Stanley Mvuyekule🇹🇿 retweeted
“Tulidhani furaha ilikuwa mbele yetu, kumbe wakati mwingine furaha yenyewe ilikuwa pale tulipokuwa”
Maisha ya shule pengine ndiyo maisha yenye furaha zaidi ukilinganisha na hatua nyingine tunazopitia katika safari ya maisha. Ilikuwa ni kipindi ambacho hakuna aliyewaza kuhusu bili ya umeme, maji, kodi ya nyumba wala gharama za maisha.
Urafiki wa kweli, wa dhati na usio na masharti ulitawala. Tulipendana bila kuangalia nani anatoka familia tajiri, nani ana uwezo mkubwa au nani hana kitu. Tulikuwa pamoja kwa sababu tulikuwa sisi. Cha kushangaza zaidi, hakuna aliyejua miaka kumi tu baadaye maisha yangempeleka wapi.
Mchana darasani, jioni uwanjani tukipiga mpira, na usiku kwenye vibanda umiza kutazama filamu za Van Damme, Rambo na Jet Li. Hizo ndizo zilikuwa burudani zetu. Tulicheka kwa moyo wote, tulitania bila kuumizana na tulifurahia hata vitu vidogo ambavyo leo tungeona havina maana.
Wakati huo, karibu wote tulikuwa sawa. Hakukuwa na matabaka makubwa kati yetu. Sote tulikuwa na ndoto zinazofanana, matumaini yanayofanana na hofu zilezile za matokeo ya mitihani. Kila mmoja alipambana kwa namna yake kuhakikisha anapata angalau Division Four ya 26, ili mradi tu asikose nafasi ya kusomea ualimu! Huo ndio ulikuwa mtazamo wetu wa mafanikio wakati ule.
Lakini miaka imepita. Maisha yametutawanya katika njia tofauti. Wengine wamefanikiwa, wengine bado wanapambana, na wengine wamejikuta katika hali ambazo hawakuwahi kuzifikiria walipokuwa wakiketi pamoja kwenye madawati yale ya shule.
Leo tukikutana tena, mara nyingi hatuoni tena tabasamu lile la zamani. Furaha haiji kwa wepesi kama ilivyokuwa. Mazungumzo yamebadilika, ukaribu umepungua na matabaka ya maisha yamejenga umbali mkubwa kati yetu. Kila mmoja ana mzigo wake, mapambano yake na simulizi yake ambayo huenda wengine hawaijui. Hata sonona imekuwa sehemu ya maisha ya wengi.
Wapo wanaotamani sana muda urudi nyuma. Wangependa kupata nafasi nyingine ya kufanya maamuzi tofauti, kurekebisha makosa, kuchagua njia nyingine na pengine kuishi maisha tofauti na haya waliyonayo leo. Lakini muda hauna mlango wa kurudi nyuma. Umesonga mbele, na baadhi ya nafasi hazirudi tena.
Pengine hatukujua kwamba tulikuwa tunaishi siku bora zaidi za maisha yetu. Tulidhani furaha ilikuwa mbele yetu, kumbe wakati mwingine furaha yenyewe ilikuwa pale tulipokuwa. Hapa niko na mwanangu @stanitoh85 🙏🏻
Stanley Mvuyekule🇹🇿 retweeted
Vyeti Vya shule vitakuwezesha kupata kazi na pengine kupanda cheo. Mafanikio baada ya hapo yatategemea sana yale mambo tunayochukulia poa kama vile mahusiano mazuri wa watu; uwezo wa kuzikabili hisia; hulka ya kupenda mafanikio; na uwezo wa kutengeneza mtandao wa marafiki.
More Blessings Son.
Stay Blessed ...#KingKelvin2020
Hakika...#ASANTESANAMUNGU instagram.com/p/CAPyx20D3wc/…
Kila mwaka Baada ya Mungu huwa pia nauamini katika huyu.
Asante sana mama kwa malezi yako yaliyo Bora kwangu wakati wote.
Heri ya mwaka mpya Mama yangu.#MamaStanJanuary2020 instagram.com/p/B6xJb21pGWV/…
Kumcha mungu ni chanzo cha hekima.
Eee mungu nijalie nisije pokonywa hizo #HEKIMA...#StellaStan instagram.com/p/BxcyvHsjdmA/…
Kumcha mungu ni chanzo cha hekima.
Eee mungu nijalie nisijepokonywa hizo hekima...💓 instagram.com/p/BxcyYG-D1Yt/…
Hakika Mungu u mwema wakati wote..!
Mungu umekua ukinifanya niwe mwenye Furaha wakati wote kwakunijalia mema na mazuri yenye thamani sana.
Hakika nitazidi kukushukuru sana na kukuhimidi… instagram.com/p/Bubirvch9g2/…
Ni mungu Pekee anayeweza kufanya kitu ambacho Binadam hawezi..!
Thank you The Lord God coz now We headin' to the Top....#onlygodcandowhatmancannot instagram.com/stanydegreat/p…
Every Challenge has a lesson in it... Please learn.Coz always challenges pave the way to success if you work on them effectively.Stay strong and keep on being… instagram.com/stanydegreat/p…
Ili usifikirie kuhusu hela inabidi uwe nazo nyingi mno au usiwe nazo kabisa...#teammoneymakers instagram.com/stanydegreat/p…
Source of my Everlasting happiness..!#StellaStan instagram.com/stanydegreat/p…
Siku zote huwa naamini Mungu amenileta katika hii Dunia ili nifaidi Furaha na sio huzuni.Na siku zote huwezi faidi furaha kama umejenga uadui na… instagram.com/stanydegreat/p…
Siku zote huwa naamini Mungu amenileta katika hii Dunia ili nifaidi Furaha.Na siku zote huwezi faidi furaha kama umejenga uadui na Upendo...#Loveisthesourceofpeace. @ Tafes… instagram.com/stanydegreat/p…







