Princess Kate retweeted
HOTUBA HII YA MWALIMU NYERERE YA MWAKA 1995 IANZE KUTUTAFAKARISHA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2030.
BADO ATAISHI MILELE.
George Michael Uledi.
October 14,2026
LEO asubuhi ya saa 06:20 hivi,kupitia UTV nilikuwa namsikiliza Mwalimu Julius Nyerere akiongea na Wananchi kupitia kumpata Mgombea wa Chama cha Mapinduzi na Baadae Mh Rais wa JMT kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2030.
Kwa mtazamo wangu mimi,hotuba hii itaendelea "KUISHI" Vizazi na VIZAZI.
Ni hotuba ambayo imenifanya niwe na tafakari nzito kuhusu mustakabali wa Taifa langu.
Kwa maoni yangu na hapa tulipofikia AMBAPO UDINI UMETAWALA/UVITA dhidi ya Rais wa sasa kutoka dini nyingine,kumenipa maswali na tafakuri nzito hasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2030.
Moja ya UFA ambao lazima TUUZIBE HARAKA kabla ya 2030 kama Taifa ni kundi fulani kudhani mwaka 2030 ni ZAMU YAO. HUU ni UPUUZI ambao unapaswa kukewa haraka sana.
NI AIBU MNO watu WAZIMA kudhani kwamba mwaka 2030 TUTAKUWA TUNAMTAFUTA RAIS "MKRISTO",na Mwalimu katukumbusha leo MANENO YAKE YA MWAKA 1995 kwamba HATUTAKI RAIS MKABILA/MDINI AU MKABURU.
HIZI NI TAFAKURI MUHIMU(TAKEAWAYS) ZA MWALIMU NYERERE KWENYE HOTUBA ILE YA MWAKA 1995ππ½ππ½
I.WATU HAWA(WATANZNIA) BADO HAWAJAWA WANZANIA.
Manaa yake niππΏππΏ.MIAKA 60+ ya Uhuru wetu hakijawa kipimo muhimu cha UMOJA wetu kiasi kwamba tuanze kujigamba kwa DINI ZETU, MAKABILA YETU NA MAENEO YETU TUNAYOTOKA.
Na hapa chokochoka za kina Ndugu Tundu Lissu na Boniface Mwabukusi kuhusu Utanganyika na Uzanzibar,kwa nyakati hizi ni TAKATAKA..
2.HATUTAMCHAGUA MTU KWA DINI KABILA WALA MKOA WAKE.
Mwalimu Nyerere anasema sifa ya kwanza ya Rais wa JMT kamwe haitokuwa DINI KABILA WALA ENEO lake katika wakati wowote na hata hiyo 2030.
3.RAIS WETU AJUE KUWA HATUMCHAGUI SABABU YA UISLAM WALA UKRISTO WAKE
Mwalimu aliamini kuwa DINI KABILA ENEO ZINAWEZA KUWA UFA mkubwa kama itakuwa ndio criteria za kumtafuta Rais na hata baadae badala ya sifa zake..
4.NA TUNATAKA MGOMBEA WETU(Urais) ALIJUE NA ALISIMAMIE.
Mwalimu anasema Mgombea Urais wa jana leo na hata baadae ni lazima ajue kuwa HATUMTAFUTI MWISLAM AU MKRISTO AU MPAGANI nyakati zozote za Chaguzi zetu za leo na hata baadae/mbeleni.
5.IKULU NI MAHARI PATAKATIFU.
Mwalimu anasema Ikulu sio MSIKITI WALA KANISANI BALI IKULU NI "MBINGUNI" kwa maoni/maneno yangu.
6.TUMPATE MGOMBEA WA CCM KWA UWAZI.
Mwalimu anasema TUTATAKA tukuulize kuwa unataka kuwa RAIS wetu,ni lazima ,UJUE LAZIMA TUKUULIZE,kwanini unautaka urais wetu?
TUKUULIZE,TUNAZO NYUFA HIZI HIZI HIZI,JE WEWE MGOMBEA UNAZIELEWA?
Kwa maoni yangu,hii inaweza kuwa ni MUONGOZO MZURI ZAIDI jinsi ya kuwapata VIONGOZI wetu wa Kitaifa.
WANAOUTAKA URAIS mwaka 2030 WANAPASWA KUJIULIZA MASWALI HAYA MAPEMA kuepuka usumbufu mbeleni.
