Digital Psychology ๐น๐ฟ๐ฎ๐ฑ retweeted
MSAIDIZI WA LISSU ALIYETEKWA AFUNGUKA MAZITO KUMBUKIZI YA WATU WALIOUAWA OKTOBA 29
SIKILIZA ZAIDI: youtu.be/hbbciGkgHb4?si=fFihโฆ
Digital Psychology ๐น๐ฟ๐ฎ๐ฑ retweeted
#TANZANIA: KAULI ZA VIONGOZI HAZINA UKWELI, KUWA MKWELI USAMEHEWE, KUENDELEA KUTEKA HAKUWEZI KUTUFIKISHA SEHEMU NZURI- SHEIKH MNGODO
Sheikh wa Shura ya Maimamu, Abubakar Mngodo leo Oktoba 29, 2026 ameungana na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu kuomboleza vifo vya wananchi waliouawa wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 nchini Tanzania amesema kauli zinazotolewa na viongozi wa serikali zimejaa uongo na kwamba hawataki kukubali kuwa watu waliuawa wengine waliuawa wakiwa majumbani, amewataka viongozi kukili ukweli ili taifa lipate uponyaji badala ya kuendelea kuteka watu wanaosema ukweli.
Zaidi: youtu.be/H23WIdF7MQY
Digital Psychology ๐น๐ฟ๐ฎ๐ฑ retweeted
PUBLIC STATEMENT: ONE YEAR ON FROM THE OCTOBER 29, 2025 EVENTS โ DEMANDING THE TRUTH, ACCOUNTABILITY & JUSTICE
Today, 29th October 2026, we remember those who lost their lives during and after the 2025 General Election.
To read the full statement: tls.or.tz/uploads/1793263574โฆ
Digital Psychology ๐น๐ฟ๐ฎ๐ฑ retweeted
Naibu Katibu Mkuu Bara, Mheshimiwa Amani Golugwa leo Alhamisi Oktoba 29, 2026 ameshiriki Misa ya kuwambuka marehemu waliouawa Oktoba 25, 2025.
Naibu na wanachama wengine walihudhuria misa hiyo kwenye kanisa kuu la Mtakatifu Joseph, jijini Dar es Salaam.
Digital Psychology ๐น๐ฟ๐ฎ๐ฑ retweeted
Sheria ya sasa ya uchaguzi haiiruhusu nchi kuwa eneo salama la kuishi, bali kuwa koloni la kifalme la mtawala ambaye atjiweka kwenye serikali na kujiondoa hadi atakapotaka
Katiba mpya ndio mzizi, tuipate kabla ya 2028
Digital Psychology ๐น๐ฟ๐ฎ๐ฑ retweeted
Mungu wetu sikia kilio chetu. Tufute machozi na uponye majeraha yetu. Uki wapi mshirika wangu Mdude?๐๐ญ
Kwamba Mh Rais @SuluhuSamia serikali nzima mmekubaliana Kwamba huu ndiyo uwe Mtindio wa kuendesha Nchi? Na Kwamba solution pekee wasomi na washauri wako wamesema ndiyo solution pekee, Kumbukumbu pote duniani hazioneshi style hii kushinda popote.
Digital Psychology ๐น๐ฟ๐ฎ๐ฑ retweeted
Report ya Uchunguzi wa DW kuhusu Mauaji ya Watanganyika Oktoba 29, 2025.๐
#Mo29 #TanzaniaMassacre
Digital Psychology ๐น๐ฟ๐ฎ๐ฑ retweeted
TAARIFA KWA UMMA:
TATHMINI YA MATUKIO YA OKTOBA 29, 2025 BAADA YA MWAKA MMOJA "UKWELI, UWAJIBIKAJI NA HAKI"
Digital Psychology ๐น๐ฟ๐ฎ๐ฑ retweeted
HAKI YA TUNDU LISSU KUSIKILIZWA KIKAMILIFU:
Kwa kuwa MAHAKAMA KUU YA TANZANIA tayari imetamka kwamba; ilikuwa ni MAKOSA kwa Magereza KUMNYIMA Tundu Lissu, HAKI YA FARAGHA NA MAWAKILI WAKE, maana yake ni kwamba; HAKUSIKILIZWA KIKAMILIFU. Yote yajayo yatakuwa ni BATILI.
