
ALT Mjumbe wa Kamati ya Taasisi za Habari Zanzibar (ZAMECO) na Mwenyekiti wa Klabu ya Wandishi wa Habari Zanzibar (ZPC), Abdallah Mfaume, akifafanua jambo wakati wa mkutano wa wanahabari kuhusiana na maazimio yaliyofikiwa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani Zanzibar yaliyofanyika Mei 23, 2024. Kulia ni Mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni Mwenyekit wa WAHAMAZA, Salim Said Salim na kushoto ni Dk. Mzuri Issa, Mkurugenzi wa TAMWA Zanzibar.

ALT WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Dk. Saada Mkuya Salum, akipata maelezo juu ya kufanya malipo kupitia mfumo wa Air Pay kabla ya kuuzindua kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, katika hoteli ya Golden Tulip, Uwanja wa ndege Zanzibar.

ALT MWANZILISHI Mwenza wa kampuni ya Air Pay Tanzania, Yasmin Chali (kushoto) akitiliana saini mktaba wa ushirikiano na Kamishna wa Kamisheni ya Ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi, Dk. Bili Kiwia, baada ya kuuzindua kwa kampuni hiyo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi na Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Dk. Saada Mkuya Salum katika hoteli ya Golden Tulip, Uwanja wa ndege Zanzibar





























