Lastborn retweeted
“Mimi nilienda kuzika mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa kitongoji -Manyoni. Kama unaweza kuua mgombea wa kitongoji, kwenye uchaguzi mkuu utafanyaje?”
Tundu Lissu.
Lastborn retweeted
Kupitia shauri la kikatiba No. 7300/2006 linaloendelea katika mahakama kuu, masijala ya Dar Es salaam, Tundu Antipas Mugway Lissu amezidi kujidhihirisha kama mchawi wa sheria “Law Sorcerer”
Ifahamike kuwa, Lissu ni specialist wa “Environmental Laws” taaluma aliyokuwa akiitegemea kumpatia mkate wake wa kila siku kabla mambo hajambadilikia alipoamua kujiingiza kwenye siasa za upinzani nchini.
Kupitia misukosuko anayoipata kwenye siasa, Lissu ameweza pia kuuthibitishia umma uwezo wake mwingine kwenye Criminal and Public Laws.
Kwenye Criminal Laws, Lissu ameweza kuonesha uwezo wake alipowatetea wamiliki wa @JamiiForums akilinda sera za faragha za mtandao huo. Kesi hiyo ilikuja kuzaa sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi.
Mwaka 2011, Lissu alijikuta akisota rumande wilayani Tarime mara baada ya mauaji ya wananchi wanne ambao ni Chacha Ngoka wa kijiji cha Kewanja, Emanuel Magige wa Nyakunguru, Mwikwabwe Marwa na Chawali Bhoke wa Mugumu.
Wananchi hawa waliuwawa kwa risasi za polisi waliodai kuwa marehemu walivamia eneo la mgodi wa Nyamongo. Katika sakata hili, Lissu alijikuta akichaniwa nguo na kuwekwa makwaya.
Kwenye Criminal Law, nyayo za Tundu Lissu ni nyingi zinazoweza kuwachosha kwani hadi niandikapo, Lissu yupo mahakamani akijitetea kwa kesi ya uhaini.
Kilichonilazimu kuinua kalamu yangu leo, ni masterpiece cross-examination ambayo Lissu amemfanyia jana mkuu wa Gereza la Ukonga anakoshikiliwa hadi sasa.
Jana, Lissu amefanya nimvulie kofia nyingine kwenye issues za Public Laws ambayo hujumisha Constitutional na Administrative Laws.
Kwa jicho la kisheria, jana Lissu amefanikiwa kuivunjavunja credibility ya ACP, Andrew Shabani Ntamamiro, Mkuu wa Gereza Ukonga,
ACP Ntamamiro, kwa kuchanganyikiwa na madodoso yaliyokuwa yakimpandisha na kumshusha, alijikuta nyakati nyingine akijicontradict, akikili uongo wake na nyakati nyingine kwa kupitiwa, mkuu huyu wa Gereza alionesha wazi kuwa hana liability yoyote ya kufata orders za mahakama jambo ambalo liliwalazimu majaji kuwa wakali dhidi yake na kutaka kutunisha misuli ya muhimili.
Tuanze kwanza na sababu za kesi hii ya kikatiba.
Msingi wa kesi hii ni malalamiko aliyokuwa akiyatoa Lissu kwenye kesi yake ya uhaini
Kuwa, ananyimwa haki yake ya usiri (confidentiality) anapokuwa akiwasiliana na mawakili wake kinyume cha sheria. Hapa Lissu alieleza jinsi mkuu wa gereza la Ukonga alivyokuwa akitoa maelezo kwa wasaidizi wake, kusikiliza maongezi ya Lissu na mawakili wake kila waendapo kumtembelea gerezani.
Pili Lissu anadai kunyimwa haki yake kuonana na kuwasiliana na baadhi ya mawakili na viongozi wengine wa chama chake. Kuwa Mkuu wa gereza Ukonga amekuwa akiwajibu watu hao hawapo kwenye orodha ya watu ambao Lissu aliorodhesha wamtembelee kinyume cha sheria.
