Voice of Bongo (@voiceofbongo) header
Voice of Bongo (@voiceofbongo) profile picture

Welcome to the Official VOB Twitter Page. (Disclaimer: The views expressed here do not necessarily reflect the views of Voice of Bongo

Tanzania
Joined July 2015
Kijana Kefasi Mtega mwenye umri wa miaka 30 anayetuhumiwa kuhusika na wizi wa miundombinu ya umeme Iganjo hadi Sumbawanga, ameomba Viongozi wamuhoji kwa Lugha ya Kiingereza pekee kwani ndiyo lugha anayoielewa pekee.
2
359
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Patrobas Katambi amezitaka Jumuiya za kiraia nchini kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuimarisha umoja, mshikamano na kulinda amani. Wito huo ameutoa wakati akizungumza katika Maadhimisho ya Miaka 70 ya Usajili wa
1
286
Jumuiya za Kiraia katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam. Katambi amesisitiza kuwa,Taifa letu lina historia nzuri katika kulinda amani na utulivu wa nchi, hivyo ni vizuri kuendelea kuilinda historia hiyo
1
102
kwa kuepuka kuingia kwenye vurugu na machafuko yanayoweza kusababisha kupoteza amani.
9
Tume ya Rais ya kuchunguza vurugu na uvunjifu wa amani uliotokea wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa oktoba 29 2025 sasa ipo katika wilaya ya Temeke. Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji mstaafu Shaaban Lila amewataka wananchi wa wilaya ya temeke kufika katika chuo kikuu kishiriki
2
318
cha elimu DUCE ili kutoa ushahidi kwa wanayoyajua kuhusu kilichotokea wakati wa vurugu hizo. Kwa upande mwingine, Jaji Shaaban Lila amewahakikishia wananchi wanaokuja kutoa ushahidi kuhusu usalama wao na usiri wa watakayoyasema katika tume hiyo.
57
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kimkakati katika kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua za El Niño zinazotarajiwa kunyesha.
1
243
Katika ziara ya kukagua maandalizi hayo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Hamad Masauni, ameeleza kuridhishwa na hatua zinazochukuliwa na TRC ambapo pia amewataka viongozi wa Wilaya ya Morogoro kuiga mfano huo kwa kuchukua hatua za
1
41
haraka na za makusudi ili kulinda maisha ya wananchi na miundombinu. Waziri Masauni pia ameeleza kuridhishwa na utayari na hatua za TRC kwa kutoa mchango wa rasilimali fedha na wataalamu kupitia mpango wake wa Uwajibikaji kwa Jamii (Corporate Social Responsibility - CSR)
5
Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega, amewasili mkoani Tabora leo, Septemba 26, 2026, kwa ajili ya ziara ya kikazi yenye lengo la kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya miundombinu inayotekelezwa na Sekta ya Ujenzi mkoani humo.
1
372
Akiwa mkoani Tabora, Waziri Ulega atakagua miradi mbalimbali ya barabara na miundombinu mingine inayotekelezwa katika mkoa huo, ili kujionea maendeleo ya miradi hiyo, pamoja na kubaini changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wake.
1
55
Waziri Ulega ameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Dkt. Charles Msonde; Mkurugenzi wa Matengenezo kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Lazaro Loshirai, pamoja na wataalam kutoka Wizara ya Ujenzi na TANROADS.
26
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawakumbusha wananchi kuchukua tahadhari ya matumizi salama ya umeme wakati wa mvua za El Niño zinazotarajiwa kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini. Ukiona hitilafu ya umeme, toa taarifa kwa kupiga namba 180, kupitia mitandao yetu ya
1
289
kijamii au makundi rasmi ya TANESCO ya _WhatsApp_ yaliyopo kote nchini. Umeme Salama, Usisubiri Athari, Chukua Tahadhari.
91
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Bw. Alban Mark Kihulla, amekutana na Waandishi wa Habari kueleza utekelezaji wa majukumu ya Wakala kwa mwaka wa fedha 2025/2026 pamoja na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka 2026/2027, akisisitiza
1
211
umuhimu wa uhakiki wa mita za maji katika kuhakikisha usahihi wa vipimo na kulinda maslahi ya wananchi. Katika utekelezaji wa majukumu hayo, WMA imeendelea kuhakiki mita za maji, zikiwemo mita mpya na zile ambazo tayari zinatumika katika makazi ya wananchi. Kwa mwaka wa
1
71
fedha uliopita, Wakala umefanikiwa kuhakiki jumla ya mita za maji 14,423. Aidha, Bw. Kihulla amewaelekeza wananchi namna ya kutambua mita zilizohakikiwa kwa kuangalia seal maalum yenye namba inayolingana na namba ya kipekee ya mita (serial number).
48
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Bw. Alban Mark Kihulla, ameeleza hatua zinazochukuliwa na Wakala katika kusimamia usahihi wa vipimo vinavyotumika katika sekta ya afya. Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya
1
194
WMA kwa mwaka 2025/2026 na mwelekeo wa mwaka 2026/2027, amesema Wakala huzingatia sheria za kitaifa pamoja na matakwa ya kikanda na kimataifa katika kuhakikisha vipimo vinakuwa sahihi na vinaaminika.
25