IMANI 🇹🇿 retweeted
I am a big believer in polygamy, when done properly, it works! #Random
IMANI 🇹🇿 retweeted
Wakuu😂😂😂. Kwanza muelewa kuwa sio kila unaedhani ni afisa usalama ni afisa usalama. Intelijensia na usalama ni network ya watu walio rasmi na wasio rasmi.
Katika taaluma ya ujasusi, kuna istilahi mbalimbali zinazotumika kuelezea watu, majukumu na rasilimali zinazohusika katika ukusanyaji, uchambuzi na usimamizi wa taarifa za kiintelijensia.
Istilahi kama Agent, Asset, Source, Informant, Case Officer na *ntelligence Officer zina uhusiano wa karibu, lakini kila moja ina maana na dhima yake. Kuzitofautisha ni muhimu katika kuelewa namna taasisi za kijasusi zinavyofanya kazi.
1. Intelligence Officer
Huyu ni afisa aliyeajiriwa rasmi na taasisi ya kijasusi na mwenye jukumu la kutekeleza majukumu mbalimbali ya kiintelijensia.
Majukumu yake yanaweza kujumuisha:
- Kukusanya na kuratibu upatikanaji wa taarifa za kiintelijensia.
- Kutambua na kuendeleza vyanzo vya taarifa.
- Kutathmini taarifa zinazokusanywa.
- Kuandaa ripoti za kiintelijensia.
- Kusaidia utekelezaji wa majukumu na shughuli za kiintelijensia.
Afisa huyu anaweza kufanya kazi katika makao makuu ya taasisi au katika maeneo mbalimbali ya kiutendaji (field operations).
2. Agent
Agent ni mtu ambaye amejiriishwa, ameelekezwa au amekubali kutekeleza majukumu fulani ya ukusanyaji wa taarifa au shughuli nyingine za kiintelijensia kwa niaba ya taasisi ya kijasusi.
Kwa mfano, taasisi ya kijasusi ya nchi moja inaweza kumshawishi mtu mwenye uwezo wa kupata taarifa nyeti ndani ya taasisi ya serikali ya nchi nyingine ili aweze kutoa taarifa kuhusu sera, mipango au shughuli za serikali hiyo.
Ni muhimu kuelewa kwamba Agent si lazima awe mwajiriwa rasmi wa taasisi ya kijasusi anayoiunga mkono.
Tofauti kuu: Agent ni mtu anayetekeleza shughuli za kiintelijensia kwa niaba ya taasisi, wakati Intelligence Officer kwa kawaida ni afisa aliyeajiriwa rasmi na taasisi hiyo.
3. Asset
Asset ni mtu, uwezo au rasilimali ambayo taasisi ya kijasusi inaweza kuitumia au kunufaika nayo katika kutimiza malengo yake ya kiintelijensia.
Katika muktadha wa Human Intelligence (HUMINT), istilahi hii mara nyingi hutumika kumaanisha mtu ambaye anaweza kutoa taarifa, kuwezesha upatikanaji wa taarifa au kutoa msaada wenye thamani ya kiintelijensia.
Kwa mfano, Asset anaweza kuwa:
- Mtu mwenye ufahamu wa ndani kuhusu mienendo ya kisiasa.
- Mtu mwenye uhusiano na watu wenye ushawishi katika taasisi muhimu.
- Mtu mwenye uwezo wa kupata taarifa kuhusu shughuli za shirika fulani.
- Mtu mwenye uelewa wa kina kuhusu nia na mikakati ya watu au taasisi mbalimbali.
Asset ni istilahi pana zaidi kuliko Agent. Si kila Asset ameajiriwa au kuelekezwa kufanya shughuli maalumu za ukusanyaji wa taarifa kama ilivyo kwa Agent.
4. Source
Source ni chanzo ambacho taarifa za kiintelijensia zinatoka.
Vyanzo vinaweza kuwa vya kibinadamu au visivyo vya kibinadamu.
Mifano ni:
- HUMINT (Human Intelligence): Taarifa zinazopatikana kupitia watu.