Hapa ndipo nilipoushangaa zaidi utulivu wa Tundu Lissu katika kupanga mikakati ya kesi yake.
Ni kwamba Lissu alihakikisha anaielezea mahakama wazi juu ya kunyimwa haki hizi katika kesi yake ya uhaini.
Hapa Lissu hakujali kama orders ambazo mahakama zitaitoa kwa Jamuhuri zitatekelezwa au kutotekelezwa. ( kwa kuamini kuna muhimili unaohisi umejichimbia zaidi)
Lissu alichojali ni madai yake tu kuwa “on record” kwenye mwenendo wa kesi yake ya uhaini.
Baada kuhakikisha hilo limefanyika, Lissu akajikita kwenye kukusanya ushaidi usio na chembe ya mashaka.
Hapa Lissu akakusanya orodha ya wageni wote waliomtembelea mahabusu, pamoja na maoni ya mkuu wa gereza aliyokuwa akitoa kwenye majina ya wageni wale.
Maoni mengi yakitoa sababu ya kuzuiwa kumuona Lissu, na mengine yakielekeza mazungumzo ya Lissu yafuatiliwe kwa karibu.
Ni vyema sasa tukianza kujiongoza kwenye mahojiano kati ya Lissu na mkuu wa gereza ili kuona jinsi ubongo huu ulivyobarikiwa kipaji cha hali ya juu cha taaluma ya sheria.
Lastborn retweeted
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 26
Tumerejea baada ya Mapumnziko ya nusu saa.
Anaanza Wakili wa waleta maombi Adv. Emmanuel Ukashu kumuhoji Maswali Mkuu wa Gereza la Ukonga Ntamamiro (Bwana Jela)
Adv. Ukashu: shahidi umewahi kuisikia TLS?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio naifahamu.
Adv. Ukashu: Ili mtu aingie Gerezani inahitajika wewe ndio umruhusu aingie?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sahihi
Adv. Ukashu: Ni sahihi ukipewa maelekezo yoyote lazima utekeleze na Kamishna General?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ni sahihi
Adv. Ukashu: Maelekezo kutoka juu maana yake nini?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ni maagizo ya kiutendaji unayopaswa kutekeleza.
Adv. Ukashu: Usipoyatekeleza unaweza kufukuzwa kazi?
Ntamamiro (Bwana Jela) : kwa mujibu wa sheria.
Adv. Ukashu: Unaweza kumbishia Boss wako?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Siwezi kufanya hivyo.
Adv. Ukashu: Soma SUPP 4 tar. 12/03/2026 entry no. 8 hebu isome hapo.
Ntamamiro (Bwana Jela): Huruma Tehejas mfungwa aliyekuja kumtembelea ni mfungwa na shida ya kisheria. Maoni hapakujazwa. Na sahihi hamna.
Adv. Ukashu: Sasa alienda wapi huyu Wakili kama hakuna uliposaini na maoni hukuweka.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Nilisahau kujaza na naamini hakukataliwa pia.
Watu wanacheka. 😂😂😂😂
Adv. Ukashu: Kwanini usifukuzwe kazi kwa uzembe wa aina hii? Maana haijulikani alikuja kufanya nini?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Nifukuzwe tu kazi kama unaweza kunifukuza. Fanya hivyo ila mimi nimesema nilijisahau.
Adv. Ukashu: Unafahamu kazi ya uwakili ina maadili yake?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Kila kazi ina maadili.
Adv. Ukashu: Maadili ya magereza tumeshayaona hapa hujajaza nyaraka na hujui wakili alipoingia alielekea wapi? Sasa tuzungumze maadili ya mawakili.
Ntamamiro (Bwana Jela) : siyajui mi sio wakili.
Adv. Ukashu: Unaijua Mandela Principle?
Ntamamiro (Bwana Jela): yes
Adv. Ukashu: soma hapa inasemaje?
