Pinned Tweet
Sheli zimeanza kufungwa.
Vyakula vimenunuliwa sana.
Maji hamna.
Mtandao umeanza kusumbua.
KESHO UNABAKI NDANI KUFANYA NINI.
TOKA NJE, SIRI NI NAMBA.
Leo nilikuwa na huzuni sana, ila baada ya kusoma COMMENTS moyo wangu umepata furaha kubwa mno!
Kumbuka hii ni sampuli ya comments walau 30, kwenye 2000+, na 97.23% tunaongea lugha moja.
WATANGANYIKA bado kidogo, ukombozi unakuja.🙏🏾
It’s Saturday lakini it doesn’t even feel like one. Nimechoka sana tangu jana, nina huzuni kubwa moyoni.
But nimekumbuka, the harder the struggle the more glorious the triumph!
Jonathan unataka kuanza kutulaumu na sisi sasa??
Mwenyekit Tundu Lissu amehukumiwa kifungo cha miaka minne kwa kosa la uchochezi ambalo, kwa mtazamo wangu, ni la kutengenezwa. Safari sasa ni kwenda Mahakama ya Rufaa, lakini tusisahau kwamba hata Mahakama ya Rufaa haiwezi kuwa mbadala wa dhamiri ya umma katika kutetea haki na kupinga matumizi mabaya ya mifumo ya dola.
Mahakama ya rufaa ya Lissu haipaswi kuwa Mahakama ya Rufaa pekee. Inapaswa kuwa umma wote tunaohofia kwamba kesi hizi zinatumika kama njia ya kuwanyamazisha na kuwadhibiti wanasiasa wakosoaji.
Hatari kubwa zaidi si kifungo cha Lissu pekee. Ni uwezekano wa kifungo kutengeneza mazoea hatimaye kuwa sehemu ya mfumo wa kawaida wa kudhibiti upinzani. Hapo ndipo tunapopaswa kuwa na wasiwasi.
Leo hukumu imetolewa, lakini nchi inaendelea na shughuli zake kana kwamba hakuna jambo kubwa lililotokea. Kana kwamba ni mtu mwingine wa kawaida tu aliyefungwa. Hii ni ishara inayopaswa kutufanya tutafakari kwa kina kuhusu hali ya dhamiri ya jamii yetu.
Watu wengi, wakiwemo wanachama wetu, tayari wako mahabusu. Tusipojiuliza kwa pamoja tunakoelekea, tunaweza kuamka siku moja na kukuta magereza yamekuwa sehemu ya kawaida ya maisha ya kisiasa ya nchi yetu.
Uonevu hauzuiliwi na nguvu ya waliouonewa pekee, bali pia na dhamiri ya jamii inayokataa kuuzoea.
Kukaa kimya mbele ya jambo linalogusa haki za msingi za binadamu kunaweza kuifanya jamii izoeane na hali ambayo kesho inaweza kumkuta yeyote kati yetu.
kosa la Uhaini lililopo kwenye hati halina "Alternative Charge" (kosa mbadala) lililoainishwa moja kwa moja kwenye hesabu ya kesi hiyo.
Ikiwa majaji watashikilia misingi hiyo, maana yake chaguo litakuwa ni aidha kumtia hatiani kwa uhaini au kumwachilia huru kabisa.
RT @BrendaRupia: Its clear that we have now movef from Treason to looking for ways to detain Tundu Lissu with smallers cases such as Sediti…
Hercules🇰🇪 retweeted
Replying to @Herculses @TunduALissu
Proverbs 28:15–16: "Like a roaring lion or a charging bear is a wicked ruler over a helpless people. A tyrannical ruler lacks great understanding, but one who hates unjust gain will lengthen his days."
Mhe. @TunduALissu, umekuwa kwenye DP yangu kwa zaidi ya siku 500.
Siku hiyo nilikuwepo, moyo ukiwa mzito, lakini smile yako ilinipa faraja.
Kesho ni siku ya hukumu. Tumeyasikia na tunajua mipango yao, lakini Mungu ndiye ajuaye yajayo.
Tunaamini utaachiwa huru.
AMEN.🙏🏾
Hercules🇰🇪 retweeted
As an American constitutional lawyer, I have personally litigated cases defending the rights to free expression and due process. These are fundamental principles of human liberty. For that reason, I am closely following the outcome of Tundu Lissu’s trial proceedings, and the broader implications for the rule of law.
Hercules🇰🇪 retweeted
Twaha always says MSIOGOPE
Lissu always says MSIOGOPE
MNAJUA KWA NINi?
Kwa sababu SILAHA PEKEE waliobaki nayo CCM na Samia na wauaji wao ni KUTUTISHA - wanateka, kuua na kufunga mmoja mmoja ili tuingiwe na Hofu
Tuwe PARALYZED with FEAR
Ndo maana wanatuchukia wengjne maana tunawaondolea wengine HOFU!
Angalieni machawa hata hawa walionunuliwa juzi tu - ujumbe wao ni kusambaza HOFU na kusema hatutaweza kuwatoa hawa wauaji eti turidhiane!
Si KWELI ❌
Tumeshashinda ila wanatunyong’onyeza na Hofu!
Tusikubali! Have courage wapendwa
This is the last push ✊🏽
Mungu wetu atasimama na kudhihirisha Utukufu wake kinachohitajika ni KUSIMAMA IMARA!
Tusimame bila hofu tuhesabiwe na tujitokeze kwa wingi mahakamani kesho
Mungu ameshamaliza anasubiri tuchukue ushindi!
#FreeTwahaMwaipaya #FreeTunduLissu
Hercules🇰🇪 retweeted
Mkiona humu si type type sana jueni kuna mambo 😁
Narudia MSIOGOPE yajayo yanafurahisha!
Kuna watu tutamalizana nao kiulaloulalo acha watambe kwa huu muda mfupi waliobaki nao!
#TutaelewanaTu