- IMINT (Imagery Intelligence): Taarifa zinazopatikana kupitia picha, ikiwemo picha za setilaiti.
- SIGINT (Signals Intelligence): Taarifa zinazopatikana kupitia uchambuzi wa ishara za mawasiliano na mifumo ya kielektroniki.
- OSINT (Open-Source Intelligence): Taarifa zinazopatikana kutoka kwenye vyanzo vya wazi vinavyopatikana kwa umma.
- Nyaraka, kumbukumbu na taarifa rasmi za taasisi mbalimbali.
Kwa hiyo, Source si lazima awe mtu. Ni istilahi inayojumuisha kila chanzo kinachoweza kutoa taarifa za kiintelijensia.
5. Informant
Informant ni mtu anayetoa taarifa kwa taasisi ya kijasusi au kiusalama kuhusu watu, matukio, mienendo au shughuli zinazoweza kuwa na umuhimu wa kiusalama.
Taarifa anazoweza kutoa zinahusu:
- Shughuli za kihalifu.
- Mienendo inayoweza kuhatarisha usalama.
- Vitendo vinavyotia mashaka.
- Maendeleo ya kisiasa na kijamii.
- Shughuli ndani ya taasisi au makundi mbalimbali.
Informant anaweza kutoa taarifa kwa hiari au katika mazingira mengine kwa misingi ya makubaliano maalumu.
Hata hivyo, si kila Informant ni Agent. Mtu anaweza kutoa taarifa muhimu bila kuwa amejiriishwa kutekeleza shughuli za kiintelijensia kwa niaba ya taasisi.
6. Case Officer (Handler)
Case Officer ni afisa wa kijasusi mwenye jukumu la kusimamia mahusiano na vyanzo vya taarifa vya kibinadamu (Human Intelligence Sources), wakiwemo Agents.
Majukumu yake kwa ujumla yanaweza kujumuisha:
- Kutathmini uaminifu na ubora wa taarifa zinazotolewa na vyanzo.
- Kusimamia mahusiano ya kiutendaji na vyanzo vya taarifa.
- Kutathmini taarifa zinazopatikana.
- Kuhakikisha vyanzo vinashughulikiwa kwa kuzingatia taratibu na usalama.
- Kuratibu utoaji wa taarifa za kiintelijensia kwa mamlaka husika.
Istilahi Handler wakati mwingine hutumika kwa maana inayofanana na Case Office, ingawa matumizi yake hutofautiana kati ya taasisi.
7. Intelligence Analyst
Huyu ni mtaalamu anayehusika na kuchambua taarifa zinazokusanywa kutoka kwenye vyanzo mbalimbali ili kubaini mifumo, mahusiano, mwenendo na viashiria vinavyoweza kuwa na umuhimu wa kiintelijensia.
Majukumu yake ni pamoja na:
- Kuchambua taarifa kutoka vyanzo mbalimbali.
- Kutathmini uaminifu na usahihi wa taarifa.
- Kubaini uhusiano kati ya matukio na wahusika mbalimbali.
- Kutambua mienendo na viashiria vya vitisho vinavyoibuka.
- Kuandaa tathmini na ripoti za kiintelijensia kwa ajili ya kusaidia maamuzi ya kimkakati.
Tofauti na Field Officer au Case Officer, Intelligence Analyst anaweza kufanya kazi zaidi katika uchambuzi wa taarifa kuliko ukusanyaji wake wa moja kwa moja.
Sasa sisi tunadhani kila mwenye uhusiano na vyombo vya usalama ni intelligence officer, sio. Na sio kila government official ni mtu wa usalama japo bila shaka watu wa usalama wako kila idara na kila ofisi 😀.
Sijui kama nimejibu swali lako. Hii ni kwa mujibu wa movies na series.
