PRAYFORTANZANIA retweeted
Join with me and my wife @UlimwenguJm as we celebrate our 36th year of Marriage. To Love and Partnership! ❤️
PRAYFORTANZANIA retweeted
Anachokiongea Ruto hapa ndio kile kile tunachokishangilia na kukilipia mabilioni Tanzania bila kujali madhara yake kwa mamilioni ya watanzania.
Mpaka VETA wanatumia kiingereza kama lugha ya kufundishia.
Yani anayeongea na anayeongeleshwa wote hawaelewi kinachoendelea lakini wanalazimika kwenda tu kwa sababu “kiingereza ndio sera ya Elimu.”
Miaka 65 ya uhuru lakini bado hatuna uhuru wa kujifunza na kufundisha kwa lugha yetu.
PRAYFORTANZANIA retweeted
Kimenukaaaaaaaaa…… Naingia kulala, nikiamka napeleka watoto shule alafu nawashushia video saa 3 usiku muda wa TZ…..
Issue ni dipu kuliko…..:::
PRAYFORTANZANIA retweeted
SINGIDA: Mkurugenzi wa taasisi ya The Women Wake Up Foundation, Dkt. Veronica Alexander, amesema hayo Novemba 10, 2026, alipokuwa akizungumza katika mazishi ya Alute Mughwai Lissu, kaka wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.
Zaidi jamii.app/VeroSiogopiKutekwa
#JamiiForums #Utawala
PRAYFORTANZANIA retweeted
Dr VERONICA ni Daktari aliempokea Mhe TUNDU LISSU Hosptal ya DODOMA for the first time na kumsaidia kumpa HUDUMA ya kwanza Mwaka 2017 Alipopigwa RISASI 16.
-Lakini baada ya pale Dr VERONICA alifukuzwa kazi
Dr VERO anasema hakujali kufukuzwa kazi kwa kuwa RIZIKI anatoa MUNGU
PRAYFORTANZANIA retweeted
Mfungwa namba 623/2026
Tarehe ya kufungwa 06/11/2026
Tarehe ya Kutoka bila kupunguziwa robo ya kifungo ambayo inapunguzwa kwa mfungwa ambaye hajatenda kosa akiwa gerezani ni Tarehe 05/11/2030
Tarehe ya Kutoka ukitoa robo ni Tarehe 05/07/2029;
Mapambano yaendelee!!
PRAYFORTANZANIA retweeted
Huyu ndo Jaji Ndunguru ambae kamfunga Mhe. Lissu kwa agizo la Nduli Idd Amin Mama.
Incase kimuona huko kanisa au mtaani maana najua kuna watu ni jirani yenu.
PRAYFORTANZANIA retweeted
ALERT: Seikali imeanza kuzima Internet. POLICE nao wameanza kukamata watu maeneo ya Ubungo, Kimara na Mbezi mwisho, wananyang'anywa na simu zao. Vijana kaeni chonjo. Serikali inapika kitu.
PRAYFORTANZANIA retweeted
Jaji Chande tutakurejea acha tumalize masuala ya msingi.
PRAYFORTANZANIA retweeted
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 499
Jaji Ndunguru anasema kwamba Mahakama inaamini kwamba mshtakiwa alikuwa na notice ya kosa dogo hivyo alikuwa na nafasi ya kujitetea na ushahidi wote uliotolewa umejikita kwenye uchochezi na alichochea umma kuzuia uchaguzi wa 2025
Kwa mujibu wa kifungu cha 390 cha Kanuni ya Adhabu Mahakama imeridhika kwamba Lissu alitenda kosa la uchochezi kwa mujibu wa kifungu cha 390 cha Kanuni ya Adhabu.
Hivyo Mahakama hii inamtia hatiani kwa kosa hili la Uchochezi.
Jaji Ndunguru: Upande wa mashtaka
Anasimama Katuga anasema Kamba kwa mujibu wa kifungu cha 339 cha CPA mahakama hii inaweza kupokea mpaka ushahidi kwenye kutoa proper sentence.
Upande wa Jamhuri tunajua adhabu ina malengo mojawapo ni kutoa onyo kwa mtu aliyetenda kosa ili asirudie kosa hilo au makosa mengine na linakuwa onyo kwa watu wengine wenye nia ya kutenda kosa hilo ambalo mshtakiwa ametiwa hatiani.
