Zanzibar Press Club (@zanzipress16) header
Zanzibar Press Club (@zanzipress16) profile picture
Joined February 2016
Photo by Zanzibar Press Club (@zanzipress16)Photo by Zanzibar Press Club (@zanzipress16)Photo by Zanzibar Press Club (@zanzipress16)Photo by Zanzibar Press Club (@zanzipress16)Photo by Zanzibar Press Club (@zanzipress16)Photo by Zanzibar Press Club (@zanzipress16)Photo by Zanzibar Press Club (@zanzipress16)Photo by Zanzibar Press Club (@zanzipress16)Photo by Zanzibar Press Club (@zanzipress16)Photo by Zanzibar Press Club (@zanzipress16)
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema matarajio ya Watanzania ni kuona mahakama inasimamia haki. Ametoa kauli hiyo Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, wakati akimuapisha Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, George Mcheche Masaju. @Kaziinaongea
38
UIMARISHAJI usafi wa mji ni miongoni mwa mambo ya msingi kwa ajili ya ulinzi wa afya za wananchi. Katika kufikia hatua hiyo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kupitia Idara Maalum na kampuni ya Hayles Tanzania Ltd, imezindua kampeni ya usafi kwenye mkoa wa Mjini Magharibi.
15
WAANDISHI wa habari wameombwa kuendelea kuihamasisha jamii kutumia bidhaa zenye ubora na kutoa taarifa kwa Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) pindi wanapobaini uwepo wa bidhaa zisizo na ubora zinazozalishwa au kuingizwa nchini.
14
WAANDISHI wa habari wamehimizwa kuzingatia sheria za taaluma yao na uchaguzi ili kuwa na uchaguzi huru na kuochochea ukuaji wa demokrasia nchini. Mkurugenzi wa Tume Uchaguzi Zanzibar, Thabiti Faina alitoa wito huo katika mkutano mkuu wa @zanzipress16 uliodhaminiwa na @psssftz
2
2
59
PUMA ENERGY YAFUTARISHA WADAU WAKE MKURUGENZI Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Fatma Abdallah, amesema wanafanya kazi kwa karibu na wadau wa sekta ya anga pamoja na na mamlaka za serikali ili kukuza biashara na uchumi wa Zanzibar na kutoa huduma za viwango vya kimataifa.
39
JANUARI 28, 2025 jijini Dar es Salam, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Organ), Dk. Samia Suluhu Hassan aliongoza Mkutano wa Dharura  wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi hiyo.
21
AfDB YAIPONGEZA TANZANIA KUSAMBAZA UMEME RAIS wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Dk. Akinwumi Adesina, amesema Tanzania ni nchi ya mfano katika uwekezaji wa miundombinu ya umeme na kusambaza umeme vijijini jambo linaloonesha uwazi na uwajibikaji wa viongozi wake. #KAZIINAONGEA
17
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania inatarajia kuwekeza kwenye miradi ya jotoardhi ambapo Megawatt 30 zitaingizwa kwenye gridi ya Taifa ifikapo mwaka 2026/2027. @Kaziinaongea @UTPCtz @usembassytz @SweAmbTZ @SwedeninTZ
16
KATIKA kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, taasisi ya ADA Cottrell ya Washington Marekeani imezindua tawi nchini kwa lengo la kuunga mkono jitihada za kupambana na dawa za kulevya.
92
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ametoa zawadi kwa kina mama waliojifungua usiku wa kuamkia kilele cha miaka 61 ya mapinduzi ya Zanzibar katika hospitali ya Mkoani Pemba ambapo watoto 82 walizaliwa katika hospitali mbali mbali Unguja na Pemba.
29
HATUA ya Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kupandisha bei ya zao la korosho ni miongoni mwa ahadi alizozitoa kuimarisha maisha ya wakulima kwa kuwapatia bei nzuri ya mazao yao.
31
ZANPRESS - JUKWAA LA HABARI : Watendaji, wadau wa uchaguzi wapatiwa mafunzo ya u... zanpress16.blogspot.com/2024…
14
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, akiwaoongoza viongozi wengine kumuombea dua aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Afrika, Dk. Faustine Ndugulile, aliyefariki dunia hivi karibuni nchini India.
36
WAZIRI wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Tabia Maulid Mwita, amezindua Jumuiya ya Maafisa Habari na Mawasiliano Zanzibar (ZICCO) na kuwataka wanachama wa taasisi hiyo kutoa taarifa za utekelezaji wa majukumu ya taasisi zao ili wananchi wajue kinachoendelea.
43