Pinned Tweet
Ukichukua 8 ukatoa 2 unapata 6, lakini 8 hiyo hiyo ukitoa 9 lazima ukope kwa 2 ili upate jibu. Maisha nayo yako hivyo, kuna muda huwezi kufika bila ya wale unaodhani wako chini yako. Heshimu kila mtu, mafanikio hayaji kwa nguvu zako tu bali pia kwa msaada wa uliowahi kuwadharau.
1
65
0 + 0 + 0 bado ni sifuri. Lakini sifuri moja ikisimama baada ya 1, thamani hubadilika kuwa 10. Maisha nayo yako hivyo, si kila kundi linaongeza thamani, wakati mwingine unahitaji mtu mmoja sahihi kuliko watu wengi wasiokuwa na mchango.
1
57
Jifunze kuheshimu kila mtu. Watu ni wale wale; usipokutana naye leo hapa, utakutana naye kesho kule. Heshima haigharimu chochote, lakini inaweza kukufungulia milango mingi kwenye maisha..✍️
42
Maji yanapochemka, yai huwa gumu lakini hufanya viazi huwa laini. Tatizo lilelile linaweza kumfanya mmoja awe imara na mwingine avunjike. Kinachofanya tofauti si tatizo, bali jinsi unavyolikabili. Jitahidi kuwa na mtazamo chanya.
1
51
TZ Quotation power🇹🇿 retweeted
You must find the courage to leave the table if respect is no longer served. Know your worth and protect it.
Kivuli chako huwa mbele asubuhi na huwa nyuma wakati wa jioni. Maisha nayo hubadilika, usijivune ukiwa juu wala usikate tamaa ukiwa chini.
Ukurasa mmoja ukichanika kwenye kitabu, simulizi haiishi hapo. Ukikosea leo, usidhani maisha yako yamekwisha, bado una kurasa nyingi za kuandika.
Ukishika mchanga kwa nguvu sana, huanza kumponyoka kati ya vidole. Kwenye maisha si kila kitu kinahitaji kukilazimisha ili kibaki, vingine viache viende.
2
103
Ukifuta digit moja kwenye namba 1,000,000 unaweza kubadilisha milioni kuwa laki. Ukilitafakari hili vizur utagundua kwamba kosa moja linaweza kufuta miaka mingi ya kujenga jina lako. Kabla ya kufanya uamuzi wa dakika moja, fikiria thamani ya miaka uliyoitumia kujenga heshima yako
2
41
Mto haunywi maji yake mwenyewe, na mti hauli matunda yake. Maisha yanatukumbusha kwamba thamani ya kweli ipo kwenye kuwasaidia wengine.
1
30
Namba 100 ina sifuri mbili, lakini bila ile namba 1 mbele yake zote zingekuwa hazina thamani. Maisha nayo yako hivyo, pesa, umaarufu na mali ni sifuri tu kama huna maadili yanayovipa thamani....✍️
1
335
Kwenye hesabu 2+8=10, 9+1=10, hata 0+10 bado ni 10. Njia ni tofauti lakini jibu ni lile lile. Vivyo hivyo katika maisha, watu wanaweza kufika sehemu moja, lakini safari zao huwa tofauti kabisa. Usijilinganishe na mtu, kila mmoja ana njia yake kuelekea mafanikio.
Ukiangalia angani utaona nyota chache lakin hizo si zote zilizopo. Ukiamua kutazama kwa makini zaidi,utakutana na nyota nyingine nyingi zaidi. Macho yanaweza kuona machache uliyo yachagua kuyaona ila moyo unapoamua huona upeo mpana zaidi. Unachoona si mwisho kuna zaidi ukithubutu
Usijidanganye kwamba kwa kuwa yuko mbali basi ni mwaminifu na hawezi kukusaliti. Broh ameamua tu kuficha. FEAR WOMAN
2
57
Mwanamke anaweza kumsamehe mwanaume msaliti, muhuni au hata mkorofi, lakini mara nyingi huumiza yule mwanaume mtulivu na mwaminifu. FEAR WOMAN.......✍️
1
53
TZ Quotation power🇹🇿 retweeted
Mwanaume asiye na Pesa leo anaweza kuwa Mkombozi wako wa Kesho Heshimu sana Safari yake hata ukihisi hana
Cha kukupa.✍🏻
Funguo ikifungua kufuri nyingi hutunzwa " MASTER KEY " lakini kufuri ikifunguliwa na funguo nyingi hutupwa "HAIFAI"
1
51