Ntamamiro (Bwana Jela): Mfungwa atazungumza na wakili wake kuwa atazungumza bila kikwazo.
Adv. Ukashu: Umeitekeleza?
Ntamamiro (Bwana Jela): Inasema nizingatie sheria za ndani pia?
Adv. Ukashu: Sasa tuambie ni kifungu gani cha sheria ya ndani ambacho kiko kinyume na Mandela Principle.
Ntamamiro (Bwana Jela): Hakipo.
Adv. Ukashu: Nimemaliza. Naomba Wakili Neema aendelee.
Anasimama Wakili Neema Saruni.
Adv. Neema Saruni: Nitakuwa sahihi nikisema mtu anayekuja kumuona mfungwa anapaswa kuwa na sababu ya msingi?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ni sahihi kwa mujibu wa Sheria.
Adv. Neema Saruni : Ulisema mjibu maombi wa nne alikuwa na orodha yake hivyo basi alipotokea hayupo mlimrudisha?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ndio tulifanya hivyo.
Adv. Neema Saruni : Nitakuwa sahihi nikisema hamkumpatia haki yake ya kusikiliza.
Ntamamiro (Bwana Jela): Sahihi.
Adv. Neema Saruni: Nilipokuja mimi kumuona Lissu nilikuwa kwenye orodha yake?
Ntamamiro (Bwana Jela): Haukuwepo.
Adv. Neema Saruni : Nilipofika ikawaje?
Ntamamiro (Bwana Jela): tulienda kumuuliza lissu.
Adv. Neema Saruni : akasemaje?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Akaruhusu ukamuone.
Adv. Neema Saruni: Kwanini huyo mwingine mlimrudisha bila kwenda kuuliza Lissu anasemaje?
Ntamamiro (Bwana Jela): Hapo sasa ndio kuna utata.
Watu wanacheka 😂😂😂
Adv. Neema Saruni: Nimemaliza.
Haya wanasimama mawakili wa Serikali, anaanza Wakili wa Serikali anaitwa Wisdom
Wakili wa Serikali Wisdom: Ulitekeleza majukumu yako kwa mujibu wa nini?
Ntamamiro (Bwana Jela): masharti yapo kwenye sheria ikiwemo PSO.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji naomba asitaje kabisa PSO maana jana haikuwepo na hatukumuuliza. Asiulize. Sect. 156(3) ya Evidence Act iko wazi kuhusu Re- examination.
Jaji: Sasa Wakili wa Serikali Wisdom uko tayari kuendelea na njia hiyo ili tumruhusu Lissu nae aanze kuuliza kwenye PSO.
Wakili wa Serikali Wisdom: Naomba tu niishie hapo. Sitaendelea mbele.
Watu wanacheka 😂😂😂😂
Part 27 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
Lastborn retweeted
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 17
Anaendelea Mhe. Lissu
Mhe. Lissu: Na mazungumzo ya Kisabo pia ulisema yasimamiwe kwenye ofisi ya kaimu mkuu wa gereza.
Ntamamiro (Bwana Jela) : ndio
Mhe. Lissu: Na tunakubaliana wale watu wote akina Mumbii, legal officer Stima, Kopro Dani, na akina mama watatu. Je hawa watu wanakuwemo humo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Si kweli. Huwa wanatoka. Wanaacha mazungumzo yafanyike.
Jaji: Lissu umeridhika na majibu ya shahidi.
Mhe. Lissu: Ngoja nataka kukamata watu waongo.
Mhe. Lissu: Kumbe maafisa wote mle chumbani wanatoka nje, sasa soma kiapo chenu ndugu yangu. Nakusomea kwenye kiapo chako
Kiapo kinasomeka kuwa walikuwepo.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Kuna ambao walikuwepo na kuna ambao walitoka.