Pumzika kwa Amani Mwalimu Mwanafalsafa,NABII,MALAIKA na Mtakatifu Mwalimu Nyerere.
Princess Kate retweeted
JOHN PAMBALU UNATUTIA AIBU NDUGU ZAKO, UTAVUNA ULICHOPANDA
Na Albert Pambalu, Magu
Haya mambo yanaumiza sana, imagine ndugu yako anafanya vitu vya hovyo unamshauri lakini hasikii eti kisa kutafuta umaarufu wa kisiasa.
Ukiwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo na ukakosa busara unaweza kufikiria wewe uko juu ya sheria, shujaa na mtu asiyegusika hata na vyombo vya dola. Kiburi cha aina hii mwisho wake ni mbaya kwa kuwa unavunja sheria huku ukitoa maneno ya kishujaa.
Kwa asiyefahamu mdogo wetu John aliamua kwa makusudi kuhamasisha vurugu zilizopelekea vifo vya watu wengi sana hapa Mwanza na maeneo mengine nchini na baadae aliamua kukimbilia nchini Kenya. Tupo tuliompa onyo mapema aache kufanya siasa zisizo na tija lakini hakuelewa.
Leo hii nimepata taarifa kuwa amekamatwa huko Arusha baada ya maisha kuwa magumu nchini Kenya alikokuwa amejificha. Hapa ndio ile kauli ya mwisho wa ubaya ni aibu inadhihirika. Wako wapi waliokuwa wanamjaza nyembe avunje sheria za nchi?
Vipi, kwani hapo Kenya amefukuzwa? Kwanini alikimbia na sasa amerudi? Sisi ndugu zako tulikupa ushauri uachane na siasa za kihuni lakini hukuelewa na ukaamini wewe ni maarufu kuliko shilingi sasa umetiwa nguvuni hujui kesho yako. Hii ni aibu kubwa kwetu!
Anyways, mchuma janga hula na wa kwao. Wategemezi wako wote umetuachia sisi huku wewe ukiendelea kumtumikia shetani kwa siasa zinazohamasisha vurugu. Sote ni mashahidi namna ulivyotumia mdomo wako kuhamasisha vurugu Octoba mwaka jana, sasa ni wakati wa kupata mavuno yako.
Fanya siasa lakini kamwe usivuke mipaka ya kutumika kuvuruga amani ya nchi yako. Tanzania ni moja tu na huu ni wito wangu hata kwa wale waliopo Canada ipo siku mtarudi na mtawajibika sawa sawa na maovu yenu "Mwenda tezi na omo, marejeo ni ngamani". Karibu ngamani mdogo wangu Mwalimu John John Pambalu.
Princess Kate retweeted
IPU YAMTAJA RAIS SAMIA MFANO WA UONGOZI BORA WA WANAWAKE
Rais wa Wabunge Wanawake wa IPU, Cynthia Lopez, amemtaja Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mfano wa uongozi wa wanawake duniani, akisisitiza umuhimu wa wanawake kushiriki na kuongoza katika nafasi za maamuzi.
Princess Kate retweeted
Wanaharakati sijui wanaelewa?
TANZANIA NI MSHIRIKA MUHIMU SANA- Sir Sindsay Hoyle π
Spika wa Bunge la Uingereza, Sir Lindsay Hoyle, amesema Tanzania ni mshirika muhimu katika kukuza uchumi na biashara, akisisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi kati ya Tanzania na Uingereza.
Sir Lindsay amesema hayo katika mahojiano yaliyofanyika pembezoni mwa Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) jijini Arusha, Sir Lindsay amesema kuimarisha uhusiano huo kutasaidia kufungua fursa mpya kwa nchi hizo mbili na kujenga zaidi juu ya uhusiano wao wa kihistoria.
Sir Lindsay amesema Tanzania kuwa injini muhimu ya uchumi wa Afrika Mashariki, kutokana na fursa zinazotokana na idadi kubwa ya vijana wenye elimu, utalii, rasilimali za gesi asilia na kuongezeka kwa uwezo wa uzalishaji wa umeme.
Sir Lindsay pia amepongeza uongozi wa Tanzania na nafasi yake inayokua katika kukuza diplomasia ya kibunge, maendeleo ya kiuchumi na ushirikiano wa kimataifa, akieleza kuwa Tanzania ina nafasi muhimu katika kukuza ushirikiano wa kikanda na kimataifa.
