Jackson (@JatJackson) profile picture
Joined July 2015
Photo by Jackson (@JatJackson)Photo by Jackson (@JatJackson)Photo by Jackson (@JatJackson)Photo by Jackson (@JatJackson)Photo by Jackson (@JatJackson)Photo by Jackson (@JatJackson)Photo by Jackson (@JatJackson)Photo by Jackson (@JatJackson)Photo by Jackson (@JatJackson)
Karibu Afrika, ukanda wa uhaini kwa wapinzani. Tanzania; Tundu Lissu amehukumiwa uhaini Uganda; Kiiza Besigye anashtakiwa kwa uhaini Rwanda; Victoire Ingabire anashtakiwa uhaini South Sudan; Riek Machar anashtakiwa uhaini Burundi; Alain Bunyoni kahukumiwa uhaini DR Congo; Joseph Kabila amehukumiwa uhaini Zambia; Brian Mundubile anashtakiwa uhaini Niger; Mohamed Bazoum anashtakiwa uhaini Lesotho; Mothetjoa Metsing anashtakiwa uhaini Chad; Succès Masra amehukumiwa uhaini Nigeria; Timipre Sylva anashtakiwa kwa uhaini Guinea-Bissau; Domingos Pereira, pia uhaini Mozambique; Venâncio Mondlane, pia ugaidi Zimbabwe; Job Sikhala anashtakiwa ugaidi Watawala Afrika wanaugua ugonjwa wa udikteta
22
171
881
29,740
TUNDU LISSU ATUZWA NA ULIMWENGU KWA KUPIGANIA DEMOKRASIA. Bunge la Ulaya limemtunza Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA nchini Tanzania Tundu Lissu, tuzo la mwaka huu la SHAKHAROV. Lissu ambaye Kwa Sasa anatumikia kifungo cha 4 jela amepewa Tuzo hilo kutokana na juhudi zake za kutetea Demokrasia na usawa nchini mwake. Thanks so much the @europeanunions @Europarl_EN 🙏
6
140
1
496
12,372
Jackson retweeted
Kama angetaka kuwa nje, angetoka kitambo sana, hata kwa kuwalaghai majamaa kwa hoja ya 'maridhiano' fake. Yuko kwenye "mission" maalum ya KUANIKA uozo wa Mfumo wa Utoaji Haki wa hii nchi. Ndio maana huwa anatabasamu muda wote. Lengo likitimia, tutamuona tu uraiani. TUMUOMBEE.
43
254
4
1,005
86,753
Jackson retweeted
BAIL PENDING APPEAL: Kwa kuwa TAL ameshinda kesi ya UHAINI ambayo haina dhamana, na kukutwa na hatia kwa kosa la UCHOCHEZI, Lissu anaweza kuwa nje kwa DHAMANA kupitia utaratibu unaojulikana kisheria "BAIL PENDING APPEAL" kwa sababu uchochezi una dhaminika, hata kama mtu amefungwa. Ila tu utaratibu ni kwamba, ni LAZIMA mfungwa aanze kutumikia kifungo chake gerezani japo kwa siku moja tu. Hii inawezekana kama mawakili watajenga hoja za AFYA ya Lissu na kwamba atashindwa kupata matibabu stahiki akiwa gerezani. Pia, siku 577 alizokaa gerezani ni fimbo ya kuomba dhamana. Imefanyika mahakama Kuu & pia kuna msimamo wa mahakama ya Rufani juu ya utaratibu huu. HAKI HAIOMBWI bali HUPIGANIWA.
17
195
6
798
27,567
Jackson retweeted
Hata huo UCHOCHEZI dunia nzima inajua LISSU sio “Mchochezi”. Tutashinda kesi zote za KIHUNI na nchi itakombolewa tuu.