Mhe. Lissu: Waliokuwepo ni akina nani?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Waliosindikiza
Mhe. Lissu: Akina nani?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sikumbuki
Mhe. Lissu: Waleta maombi wote wamewataja majina akina Mumbii, Koplo. Dani, Akina mama watatu mle ndani, legal officer na mtu wa usalama. Wamewataja majina. Wewe unasemaje?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sikubaliani nao mimi.
Mhe. Lissu: Twende kwenye ofisi ya Recha ACP. Soma SUPP 4 Tar. 24/12 ulisema alipokuja Kisabo. Asimamiwe kwa kaimu mkuu wa gereza na kusema wayafanyie ofisini ukawataja majina ambao wanapaswa wasimamie. Waeleze majaji kuwa wakati wote Recha anakuwepo, asipokuwepo atakuwepo Mumbii, Mohamed lazima awepo au Hamisi na anakuwepo Stima na maaskari wanaonifuata muda wote.
Ntamamiro (Bwana Jela) : sio kweli
Mhe.Lissu: Umewahi kuhudhuria mazungumzo hayo kwa Recha?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sijawahi.
Watu wanacheka. 😂😂😂😂
Mhe. Lissu: Tumewahi kufanya mazungumzo ofisi kwako mimi na mawakili wangu?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli.
Mhe. Lissu: Tar. 12/12 imeandikwa SUPP 6 Umeiona?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sioni
Mhe. Lissu: Mawakili msaidieni mmeleta wenyewe.
Ukiiona siku hiyo niliyosema tar. 12/12 ulielekeza hivi kaimu mkuu wa gereza, Mtu wa usalama na mwanasheria wa gereza ulisema mazungumzo yawe ya kisheria zaidi. Kweli au sio kweli?
Ntamamiro (Bwana Jela): Kweli
Mhe. Lissu: Je hawa uliowaelekeza wote zaidi ya watu watatu walikuwepo au hawakuwepo kwenye haya mazungumzo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hawakuwepo.
Mhe. Lissu: Walisikiliza au hawakusikiliza?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hawakusikiliza.
Mhe. Lissu: Waliwezaje kusimamia mazungumzo wakati hawakuwepo na hawakusikiliza?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Kuna facial impression.
Majaji wanacheka.😂😂😂😂
Ntamamiro (Bwana Jela): Naomba nifafanue.
Mhe. Lissu: Sitaki unifafanulie. Sasa kama hawakuwepo facial expression walizionaje wakati hawapo.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hili suala ni la kisheria tunamkagua wakili kitambulisho.
Mhe. Lissu: Nani kakuuliza hayo.
Jaji: Usitupotezee muda. Hebu soma maelekezo yako kuwa wasimamie mazungumzo na watu hawakuwepo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ukiona wanakumbatiana hayaruhusiwi.
Jaji: Uliwaelekeza wafanye nini kwenye mazungumzo hayo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Walisimama mbali wakawa wanaangalia.
Mhe. Lissu: Sasa waeleze majaji kama kitendo cha kukumbatiana ni maneno au kitendo.
Ntamamiro (Bwana Jela) : ni kitendo.
Mhe. Lissu: Ulisema wakasimamie vitendo au maneno?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Mazungumzo yaani maneno.
Watu wasonya tu. Majaji pia wamekasirika sana kwa majibu haya. Watu wengine wanacheka kimya kimya.
Mhe. Lissu: Sasa twende SUPP 6 ukurasa unaofuata. Wapo mawakili watatu ambao ni Catherine Chanjarita, Shamumoyo na Constatine kwenye comment zako umesema Adm. Officer simamia mazungumzo yao kwa karibu. Sasa swali langu simamia kwa karibu yanawezekana kutekelezwa bila maaskari hao kuwepo kwenye mazungumzo hayo?
Ntamamiro (Bwana Jela): Sijasema wasikilize nimesema wasimamie kwa karibu.
Part 18 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako.
Lastborn retweeted
Replying to @HildaNewton21 @goodluckkissang
Shimo la LUKUVI limekamilika. Kubabake😂
Lastborn retweeted
Unamuweka ndani Niffer kwa challenge ya Nywinwinywi.