βKuimarisha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi kati ya Tanzania na Uingereza kutakuwa muhimu katika kufungua fursa na kutumia ipasavyo uwezo wa nchi zote mbili, sambamba na kujenga juu ya uhusiano wetu wa kihistoria,β amesema Sir Lindsay
Katika eneo la usawa wa kijinsia, Sir Lindsay ameipongeza Tanzania kwa hatua ilizopiga katika kuongeza ushiriki wa wanawake katika kufanya maamuzi ya kisiasa.
Mwisho amesema Tanzania kuwa na Rais wake wa kwanza mwanamke pamoja na wanawake kuwa na uwakilishi wa 39.5% Bungeni ni ishara ya hatua kuelekea usawa zaidi wa kijinsia.
#KigogoMediaUpdates
Princess Kate retweeted
KASI MPYA YA MIVUTANO MASHARIKI YA KATI MAFUTA KUPANDA BEI
Hapo jana, kiongozi wa PLC, Rashad al-Alimi ametangaza operation ya kuwakabili wapiganaji wa Houthis ndani ya Yemeni. Hivi karibuni Houthis walifanikiwa kuteka sehemu ya mfereji wa Bab al-Mandeb na maeneo mengine ya kimkakati katika routes za Usafirishaji wa mafuta.
Ikumbukwe pia Houthis waliweza kushambulia miundombinu muhimuu kwa biashara ya mafuta iliyochini ya kampuni ya mafuta ya Saudi Arabia, ARAMCO ndani ya Jiji la Riyadh na Mashariki kwa Mkoa wa Khurais. Mivutano hii inaathiri kwa kiwango kikubwa soko la mafuta Duniani.
Nchi za Afrika Mashariki zinashauriwa ziijiandae kwa uwezekano wa kupanda kwa bei ya mafuta, kutokana na mivutano inayoendelea Mashariki ya Kati ikitishia kupandisha bei ya mafuta ghafi duniani kufikia zaidi ya dola 120 kwa pipa kuanzia Mwezi huu wa Octoba.
Hali mbaya katika njia kuu za usafirishaji wa mafuta kwenye Bahari Nyekundu na Mlango-bahari wa Hormuz inachangia kwa kiasi kikubwa juu ya uwezekano wa jambo hili. Kwa
Princess Kate retweeted
TANGA VS LAMU: VITA YA REFINERY NI VITA YA CORRIDOR YA AFRIKA MASHARIKI
Na: Mtaalam wa Masuala ya Uchumi Duniani
01.10.2026
Kuzinduliwa kwa mradi wa Dangote wa US$16 bilioni huko Lamu, Kenya, jana si habari ndogo kwa Afrika Mashariki. Refinery hiyo imepangwa kuwa na uwezo wa kuchakata mapipa 700,000 ya mafuta kwa siku, ikiambatana na mtambo wa umeme wa MW 1,000, pamoja na uzalishaji wa mbolea na kemikali. Kenya inatarajia mradi huo kuunda zaidi ya ajira 60,000 katika kile kinachoelezwa kuwa uwekezaji mkubwa wa viwanda katika ukanda huu. Dangote pia ameweka mezani uwezekano wa serikali za nchi za Afrika Mashariki kushikilia kwa pamoja hadi asilimia 30 ya mradi huo.
Lakini Tanzania nayo haikukaa na kuangalia Lamu ikiondoka na fursa. Mpango wa Tanga Regional Energy Hub unaounganisha Tanzania, Uganda na Vitol Bahrain unalenga kuwekeza zaidi ya US$20 bilioni katika mfumo mpana wa nishati unaojumuisha refinery, matanki ya kuhifadhi mafuta, jetty ya kupokea mafuta ghafi, miundombinu ya baharini, biashara na usambazaji wa bidhaa za mafuta, pamoja na bomba la bidhaa za mafuta linalounganisha Tanga na Uganda. Serikali ya Tanzania imesema utekelezaji wake unalenga kuongeza ajira, local content, ujuzi wa wataalamu wazawa na biashara ya nishati. Muhimu zaidi, Tanga haianzi kutoka sifuri: inajengwa juu ya EACOP yenye urefu wa takribani kilomita 1,443, inayounganisha maeneo ya mafuta ya Uganda na Tanga, na yenye uwezo uliopangwa wa kusafirisha hadi mapipa 230,000 kwa siku.