15
152
2
1,249
22,798
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 502 Mhe. Lissu anaendelea Anasema uamuzi huu wa kunikuta na hatia na kosa ambalo sikushtakiwa nalo, sikujitetea ni kosa la kutengeneza, effect yake ni kwamba unatoa kinga ya kisiasa kwa wale ambao walihusika mauaji amkubwa ya kisiasa, watatoka na kusema wauaji walishapataikana. Serikali ya Samia imeua watu wengi zaidi ukiachilia historia ya vita vya majimaji, hawa mass murderers watashangilia sana na uamuzi huu kwasababu mmewapa sababu ya kusema aliyesababisha mauaji ya Oktoba 2025 amepatikana na hatia lakini hii haitafunika ukweli. Serikali ya Mwalimu Nyerere iliuwa watu 37 mwaka 1977 na iliwajibika, Peter Kisumo alikuwa Mkuu wa Mkoa w Shinyanga alijiuzulu, na wengine akiwemo Mwinyi. Leo watu 518 walioripotiwa kwa uchache hakuna aliyewajibishwa, uamuzi wenu hautaficha hiyo kashfa. Kwenye sentences guidelines za Mahakama hii, inasema lazima adhabu ya faini itolewe isipokuwa kama ni grave offence, kosa nililoshtakiwa nalo sio grave. Waheshimiwa Majaji hukumu mnayo, ambayo mmeagizwa muitoe, itoeni nawashukuruni sana. Jaji Ndunguru anawasha mic anasema tumesikiliza hoja za pande zote na katika kutoa adhabu tumezingatia sababu kadha wa kadha. Kwanza mshtakiwa umeomba dhamana ili ukate rufaa, tumeangalia hoja ya ugonjwa na kuwa wewe ni mkosaji wa kwanza, hoja ya adhabu ya faini au kifungo. Kifungu cha 390 hakijatoa adhabu na ukisoma kanuni ya adhabu kifungu cha 35 kinahusika pale ambapo hakuna adhabu. Adhabu ni kifungo kisichozidi miaka 5 au fani au vyote viwili na hakijaelekeza faini ni kiasi gani. Tunajua kuwa pale ambapo fani na kifungo vinakuwa vinatolewa first option ni faini. Tumesoma na maamuzi mbalimbali na mengine ambayo tumeshayasema mfano kuzuia uchaguzi ni kukiuka katiba, ukisoma Ibara ya 30(1) imeeleza kuwa hutakiwa kuingilia haki za mtu mwingine. Mahakama inatoa adhabu kwa mshitakiwa kutumikia kifungo cha muda wa miaka 4 na una haki ya kukata rufaa. Majaji wanatoka. Naomba Repost yako.
154
482
28
1,352
80,295
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 498 Jaji Ndunguru anasema katika kutafisiri hicho kifungu cha 319(1-2) cha CPA Mahakama ya Rufani ilielezea kwa marefu na mapana kwenye kesi ya DPP vs Zombe kuhusu kifungu hicho kuwa sio automatic. Kwakuwa mshtakiwa hakushtakiwa na kosa dogo, Mahakama pia haiwezi kutumia kifungu hicho bila kumpa mshtakiwa haki ya kusikilizwa au kumpa notice. Kwa mujibu wa ushahidi uliopo kuwa maneno hayo yalirushwa live ili kuuhabarisha umma na video hizo video hazikutolewa mahakamani na kwa vile hajakanusha kutamka maneno hayo na upande wa jamhuri umesema kuwa alilenga kuchochea umma na mashahidi wa upande wa utetezi nao hawajakataa kuhusu mshtakiwa kutamka maneno hayo. Tumeridhika kwamba mshtakiwa kutamka maneno hayo hadharani mbele ya umma alilenga kuchochea umma ili kuvuruga uchaguzi wa 2025 kwa njia isiyo ya amani kutokana na maneno yake hivyo basi tukiongozwa na maamuzi mbalimbali na kwa muktadha wa kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu kosa lililotengenezwa na kifungu cha 390 ni kosa dogo la uhaini, kifungu cha 390 kinalengo la kuzuia crime katika hatua ya mwanzo before public harm. Kwa tafsiri yetu tunasema kifungu hiki kina prevent nia na present danger. Upande wa mashtaka wanapaswa kuthibitisha kuwa maneno ambayo mshtakiwa aliyatamka kufanya instigation yalikuwa communicated, pia mshtakiwa alilenga kuwa mtu au watu watende kosa. Tunaelewa kwamba kifungu cha 390 kinatumika kwenye kosa lolote hakijataja kosa lolote pale, tunaamini kwamba kufanya kosa la uchochezi kunaweza kupelekea present danger, tunaamini ni minor offence na ni cognate offence kwa mujibu wa 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu. Ni kwa mtazamo wetu sasa kwamba ni common sense kwamba incitement ni component ya offence ya treason hivyo sio lazima mtu awe charged independently. Kulingana na ushahidi uliotolewa mshtakiwa alichochea umma kuvuruga uchaguzi, kuzuia uchaguzi, kuhamasisha uasi na kukinukisha vibaya sana. Upande wa utetezi haujaonyesha ni kwa namna gani walipanga kuzuia uchaguzi, kuhamasisha uasi, na mashahidi wa upande wa Jamhuri walieleza namna ambavyo walishawishika na maneno ya mshtakiwa mfano shahidi wa 4, 5,8 ,11, 13, 14 walishawishika na kujiunga na wale ambao walishawishika ili waweze kuvuruga uchaguzi. Part 499 itaendelea kwenye post inayofuata, Naomba Repost yako.