Madicteta wana tatizo kubwa sana la self esteem.
#D9 #SamiaMustGo
Lastborn retweeted
Inasikitisha sana kuona watu waliosoma wanashindwa kuona ukweli huo. Kulikuwepo amani wakati wakoloni wanatawala hiyo hakuwazuia wazee wetu kupigania uhuru. Tukaupata na baadaye tukawa Jamhuri maana yake nchi ya watu na si ya kifalme. Lengo kuu ni kustawi pamoja katika nchi ambapo watu wako huru na wanachagua viongozi wao.
Tulianza vibaya bila kuwa na Haki za Binadamu katika Katiba yetu na tukaharamisha vyama vingi. Mwaka 1984 Haki za Binadamu zikaingizwa kwenye Katiba na mwaka 1992 tukaruhusu vyama vingi. CCM wakakataa mabadiliko ya Katiba ya kuwezesha Tanzania kuwa kweli nchi ya vyama vingi. Kila uchaguzi tumeshuhudia uporaji wa uchaguzi na hali ikaharibika 2015.
Ushindi wa Magufuli dhidi ya Lowassa ulikuwa ni wa utata. Upinzani kwa kushikilia amani wakakubali kuibiwa ushindi wao. Vivyo ule 2020 ambapo Magufuli na CCM walipora uchaguzi mchana kweupe. Usisahau ule wa 2019 na 2024 wa Serikali za Mitaa.
Waswahili wana msemo usemao "Mwenye macho haambiwi tazama" na Walatini, kupitia Wanasheria,wanasema "Res ipsa loquitur"(the matter speaks for itself) au suala linajieleza lenyewe. Ukweli huo umedhihirika mwaka huu. Hivi nani mtu mwenye dhamiri na roho iliyo hai anayeweza kusema kuwa tarehe 29 Oktoba, Samia alichaguliwa na Watanzania milioni 32?
Nani anaweza kusema huku,akikumbuka amri ya kutosema uongo, kuwa kura zilizopigwa nchi nzima zilihesabiwa, matokeo yakatangazwa vituoni, yakatumwa kwenye Tume na mshindi halali akatangazwa? Nani anaweza kusema kuwa nchi hii ombaomba, inaweza kuzima mtandao kwa siku tano huku kukiwa na zuio la watu kutotoka nje, lakini Tume ikawa na uwezo wa kuhesabu kura na kumtangaza mshindi!
Sasa kampeni ya kupigania mabadiliko ya Katiba ina miaka 32. CCM imekuwa inatumia kila mbinu kukwamisha mabadiliko hayo na kuwapachika majina ya ajabu ajabu wapinzani. Mara ni "vibaraka wa mabeberu", "wana uchu wa madaraka" " wanaotaka kuharibu amani ya nchi" na mengineyo mengi. CUF miaka ya 2000 mwanzoni kiliitwa chama Cha Kiislamu, Chadema chini ya Mbowe, chama cha Wachaga, na sasa kwa Lissu eti ni cha "wahaini na magaidi".
Ukweli umedhihiri kuwa unaweza kudanganya watu wote kwa muda au kipindi fulani lakini si muda wote. Sasa uongo na propaganda za CCM zimeonekana na kubainika kwa vijana wengi ambao hali zao zinaendelea kuwa mbaya kila uchao. Vijana wametambua kuwa viongozi lazima wapatikane kupitia uchaguzi huru na WA haki. Kudai Hilo ambalo halitakiwi kupingwa na hata mmoja wetu kumesababisha Vifo vya Maelfu ya Watanzania wenzetu. Wameuawa si na Wapinzani bali vyombo vya dola. Serikali Gani halali inaamrisha Polisi na vikosi vya Usalama kuua watu au raia wake? Hiyo si Serikali inayofahamu wajibu wake wa Kikatiba wa kulinda uhai wa raia wake.