Hapa ndipo tofauti ya kimkakati inapoonekana. Lamu inaleta refinery kubwa sana na inaweza kuwa kituo muhimu cha mafuta kwa Kenya na nchi jirani. Tanga, kwa upande mwingine, inalenga kujenga mfumo mzima wa corridor ya nishati unaounganisha mafuta ghafi ya Uganda, Bandari ya Tanga, storage, refining, pipeline ya bidhaa, biashara na masoko ya Tanzania, Uganda na nchi nyingine za ndani ya Afrika Mashariki. Uganda yenyewe inaendelea na refinery yake ya Hoima yenye uwezo wa mapipa 60,000 kwa siku, na serikali hizo mbili zinasema Hoima na Tanga zitakamilishana badala ya kushindana. Hii ina maana Tanzania inaweza kutengeneza mnyororo ambao thamani yake haishii kwenye kiwanda, bali unaendelea kwenye usafirishaji, bandari, maghala, biashara, huduma za kitaalamu, viwanda vinavyotumia bidhaa za petroli na ajira.
Kwa Mtanzania, hiyo ndiyo sehemu muhimu ya kuangalia. Kila pipa la mafuta linalopita kwenye miundombinu ya Tanzania linaweza kuunda shughuli za kiuchumi katika bandari, trucking, engineering, insurance, banking, warehousing, logistics, catering, construction na huduma nyingine. Na refinery inapozalisha ndani ya ukanda, thamani haishii kwenye kuuza mafuta ghafi nje na kununua bidhaa zilizokwisha chakatwa. Tanzania inaweza kuwa sehemu ya mnyororo wa thamani. Serikali tayari imeweka wazi kuwa Tanga Energy Hub inalenga kuongeza ushiriki wa wazawa kupitia local content na kujenga uwezo wa wataalamu wa ndani.
Hata hivyo, hapa ndipo tunapaswa kuwa wakweli kwenye namba. US$20 bilioni za Tanga si US$20 bilioni ambazo tayari zimewekwa benki kwa ajili ya refinery. Ni makadirio ya uwekezaji wa energy hub nzima, na bado kuna vipengele vinahitaji feasibility studies, financing arrangements na final investment decisions. Kwa upande wa Lamu, US$16 bilioni ni thamani ya mradi mkubwa wa refinery na complex yake, lakini pia una changamoto zake, ikiwemo masuala ya ardhi na kesi za kisheria zilizoripotiwa kabla na baada ya uzinduzi. Kwa hiyo, ushindani wa Tanga na Lamu haupaswi kupimwa kwa ukubwa wa headline pekee. Unapaswa kupimwa kwa swali moja: ni mfumo gani utakaobakiza thamani zaidi ndani ya uchumi wa Afrika Mashariki, na kila nchi itapata sehemu gani ya thamani hiyo?
Na hapo Tanzania ina sababu ya kujiamini. Hatuna haja ya kupigana na Kenya kwa kelele wala kujaribu kuiga Lamu kwa kila kitu. Tanzania ina EACOP, Bandari ya Tanga, eneo la kimkakati kwenye Bahari ya Hindi, ardhi, masoko yanayounganisha Tanzania na nchi za ndani, na uzoefu wa kuendesha miradi mikubwa ya miundombinu ya
Princess Kate retweeted
Kutoka kwenye mijadala ya kimataifa hadi kwenye maajabu ya asili, wajumbe wa IPU wanaendelea kupata fursa ya kuifahamu Tanzania kupitia vivutio vyake vya kipekee. Ngorongoro, yenye mandhari ya kuvutia na wanyamapori wa aina mbalimbali, ni miongoni mwa hazina zinazoiweka Tanzania kwenye ramani ya utalii wa dunia.
#IPU #Ngorongoro #VisitTanzania #TanzaniaTheLandOfWonders #Tourism
Princess Kate retweeted
Tanzania kwa sasa ndo habari ya dunia.
