Hatupaswi kuruhusu safari ya mapambano yako iishie katika njia hii kaka, Mungu akupiganie na kukulinda kaka upatikane ukiwa salama.
#FreeTwahaMwaipaya
Baada ya Mwenyekiti @TunduALissu kuhukumiwa kwa kesi isiyokuwepo watawala dhalimu wameendeleza mashambulizi dhidi ya chama chetu kwa kutumia polisi. Katibu BAWACHA Kigoma amekamatwa jana, Gwamaka mbughi na Issa kwisa Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Songwe wamekamatwa leo ahsubuhi.
"Waheshimiwa Majaji mnatambua kwamba nina msiba mkubwa, msiba wa mtu ambaye amenifanya niwe Mwanasheria, mtu aliyenilea na kunifanya kuwa mimi. Kwa kuwa hakuna kesi ninatumaini mahakama hii itaniacha nikamzike kaka yangu nilishindwa kumuunguza nisishindwe kumzika."@TunduALissu
I have never ever, never ever been convicted of a criminal offense. Never ever. Mheshimiwa @TunduALissu akiwaambia Majaji.
"Na hivyo kw ushahidi huo tunasema Treason haijathibitishwa bila kuacha shaka yoyote" anasema Jaji Nduguru kutoka chumba namba 01 cha mahakama kuu. @TunduALissu
Ndani ya chumba cha mahakama kusubiria hukumu ya kesi ya uhaini dhidi ya Mwenyekiti wetu Mheshimiwa @TunduALissu .
#LissuSiyoMhaini.
Kuna watu wamewahi kujigamba hadharani kumiliki magenge ya uhalifu na ya kiuni wakitaja majina yao mara chui mweusi na mbwa mwitu maajabu ya nchi yetu ni kwamba hawakuwahi kuchukuliwa hatua yeyote. Binti mdogo anapewa kesi ya Ugaidi kwa sababu tu ya msimamo wa kupigania haki.
Felius Festo retweeted
“Mange Kimambi ndo Project ya kuigawa Chadema, cha ajabu ni kuona makada wa CHADEMA wanamsikiliza na kumuamini” Godbless Lema
“Hilda Newton anachukua maneno ya Mange kama yalivo Hilda huyu kiongozi wa Chama hatuwezi kuwa na viongozi wa namna iyo” Lema
Utekaji haiwezi kuwa suluhu ya mkwamo wa taifa, Muachieni Twaha Mwaipaya na kama ana makosa afikishwe mahakamani. Kila kijana anazo ndoto, malengo, matamanio, familia na wanaomtegemea utekaji unazima yote ayo. Free Mwaipaya.
Kufikiria kwamba CCM wanahitaji maridhiano ni kujidanganya, CCM wanahitaji picha katika meza ya maridhiano zitumike kuadaa jumuiya za kimataifa.
Felius Festo retweeted
TAARIFA KWA UMMA.
@ChademaTZ2 @HecheJohn @AdvMahinyila @NectoKitiga @duahamud @RevlineMbugi @FeliusFesto
Mungu akupiganie na kukulinda kaka upatikane ukiwa mzima.
#FreeTwahaMwaipaya
Felius Festo retweeted
Tundu Lissu was charged with (politically motivated) Treason after calling for electoral reform.
The sentence for Treason in Tanzania is nothing else other than DEATH.
The world is waiting for November 06
Thanks Hon Pam Cox for raising this matter in the House Of Commons
Felius Festo retweeted
“Mauaji ya 29 Oktoba 2025 ni makubwa na yakutisha kuliko mauaji ya Sharpeville ya Afrika ya kusini ya 21 Machi 1960 kipindi cha ubaguzi wa rangi”
#UkweliHakiUwajibikaji
#FreeTwahaMwaipaya
#FreeCollethaNtidyicha
Felius Festo retweeted
Mwaka mmoja baada ya matukio ya Oktoba 29, 2025, maumivu ya waathirika bado hayajaisha na haki haijapatikana.
Tunasimama pamoja na familia za wahanga kudai ukweli, uwajibikaji wa Sheria , na haki thabiti kwa wote.
