TRT Afrika Swahili (@trtafrikaSW) header
TRT Afrika Swahili (@trtafrikaSW) profile picture

Afrika kama ilivyo

Joined August 2022
Photo by TRT Afrika Swahili (@trtafrikaSW)Photo by TRT Afrika Swahili (@trtafrikaSW)Photo by TRT Afrika Swahili (@trtafrikaSW)Photo by TRT Afrika Swahili (@trtafrikaSW)Photo by TRT Afrika Swahili (@trtafrikaSW)Photo by TRT Afrika Swahili (@trtafrikaSW)Photo by TRT Afrika Swahili (@trtafrikaSW)Photo by TRT Afrika Swahili (@trtafrikaSW)Photo by TRT Afrika Swahili (@trtafrikaSW)Photo by TRT Afrika Swahili (@trtafrikaSW)
Shirika la Huduma za Wanyamapori Kenya (KWS) limeripoti kuwa shughuli za kumtafuta Elder David Kenneth Kihuna katika Hifadhi ya Aberdare nchini Kenya zinaendelea, huku vikosi vya uokoaji vikiongeza juhudi za kumpata. Helikopta, droni na zaidi ya waokoaji 200 wanaripotiwa kushiriki katika shughuli hiyo, licha ya changamoto za hali ya hewa na uoto mnene wa msitu. Kihuna aliripotiwa kupotea Novemba 14, 2026, wakati wa matembezi ya milimani.
1
52
Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amejiandikisha katika daftari la mpiga kura katika Kituo cha Kujiandikisha cha Hai Gonya, Jimbo nambari 1, mjini Juba. Baada ya kukabidhiwa kadi yake ya kupiga kura, aliwataka raia wa nchi hiyo wenye sifa za kupiga kura kujitokeza kwa wingi, kujisajili na kuchukua kadi zao. Sudan Kusini iko katika maandalizi ya kufanya Uchaguzi Mkuu wa kwanza tangu nchi hiyo kupata uhuru 2011. Tarehe ya awali iliyopangwa ilikuwa ni Disemba, 2026, hata hivyo, tarehe hiyo imesogezwa mbele hadi mwezi Februari 2027. Kwa upande wake, Rais mstaafu wa Tanzania ambae pia ni Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Afrika (AU) katika Pembe ya Afrika na Bahari ya Sham, Jakaya Kikwete, ameutaka Umoja wa Mataifa na Jumuia ya Kimataifa kuisadia Sudan Kusini kifedha na kiusalama ili taifa hilo changa liweze kufanya Uchaguzi Mkuu kwa amani. Kikwete alitoa wito huo Novemba, 2026 alipokuwa akizungumza kwa njia ya video na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
73
Tanzania imekuwa katika orodha ya kumi bora ya nchi zenye ufasaha wa lugha ya Kiingereza Afrika kwa mwaka 2026. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya kimataifa ya kila mwaka inayopima kiwango cha umahiri wa lugha ya Kiingereza miongoni mwa watu wazima katika kila nchi iliyofanywa na Education First. Kwa mujibuwa ripoti hiyo, Tanzania imepata alama 477, na kushika nafasi ya 70 duniani. Afrika Mashariki, Kenya inaongoza, ikifuatiwa na Uganda, baadae Tanzania. Afrika Kusini ndiyo iliyoibuka kidedea Afrika kwa alama 588, ikichuana na Zimbabwe yenye alama 587 na Kenya yenye alama 582. Nchi nyengine zilizoingia katika orodha hiyo ni pamoja na Nigeria, Ghana, Ethiopia, Morocco na Tunisia.
76
Fausto Isidro Meza Flores, anayejulikana kwa jina la El Chapo Isidro, amekamatwa nchini Mexico katika operesheni ya vikosi vya usalama katika jimbo la Sinaloa. El Chapo Isidro anadaiwa kuwa mmoja wa viongozi wakubwa wa mtandao wa biashara ya dawa za kulevya nchini Mexico na amekuwa akitafutwa kwa muda mrefu na mamlaka za Marekani na Mexico. Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa, operesheni hiyo ilihusisha jeshi la Mexico na vikosi vya usalama, huku kukiwa na mapigano yaliyosababisha vifo vya watu kadhaa.
150
Waziri wa Elimu wa Korea Kusini, Choi Kyo-jin, amejiuzulu kufuatia sakata la udanganyifu katika mitihani ya kuingia vyuo vikuu iliyohusisha matumizi ya teknolojia ya Akili Mnemba (AI). Akizungumzia uamuzi huo, Choi amesema wizara yake imeshindwa kujiandaa mapema kukabiliana na changamoto hiyo, akisisitiza kuwa hawezi kukwepa wajibu wake kama kiongozi wa sekta ya elimu nchini humo. Sakata hilo limezua mjadala kuhusu usimamizi wa mitihani na changamoto zinazoletwa na matumizi ya teknolojia ya AI katika sekta ya elimu.