Arusha kumechangamka IPUπ₯π₯π₯
DSM kumechangamka COP12π₯π₯π₯
Instagram mamiss wetu wanaendelea kuimarisha usalama na kuliheshimisha Tanzania πΉπΏπ₯π₯
X- ni vururu wanaharakati wanapigwa za uso, Konde boy anaendelea kuachia episodes, IPU, COP12 yan heeeπ
Princess Kate retweeted
hawa ndo waandamanaji wa Wanaharakati wenu! Yan mnaambiwa huyu ni mdigo anawapambania akiwa Marekani! Hawa watu sijui wanatuonaje π€
Princess Kate retweeted
Tanzania kupitia mrembo wake Jihan Dimack ambaye ni Miss Grand Tanzania 2026 imeorodheshwa katika kipengele cha 'Country's Power of the Year' raundi ya kwanza ya Miss Grand International 2026, ikiwa ni miongoni mwa nchi 50 zilizotajwa kwenye safu (ranking) iliyotolewa Septemba 27, 2026 ikiwa ni ya 8 kwenye orodha.
Watanzania wameaswa kumpigia kura Mrembo wa Tanzania kupitia Instagram ya @missgrandinternational kwenye kipengele cha Country's Power of the Year - Round 1.
Kwa mujibu wa waratibu wa Miss Grand International, ni washiriki 40 pekee watakaosonga mbele kwenda hatua inayofuata, hivyo kura za wafuasi ni muhimu katika kuiwezesha Tanzania kuendelea na hatua hiyo.
Kura zinafungwa leo, Septemba 27, 2026, saa 10:30 usiku (GMT+7).
Princess Kate retweeted
INAONEKANA "UKOO" WA JOHN HECHE NDIO HAWATAKI MARIDHIANO NA SERIKALI NA SIO CHADEMA YOTE.
Golf Mike Uniform.
August 2,2026.
Katibu wa Chadema Mkoa wa Mara Ndugu Donald Mwembe juzi aliitisha kikao cha Waandishi wa habari akisema kwa mahali walipofikia,Chama chao kwa haraka kinahitaji kukaa meza ya Maridhiano na Serikali ili kiweze kuondoka kwenye Mkwamo wa kisiasa ambao upo kwa sasa.
Na huo ndio umekuwa msimamo wa wananchama na wafuasi wengi ndani ya Chadema kwa sasa kwamba Chama hicho kinapaswa kwenda mezani kuzungumza na Serikali ili waweze kuondoka katika mkwamo huo wa muda mrefu.
Msimamo.huo wa Wanachama wengi wa Chadema unakwenda kinyume na MSIMAMO.wa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Ndugu John Heche pamoja na ndugu zake ambao wengine ni Viongozi wa Mikoa na Wilaya wa Chama hicho.
Sept 1,2026,Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mara ambaye pia ni mdogo(Ukoo) wa Ndugu John Heche kwa jina la Chache Heche aliwaita wanachama mbele ya waandishi wa habari na kutangaza/kumtisha Katibu wake wa Chama Mkoa wa Mara Ndugu Donald Mwambe kwamba yeye sio msemaji wa Chama hicho na hapaswi kuongelea mambo ya Chama mbele ya waandishi wa habari.
IPO HIVI.
Hata kufutwa/kusogezwa mbele gafla kwa Mkutano wa Baraza Kuu la Chama hicho ambacho kilipangwa kufanyika mwezi huu(9) ni uwepo wa HOFU ya Makamu Mwenyekiti John Heche kwamba wajumbe wa Baraza Kuu walikuwa wanaenda kuazimia KUYATAKA MARIDHIANO NA SERIKALI haraka iwezekanavyo.
Na hicho ndio kitu ambacho John Heche na "UKOO" wake hawataki kukisikia kamwe.Hasira hiyo ya "UKOO" wa John Heche dhidi ya Serikali inatajwa kuchochewa na kile kinachoitwa kifo cha ndugu yao mikononi mwa Polisi miaka ya nyuma.
John Heche mara kwa mara amekuwa akijitetea kuwa msimamo wa kukataa maridhiano sio msimamo wake bali ni msimamo wa Chama lakini wakati huo huo amekuwa AKIZIMA SAUTI za KUTAKA MARIDHIANO za Viongozi wenzake ndani ya Chama pamoja na Wanachama.
Hesabu za Makamu John Heche za kusogeza mbele Mkutano wa Baraza Kuu Chadema ni kutaka kutengeneza USHAWISHI wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu pindi ukiitishwa kwamba tunakwendaje kwwnye maridhiano wakati Mwenyekiti wetu tayari kashahukumiwa?