Kuandamana ni haki ya msingi kabisa ya wanadamu katika nchi yoyote ile. Mahatma Gandhi aliwaongoza Wahindi milioni 300 kuwapinga Waingereza na kusababisha India na Pakistani kuwa huru. Martin Luther King Jr, aliwaongoza Waafrika wa Kimarekani kupinga ubaguzi wa rangi huko Marekani. Hapa Tanzania,nchi iliyokuwa mstari wa mbele kukomboa nchi nyingine Afrika, kuandamana kunageuzwa kuwa uhaini na ugaidi? Ikumbukwe kuwa Samia ni kiongozi ambaye katika kipindi cha miaka 4 na miezi 4 ya utawala wake, amewaweka ndani kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja na miezi minne viongozi wa Chadema na kuwafungulia mashitaka makubwa yau ugaidi na uhaini. Mbowe alikaa ndani miezi minane. Lissu naye sasa huu ni mwezi wa Saba. Mbowe alikuwa mwenyekiti na Lissu sasa ni Mwenyekiti.
Sasa watu wanaona na wanadai mabadiliko. Samia na CCM walikataa. Samia akaunda Kikosi kazi kikatoa mapendekezo akayaweka kapuni. Akaunda Tume ya Haki Jinai, chini ya Jaji Mkuu Mstaafu Othman Chande na Ombeni Sefue. Tume hiyo ikasema Jeshi la Polisi livunjwe liundwe upya, Samia akakataa. Tulichovuna kutokana na kukataa huko pamoja na kutokuwepo Tume Huru ya Uchaguzi mauaji makubwa na kuaibisha ya Watanzania wenzetu. Cha ajabu hata Serikali hii haijasema hata tuwaomboleze. Mara ya kwanza iliwaita "wahuni.
Lastborn retweeted
Bango Linasomeka Loud and Clear....
#December9
Hata Mimi nataka maridhiano lakini tunahitaji uaminifu wa Mchakato huo kuanzia Kwa vyomba vya usalama, Mahakama, Bunge na Serikali yote Kwa ujumla.
Nipo tayari kuunga mkono maridhiano ikiwa wawakilishi wetu ni:
1. Humphrey Polepole
2. Deus Soka
3. Mdude Nyagali
Lastborn retweeted
Replying to @C_NyaKundiH
It's not over until samia either awe Gerezani au kaburini.
Lastborn retweeted
December 9....bila kuchoka ✌️
Au mnaoneje....
#maandamanoPart2
Nakumbuka 30/10 nilikua kama mstari wa 3 hivi tupo nyomi. Ni wazi wapo waliokua wanasema jamani Kuna kufa kama wewe muoga jitoe pembeni ila ndo kwanz ni kama morali ndo ilikua inapanda watu wakisema hivyo. We knew there was death it was a matter of time. Dak kadhaa mbele..
Ziliingia cruiser za askari hawakua na sare ya kijani na kaki ila full black na face mask. Kilichofata ni mziki wa risasi aisee, frontline kadhaa walilala palepale hawana usemi, baadhi majeruhi. Njugu zilipenya mpaka tulipo Mimi nilikua katikati ya wadada wawili na waliniambia..
Tushike mikono, nilimshika wa kushoto ile nataka nimshike wa pili alikula ya kifua hakupga ukelele she went quietly down. It was chaos lakini cha ajabu nilijihisi wajibu wa kumlinda yule binti mwingne hofu ilikata ghafla nikajisemea labda nife Mimi japokua hatujuani kabisa.
Lastborn retweeted
SARIKALI ILIFANYA MACHAFUKO YA KUUA NA KUTEKA WATU, WANANCHI WAMEFANYA MACHAFUKO YA KUCHOMA MOTO MALI ZA NCHI.
