GASTON SHUNDO GARUBINDI retweeted
6.11.2026: Hukumu ya TUNDU LISSU NA KUMBUKUMBU YA KESI YA MWALIMU NYERERE YA MWAKA 1958. HISTORIA INATUFUNDISHA NINI?
Leo, tarehe 6 Novemba 2026, Tundu Lissu ameshinda kesi ya uhaini lakini mahakama ikasema amepatikana na hatia ya uchochezi (incitement) na kuhukumiwa kifungo cha miaka 4. Tunamshukuru Mungu kwa kesi ya uhaini kutupiliwa mbali na kumpongeza Lissu kwa umahiri na ujasiri wake hadi kujitetea. Lakini hukumu ya uchochezi inasikitisha, inafikirisha na inatukumbusha historia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, ambaye naye mwaka 1958 alikutwa na hatia ya jinai ya kashfa (criminal libel) wakati wa harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Makosa haya mawili ni tofauti kisheria, lakini kesi hizi zinafanana katika jambo muhimu: zote zilihusu kiongozi mkuu wa upinzani aliyeshtakiwa na Serikali kutokana na kauli zake za kisiasa.
Turejee historia.
Tarehe 27 Mei 1958, Mwalimu Nyerere alichapisha makala katika gazeti la Sauti ya TANU, Toleo Na. 29, akiwakosoa Wakuu wawili wa Wilaya wa Serikali ya kikoloni kwa madai ya kutumia madaraka yao vibaya na kuihujumu TANU.
Akafunguliwa kesi ya jinai Na. 2207/1958 chini ya kifungu cha 187 cha Kanuni ya Adhabu (Penal Code). Serikali ya Uingereza ilitoa maelezo kuhusu mashtaka hayo katika Bunge lake (House of Commons) tarehe 26 Juni 1958.
Nyaraka za UN zinathibitisha kwamba Mwalimu alikutwa na hatia katika mashtaka mawili na kuhukumiwa kulipa faini ya shilingi 3,000 za Afrika Mashariki, sawa na pauni 150 za wakati huo, au kifungo cha miezi sita. Alilipa faini tarehe 12 Agosti 1958 na hakukata rufaa.
Kesi hiyo ilizua mjadala mkubwa. Wanaharakati wa kupigania uhuru huko London walihoji iwapo Mwalimu angepata haki katika mahakama za kikoloni na kudai kuwepo kwa waangalizi huru. Serikali ilikataa, ikisisitiza kuwa uamuzi wa kufungua mashtaka ulikuwa chini ya mamlaka ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Miaka 68 baadaye, tunajikuta tena tukitafakari maswali kuhusu uhuru wa kisiasa, matumizi ya sheria za jinai na nafasi ya mahakama katika mfumo wa kidemokrasia.
Pamoja na hukumu ya mwaka 1958, Mwalimu Nyerere aliendelea na harakati zake hadi Tanganyika ilipopata uhuru mwaka 1961.
Funzo muhimu ni kwamba hukumu ya jinai dhidi ya kiongozi wa kisiasa si lazima iwe mwisho wa safari yake ya kisiasa. Historia inaonesha umuhimu wa kuendeleza majadiliano (dialogue) badala ya mapambano na vurugu (confrontation).
Kwa wanaothamini demokrasia, mfumo wa vyama vingi, haki za binadamu, uhuru wa kujieleza na utawala wa sheria, hukumu ya uchochezi dhidi ya kiongozi mkuu wa upinzani inaibua maswali mazito yanayohitaji mjadala mpana wa kitaifa.
Je, mipaka kati ya ukosoaji halali wa Serikali na uchochezi wa jinai ikoje?
Je, mwanasiasa awe mpinzani au wa chama tawala atakosoa je Serikali au kudai maboresho au mageuzi bila kuhofia kutafsiriwa kuwa mchochezi?
Je, wananchi watawezaje kudai haki zao kwa nguvu ya hoja bila kuonekana wanachochea uvunjifu wa amani?
Walimu na wanataaluma tutawezaje kufundisha, kuchambua sera, kutoa mapendekezo na kukosoa mifumo ya utawala bila kuhofu kuitwa wachochezi?
Viongozi wetu wa dini watawezaje kutekeleza wajibu wao wa kinabii wa kukemea maovu na kusimamia haki bila kuonekana wanachochea waumini wao?
Uhuru wa kujieleza una mipaka yake na hauhalalishi haki ya kukashfu, kuchochea vurugu au uhalifu. Lakini ni muhimu sana kuweka mipaka iliyo wazi kati ya uchochezi wa jinai na ukosoaji halali wa kisiasa.
Iwapo sheria za jinai zitatumika kudhibiti ukosoaji halali wa kisiasa au kitaalamu, tunaweza kujikuta tunadhoofisha demokrasia, haki za binadamu, kuongeza hofu na kuzidisha mkwamo wa kisiasa na kiuchumi badala ya kuutatua.
Hukumu ya leo inatupa sababu nyingine ya kujadili kwa kina uhuru wa kujieleza, uhuru wa mahakama, haki za raia na za vyama vya upinzani na mipaka ya matumizi ya sheria za jinai katika siasa.
Ninarejea msisitizo wangu wa muda mrefu kuhusu falsafa ya Rais Samia ya 4Rs. Tujenge utamaduni wa kusikilizana na kukosoana kwa hoja
TUJISAHIHISHE
GASTON SHUNDO GARUBINDI retweeted
Mhe. @HecheJohn amewakaribisha na kuwapokea wanachama wapya waliojiunga na chama wakitokea CUF na CCM, Wilaya ya Masasi.
