Matokeo ya chaguzi zisizo huru na za haki zinazopelekea akili ndogo zilizojificha katika kivuli cha uongozi kutawala akili kubwa!
Hii ndio sababu ya hitaji la Katiba Mpya itakayopelekea upatikani wa Tume Huru ya Uchaguzi na "yenye meno" itakayosimamia "Uchaguzi huru na wa Haki"
Povu lote la UVCCM ni kwa sababu hawataki kuambiwa ukweli kuhusu matendo yao, au wanataka hata wale waliojifunza mbinu chafu za rushwa kutoka kwao wawajibishwe?
Mende hawezi kuangusha kabati, Badala ya kumshambulia anayeibua kero, ni vyema UVCCM wajibu tuhuma kwa hoja!
“Msingi wa amani ni haki, iwe ni haki yenyewe pale ilipo, au matumaini ya kujenga taifa lenye haki. Mahali ambapo hakuna haki, wala matumaini ya kuipata haki, hakuwezi kuwa na amani.”
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, hotuba ya mwaka 1987.
Aliyekuwa Rais wa DRC Joseph Kabila, ametangazwa kuongoza muungano mpya wa kisiasa na kijeshi, Front for the Refoundation of the Nation (FRN), uliozinduliwa Oktoba 12, 2026 mjini Goma. Muungano huo unalenga kuunganisha nguvu za upinzani dhidi ya serikali ya Rais Félix Tshisekedi.
Ni jambo la kawaida kwa mtu mjinga kufikiria kijinga, kuandika ujinga na kujiona ameandika jambo la maana bila kujua anaweza pia kupata mashabiki wajinga kama yeye!
Kama una akili badala ya kujisifu utaacha watu wakusifie!
Replying to @robkidayo_
The creativity behind my posts!!
Wangapi wanapost lakini hawapo kama mimi?
Ule umimi!
That's why everybody can post but no one can be like me 🫴
Watu walioapa kuilinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo hii ndio wanaoibeza!
Mtu aliyeshiba posho za Ubunge zinazotokana na kodi za wananchi, anasimama na kusema Katiba ni karatasi tu, haina maana wala haiwezi kubadili maisha ya watu!
Mbunge anayebeza Katiba anasahau kuwa Katiba hiyo hiyo ndiyo iliyoweka nafasi ya Ubunge na msingi wa yeye kuwa Bungeni leo.
Ukipata madaraka bila kujali na kuheshimu Katiba, ni rahisi kudharau umuhimu wake. Kwa CCM nadhani huyu sio mtu wa kwanza kutoa kauli za kebehi na kuibagaza Katiba.
Kama Katiba ni karatasi tu isiyoweza kubadili maisha, kwa nini mnaogopa kuibadilisha?
Duniani wawili wawili, Usiniulize namfananisha na nani!
Anaitwa Ngozi Ezeonu ni muigizaji mkongwe wa Nigeria (Nollywood) na Afrika kwa ujumla, anayejulikana kwa uwezo wake mkubwa wa kuigiza nafasi mbalimbali za mama na familia kwenye filamu za Kiafrika.
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa imemteua Faris Buruhan (Buruhani) kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) leo tarehe 11 Oktoba 2026.
Kabla ya uteuzi huu wa nafasi ya kitaifa, ndugu Faris Buruhan alikuwa akihudumu kama Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera.
Hii sijapenda hata kidogo!
Imenikumbusha miaka ile ya 1997 mambo ya Air Msae vs Dar Express vs Tawfiq... Moshi Dsm masaa5! 🙌🙌
LATRA INATILIA SHAKA UWEZO WA VETA NA NIT?
LATRA si taasisi ya elimu wala mafunzo ya kitaaluma. Sasa kwa nini inawafanyisha madereva mitihani baada ya kuhitimu VETA au NIT na kupata vyeti vyao?
Je, hii ina maana kwamba VETA na NIT ambazo ni taasisi za umma zilizoanzishwa kutoa mafunzo ya kitaaluma, haziwezi kuaminika kuthibitisha uwezo wa wahitimu wao?
Kama taasisi za elimu haziaminiki, LATRA ambayo si taasisi ya elimu ina msingi gani wa kuaminika zaidi katika kutathmini uwezo wa madereva?
Kama kuna sababu za kiusalama zinazohalalisha mitihani hiyo, je, LATRA ina mamlaka gani ya kisheria na kitaaluma ya kufanya hivyo?
Serikali haiwezi kuanzisha taasisi za mafunzo, kuzipa mamlaka ya kutoa vyeti, halafu taasisi nyingine ya umma ikazifanya vyeti hivyo vionekane havina thamani bila maelezo ya msingi.
LATRA inapaswa kueleza wazi msingi wa kisheria na madhumuni ya mitihani hiyo. Usalama barabarani ni muhimu, lakini haupaswi kuwa kisingizio cha urasimu unaodhoofisha uaminifu kwa taasisi za umma zinazotoa mafunzo.
Natamani kusikia maoni ya wengine