116
567
27
1,581
148,300
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 496 Upande wa mashtaka walieleza kuwa kauli ya mshtakiwa inatakuwa itazamwe katika muktadha mzima kuwa aliitishia serikali na kuwa mshtakiwa alikuwa na lengo la kuitisha serikali regardless kama serikali ilitishika au la! Ushahidi wa upande wa utetezi mshtakiwa alisema maneno hayo lazima yapimwe katika muktadha wa kisiasa na lengo kwa kauli hiyo ilikuwa ni kueleza msimamo wa kisiasa wa Chadema na lengo lake halikuwa kuitishia Serikali, mtazamo huu ulingwa mkono na shahidi wa 2,3,4 na 5 kuwa kauli ya No reforms, No election ililenga kueleza ushawishi wa kisiasa. Upande wa utetezi ulisema neno uasi lazima nilitazamwe katika muktadha wa kisiasa na kauli hiyo haikuwa na lengo la kuitishia Serikali au kuchochea vurugu. Mshtakiwa alieleza kuwa upande wa mashtaka walipaswa kuthibitisha nia hiyo kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia serikali na sio hisia tu. Mshtakiwa alieleza kuwa upande wa mashtaka walishindwa kuthibitisha Kwa ushahidi uliotolewa kuna mambo ambayo hayabishaniwi, kwanza Chadema imekuwa inatetea mabadiliko ya kikatiba, na mfumo wa uchaguzi na msimamo wa No reforms, No election, kupitia mkutano huo wa 3/4/2025 mshtakiwa alitoa hayo maneno mbele ya viongozi wenzake, wanachama, watia nia na waandishi wa habari na mkutano huo ulirushwa live. Upande wa utetezi wamemaintain kuwa kauli hiyo ni ya kisiasa ililenga umma to boycott uchaguzi na sio kuitishia serikali. Tumeangalia kauli zilizotolewa na mshtakiwa na tumeona kuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja hatujaona kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia Serikali, tumeangalia tafsiri ya shahidi wa 1,2 na 16 tumeona ni assumption haziwezi kuthibitisha kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia Serikali. Tumeona kwamba ushahidi uliotolewa na mashtaka una fall short kuthibitisha shitaka la uhaini hivyo katika kiini hiki cha pili tunaona ushahidi haujakidhi kuonyesha nia ya uhaini. Kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) kuna vitu vitatu ikiwemo factuai issues, mahakama lazima iangalie ushahidi kujiridhisha na tatu ni ushahidi uoi umetolewa. Mahakama inaona kwamba tafsiri ya maneno ya Lissu bila tangible evidence tumeongozwa na kanuni kwamba nia (mens rea) ni internal state of mind lazima liambatane na ushahidi wa kimazingira na vitendo vya kufanya uhaini. Nia ovu siku zote inakuwa inferred kutoka kwa maneno na matendo ya mshtakiwa. Part 497 itaendelea kwenye post inayofuata. Naomba Repost yako.