GASTON SHUNDO GARUBINDI retweeted
KAHAMA – SHINYANGA. Look at my guy @TheRealJongwe tearing it up with the breakdance!
GASTON SHUNDO GARUBINDI retweeted
LHRC is closely following up on the reported news that the Tanzania Police Force has arrested several women from the CHADEMA Women’s Wing (BAWACHA) who were on transit to Musoma for the International Women’s Day celebrations.
LHRC is pursuing all necessary legal actions in relation to the matter. We urge the Tanzania Police Force to abide by human rights standards as enshrined in domestic, regional, and international human rights instruments to which Tanzania is a signatory, including respecting the right to bail and the right to a fair trial.
#FairTrialAndHumanRights
GASTON SHUNDO GARUBINDI retweeted
The Tanzanian and Ugandan governments should be immediately suspended from the Commonwealth to protect the integrity of the institution. Our two applications on behalf of CHADEMA and the NUP, respectively, lay out why.
Press Release: Amsterdam & Partners LLP Files Applications on Behalf of Uganda’s NUP and Tanzania’s CHADEMA, Respectively, Calls for Immediate Commonwealth Suspensions
amsterdamandpartners.com/pre…
GASTON SHUNDO GARUBINDI retweeted
Replying to @ShundoGaston
Wakizichukua wawape watoto wachezee magemu. Na wabadili emails zao
GASTON SHUNDO GARUBINDI retweeted
Nimetoka Ukonga kumuona Mwenyekiti, Yuko imara na anawasalimia wote.
Anatoa pole kwa Watanzania wote waliopoteza maisha, familia ndugu na marafiki.
Anatambua watu waliopoteza viungo na kubaki na ulemavu.
Ametoa pole kwa wote waliopoteza mali pia.
Damu ya wenzetu haijamwagika bure na hakuna atakaefunika jambo hili bila uwajibikaji.
Msimamo wa Mwenyekiti uko thabiti, Yuko imara na mwenye afya njema.
GASTON SHUNDO GARUBINDI retweeted
🔥🔥 Kanda maalum Tarime!
Jamani inatia hasira sana!!
Yaani @SuluhuSamia is going to burn tuis country! There is only that much repression any people can tolerate!
Allow @HecheJohn to bury Odinga!
Aibu tupu!
GASTON SHUNDO GARUBINDI retweeted
Mhe. @TunduALissu anauliza;
1. Humphrey Polepole amepatikana au ni yale yale ya Mohamed Ali Kibao?
2. Mama anasemaje juu ya balozi wake Humphrey Polepole au ni kazi na utu?
GASTON SHUNDO GARUBINDI retweeted
As Tundu Lissu faces trial today on trumped-up treason charges, we will do our utmost to keep international pressure on the Tanzanian regime — building on our recent meetings in Washington, DC, on this matter.
GASTON SHUNDO GARUBINDI retweeted
We ukikutana hii repost tu🤚🏻
✊🏾 We demand justice!
Tag @elonmusk @Support and tell them to #UnsuspendSativa255.
143K voices silenced. He is a human rights defender. Bring back his voice NOW!
#FreedomOfSpeech #BringBackSativa
GASTON SHUNDO GARUBINDI retweeted
Kutoka Mahakama Kuu, Kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu.
GASTON SHUNDO GARUBINDI retweeted
Son of the soil.
#IamTunduLissu #FreeTunduLissu
GASTON SHUNDO GARUBINDI retweeted
📍VIDEO:
Usiku huu Aprili 07, 2025 wananchi wa kijiji cha Msanga kata ya Mitesa, Jimbo la Lulindi Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, wameuzuia msafara wa Makamu Mwenyekiti wa @ChademaTz Bara Mhe.John Heche @HecheJohn ukitokea Newala mjini kwenye mkutano kuelekea Masasi, wakimataka azungumze neno.
#NoRefomsNoElection
GASTON SHUNDO GARUBINDI retweeted
Hongera sana brother Gaston! Wewe ni mtu na nusu. Piganieni Azimio la Mkutano Mkuu kwa nguvu na maarifa yote: #NoReformNoElection.
Upo kwenye kitengo muhimu sana cha sheria na HAKI za binadamu. Hakikisha haki za Raia na wanachama wetu zinalindwa na kuheshimiwa kwa gharama yoyote.
USHAURI: Usilinde chama, linda haki za Raia na wanachama.
#NIMO
GASTON SHUNDO GARUBINDI retweeted
Marais Wastaafu wa TLS tumealikwa na Rais wa TLS tukutane na Governing Council ili tujadili mustaqbali wa HAKI za Uchaguzi.
GASTON SHUNDO GARUBINDI retweeted
Tarehe 24 Februari 2025 nilimtumia ujumbe kuwa majibu ya barua yake yako tayari aje achukue ofisini kama alivyoleta barua ya awali. Akasoma ujumbe huo ukawa na blue tick na akajibu.
Badala ya tarehe 25 Februari 2025 kutaka Katibu Mkuu amjibu ni kwanini hakusema ukweli kuwa majibu yake yako tayari isipokuwa yeye mwenyewe hujayafuata au kupendekeza atumiwe kwa njia ipi mbadala?
Ana nia gani kuendelea kusema uongo dhidi ya Katibu Mkuu na dhidi ya Chadema?

