Ni wazi sasa Rasmi serikali Iko vitani na Wananchi wake, ni suala la Wananchi kufanya maamuzi ya kuingia vitani kwa migomo au kuchagua kwendelea kulialia. Msimamo wao uko wazi, msimamo wetu ni chaguo letu.
Digital Psychology ๐น๐ฟ๐ฎ๐ฑ retweeted
#BREAKING: DEREVA WA ROLI ATEKWA NYUMBANI KWAKE NA WATU WASIOJULIKANA, MADEREVA WATOA TAMKO ZITO
Madereva wa mabasi na malori nchini Tanzania, kupitia viongozi wao, wamelaani vikali tukio la kutekwa kwa mwenzao Rodgers Peter Kateba ambaye wanadai alichukuliwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana Oktoba 16, 2026 na hadi sasa hajapatikana.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Taasisi ya Taifa ya Madereva Tanzania (TATAMATA), Yohana Mwanyaga amesema taarifa za tukio hilo ziliripotiwa polisi na kwamba wamekuwa wakifuatilia suala hilo kwa kufika kituoni mara kadhaa, lakini bado hawajapata majibu kuhusu alipo mwenzao.
Zaidi: youtu.be/-EGESEh5U1w
Kwa Watanzania mtu yoyote au Taasisi yoyote inayo fanya tenda la uhuruma na upendo na unyenyekevu mbele za Mungu, kuwakumbuka Watanzania wenzetu ktk mauwaji ya kutisha ya October 29, 2025. Bila kujali nguo yake au rangi yake tunamshukuru na kumpenda mno.
Digital Psychology ๐น๐ฟ๐ฎ๐ฑ retweeted
29.10.2026. SIKU YA MAOMBOLEZO YA KITAIFA. SIKU YA KUJITATHMINI NA KUJISAHIHISHA.
Nilianza kumbukizi hii kwa kusali Misa Takatifu asubuhi katika kanisa langu la Mtakatifu Martha, Mikocheni. Baadaye nikashiriki mazungumzo na Jenerali Ulimwengu kupitia Post:
youtube.com/live/lTdENudIxCcโฆ
Sasa napenda kutoa ujumbe wangu kuhusu siku hii, maana yake kwa Taifa letu na nini kifanyike ili tutoke katika mkwamo unaotukabili.
1. TUKUBALI MSIBA ULIOLIPATA TAIFA.
Takwimu za Tume ya Rais iliyoongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman: vifo 518, wakiwemo raia 502 na maafisa wa vyombo vya ulinzi na usalama 16. Watoto 21 walipoteza maisha. Tume yenyewe ilitahadharisha kuwa idadi hii inaweza isiwe ya mwisho.
Huu ulikuwa msiba wa Taifa, bila kujali tofauti zetu za kisiasa. Kila uhai una thamani.
2. POLE KWA WAHANGA WOTE.
Familia zilizopoteza wapendwa wao, watoto waliobaki yatima, wajane, wagane, majeruhi na wote walioathirika.
Nyuma ya kila takwimu kuna binadamu, familia na matumaini yaliyokatizwa. Kwa wote waliofiwa nasema: Hatujawasahau. Machungu yenu ni machungu yetu sote.
3. KWA NINI TUIKUMBUKE OKTOBA 29?
Tume ya Chande ukurasa wa 52 wa hotuba ya Mwenyekiti wake ilipendekeza:
โ..Serikali kutenga siku ya Maombolezo ya Kitaifa kuwakumbuka Watanzania zaidi ya 500 waliofariki kwenye ghasia za wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025;โ
Bado tunaisubiri Serikali itangaze siku rasmi ya maombolezo. THRDC imependekeza tarehe 29 Oktoba iwe siku ya kumbukizi ya kila mwaka, na viongozi wa dini wamehimiza sala na tafakari.
Kwa hiyo, tunapoitumia siku ya leo kuomboleza, tunafanya hivyo kwa nia njema, kuonesha mshikamano na kuwafariji wahanga wasije wakadhani Taifa limewasahau.