167
634
28
1,737
148,917
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 495 Suala la uhalali wa hati ya mashtaka liliwahi kulalamikiwa mwanzoni mwa shauri hili na Mshtakiwa na katika uamuzi wake wa Sept 2025 ilieleza kuwa hati ya mashtaka ilikuwa sahihi. Mshtakiwa alisema kuwa Kifungu cha 39(2)(d) kinahitaji kushawishi kikundi cha watu na sio umma kama ilivyoandikwa hivyo alisema hati hiyo inakinzana na Ibara ya 13 ya Katiba ya Tanzania inayohusu uhalali wa kisheria (principal of legality) Katika pingamizi la pili alisema upande wa mashtaka haukueleza taasisi ya serikali ambayo anadaiwa kuitishia na katika hoja ya tatu mshtakiwa alisema haijasema nia au lengo la kufanya huo uhaini kwasababu pia maneno ambayo hayajatumika katika sheria hivyo alisema mahakama ione hati ina mapungufu Upande wa mashtaka walikiri kuwa ni kweli hati ya mashtaka imetumia neno public lakini tafsiri ya neno public kinajumuisha mtu yeyote au kikundi cha watu hivyo walikidhi matakwa ya sheria, katika hoja ya pili walisema hati ya mashtaka imetumia neno executive. Upande wa mashtaka walieleza kuwa majukumu ya Executive ni kutekeleza sheria hivyo mshtakiwa alikuwa anaelewa maana ya neno Serikali na hivyo aliweza kuelewa na kutoa utetezi wake. Mahakama inaona kwamba mapingamizi ya mshtakiwa kuhusu hati ya mashtaka hayana mashiko kwasababu ilishatolea uamuzi huko nyuma na inamaelezo ya kutosha. Neno public katika tafsiri ya kifungu cha 5 cha Kanuni ya Adhabu kinazumzia mtu yeyote au kikundi cha watu, tumeangalia pia kwa umakini ushahidi na utetezi hivyo mshtakiwa alielewa hati ya mashtaka. Maelezo katika hati ya mashtaka yanajitisheleza kabisa na kwa mujibu wa shauri la Nasibu Mahakama inatakiwa kutumia neno kama lilivyo hivyo neno executive linaeleweka kama lilivyotajwa kwenye hati ya mashtaka. Katika hoja ya tatu tunakubaliana kuwa upande wa mashtaka lazima waeleze nia mahususi kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d), hivyo tunaona kwamba mapingamizi yote hayana mashiko kwasababu tulishayatolea uamuzi. Kinachofuata sasa ni kuangalia viini vitatu, viini hivyo ni-; 1. Endapo mshtakiwa yuko chini ya utii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d). Ni jukumu la upande wa mashitaka kuthibitisha hili, pande zote mbili wanakubaliana kwamba 3/4/2025 mshtakiwa alikuwa chini ya utii wa JMT. Hata katika usikilizwaji wa hoja za awali mshtakiwa alikubali kuwa alikuwa na utii wa JMT ni mzaliwa wa Tanzania, ana pasipoti ya Tanzania na 3/4/2025 alitoa maneno hayo akiwa ndani ya JMT, Mahakama inaona kwamba mshtakiwa alikuwa na utii wa JMT. 2. Kiini cha pili ni endapo mshtakiwa alitenegeneza nia ya kuhamasisha umma kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025 kwa lengo la kuitishia serikali kinyume na kifungu cha 39(2)(d). Upande wa mashataka wana wajibu wa kuthibitisha nia hiyo tofauti na political criticism, nia ni internal state of mind na lazima kifafanuliwe na ushahidi, matendo ya mshtakiwa. Upande wa mashtaka waliegemea kwenye hoja kwamba 3/4/2025 mshtakiwa alisema tutazuia uchaguzi, tutahamasisha uasi, tutauvuruga uchaguzi, upande wa mashtaka waliegemea kuwa mshtakiwa alikuwa na nia ya kuitishia Serikali na waliegemea kwa upande wa ushahidi wa mashahidi wao kuwa mshtakiwa ni mtu mwenye ushawishi ndani na nje ya Tanzania. Upande wa Jamhuri waliegemea upande wa ushahidi wa shahidi wa kwanza ambaye aliona maneno hayo yanaviashiriia vya uhaini. Shahidi alieleza kuwa mshtakiwa kutoa maneno hayo mbele ya waandishi wa habari na kusambazwa maneno hayo, mshtakiwa alikusudia kuitishia serikali. Shahidi wa 16 upande wa mashtaka alieleza kuwa alipoona hayo maneno walipanga kuwapiga mawe wapiga kura, shahidi wa 17 alisema alikuwepo kwenye mkutano na kuwa ulirushwa live kwenye mitandao ya kijamii, alisena maneno aliyotamka Lissu hakuona kama yanashida yoyote ile. Part 496 itaendelea kwenye post inayofuata, Naomba Repost yako.