John Heche anajaribu "kubuy time" mpaka kesi ya Ndugu Lissu iiishe ambayo anajua kabisa kuwa Tundu atakutwa na hatia na baadae kuhukumiwa na hivyo kwanza (I) wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu utakapoitishwa atataka kushawishi wajumbe kuwa kwa sasa Chama hakina Mwenyekiti hivyo yeye anapaswa kubeba mikoba ya nafasi hiyo.
Pili(II)John Heche na Ukoo wake wanataka kufanya Mapinduzi ya Kimkakati dhidi ya Mwenyekiti Lissu KISAYANSI.
Ni wazi John Heche na UKOO wake wanajua kuwa kama Baraza Kuu lingefanyika kabla ya KESI ya Lissu kuisha upo uwezekano wa wajumbe wa Baraza Kuu la Chadema kukubaliana kuhusu maridhiano hivyo ndugu Tundu Lissu angeweza KUACHIWA huru kama sehemu ya Maridhiano hayo.
Kuachiwa kwa Tundu Lissu kwa John Heche na ndugu zake litakuwa pigo kubwa katika safari yao ya kusaka Madaraka Makuu ya Chama hicho.
Pamoja na hayo,pia John Heche amekuwa na shutuma nyingine za matumizi mabaya ya fedha za Chama suala ambalo lilipigiwa sana kelele na viongozi wa Chadema Mikoa na Wilaya mpaka kupelekea kusimamishwa kwa baadhi ya Viongozi waliibua shutuma hizo akiwemo Katibu wa Chadema Mkoa wa Morogoro.
John Heche amekaririwa juzi akilalamika kwamba kuna mgogoro unatengenezwa ndani ya Chadema lakini kimsingi ni kwamba ana hofu kubwa juu ya shutuma hizo kama sinaweza kumuacha salama mbele ya Mkutano huo wa Baraza Kuu.
Hofu nyingine ya John Heche kwa sasa ni endapo Uchaguzi Mkuu Utaitishwa tena wa Chama kutokana na mwenyekiti kutumikia kifungo,basi ni wazi kuwa
Mzee Freeman Mbowe anaweza kurudi kukalia nafasi hiyo ya Mwenyekiti wa Chama.
Juzi Makamu Mwenyekiti John Heche alikaririwa na Chombo cha habari kimoja akisema BILA REFORMS HATA 2030 hawatashiriki Uchaguzi tena.
Kauli hiyo imeendelea KUCHOCHEA tena na tena mgogoro wa chini chini kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya pamoja na wanachama kwamba kama Chama hakitaki
Princess Kate retweeted
Sheria inasema foreigner anaweza kupewa derivative right ya kumiliki ardhi kwaajili ya uwekezaji tu. Kuhusu swala la disposition (kuuza/kurithisha) ardhi husika Sheria ya ardhi imewaka restrictions kwamaana kwamba mwekezaji atatakiwa kurudisha ardhi kwa wamiliki waliompatia haki ya kuwekeza ndiyo watakao amua namna gani hiyo ardhi itakua disposed. Nilipoona ile post ya foreigner akitangaza kuuza hicho kisiwa nilishangaa. NB: haya mambo yatolewe ufafanuzi mzuri kwa wananchi.
Princess Kate retweeted
Mil. 300 tayari zimepigwa. Kwani kipindi wanachangisha hawakujua kama Lissu hayupo uraiani?
Princess Kate retweeted
Huyu @HecheJohn ni makamu wa kinachojiita Kikundi Kikuu cha Upinzani nchini, na katika comments kuna ng'ombe wake kadhaa wanamuunga mkono! Na ikumbukwe huyu ni mwalimu, Unajiuliza ameamua kupotosha kwa Maslahi ya nani?
Ni kweli Heche hajui kuwa zaidi ya asilimia 60 ya wananchi wa DR Congo wanategemea kilimo? Hata katika GDP kilimo kinachangia hadi asilimia 20. Hapa Heche anakwambia Mkongo sio Mkulima!