Replying to @thomasjkibwana
Kwa nilivyokuelewa hapa wachambuzi wa masuala ya kiuchumi, kisiasa na kijamii wenyewe sio lazima wawe directly recruited kwenye Chombo. Hapa nikikuelewa zaidi ni ngumu kuwatofautisha government officials na majukumu ya chombo 😂😂😂
IMANI 🇹🇿 retweeted
Maelezo ya TRA yamenyooka sana... Sakata la Ommy Dimpozi... Baba Levo alizingua sana
Remittances: Tanzania Edges Out Saudia
Tanzania has edged out Saudi Arabia as a leading source of remittances to Kenya for the first time.
In August 2026, Kenyans in Tanzania sent home Sh1.52 billion, narrowly beating Saudi Arabia's Sh1.50 billion.
#NTVTonight @Karanja_Ibrah @SylviaKathoni
IMANI 🇹🇿 retweeted
Utawala unapaswa kuwa na hela na ndo maana kila siku nasema Mungu abariki wanaume wote pesa. Yani pesa ni muhimu sana mwanaume kuwa nayo
Ni maombi yangu leo wanaume wote mbarikiwe na kufunguliwa milango ya kifedha🙏
IMANI 🇹🇿 retweeted
Leo tumeshuhudia burudani katika Dabi nyingine ya Kariakoo kupitia mchezo wa Ngao ya Jamii. Pongezi kwa Klabu ya Yanga kwa ubingwa wa 10 wa Ngao ya Jamii.
Ninazitakia kila la heri timu zote katika msimu mpya wa Ligi Kuu, pamoja na mashindano mengine ya kitaifa na kimataifa.
IMANI 🇹🇿 retweeted
Ninawapongeza Klabu ya Simba kwa tamasha lililofana la Simba Day 2026, lililoambatana na maadhimisho ya kutimiza miaka 90. Ninawatakia kila la kheri katika msimu ujao wa Ligi Kuu.
IMANI 🇹🇿 retweeted
ASANTE GSM. ASANTE BILIONEA
Straika bora Afrika PETER SHALULILE ni mali yetu Wananchi🔰
#TimuYaWananchi
#DaimaMbeleNyumaMwiko
IMANI 🇹🇿 retweeted
I stated that Tanzania is wealthier, has better planning compared to Kenya. Round II. In fact second only to Egypt in Africa.
Tanzania is constructing 2500km of SGR and financing 60% from Exchequer. About US$ 5B and borrowing only US$2B.
Kenyan SGR is only 600km so far and it is borrowing 100%.
Kenya can't do 200km of a mere Bitumen Road Limuru Mau Summit and has to resort to a PPP which is a very expensive Loan???
Tanzania has just completed Julius Nyerere 2115MW HPP at a cost of US$ 2.9 Billion from Exchequer and has paid 100% No loan.
Kenya doesn't have money for for a much smaller Grand Falls 1000 MW.
Kenya's Debt is KShs 13 Trillion. Tanzania is 50% of that figure.
In fact which is the biggest Project Kenya has financed from its own resources the last 20 years?
I can't think of any.
Forget the cooked GDP figures that Kenya is the biggest Economy.
IMANI 🇹🇿 retweeted
#TajiriLaKihaya
Habari za Asubuhi JANJA wa Timber…
Kulikua na haja gani ya kunitukana na kuniMention kwenye mambo yenu??
Mbona nlisha KuBLOCK kila mtu afanye mambo yake?
Jana nlikua Safarini nlichoka saana,sikupata muda wa kukujibu on time! Aahh nmesahau nlikua nasafiri na ndege ya kuunganisha Bukoba-mwanza alafu Dar…
Ila saa hizi muda ninao wa kutosha nkasema nianze Na hili kabla sijasahau!
Iko hivi, kwanza kabisaa Naomba Mnisamehe kama nliwakwaza nlikosea saana mimi naomba yaishe 🙏🏽
Ila hata nkiishia hapo kwenye msamaha najua uta QUOTE Na matusi yako kama kawaida,Maana akili zako kidogo bangi iliharibu😅
BADO mimi ntasimama kwa maneno yangu nlioyasema kipindi kile Na hii Post yako imekuja KU Confirm my Points vividly!
