
ALT Katibu Mkuu wa Zanzibar Press Club (ZPC), Mwinyimvua Nzukwi, akieleza namna klabu hiyo ilivyotekeleza mradi wa ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari kwa maofisa ubalozi wa Uswizi nchini Tanzania wanaosimamia miradi inayohusiana na masuala ya haki za binadamu, uhuru wa kujieleza, demokrasia na utawala bora Consuela Natale na Erick Kalunga walioambatana na maofisa wa International Media Saport (IMS), Fausta Musokwa Mratibu wakati wa kikao cha tathmini ya mradi huo kilichofanyika Julai 23, 2024 katika ofisi za klabu hiyo Kijangwani, Zanzibar.

ALT Mkuu wa shirika la International Media Suport (IMS) Afrika, Esben Harboe akifafanua jambo katika kikao cha tathmini ya mradi wa ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari uliotekelezwa na Zanzibar Press Club (ZPC) alipokutana na wanachama wa klabu hiyo Julai 23, 2023. Wengine ni Ofisa Ubalozi wa Uswizi nchini Tanzania anayesimamia miradi inayohusiana na masuala ya haki za binadamu, uhuru wa kujieleza, demokrasia na utawala bora, Consuela Natale (kulia) na Mratibu wa IMS Tanzania, Fausta Musokwa (kushoto). Kikao hicho kilifanyika katika ofisi za ZPC Kijangwani na kushirikisha baadhi ya wanachama walionufaika na mradi huo ambapo ujumbe huo pia ulikutana na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi, ACP Abubakar Khatib Ali na uongozi wa Chuo cha Polisi Zanzibar (ZPC).

ALT MAOFISA wa Ubalozi wa Uswizi nchini Tanzania wanaosimamia miradi inayohusiana na masuala ya haki za binadamu, uhuru wa kujieleza, demokrasia na utawala bora Consuela Natale (kushoto) na Erick Kalunga (wa pili kushoto) wakiwa katika kikao cha tathmini ya mradi wa ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari uliotekelezwa na Zanzibar Press Club walipokutana na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi, ACP Abubakar Khatib Ali (hayupo pichani) katika makao makuu ya polisi mkoani humo Julai 23, 2024. Wengine ni Wakaguzi Wasaidizi wa Polisi Seif Rashid Jumbe (kulia) na Abubakar Khatib Mattar.






