92
Shirikisho la Mpira Barani Afrika (CAF) limeidhinisha Lugha ya Kiswahili kuwa moja ya lugha rasmi za shirikisho hilo baada ya kufanya mabadiliko madogo katika Katiba ya CAF. Rais wa CAF Patrice Motsepe ametangaza hatua hiyo baada ya kupigiwa kura nyingi na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 48 wa CAF uliofanyika Jijini Abuja, Nigeria. Kufuatia uamuzi huo, Kiswahili kinaungana na lugha nyingine nne ambazo Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu na Kireno kuwa lugha rasmi zinazotumika katika shughuli za CAF ikiwemo mikutano na matukio mbalimbali yanayoandaliwa na CAF.
1
94
Tanzania imepata nafasi ya kuongoza kwa idadi ya miji itakayotumika kuandaa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027, baada ya kutengewa miji mitatu kati ya sita itakayotumika katika michuano hiyo. Miji ya Dar es Salaam, Arusha na Zanzibar ndiyo itakayoiwakilisha Tanzania katika michuano hiyo, huku Uganda ikipata miji miwili ambayo ni Kampala na Hoima. Kwa upande wa Kenya, itakuwa na mji mmoja pekee wa Nairobi kwa ajili ya kuandaa michezo ya AFCON 2027. Michuano hiyo itafanyika kuanzia tarehe 19 Juni hadi 17 Julai, 2027.
2
169
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan, amesema kuwa sera ya Uturuki inaweka kipaumbele katika ulinzi wa Saudi Arabia, huku akithibitisha kuwa hakuna uamuzi ambao umefikiwa kuhusu kupeleka wanajeshi wa Uturuki nchini Yemen. Fidan alisema kuwa mkataba wa usalama wa Makkah haulengi nchi yoyote. Badala yake, alisema, nchi wanachama zinalenga kujenga suala la kuaminiana na kuimarisha ushirikiano mpana wa kiuchumi. Alifafanua kuwa kifungu cha ulinzi wa pamoja kinachofanana na Ibara ya 5 ya mkataba wa NATO hakimaanishi kwamba hatua za kijeshi zitachukuliwa moja kwa moja kila tishio linapotokea. Badala yake, hatua hizo zinahitaji tathmini ya vitisho, ushirikiano wa kiintelijensia, mipango ya pamoja ya ulinzi na idhini ya Bunge la Uturuki.
1
117
Mkuu wa Ujasusi wa Uturuki Ibrahim Kalin amekutana na kiongozi wa kisiasa wa Hamas Khalil al-Hayya na ujumbe wa viongozi waandamizi jijini Istanbul: - Majadiliano yamegusia muendelezo wa mashambulizi ya Israel katika eneo la Gaza na eneo linalokaliwa la Ukingo wa Magharibi - Vurugu za walowezi wa Israel na kuondolewa kwa lazima kwa Wapalestina katika makazi yao pia limejadiliwa - Kalin ametilia mkazo nafasi ya Uturuki katika kuwaunga mkono Wapalestina na jitihada zake na wapatanishi na washirika za kupeleka misaada ya kibinadamu Gaza
111
Mwanariadha wa mbio ndefu kutoka Kenya, Diana Wanza, ameitengea nafasi kama mmoja wa nyota mahiri na wa kusisimua wa riadha barani Afrika. Kuanzia kushinda mataji ya Afrika na medali ya fedha katika Michezo ya Jumuiya ya Madola, hadi kushika nafasi ya pili katika Nusu Marathon ya Valencia, Wanza anajenga taaluma ya kuvutia katika mbio za uwanjani na barabarani. Katika sehemu hii ya mfululizo wetu kuhusu wanariadha, tunamwangazia na azimio lake linalomsukuma kuelekea kwenye jukwaa la kimataifa.
121
Tamasha la Utamaduni la Ethnosport linaendelea nchini Saudi Arabia na hii ndio mara ya kwanza kufanyika nje ya Uturuki. Washiriki kutoka sehemu mbalimbali wanaonesha umahiri wao katika michezo ya jadi na shughuli za kitamaduni katika mji mkuu Riyadh, kama sehemu ya Msimu wa Riyadh (Riyadh Season). Tamasha hilo limeandaliwa na Umoja wa Dunia wa Ethnosport (World Ethnosport Union) chini ya kauli mbiu “Mila za Dunia mjini Riyadh,” na litaendelea hadi Novemba 28.
