Voice of Bongo (@voiceofbongo) header
Voice of Bongo (@voiceofbongo) profile picture

Welcome to the Official VOB Twitter Page. (Disclaimer: The views expressed here do not necessarily reflect the views of Voice of Bongo

Tanzania
Joined July 2015
Photo by Voice of Bongo (@voiceofbongo)Photo by Voice of Bongo (@voiceofbongo)Photo by Voice of Bongo (@voiceofbongo)Photo by Voice of Bongo (@voiceofbongo)Photo by Voice of Bongo (@voiceofbongo)Photo by Voice of Bongo (@voiceofbongo)Photo by Voice of Bongo (@voiceofbongo)Photo by Voice of Bongo (@voiceofbongo)Photo by Voice of Bongo (@voiceofbongo)Photo by Voice of Bongo (@voiceofbongo)
Wakili mwenzetu hajui msingi huu muhimu wa kisheria?? Kwamba hajui moja ya jambo ambalo Mahakama imeshaweka msingi wa marejeo ya kisheria (precedent) katika kesi kama hizi ni ushahidi usioacha shaka kuwa ili mahakama itoe amri ya mtu ambaye anashikiliwa isivyo halali kufikishwa mahakamani (the writ of habeas corpus) lazima kuwepo ushahidi kuwa mlalamikiwa ndiye anayemshikilia mhusika? Wakili huyu hajui kuwa kanuni ya msingi ya mahakama ni kuangalia na kuchambua ushahidi uliowasilishwa mahakamani na si kusikiliza kelele, huzuni, furaha au masikitiko au mitazamo ya jamii katika suala husika?? Labda kwa faida ya jamii kabla hatujaitusi Mahakama nitoe elimu kudogo maana wenzetu wanaonekana wamechagua kuwa wanaharakati zaidi ya wanataaluma wa sheria. Nimesoma uchambuzi wa wanasheria mabingwa katika Forbes Legal wanaandika kuhusu kesi hizi kuwa: “For example, habeas corpus petitions in California can only be filed if the person is already in custody. In most states, judges will deny a habeas corpus case if the petition does not bring up any new evidence.” Kwamba msingi muhimu wa kwanza wa kesi za “habeas corpus” ni uthibitisho kuwa mtu anayatakiwa amri itoke kweli yuko mikononi mwa mlalamikiwa (already in custody) na pili ushahidi wa kushikiliwa kwake. Rejea: forbes.com/advisor/legal/cri… Mahakama za Tanzania pia zina msimamo huo huo kisheria. Shauri muhimu la hivi karibuni linaloweka msingi wa kesi kama hii ni la Mahakama Kuu ya Tanzania katika Michael Daniel Nyambore na Wenzake 6 Dhidi ya IGP na Wenzake (Misc. Criminal Application No. 38, 2022). Katika kesi hii ambapo watuhumiwa waliachiwa huru na Mahakama na kisha kukamatwa na Polisi mchana kweupe na hawakufikishwa Mahakamani (tofauti na kesi ya kina Soka ambao hawajulikani walikamatwa au walitekwa na nani na wapi) Mahakama iliiamuru Polisi (kwa kuwa ushahidi ulikuwa wazi na umekidhi) iwafikishe haraka Mahakamani watuhumiwa (the writ of habeas corpus)! Akifafanua msingi muhimu wa kisheria katika kesi kama hizo Jaji E. L. Ngigwana aliandika: “We need to EMPHASIZE that, it is now well established that the writ of habeas corpus will only issue if it is demonstrated that the person whom the writ is sought is in unlawful custody of the respondent.” Kwa tafsiri yangu Jaji anasema: “Ni vyema IKASISITIZWA kwamba kwa sasa ni kanuni ambayo IMESHAKUBALIKA kwamba maombi ya kutaka kuamrisha mtu anayeshikiliwa isivyo halali aletwe mahakamani lazima YATHIBISHE kuwa mlalamikiwa mahakamani ndiye anayemshikilia mtu huyo.” Msisitizo ni wangu). Namuuliza tena Wakili Msomi Madeleka na kundi lake akiwemo rais wetu Mwabukusi, mnasoma maamuzi ya nyuma yanayotoa miongozo kwa sisi mawakili au mmejaa mate