharaff, kilicho mpakani mwa kaunti za Meru na Isiolo, kufuatia mgogoro wa umiliki wa ardhi.
#NTVAdhuhuri @ruga_eval
Wito wa kudumisha amani watolewa na viongozi katika maeneo ya Kuria Magharibi na Mashariki kaunti ya Migori baada ya watu wawili kufariki katika kisa cha wizi wa mifugo.
#NTVAdhuhuri @ruga_eval
Wabunge kutoka kaunti ya Nandi warai Wakenya kuunga mkono rais Ruto mwaka ujao, wakisema ametimiza ahadi zote.
#NTVAdhuhuri @ruga_eval
Muthama na Sonko wapa kuunganisha viongozi wa jamii za Wakamba wakiwemo Kalonzo Musyoka na gavana wa zamani wa Machakos Alfred Mutua kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027.
#NTVAdhuhuri @ruga_eval
Seneta wa Embu Alexander Mundigi ashutumu vikali vurugu zilizoshuhudiwa wakati wa mkutano wa chama cha Justin Muturi cha DP Alhamisi iliyopita, akiwataka wanasiasa kuheshimu maamuzi na uhuru wa wananchi kuunga mkono vyama tofauti vya kisiasa.
#NTVAdhuhuri @ruga_eval
Mvutano Wa Shamba La Joseph Gachoka
Mvutano kati ya familia ya mfanyibiashara marehemu Joseph Gachoka na kampuni ya kimataifa yq Floriculture Limited umechukua mkondo mwingine.
Hii ni baada ya familia hiyo kudai kuwa kuna zaidi ya watu 200 wanaodaiwa kuwa walijihami na kuwavamia katika ardhi hiyo na makazi yao.
#NTVJioni @ruga_eval