58
537
10
1,471
101,900
KWANINI HUKUMU IVUJE KAMA MAHAKAMA IKO HURU?
9
101
2
527
22,766
Thank you to every influential person around the world who is speaking out against the mass killings of Tanzanian citizens by a government determined to cling to power. Tanzanians cannot fight these gun-wielding killers alone. We need the international community to stand with us, amplify our voices, and support our struggle for justice, freedom, and democracy. KISWAHILI Asanteni kwa kila mtu mwenye ushawishi duniani anayepaza sauti kupinga mauaji ya kikatili ya raia wa Tanzania yanayofanywa na serikali inayong’ang’ania madaraka. Watanzania hatuwezi kupambana na wauaji hawa wenye silaha peke yetu. Tunahitaji jumuiya ya kimataifa kusimama nasi, kueneza sauti zetu na kuunga mkono mapambano yetu ya kudai haki, uhuru na demokrasia.
FORMER BOTSWANA PRESIDENT IAN KHAMA, SPEAKING ABOUT TANZANIA AND THE EVENTS SURROUNDING THE 2025 ELECTION: “What you see in Tanzania is where a person is prepared to kill and murder and slaughter her own citizens in order to stay in power. I think it is just a situation that we never thought we would ever experience and the regional and continental organizations should really be ashamed of themselves for allowing this situation to have happened.” - Ian Khama THE BLOOD BENEATH THE FLAG highlights the events before, during and after Tanzania’s 29 October 2025 election and the unanswered questions left behind. Watch here: youtube.com/playlist?list=PL… #MO29 #TanzaniaMassacre
4
243
1
1,194
57,755
Dainess mdogo wangu walikupiga risasi tabata na mwili wako haukuonekana tukafanya ibada ya picha kanisani 😞 baadae mwili ukapatikana kitunda ukiwa umeharibika sana na kubadilika Ni mwaka sasa tunakukumbuka sana ni ngumu kusamehe na kusahau 🙏🏻
75
449
12
1,568
25,631
Jackson retweeted
On this day, bullets took your life away. Since October 29, 2025, your parents have missed you deeply. Your dream of seeing Arsenal win the Premier League finally came true in 2026. Rest in peace, brother. You and everyone else we lost will never be forgotten. 💔🕊️
58
394
11
1,562
34,472
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Dkt. Charles Kitima, amesema viongozi wa Kanisa hilo walitoa tahadhari mapema kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhusu hatari ya kutorekebisha kasoro za uchaguzi, akieleza kuwa walionya kuwa hali hiyo ingeweza kusababisha maafa nchini. Akizungumza Oktoba 29, 2026, wakati wa misa ya kuwaombea marehemu na waathirika wa matukio ya Oktoba 29, 2025, Padre Kitima amesema Januari 8, 2024, Maaskofu walikutana na Makamu Mwenyekiti wa CCM mjini Dodoma na kumweleza wasiwasi wao kuhusu mwenendo wa uchaguzi, wakirejea changamoto walizoziona katika chaguzi za mwaka 2019 na 2020. Amesema katika mazungumzo hayo, kiongozi huyo wa CCM aliwaahidi kuwa masuala waliyoyawasilisha yangefanyiwa kazi ili yasijirudie, lakini baadaye walishuhudia matukio ya kutoweka na kuuawa kwa baadhi ya watu, hali iliyozidisha wasiwasi wao kuhusu usalama na mwenendo wa siasa nchini. Padre Kitima ametaja matukio ya kutoweka kwa Shadrack Chaula mwezi Agosti 2024 na Deusdedit Soka Agosti 13, 2024, pamoja na kuuawa kwa Aliyef Kibao mwezi Septemba mwaka huo, akisema matukio hayo yalihitaji hatua za dhati za kuhakikisha haki inatendeka na watu wanawajibika kwa matendo yao. Amesema pia matukio yaliyowakumba wanaharakati kutoka Kenya na Uganda, akiwataja Agatha na Boniface, yanaonesha umuhimu wa kutambua makosa yaliyofanyika na kuomba msamaha kwa waathirika, huku akisisitiza kuwa jamii ina wajibu wa kutafakari matendo yake na kutafuta njia ya kurejesha haki na utu. Akihusisha tahadhari hizo na kumbukumbu ya matukio ya Oktoba 29, 2025, Padre Kitima alisema Watanzania wanapaswa kutubu, kuomba msamaha kwa Mungu na kuwaombea waliopoteza maisha, akieleza kuwa maombi hayo yanapaswa kwenda sambamba na kujirekebisha ili matukio kama hayo yasijirudie. Amesisitiza kuwa toba ya kweli inahitaji kuondokana na kiburi na kupanda mbegu za ukweli, unyenyekevu na upendo, akieleza kuwa hayo ndiyo msingi wa msamaha na maridhiano ya kweli katika jamii.