ya matusi, kejeli, kulaghai umma hasa kila mnaposhindwa kesi Mahakamani?? Huu ndio msingi wa Section 4 ya TLS Act?? Kwa nini afisa wa Mahakama ushiriki kuichafua Mahakama na kuifanya idharaulike, ibezwe na kusiginwa na wananchi kumbe kosa si la mahakama ni lako wewe afisa na ntaalamu uliyetakiwa kuithibitishia Mahakama kwa ushahidi wa wazi ili ikupe haki unayoitaka na hukufanya hivyo? Ndio maana Kwa kauli ya wakili Madeleka hadharani akiitusi Mahakama wasiojua misingi hii ya sheria wamebeba kama ilivyo kejeli hiyo na wanamuamini wakili msomi na wao sasa wanaendeleza kueneza kejeli dhidi ya mhimili ambao umetimiza wajibu wake. Hii ni aibu kwetu sote mawakili kuanza kuwa “spin doctors” kwenye masuala ya Kimahakama. Nasema tena na tena: lazima sisi maafisa wa Mahakama na wanachama wa TLS tunaofuata misingi ya “Section 4” tupaze sauti zetu na tuseme ukweli na kama alivyosema Rais Mwabukusi ikiwezekana tufike mahali tushinikize mawakili wenzetu kutoivua nguo taaluma ya sheria na vyombo vyake vya usimamizi wa sheria ikiwemo Mahakama. Kamwe tusikubali kuibuka kwa wafifishaji badala ya maafisa wa Mahakama. Hawa ni wahuni kama wahuni wengine kwenye taaluma nyingine. Tuwakatae. Ukweli lazima usemwe na nipingwe kwa vifungu vya sheria. Nitashukuru zaidi.
1
1
123
forbes.com/advisor/legal/cri… “Section 4” Inavyoanza Kutusiwa na Kubanagwa na Kundi la Mwabukusi TLS! Niliwahi kuandika makala haya na kuonya wakati wa uchaguzi wa TLS nikihoji: “Hisia, Uanaharakati au Misingi ya Sheria Isimame Uchaguzi TLS?” Katika makala hayo nilihoji na kuwakumbusha wanaTLS wenzangu kuwa katika uchaguzi huo msingi wa kumpa rais bora wa kutuongoza mwaka mmoja ujao sio uanaharakati wake bali mlinzi makini wa malengo ya kuanzishwa taasisi hiyo yaliyomo kwenye kifungu mashuhuri kama “Section 4.” Niseme leo Mwabukusi na kundi lake ameshinda na hakuna ubishi juu ya hilo lakini taasisi hii imezidi kupotea sio kuanzia yeye tu bali tangu kitambo. Huenda baadhi tulidhani atairejesha heshima hiyo, lakini mwezi mmoja sasa madarakani hakuna matumaini yoyote na TLS inekuwa ya marusi, kejeli, uongo na propaganda dhidi ya mihimili mingine ya Dola. Jana nimesikitishwa mno na kauli za dharau na za matusi kwa mhimili wa Mahakama ya Tanzania zilizotolewa na mawakili wetu na wanachama wenzetu wa TLS tena wakiongea mbele ya rais Mwabukusi baada ya maombi yao kukwama Mahakamani. Awali nilimuona Wakili Peter Madeleka akisema anaushahidi zaidi ya fuso mbili kuonesha mahakamani kuwa kijana Soka aliyepotea kwamba anashikiliwa na polisi! Hapa aliongea kitaalam kweli kweli na alitimiza Section 4 (hata kama katika sayansi ya ushahidi wingi wa nyaraka sio hoja)! Lakini cha kushangaza wakili huyu huyu mwanachama mwenzetu wa TLS baada ya kutoka Mahakamani tu na kushindwa kesi aligeuka mporomosha matusi na dharau kwa Jaji, Mahakama na hata taaluma ya sheria na anaendelea hivyo katika mitandao yake ya kijamii hasa X. Hili halikubaliki kitaaluma na ndio msingi wa hoja yangu leo tena kuwa tunapaswa kukataa TLS hii ya kiharakati. Tujikumbushe “Section 4” Niliandika hivi: “Katika majukumu tisa mengi yanahusu kazi za chama hiki kuendeleza wanachama wake kitaaluma zaidi, maadili, taasisi kumiliki mali na kusimamia maslahi ya mawakili katika utendaji wao (Kifungu cha 4 chote isipokuwa kwa minajali ya hapa achana kwanza na 4c).” Sasa