Pinned Tweet
Ama kweli Waafrika unyani umetuathiri sana ukitaka kuamini hilo mletee mkeo mtoto uliyezaa na mzungu uone kama ata mnyanyasa?🤣🚶🚶
Mapung'o retweeted
RAIS SAMIA AKUTANA NA VIONGOZI WA DUNIA COP31
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wanaoshiriki Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31).
Mkutano huo unafanyika katika Kituo cha Maonesho cha Antalya (Antalya Expo Center), nchini Uturuki siku ya leo tarehe 11 Novemba 2026.
#KigogoMediaUpdates
Mapung'o retweeted
Ninawatakia kila la kheri wanafunzi wa Kidato cha Nne mnaoanza mitihani ya kuhitimu Elimu ya Sekondari leo katika vituo 7,067 nchi nzima.
Nina imani kuwa mmejiandaa vyema kwa ajili ya hatua hii muhimu katika safari yenu ya kielimu. Ninamwomba Mwenyezi Mungu awajalie afya njema, utulivu na uwezo wa kufanya mitihani yenu kwa umakini na kujiamini.
Aidha, ninatoa wito kwa wote wenye dhamana ya kusimamia mitihani hii kutekeleza majukumu yenu kwa weledi, umakini na uadilifu, na kuhakikisha mitihani inafanyika kwa haki, amani na usalama.