19
130
9
507
22,418
Jackson retweeted
Tusambaze huu ujumbe kwa REPOST ZA KUTOSHA labda wakenya watatuelewa. #FreeTwahaMwaipaya
12
772
7
1,629
25,386
Jackson retweeted
Mpigania HAKI MWENZETU aliekuwa ukimbizini KENYA ametekwa akiwa "Makuru". Twaha hakupenda kuwa MKIMBIZI hii ni baada ya KUTEKWA mara kadhaa akiwa Tanzania na kuteswa sana na WAKOLONI WEUSI. Twaha amekaa jela muda mrefu kwa misimamo yake ya kudai haki. Leo ANATEKWA AKIWA UKIMBIZI KENYA. WAKENYA TUSAIDIENI KUPAZA SAUTI KUMTAFUTA NDUGU YETU. #FreeTwahaMwaipaya REPOST 200
28
304
4
854
19,943
Jackson retweeted
Today, the European Parliament’s Foreign Affairs and Development committees and its Subcommittee on Human Rights will shortlist candidates for this year’s Sakharov Prize. Among the nominees is Tanzanian opposition leader Tundu Lissu, nominated by the EPP Group. "Tundu Lissu has been at the forefront of the struggle for electoral reform, political fairness and the restoration of democracy in Tanzania. Despite relentless persecution, he has remained steadfast in his fight. His nomination sends a powerful message of solidarity with democracy defenders around the world and reaffirms our support for their courage and determination," says @ReinholdLopatka MEP, who spearheaded his nomination. Read more: epp.group/9denr4yj
54
322
9
772
10,102
MUSIOGOPE! Yesu ninayemwamini ndiye Njia, Kweli na Uzima. Taifa letu linahitaji UKWELI, HAKI NA UWAJIBIKAJI. Amani ya kweli haipatikani kwa kuua, kutisha au kutumia vibaya mamlaka ili kumnyamazisha Boniface Mwabukusi. Amani ya kweli hujengwa kwa kutenda haki, kuheshimu utu na kuwajibika kwa matendo yetu. Kwangu mimi, kuishi ni Kristo, na kufa ni faida. Ni bora nikose vyote, lakini nibaki upande wa wanyonge wanaonyanyaswa, wanaodhulumiwa na kupuuzwa katika harakati za kutafuta haki. Mungu ninayemtumikia ni Mungu wa haki. Hata tukipita tena na tena katika bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya, kwa maana najua kuwa makusudi ya Mungu yatasimama. MUSIOGOPE! Ukweli unaweza kucheleweshwa, haki inaweza kuzuiwa, na sauti ya mtu inaweza kutaka kunyamazishwa, lakini hakuna mamlaka ya mwanadamu inayoweza kuishinda kweli ya Mungu. Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.” — Mathayo 6:33 UKWELI. HAKI. UWAJIBIKAJI. Mungu mbele, hofu nyuma, na haki daima! HAKI ITASHINDA. BAK MWABUKUSI .
83
462
16
1,676
41,676
Video ya mwisho, I promise…. NAWAPENDA MNOOO WATANZANIA
70
310
7
2,642
183,832
Replying to @anbeanews
Bu olay Endonezyada 26 ocak 2026 tarihinde yaşandı oradaki iki bayanda ortaokul çocuğu ayrıca panonun üstüne devrildiği çocuk ölmedi hafif bir beyin kanaması geçirdi ve çocuk amelyata gerek kalmadan ilaçla tedavi edilerek hasarsız bir şekilde iyileşti yalan haber yaymayın utanın
69
43
2
3,069
289,378