131
Raia 16 wa China na raia 4 wa Zambia wamekamatwa kwa tuhuma za uchimbaji haramu wa dhahabu na uchafuzi wa Mto Muneshi, katika eneo la Chifu Mukungule, Wilaya ya Mpika, Mkoa wa Muchinga nchini Zambia. Kukamatwa kwao kulifanikishwa na Tume ya Udhibiti wa Madini (MRC), Shirika la Usimamizi wa Mazingira la Zambia (ZEMA) pamoja na vyombo vya usalama vya serikali. Watuhumiwa hao walikutwa wakijihusisha na shughuli za uchimbaji na usindikaji wa dhahabu bila kuwa na leseni zinazohitajika wala vibali kutoka kwa mamlaka husika. Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa watu hao walikuwa wakichimba dhahabu kutoka mtoni kwa kutumia kemikali isiyotambulika, ambayo inashukiwa kuchangia katika uchafuzi wa mto huo.
1
3
228
Viongozi mbalimbali pamoja na zaidi ya wajumbe 1,700 kutoka duniani kote wamekutana nchini Tanzania katika sherehe ya Usiku wa Madini, ambayo lengo lake ni kufurahia hatua iliyopigwa katika kubadilisha madini na kuyaongezea thamani hadi kufikia bidhaa ya mwisho sokoni. Mgeni rasmi wa sherehe hizo alikuwa ni Waziri Mkuu wa Tanzania Mwigulu Nchemba. Sherehe hiyo pia imehudhuriwa na Waziri wa Madini wa Kenya Hassan Ali Joho ambae ameandika katika ukurasa wake wa X, “Tanzania inajivunia madini ya Tanzanite, madini ya kipekee yanayopatikana Tanzania pekee, Kenya nayo ina Travorite, inayopatika Kaunti ya Taifa Taveta, madini ya kipekee nchini Kenya ambayo tutayaongezea thamani na kuyafanya sehemu ya ukuaji uchumi wetu.” Mawaziri wengine wa madini waliohudhuria pia ni kutoka Uganda, Rwanda, Ghana, Saudi Arabia na Somalia.
167
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akizungumza wakati wa sherehe za ufunguzi wa Mahakama ya Gaziosmanpasa jijini Istanbul
1
237
Maafisa wanafunzi kutoka nchi tisa za Afrika wamehitimu mafunzo ya kijeshi katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) kilichopo Monduli mkoani Arusha nchini Tanzania. Maafisa hao wamehitimu katika taaluma mbalimbali ikiwemo urubani, udaktari bingwa, uhandisi, ualimu na uchumi. Wahitimu hao wanatoka Afrika Kusini, Ethiopia, Burundi, Kenya, Msumbiji, Namibia, Rwanda, Uganda na Zambia. Rais Samia Suluhu Hassan ambae pia ndiye Amiri Jeshi Mkuu, ameongoza shughuli ya kuwatunuku shahada maafisa hao.
1
154
Waziri wa Ujenzi nchini Tanzania Masanja Kadogosa, ameagiza kusimamishiwa usajili wa aliyekuwa Mhandisi Mshauri (Doch Limited) wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Tanga - Pangani yenye urefu wa kilomit 50 ambayo imeanza kupata nyufa kabla ya kukamilika. Wakati huo huo, ameiagiza Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) kufanya uchunguzi wa kina kuhusu utendaji wa Mhandisi Mshauri huyo, ili kubaini iwapo kulikuwa na uzembe au ukiukwaji wa maadili ya taaluma katika usimamizi wa mradi huo. Kadogosa ametoa maelekezo hayo alipokuwa Pangani mkoani Tanga wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya miundombinu ya Barabara ya Tanga - Pangani Pamoja na Daraja la Pangani.
1
284
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, ametuma salamu zake za rambirambi kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Naibu Rais wa nchi hiyo Phumzile Mlambo-Ngcuka. Katika ujumbe wake, Rais Ramaphosa amesema, muda mfupi amepokea taarifa za kifo na amehuzunika kwa sababu, alikuwa mzalendo wa kweli aliyeitumikia nchi yake kwa upendo. Phumzile Mlambo-Ngcuka amewahi kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya Makamu wa Rais wa Afrika Kusini kati ya mwaka 2004 hadi 2008. Mpaka kifo chake, alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji Umoja wa Mataifa kitengo cha Wanawake chini ya Katibu Mkuu wa UN.
1
3
212