Upande wa Jamhuri mbali na kutokuwa na previous records za mshtakiwa za makosa ya nyuma, kwa mujibu wa taarifa zilizopo polisi kumekuwa na ongezeko kubwa sana la watu wenye kutenda kosa la kuchochea umma wa watanzania kwa maslahi yao binafsi either ya kisiasa au ya kiuchumi.
Vitendo ambavyo mara zote vinaharibu amani ya nchi, vinaathiri uchumi wa nchi kwa maana ama vinapelekea uharibifu wa mali za umma zikiwemo na mali binafsi.
Hivi vitendo vya kichochezi vinaathiri uchumi wa nchi na vimepelekea umma wa watanzania kuwa na hofu kuwa kutakuwa na matukio ya uvunjifu wa amani hivyo wanashindwa kufanya shughuli za kiuchumi.
Waheshimiwa vitendo vya kiuchochezi vinaathiri uchumi wa wananchi na hili ni kosa kisheria, wakati mnatoa adhabu tunawaalika katika hotuba halali ya Jaji Chande na Tume yake baada ya kufanya uchunguzi bila kuchagua upande wowote walisema sababu za vurugu wakati na baada ya uchaguzi wa 2025 zilisababishwa na kauli za baadhi ya wanasiasa.
Kifungu cha 35 kinatoa general punishment ambayo adhabu yake ni miaka 5 hivyo tunaomba mahakama hii iangalie athari ambazo zimetokea kutokana na kauli ambazo mshtakiwa ametiwa hatiani pamoja na hotuba ya jaji chande.
Taarifa ya Chande inaonyesha hasara inayotokana na uchochezi uliotokana na kauli hizo.
Tunaomba adhabu kali Waheshimiwa majaji ili iweze kukidhi nia ya adhabu kisheria.
Waheshimiwa kifungu hiki kinasema adhabu kubwa ni miaka 5 au pamoja na faini.
Ni faini kiasi gani ni Mahakama kuangalia athari kutokana na athari zilizotokea. Ni hayo tu.
Jaji Ndunguru anamuuliza Mshtakiwa kama analolote la kusema?
Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa majaji nina maneno ya kuzungumza ila naomba dakika 5 nifanye consultations na mawakili wangu ili niweze kuzungumza hayo ninayotaka kuzungumza.
Jaji Ndunguru:Sawa
Part 500 itaendea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost.
PRAYFORTANZANIA retweeted
#Updates Katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Mhe. Tundu Lissu, Mahakama haijamkuta na hatia ya kosa la uhaini. Hata hivyo, Mahakama imemtia hatiani kwa kosa dogo la uchochezi ndani ya shtaka hilo.
PRAYFORTANZANIA retweeted
Kesi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, inaendelea kusomwa leo Ijumaa, Novemba 6, 2026, katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam ambapo katika mwendelezo wa hukumu hiyo ya kesi hiyo mahakama imebainisha kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kiini cha pili cha kosa la kuitishia Serikali.
Kwa mujibu wa kiongozi wa jopo la majaji watatu waliosikiliza kesi hiyo, Jaji Dunstan Ndunguru, kosa la kuitishia Serikali lina misingi au viini vitatu vikuu ambavyo upande wa Jamhuri unapaswa kuvithibitisha bila kuacha shaka yoyote. Viini hivyo ni pamoja na mshtakiwa kuwa katika utii wa Jamhuri, kujenga nia ya kuitishia Serikali, pamoja na kudhihirisha nia hiyo kwa vitendo au maandishi.
Jaji Ndunguru alifafanua kuwa ili nia hiyo ionekane imedhihirika, lazima kuwepo na uchapishaji wa maandishi, machapisho, au kupitia kitendo cha siri kinachojidhihirisha wazi. Aliongeza kuwa viini viwili vya mwisho ndivyo vilivyokuwa kiini cha ubishani mkubwa wa kisheria kati ya upande wa utetezi na upande wa mashtaka wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo.
Mwishoni, mahakama imesisitiza kuwa uthibitisho thabiti wa viini hivyo viwili ndio unaobeba hatma ya shauri hilo na ungetumika kuamua iwapo Lissu ana hatia au hana hatia. Uamuzi huo mdogo umetolewa huku usomaji wa hukumu kamili ukiendelea mahakamani hapo ili kutoa mwelekeo wa mwisho wa kesi hiyo.
#KitengeUpdates
PRAYFORTANZANIA retweeted
The prosecution collapsed on treason, so Section 319 is the backup plan: just swap in sedition and keep him locked up anyway. Same evidence, same outcome, thinner charge.
#FreeTunduLissu