Serikali imelalamikiwa mara nyingi juu ya machafuko ya utekaji, mauaji imekaa kimya haikuchukua hatua yoyote, Serikali imelalamikiwa juu ya upotevu wa pesa za umma kwenye Ripoti ya CAG inayotolewa kila mwaka imekaa kimya, haya hayaja iumiza Tanzania tu bali tujikumbushe ya Kenya.
Kenya mwaka 2007 yalitokea maandamano makubwa kipindi cha uchaguzi kama yaliyotokea Tanzania watu zaidi ya 1500 waliuwawa.
Wakenya walichoma mali za Serikali na vibaraka wake, maandamano yale yalipelekea Kenya ikapata katiba mpya ili kukomesha machafuko mengine yasijirudie ndio maana leo wakenya wakiandamana hawachomi moto mali za umma, leo Tanzania imepita katika mapito yaleyale ya Kenya ya 2007 badala viongozi wawape wananchi walichokuwa wanakitaka wao wanaaidi kupambana na wananchi wenye maumivu makali mioyoni mwao ambayo hayajapata tiba.
Wapeni wananchi KATIBA MPYA hii ndio Dawa ya kukomesha machafuko vinginevyo hamtakuwa salama.
Jiulizeni Mlimuua Ally Kibao, Mlimuua Alphonce Mawazo kwa kumkatakata kwa mapanga na Mashoka yaani kifo cha kutisha, Mkamteka Mdude Nyagali Damu yake ikatapakaa Ardhini, Mmemteka Deusdedith Soka, Mkamteka Humphrey Polepole damu yake ikatapakaa Ardhini mmeteka watu zaidi ya 200 kabla ya uchaguzi.
Hayo yote hayakuwafanya watanzania waogope na hawakuogopa kwa sababu hayakuwapa walichokuwa wanataka, ambacho ni mateka wote waachiliwe huru, Tume huru ya uchaguzi, Katiba Mpya,Mahakama huru na Bunge Huru.
Kwahiyo Serikali ya Samia Suluhu Hassan inataka damu za watanzania zaidi ya 3000 ziende bure? Wakenya walijenga nchi yao kwa Damu ya zaidi ya watu 1500.
Leo mmeelekeza bunduki kwenye vichwa vyao, matumbo yao na miguu yao mkawauwa kama panya, msidhani mmetibu tatizo bali mmeongeza tatizo.
Wapeni wananchi wanacho kitaka kwani awamu ijayo hawata choma moto mali za umma bali watawachoma moto wale waliopuuza kilio chao cha muda mrefu.
REPOST
Imeandikwa na
Twaha Mwaipaya.
Share isomwa zaidi.
TUTAKUWEPO🫵😎
Lastborn retweeted
Anaandika Askofu Bagonza PhD.
“NGUVU” ALIFUNGA NDOA NA “HEKIMA” HUKO KENYA 2017.
Tujikumbushe:
1. Uchaguzi Mkuu ulifanyika 8/8/2017 huko Kenya. Rais Kenyatta akashinda. Odinga akakataa matokeo. Mahakama ikafuta matokeo, Uchaguzi ukarudiwa. Odinga akasusia kushiriki. Uchaguzi ukafanyika. Mahakama ikamtangaza Kenyatta kuwa mshindi.
2. Odinga akaandaa mgomo na maandamano. Majeshi yakajipanga. Kabla maandamano hayajaanza, Bw. Nguvu akamwona Bi. Hekima akamtamani na kumpenda. Akamvisha pete ya uchumba. Majeshi yakatoka mitaani, maandamano yakafanyika kwa amani.
4. Odinga akaapishwa kuwa Rais wa wananchi, Kenyatta akaapishwa kuwa Rais wa Jamhuri. Bw. Nguvu na Bi. Hekima wakawaalika Kenyatta na Odinga kwenye breakfast ili kuwapongeza. Wakakumbatiana hadharani. Kenya ikashinda, Odinga na Kenyatta wakashindwa.
5. Kila mmoja akajitukana badala ya kumtukana mwenzake. Tangu siku hiyo Kenyatta na Odinga wakawa kama kumbikumbi. Bibi mbele, Bwana nyuma au kinyume chake.