Vilevile Uvuvi kwa Congo uachangia takribani asilimia 12 ya Pato la Ndani la Kilimo (AGDP), Wananchi wanaoishi maeneo yenye yale maziwa makubwa (7) shughuli yao kubwa ni uvuvi, na ikumbukwe hawa watu ukijumlisha maziwa makubwa na madogo ni kama 80 hivi ongezea Bahari ya Atlantiki pia huyu Heche anaongea pumba gani?π€·ββοΈ
Sasa hadi hapo wanapokutana Marais wa hizi nchi 2 kwa nini haya mambo yanayohusisha idadi kubwa ya shughuli za wananchi wao yasijadiliwe? Nchi hii tuna upinzani wa hovyo jamani π
Princess Kate retweeted
CHADEMA faces backlash over 'naive' stance on Tanzania-DRC relations
Africa J&L Correspondence, Dar es salaam
Tanzaniaβs leading opposition party CHADEMA faces sharp criticism after Vice Chairman John Heche @HecheJohn questioned the strategic necessity of bilateral ties with the Democratic Republic of Congo (DRC).
The remarks, made after DRC President FΓ©lix Tshisekediβs official working visit, drew immediate pushback from political analysts and regional experts. They labelled the stance βnaiveβ and warned that undermining these diplomatic channels threatens vital national interests.
The fallout highlights critical economic ties between the neighbours:
β’ Massive trade volume: The nations share a $794 billion trade relationship.
β’ Logistical gateway: Tanzania acts as the primary maritime trade corridor for eastern DRC.
β’ Infrastructure pipeline: Dar es Salaam is expanding its new Standard Gauge Railway (SGR). which currently runs electric trains between Dar es Salaam and Dodoma to link DRC, Rwanda and Burundi.
Critics argue that failure to grasp these geopolitical fundamentals disqualifies politicians from national leadership and call for swift re-education on the regionβs shared economic future.
Princess Kate retweeted
JNHPP IMEWASHWA NA NDOTO ZA WATANZANIA ZIMETIMIA
Julius Nyerere Hydropower Project ni miongoni mwa miradi mikubwa zaidi ya miundombinu ya nishati nchini ikiwa na uwezo wa MW 2,115.
Ukubwa wake unaonyesha dhamira ya Tanzania kuongeza uwezo wake wa kuzalisha nishati na kuimarisha msingi wa uchumi wake kwani ni mradi mkubwa wenye maono makubwa na unaobeba matumaini ya kizazi cha sasa na kijacho.
Princess Kate retweeted
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mhe. FΓ©lix Antoine Tshisekedi Tshilombo baada ya kuwasili Ikulu Ndogo ya Zanzibar, tarehe 18 Agosti, 2026.
Princess Kate retweeted
*MWISHO WA UBAYA NI AIBU: KWANINI JOHN HECHE AMEPANIKI SUALA LA KULA MICHANGO YA TONETONE?*
Na NULPHIN CHARLES, Katibu Mstaafu wa CHADEMA-Serengeti
Hivi karibuni wengi tulijiuliza John Heche alipata wapi fedha za kugharamia familia yake kwenda mapumzikoni Dubai, ilihali wanachama wanahamasishwa kutoa fedha kuchangia chama na hakuna taarifa yoyote ya mapato na matumizi.
Leo, katika hali isiyotarajiwa, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, ametoa ushahidi kuwa yeye ni mnufaika wa fedha za chama zinazokusanywa kupitia michango ya Tonetone. Hii inatokana na kitendo chake cha kupaniki na kushindwa kueleza uhalisia baada ya kuulizwa swali kuhusu tuhuma zinazomkabili na mwandishi wa habari, Stanslaus Lambati.
John Heche, kama alivyo Godbless Lema, wamekuwa wakituhumiwa mara nyingi kukusanya michango na kuitumia bila kuwasilisha hesabu hizo ndani ya chama. Paniki ya leo imetoa picha halisi ya wezi wanaotumia jina la chama kujinufaisha wenyewe. CHADEMA ni chama kinachokosa sifa ya kuendelea kuwa chama cha siasa nchini; ni kikundi cha matapeli wanaotumia siasa kujipatia fedha.
Utajiri unaokusanywa na John Heche kupitia utapeli wa kisiasa unapaswa kukemewa na kila mtu mwenye akili timamu. Ikiwa ndani ya chama tu viongozi hawa wanaiba fedha bila aibu, je, wakishika dola itakuwaje? Uwajibikaji ni msingi wa maendeleo kwa taasisi yoyote, lakini kwa bahati mbaya, hakuna anayeweza kumuhoji Heche kwa hofu ya kushughulikiwa ndani ya chama hicho



