twende kwenye muradi wa kifungu 4c: Hiki ndio kifungu pekee kwa maoni yangu kinachoipa TLS jukumu la nje ya masuala ya taasisi na yale ya wanachama wake. Labda tukisome wote kwa sauti: “To assist the Government and the Courts in all matters affecting legislations and the administration and practice of the laws in Tanzania.” Muradi wa kifungu hiki kwa maoni yangu ndipo lilipojukumu la msingi la TLS na sisi mawakili wake ambapo kwanza ni “Kusaidia/Kushauri” Serikali na Mahakama katika masuala mengi sana ya utungaji wa sheria na utekelezaji wa sheria hizo. Hapa ndipo inapokuja ile dhana maarufu kuwa mawakili ni sehemu ya maafisa wa mahakama. Sisi kazi yetu sio kuvaa ukosaji au kutokuwa na ukosaji kwa watuhumiwa bali tunakwenda mahakamani kuisaidia Mahakama itende haki. Ndio maana wakili anaweza kumtetea hata mtu ambaye kwa nje wewe unaona ni muuaji au mbakaji. Hawaungi mkono hayo bali wako mahakamani kuisaidia Mahakama itende haki. Basi. Sasa mawakili wa siku hizi akishindw kesi yese ni bonge la wakili na atajinasibu hivyo akishindwa mahakamani badala ya kufuata taratibu za kimahakama za rufaa (kwenda mahakama ya juu ya ile iliyoamua) au marejeo (kwa mahakama ya ngazi ile ile) ataachana na msingi wa “Section 4(c)” atakimbilia mitandaoni na kwenye vyombo vya habari na kuponda, kutukana, kuropoka na kukashifu majaji na mahakama! Hivi nini kimetokea kwenye taaluma hii? Yani wakili yule yule ambaye siku kadhaa nyuma alisimamia kesi ya Mwabukusi na Mahakama ile ile ikampa ushindi na mteja wake kurejeshwa kwenye uchaguzi na akatoka amefurahi leo mahakama hiyo hiyo inakuwa mbaya na isiyofaa kwa sababu imemuhoji na kuhitimisha kuwa ushahidi wake aliowasilisha mahakamani hauungi mkono maombi yake bila kuacha chaka ya maana?? INAENDELEA….
1
1
137
China does not pursue modernization for itself alone. We’d like to work with fellow developing countries for global modernization characterized by peaceful development, mutually beneficial cooperation and shared prosperity.
1
10
47
7,940
President Xi Jinping met with Hon. @TuliaAckson together with other leaders of Parliaments attending the Commemoration of the 40th Anniversary of the NPC’s Affiliation to the @IPUparliament & 2024 Interregional Seminar on the Achievement of the SDGs for Parliaments of Developing Countries.
8
43
3
172
12,315
Voice of Bongo retweeted
Hongera sana Mheshimiwa @ummymwalimu kwa kuendelea kuaminiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri wa Afya Nchini. Makubwa yanafanyika Sekta ya Afya Nchini!! 💪
126
32
25
651
60,136
Voice of Bongo retweeted
Nawapa pole wafiwa waliopoteza ndugu, jamaa na marafiki katika ajali ya basi iliyotokea eneo la Mtama mkoani Lindi na kusababisha vifo vya watu 15. Mwenyezi Mungu awe faraja kwetu sote, awarehemu ndugu zetu hawa waliotutoka na kuwajalia majeruhi pona ya haraka. Tunapoelekea msimu wa mwisho wa mwaka, naviagiza vyombo vya ulinzi na usalama barabarani kuongeza usimamizi wa sheria na ukaguzi.
241
202
11
1,460
134,277
UTABIRI WA HALI YA HEWA 11.11.2023
5
13
3,005
Natumia mdomo kuchora na kuandika, nafundishwa na watoto wenzangu…nimeshindwa kwenda shule kutokana na wazazi kukosa fedha za kununua baiskeli ya walemavu (kitimwendo)’’, ndivyo anavyosimulia Rose Mathias (16) mkazi wa Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi, mkoa wa Simiyu.