Kurejea kwa shughuli na maisha kama kawaida haimaniishi kuwa kila kitu kiko sawa.
#Oktoba29 #UtawalaWaSheria #HakiNaUwajibikaji #HakiZaBinadamu #TanzaniaMassacre
Felius Festo retweeted
Leo umetimia mwaka mmoja tangu mauaji yaliyofanywa kwa makusudi na vyombo vya dola vya Tanzania dhidi ya Watanzania wasio na hatia.
Mauaji ya October 2025 yalikua yanaweza kuepukika na uchaguzi ukafanyika kwa amani na usalama.
Kwasababu ya kiburi na uchu wa madaraka watawala waliamua kupuuza wito wa mda mrefu wa viongozi wa dini, vyama vya siasa, mashirika yasiyo ya kiserikali na hata watu maarufu ya kutaka mabadiliko ya katiba na sheria za uchaguzi ili kuwezesha uchaguzi huru na haki.
Mpaka sasa mwaka mmoja baadae Nchi iko kwenye mkwamo mkubwa wa kisiasa, watu wanaendelea kutekwa, kuuawawa na kupotezwa.
Kila anaetoa sauti ya kukemea uovu na kutaka maridhiano na uwajibikaji wa kweli anakabiliwa na kifo au mashitaka ya uongo.
Inaonekana hawa watawala wameshindwa kujifunza kwa yale mabaya yaliyotokea, Inaonekana wanafurahia kuendeleza utawala wa mkono wa chuma, udikteta na ubabe, mauaji, utekaji na kunyamazisha badala ya kushawishi na kutatua matatizo.
Kwa kutumia njia hizi mbele ni giza tupu, hakuna sehemu ambayo utawala wa kibabe Umefanikiwa kunyamazisha watu wote, Nchi hii ina watu zaidi ya milioni 70, hakuna siku watu wote hawa watanyamazishwa kwa uongo na kikundi kidogo cha watu kwa kutumia ubabe.
Njia pekee ya kutatua mkwamo huu ni.
1. Kumuachia Mwenyekiti Lissu na kufuta kesi za uongo dhidi ya wanachama wetu wote.
2. Kuachia mateka wote na kusitisha utekaji na mauaji ya kiholela.
3. Kuruhusu msuluhishi huru (mediator) kuleta watu pamoja na kuzungumza kwa ukweli na uwazi.
4.Uwajibikaji bila upendeleo kwa wahusika wa mauaji, kulipa fidia familia za wahanga, kutibu majeruhi wote na kuwapa fidia.
5. Kuruhusu Uchunguzi huru na kuomba radhi mbele ya Watanzania kwa makosa makubwa yaliyofanywa na vyombo vya dola dhidi ya raia wake.
6. Kuandika katiba mpya ya Nchi na sheria za uchaguzi ambazo zitarudisha umoja na haki kwa kila mtu.
7. Kutamka kwa uwazi kwamba makosa kama yale hayatajirudia tena kwenye Nchi yetu.
8. Kuhakikisha familia zinapata miili ya wapendwa wao na kufanya maziko ya heshima, kiafrika na kidini.
Kuendelea kutumia ubabe ni kuchochea chuki, uhasama na visasi kwa siku zinajazo…
Watawala badala ya kutumia chawa na ubabe kujaribu kuhujumu Chadema na uongozi wa Chadema, Tumia busara kufanya jambo sahihi la kuponya Nchi hii.
Tunajua mipango yenu dhidi yetu, lakini haki haijawahi kushindwa.
Endeleeni kupumzika kwa amani wote mliouwawa kikatili na kibabe, poleni majeruhi na wahanga wote.
Haki inaweza kuchelewa Lakini haki itapatikana tu.
Felius Festo retweeted
Today, the U.S. Embassy community joined me to honor the memory of all those who lost their lives in the violence surrounding Tanzania’s October 2025 general elections. We remember them, and the families who still grieve and seek answers. As I said to the U.S. Senate during my confirmation hearing, this will not be swept under the rug.




