4. TUELEWE CHANZO CHA MGOGORO, SI VICHOCHEO PEKEE.
Tume ya Chande ilitofautisha kati ya vyanzo vya ghasia na vichocheo vyake. Vyanzo ni kama mafuta, vichocheo ni kama kiberiti.
Ilitaja vyanzo vitano: matatizo ya kisiasa na madai ya Katiba Mpya na mageuzi ya uchaguzi; ugumu wa maisha, ajira na fursa za kiuchumi; matatizo ya kijamii, rushwa na utekaji; udhaifu wa utendaji wa taasisi za umma; na changamoto za mahusiano ya kimataifa.
Tume ilijadili pia vichocheo, vikiwemo kauli za baadhi ya wanasiasa na matumizi ya mitandao ya kijamii.
Hata tukidhibiti vichocheo, hatutakuwa tumetatua tatizo kama mafuta yataendelea kuwepo.
Ndiyo maana nimekuwa nikisisitiza umuhimu wa kutekeleza kwa vitendo falsafa ya Rais Samia ya 4Rs: Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi na Kujenga Upya. Vijana wanahitaji kusikilizwa. Malalamiko yao yashughulikiwe, huku kila mmoja akiheshimu sheria na haki za wengine.
TUTOKEJE KATIKA MKWAMO HUU?
Ninapendekeza hatua zifuatazo:
Serikali itoe msimamo kuhusu siku rasmi ya maombolezo iliyopendekezwa na Tume ya Chande.
Wahanga wote wabainishwe, wafikiwe na kusaidiwa kulingana na mahitaji yao halisi.
Uchunguzi huru wa matukio yenye viashiria vya jinai, mauaji na utekaji ufanyike, na wahusika wawajibishwe kwa mujibu wa sheria.
Mapendekezo ya Tume kuhusu Katiba Mpya, mageuzi ya uchaguzi, uwajibikaji wa taasisi na maridhiano yafanyiwe kazi.
Wazee, viongozi wa dini, wanawake na vijana washirikishwe kikamilifu katika kujenga uelewano wa kitaifa.
Maridhiano si kufuta ukweli, kusahau wahanga au kuacha kuwajibisha waliovunja sheria. Maridhiano ni kuwa na ujasiri wa kukiri mapungufu, kutenda haki, kurekebisha makosa na kujenga upya imani ya wananchi katika taasisi zao.
Ndugu zangu Watanzania, Oktoba 29 isiwe siku ya kuchochea visasi. Iwe siku ya kujitathmini na kujisahihisha, kuthamini uhai wa binadamu na kujiwekea dhamira kwamba madhila haya hayatatokea tena.
Tusisahau waliopoteza maisha. Tusiwaache wahanga peke yao. Tusifanye hofu kuwa mbadala wa amani.
TUKUMBUKE. TUJITAFAKARI. TUJISAHIHISHE. TUTENDE HAKI. TUPONYE MAJERAHA. TURIDHIANE NA TUSONGE MBELE KAMA TAIFA MOJA.
Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, awafariji wafiwa, awaponye majeruhi na alijalie Taifa letu amani ya kweli, amani yenye haki.
Amina.
Digital Psychology ๐น๐ฟ๐ฎ๐ฑ retweeted
KUMBUKUMBU YA MO29
Mwaka mmoja uliopita leo, tarehe 29 Oktoba 2025, maisha ya ndugu zetu yalipotea Tanzania. Vikosi vya ulinzi & usalama vilitumia nguvu ya kifo, na maelfu ya watu waliuawa kinyama.
Tunawakumbuka waathiriwa na familia zao. Kumbukumbu yao iimarishe wito wa haki, ukweli na amani. Hamko peke yenu.
Hatutasahau. ๐ฏ๏ธ
Digital Psychology ๐น๐ฟ๐ฎ๐ฑ retweeted
Mashirika ya kijamii Tanzania zataka waliohusika na vifo vya Oktoba 29 kuwajibishwa
bbc.in/4kmo5AT
Digital Psychology ๐น๐ฟ๐ฎ๐ฑ retweeted
Clouds ata msipo mkumbuka master tidwa sisi hatutochoka
R. I. P MASTER WA CLOUDS FM 29/10/2025
Repost bila kuchoka โ๏ธ @CloudsMediaLive




