6. Mtoto mshamba huwa anadhani mama yake ndiye bingwa wa mapishi duniani. Hatembei, kwa hiyo nyumbani ndiyo dunia yake na mapishi ya mama yake ndiyo "chiboko" yao. Tujiulize:
7. Tungepoteza nini kuwaruhusu “wahuni” wanaotaka kuandamana? Tukawapisha njia yao. Wakaenda waendako. Wakapokelewa na Afisa Mtendaji wa kata. Wakasoma risala yao. Kesho yake wakarudi, wakapokelewa na kada aliyeshindwa kura za maoni. Siku ya tatu wakaja, wakapokelewa na Afisa aliyetumbuliwa kwa rushwa wakati rushwa haikutumbuliwa. Mwishowe mwenye nyumba akajitokeza.
8. Mwenye akawasikiliza, wakamsikiliza. Kwa pamoja wakaubariki wizi au kwa pamoja wakaulaani wizi. Kama ni wizi kwani yeye aliiba? Kama kuns walioiba kwa niaba, Mkuu akaahidi kuwafuatilia.
Mbona ni suala la muibiwa kura na mnufaika na wizi "kujifanya" wanamlaani mwizi na kupatana kumshughulikia kwa pamoja?!
Hiyo ndiyo ndoa kati ya nguvu na hekima. Lakini sasa?;
a. Mabomu na risasi zetu vimelipuka!
b. Ardhi imekunywa damu badala ya
maji. Familia zooote poleni😭😭
c. Polisi wanashughulika na waandamanaji badala ya kushughulika na walioiba,
d. Viongozi wa dini wanawasikiliza watuhumiwa kuliko wanavyomsikiliza Mungu
e. Walioiba hawana amani, walionufaika na wizi hawana amani, walioua hawana amani, hata wasioamini kuna wizi nao hawana amani.
f. Mtandao wetu usingefungwa na kusababisha hata walioufunga nao wakose mawasiliano.
g. Walioshinda wamezuiwa kufanya sherehe na walioshindwa wamezuiwa kufanya matanga. Waliofiwa hawana uhuru wa kuomboleza kwa sababu walitoka nje ya nchi.
h. Makanisa ambayo hayakufunga kwa COVID, yakafunga kwa Gen Z wa kigeni!
Kweli, Ukikosea njia, kila njia ni sahihi.
Bila nguvu kuoana na hekima, tutapanda bangi tutegemee kuvuna mchicha.
Atakayekubali kurudi nyuma ndiye mshindi. Nchi ina mipaka lakini magonjwa, haki, uovu, na uhalifu havina mipaka.
Mataifa yenye amani ya kudumu ni yale yanayowaogopa raia wake. Mataifa yenye mashaka ya kudumu ni yale yanayoogopwa na wananchi wake.
Internet karibu, tulikumiss kweli.
Wamefunga uwanja wa comment na ving'amuzi wanashawishi tulipie
#NBCPremierLeague inaendelea wikiendi hii
Jumamosi Novemba 8, Saa 10:00 jioni Pamba Jiji watakuwa uwanja wa nyumbani CCM Kirumba wakiwakarobisha Singida BS.
Saa 1:00 usiku, JKT Tanzania watakuwa dimba la nyumbani Meja Jenerali Isamuhyo wakiwaalika Simba SC.
Jumapili Novemba 09,mabingwa watetezi Yanga SC watakuwa uwanja wa KMC Complex wakicheza na KMC FC.
Saa 1:00 usiku, Namungo FC watakuwa nyumbani uwanja wa Majaliwa wakiwaalika matajiri wa jiji AzamFC.
Kwa kifurushi cha shilingi 28,000 unatazama michezo hii mbashara kupitia AzamSports1HD.
#NBCPL #Azamtvsports



