3
4
381
Voice of Bongo retweeted
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumefanikiwa kuwa wenyeji wa michuano mikubwa ya soka Afrika (AFCON2027), tukishirikiana na Kenya na Uganda. Nawapongeza nyote mlioshiriki kuhakikisha nchi yetu inapata fursa hii adhimu. Nawaagiza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhakikisha tunafanya maandalizi mazuri, ikiwemo kukamilika kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu, viwanja viwili vipya vya kisasa vya michezo Arusha na Dodoma.
678
829
72
5,042
384,285
Voice of Bongo retweeted
Hongereni vijana wetu wa Taifa Stars kwa kufuzu michuano ya kuwania kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (2023 Africa Cup of Nations). Mmeandika historia kwani hii ni mara yetu ya 3 kufuzu tangu kuanzishwa kwa mashindano haya. Nawatakia kila la kheri.
646
884
60
8,316
233,737
Voice of Bongo retweeted
Moja ya tukio ambalo amewahi kulifanya Mmiliki wa klabu mpya wa samatta PEOKFC, #IvanSavvidis Aliwahi kuingia na Mguu wa kuku (Bastola) ndani ya Uwanja wakati ya Mechi dhidi ya #AekAthens (Ligi kuu Ugiriki) na kutaka kumfyatua Refa wa mchezo huo baada ya kukataa bao lao la
1
3
14
1,553
Voice of Bongo retweeted
Mtawala wa Kirumi Vespasian (24-79) Aliweka Ushuru Kwenye Mkojo, Kila Ukiuza Mkojo Unalipa Kodi, Waroma Walikuwa Wanakusanya Mikojo Yao, Baadaye Wanaiuza Kwaajili ya Utengenezwaji wa Kemikali Fulani. Vespasian Alikuwa Anasema: "Pecunia non olet" Akimaanisha "Pesa Haina Harufu."
1
2
14
599
Voice of Bongo retweeted
Watu wa Jamii ya Baka Kutoka Cameroon na Gabon Huwinda Nyoka Wakubwa Misituni Kwa Kutumia Miguu Yao. Huingiza Mguu Kwenye Shimo Wanalohisi Kuna Nyoka na Nyoka Huanza Kumeza Mguu Huo, Wanamvuta Nje na Kumkata Kichwa Chake. Watu Jamii ya Baka Wanapatikana Congo Pia.
3
2
23
1,835
HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA IRINGA KINARA KATIKA KUBORESHA HUDUMA ZA UTENGAMAO NA TIBA MAZOEZI, MATENGENEZO YA VIFAA TIBA NA MIUNDOMBINU Na. WAF, Iringa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe amezitaka Hospiatali za Rufaa nchini kuhakikisha zinatoa huduma za utengamao na tiba mazoezi ili kuwezesha wananchi wenye uhitaji wakiwemo watoto wenye ulemavu kuishi maisha yenye ubora na kuweza kujihudumia wao wenyewe Dkt. Magembe ametoa wito huo leo Mkoani Iringa katika ziara ya kikazi inayofanywa kwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Dtk.Charles Mahera kukagua utoaji na ubora wa huduma kuanzia ngazi ya msingi hadi rufaa, ambapo wamekagua hali ya utoaji Huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Iringa na Hospitali ya Halmashauri ya Iringa Frelimo. Viongozi hao walijionea namna Hospitali hiyo ilivyokuwa na karakana ya kisasa ya kutengeneza viungo bandia ikiwemo miguu, mikono na vifaa saidizi mbalimbali. Wameweza kupata ufafanuzi kutoka kwa wataalamu waliobobea katika taaluma ya kutoa huduma za utengemao na mazoezi tiba waliopo katika Hospitali hiyo. Pia, wameona karakana ya kisasa yenye uwezo wa kufanya matengenezo na marekebisho vifaa tiba vyote vya hospitali hiyo pamoja na Hospitali za Wilaya, Vituo vya Afya na Zahanati za Mkoa wa Iringa. “Niwapongeze kwa kuwa na karakana hii kubwa na nzuri ya kutengeneza vifaa tiba na viungo bandia ambayo inasaidia Mkoa mzima ikiwemo vituo vilivyopo kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa. "Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa fedha nyingi kununua vifaa tiba vya kisasa kuanzia ngazi ya msingi hadi taifa, ni lazima tuwe na mpango wa matengenezo, ili vikiharibika kidogo visiwekwe stoo kwani itakuwa ni hasara kwa serikali na kuwanyima wananchi huduma”, amesisitiza Dkt. Grace. Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI, Dkt. Charles Mahera ameelekeza Mganga Mkuu wa Mkoa huo kuandaa mpango kazi wa kuhakikisha wataalamu wa Hospitali ya Mkoa wanakwenda katika hospital za Halmashauri na kufanya matengenezo ya vifaa tiba na vile vinavyohitajika kupelekwa kwenye karakana, basi visafirishwe na kufanyiwa matengenezo kwa wakati ili virudi katika ubora wake na vitoe huduma kwa wananchi. Katika hatua nyingine, viongozi hao pia wamekagua uboreshaji wa wodi na vyumba vya kulaza wagonjwa uliofanyika na kuzifanya wodi hizo kuwa na mwonekano mzuri wa hadhi ya kimataifa. "Huu ni ubunifu mkubwa, watanzania wanayo haki ya kupatiwa huduma katika majengo yenye hadhi ya kimataifa wakiwa hapa hapa nchini na sio lazima wasafiri kufuata huduma hizo nje ya nchi, kitu cha msingi uboreshaji huu uandane na huduma nzuri kwa mteja, lugha zenye staha, hongereni sana kwa maboresho haya" ameongeza Dkt. Grace Amewakumbusha watumishi wa afya kuzingatia miongozo inayotolewa na Wizara ya Afya ya kuzuia maambukizi ya magonjwa mbalimbali katika maeneo ya kazi kwa kufuata kanuni na miongozo ya afya hususani wanapohudumia wagonjwa ili kujikinga wao wenyewe na kuwakinga wagonjwa pamoja ndugu dhidi ya maambukizi ya magonjwa wanapokuwa wakitoa na kupatiwa huduma. Ziara hiyo ya pamoja kati ya Wizara ya Afya na OR-TAMISEMI imelenga kukagu ubora wa huduma kwa wanachi kuanzia ngazi ya msingi hadi rufaa, ikishirikisha Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. – at Iringa, Tanzania
4
1
27
14,503
Jimboni Butiama
1
5
26
1,517
Voice of Bongo retweeted
Mbona kama imeenda hii
1
4
29
1,194
Voice of Bongo retweeted
Golden Raspberry Awards ni Tuzo za Filamu Zenye Vipengele Kama Filamu Mbaya Zaidi ya Mwaka na Mwigizaji Mbaya Zaidi wa Mwaka. Katika Tuzo Hizo Mwigizaji Maarufu Sylvester Stallone (Rambo) Amekuwa Nominated Mara 15, na Ameshinda Mara 4 Kama Mwigizaji Mbaya Zaidi 1983/84/87 na 91.
1
1
4
633
Voice of Bongo retweeted
Baada ya Kugombana na Mumewe Mwaka 1954 Nadezhda Lebedina (34) Mwanamke Raia wa Ukraine Akalala, Hakuamka Tena Mpaka Mwaka 1974 Baada ya Mama Yake Kufariki. Muda Wote wa Miaka Hiyo 20 Alikuwa Anapumua na Kujigeuza Vizuri tuu Kitandani, Lakini Hakua Anamka. Alifariki Mwaka 1994.
8
3
1
51
5,333
Voice of Bongo retweeted
Mwaka 1982 Mtumishi wa Dini Daniel Everett (69) Raia wa US Aliingia Ktk Misitu ya Amazon Ili Kuwabadilisha Watu wa Makabila ya Misituni Humo Wauache Ukabila na Kuifuata Dini. Alikaa Humo Miaka Mitatu na Mwaka 1985 Yeye Ndio Akajikuta Anaiacha Dini na Kuufuata Ukabila wa Huko.
1
2
1
12
1,940
Voice of Bongo retweeted
Baada ya Bibi Harusi (Surabhi) Kufa Ghafla kwa Mshtuko wa Moyo Wakati Sherehe ya Harusi Yake na Mumewe Manjesh Kumar Inaendelea, Bwana Harusi Akaamua Kumuoa Dada wa Marehemu Mida Hiyo Hiyo na Sherehe Ikaendelea. Hii Ilitokea Mei 2021 Huko Uttar Pradesh India.
1
2
10
1,055