Siku zote mimi huwa nasema kinacho tuponza sisi waTanzania ni UBINAFSI na UMIMI…
Kwanza kabisa HONGERENI saana kwa ushindi huu mnono ma milionea tunazidi kuongezeka jambo zuri saana - 13m sio hela ndogo mtaji kabisaa huu..
Ila swali la msingi la kujiuliza 13m at WHAT COST???
Hebu turudi nyuma kidogo labda utanielewa vizuri-
Kipindi bwana mdogo katekwa- watu wote tuliStopisha mambo yetu ya kila siku, tukawa tunashinda SPACE humu hadi tukaunda na chama cha vijana wa X ,kupush #FreeSativa hadi ikafikia hatua kuwaBlock wale wote waliokua wanaPush # tofauti na hio wakiwemo mboga mboga…
Baada ya Sativa kupatikana kila mtu alisikitika saana kutokana na yale mazingira - Nchi nzima magazeti,vyombo vya habari vyote ikawa habari ni SATIVA hadi vyombo vya kimataifa ikiwemo BBC ilireport- hadi watetezi wa haki za binadamu waliingilia kati-
That was a Golden Opportunity ya kupata #JusticeForSativa … hadi serikali tuliwabana vizur saana!
Na tulitaka SATIVA ndio awe kijana wa mwisho kutekwa- jambo hilo lisiwahi tokea tena!
Lakini Ghafla mtu ambae dunia nzima inasubir atoe Tamko anaanza kupost mikeka😅 it was a big disappointment!
Na hapo ndipo kupata haki kulipo potea hadi leo hii!
Alafu unakuja kutuambia, tulipoteza jambo la msingi kama hili kisa milion 13???
Laiti tungebaki kwenye mstari Na kuwabana vile kwa UMOJA ule… leo hii hatungekuwa tunaongea habari za akina SOKA Na wengineo KUTEKWA tena…
Vijana wanaendelea kutekwa kwa sababu ya 13m what a JOKE!
Sisi ambao kidogo tulikua tunakutana Na wabunge/mawaziri kipindi hicho tunafaham ni jinsi gani tulikua tumewakamata pabaya serikali Na walikua wanakiri.
Kama unakumbuka kipindi kile nliwauliza kama ni hela ndio tatizo semeni tujichangishe tena!
Au mliona kipindi kile kwa kua ana viewers wengi mtumie huo mwanya kupush mambo yenu? Kwa hio mlitutumia? Then you are an opportunistic.
Laiti kama mngeliweka wazi hili toka mwanzo- tungetumia account nyingine Au hata ya kwako na labda angekuwa namba moja africa nzima!
Mbona kipindi ametekwa wewe JANJA. Haukua unapost mikeka?? Maana shindano lilikua bado linaendelea?
Maana ulikua unatupatia update kila siku ya kinachoendelea hadi muda mwingine ulikua unapost umezunguka vituo vya polisi hadi umeishiwa nauli ya Bolt- alafu leo unakuja kutamba online jinsi mna mamilion kwenye account 😅 kwa hio kipindi kile ulikua unatudanganya-ulitaka Huruma?? Huu kama sio Utapeli ni nn?
Anyway- tumewaelewa from your Post mlifaham mnachokifanya sio sawa kutoa watu kwenye Reli Ila mliona kwa wakati huo HELA kwanza..
Sasa kuanzia leo, Hamna morale authority ya kuwakemea wa push hashTag, Maana na wenyewe wanapata pesa!
Kuanzia leo hamna morale authority ya kumkemea spika wabunge na wabunge ambao wameshindwa kuongea maswala ya UTEKAJI bungeni Maana na wenyewe wana linda Kibarua chao…
Kuanzia leo hamna morale authority ya kumsema Shangaz Fatma kukataa kumuita huyu raisi Evil wakati hayati alimuita hivyo…
KARIBUNI MNIPIKE- muda leo ninao wa kutosha kabisaaa😅







































